Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MBUNGE GEOFFREY MWAMBE AZINDUA ZAHANATI MATAWALE
• Imegharimu Milioni 200
• Wananchi wampongeza
Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mheshimiwa Geoffrey Mwambe, leo amezindua zahanati mpya katika kijiji cha Matawale kata ya Matawale.
Ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu TZS. 200,000,000/= (Milioni Mia Mbili) kutoka Serikali Kuu.
Kata ya Matawale yenye vijiji saba haikuwa na zahanati na hivyo kuwalazimu wananchi kutembea zaidi ya kilomita thelathini kufuata huduma za matibabu katika kituo cha afya Mbonde au hospital ya Mkomaindo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mbunge Geoffrey Mwambe alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kwa namna anavyomuunga mkono na kumpatia fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Jimbo la Masasi Mjini ikiwemo ujenzi wa zahanati hiyo ya Matawale.
Mheshimiwa Mbunge Geoffrey Mwambe aliwaomba Wana Matawale kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani, Diwani Mnela pamoja na yeye ili nia yao ya kuwaletea maendeleo iweze kufikiwa kwa uharaka zaidi.
Mheshimiwa Geoffrey Mwambe(MB) aliwaeleza wananchi waliohudhuria hafla hiyo kuwa serikali imedhamiria kuhakikisha suala la elimu linapewa kipaumbele ndani ya Mji wa Masasi na yeye kwa nafasi yake atahakikisha kata ya Matawale inapata shule ya sekondari ya kata ili kupunguza adha ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya shule kwenye kata za Napupa na Mwenge Mtapika.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mbunge Geoffrey Mwambe aliongozana na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Masasi wakiongozwa na
Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg Twahili Mayola, Kaimu Katibu wa CCM wilaya Ndg Pius Amoli, pamoja na Mwenyekiti wa umoja wa vijana wilaya Ndg Seif Abdul
Namtusi.
Akizungumza katika hafla hyo ya uzinduzi wa zahanati kwa nyakati tofauti tofauti viongozi hao wa CCM wilaya walimpongeza Mheshimiwa Mbunge Geoffrey Mwambe kwa namna anavyotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo la Masasi Mjini na kuwaomba waendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Mbunge kwani anaonesha dhamira ya dhati ya kuijenga Masasi Mjini na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri Mheshimiwa Hashimu Namtumba (Sugu) alimpongeza Mheshimiwa Geoffrey Mwambe (MB) kwa namna anavyoshirikiana naye vizuri kuhakikisha kero na changamoto za Wana Masasi Mjini zinapatiwa ufumbuzi.
Wakizungumza kwenye hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Andrew Kalinga na Mganga Mkuu wa Halmashauri Salumu Gembe, wamempongeza Mheshimiwa Geoffrey Mwambe(MB) kwa juhudi anazozifabya kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za kijamii zikiwamo huduma za afya. Wamemuahidi kusimamia utendaji wenye tija kwa watumishi wa zahanati hiyo na maeneo mengine ya halmashauri.
#MASASI MPYA
Imetolewa na OFISI YA MBUNGE JIMBO LA MASASI MJINI
Facebook: Ofisi ya mbunge jimbo la masasi mjini
Instagram: Ofisi ya mbunge jimbo la masasi mjini
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.37.34.jpeg121.9 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.37.34(1).jpeg116.8 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.37.35.jpeg200.6 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.37.35(1).jpeg190.4 KB · Views: 1
-
WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.37.35(2).jpeg101.7 KB · Views: 3