Fursa soko la pilipili nchini China

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,036
Kampuni ya Greenchain ya Shanghai, nchini China itatembelea Tanzania mwezi Machi 2023 kwa ajili ya kukutana na wazalishaji wa Pilipili aina ya Tajin (Sweet And chili pepper au kitaalamu Capsicum annuum.)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mkutano wa Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki na Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Grenchain Bi Rossella Lyu uhitaji wa Pilipili hizo ni takribani tani 42,000.

Kufunguka kwa fursa hizi ni mwendelezo wa kazi kubwa ya kuimarisha Diplomasia ya Uchumi ikiwemo safari ya hivi karibuni ya Rais Samia nchini China.

licensed-image.jpeg
 
Back
Top Bottom