CIIE yasaidia bidhaa za kilimo za Afrika kuingia katika soko kubwa la China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111463250967.jpg

Alfajiri na mapema kwa saa za Kenya, wakulima wa maua nchini humo walichuma waridi katika mashamba yao yaliyoko Naivaisha. Kutokana na ndege za moja kwa moja kati ya Kenya na China na njia maalumu ya forodha nchini China kwa bidhaa za Afrika, maua hayo yanaweza kufika mikononi mwa wateja wa China ndani ya saa 17. Hivi sasa waridi za Kenya zinaongoza katika soko la China kufuatia ubora wake, na yanapatikana katika maduka mengi ya maua katika miji mbalimbali nchini China.

Umaarufu wa maua ya Kenya katika soko la China haswa unatokana na majukwaa mbalimbali ya kuhimiza biashara, ikiwemo Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa za Nchi za nje ya China (CIIE). Wakati China ilipofanya Maonesho hayo ya kwanza mwaka 2018, mawaridi ya rangi mbalimbali yaliwekwa katika kibanda cha Kenya, yakiwa bidhaa muhimu ya nchi hiyo iliyokuwa inataka kuingia katika soko la China. Baadaye mawaridi ya Kenya yakapata umaarufu mkubwa, na mauzo yake nchini China yameongezeka mwaka baada ya mwaka.

Waridi ya Kenya ni moja ya mifano tu ya mazao ya kilimo ya Afrika yaliyochukua fursa ya CIIE kupata umaarufu katika soko la China. Licha ya maua hayo, pombe kutoka Afrika Kusini, kahawa ya Ethiopia, pilipili ya Rwanda, korosho ya Tanzania, asali ya Zambia, na bidhaa nyinginezo za nchi za Afrika zinazopendwa nchini China zote ziliwahi kuoneshwa katika CIIE. Katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa za kilimo za Afrika zimependwa sana na wateja wa China kutokana na ubora na ladha ya kipekee. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka kumi iliyopita, mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika kwa China yameongezeka kutoka dola bilioni 2.84 za Kimarekani hadi dola bilioni 5.3 za Kimarekani, na tangu maonesho ya kwanza ya CIIE, mauzo hayo yameongezeka kwa miaka sita mfululizo, na China imekuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa maagizo ya bidhaa za kilimo za nchi za Afrika.

Katika Maonesho ya sita ya CIIE yanayoendelea mjini Shanghai, makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Shipokosa Mashatile ameipongeza China kwa kufungua soko lake kwa dunia, hasa nchi za Afrika, na kusema CIIE inatoa fursa nzuri kwa makampuni ya nchi mbalimbali kuonyesha bidhaa na huduma zao kwa wateja wa China. Maonyesho hayo yamevutia zaidi ya makampuni 50 ya bidhaa za kilimo kutoka nchi 20 za Afrika. China pia imeshirikiana na balozi za Afrika nchini China na Shirika la Biashara la Umoja wa Mataifa kutoa vibanda maalum kwa makampuni ya nchi tisa za Afrika zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo.

Benin ni moja ya nchi tisa zilizopata kibanda hicho. Safari hii, Benin imeleta nanasi yake maalum inayojulikana kama “Mkate Mtamu”. Balozi wa Benin nchini China Simon Adowelander amesema, kama maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji bidhaa za nchi za nje duniani, CIIE ni jukwaa bora kwa makampuni ya Afrika kuingia katika soko la China. Anaamini kuwa kupitia maonesho hayo, nanasi ya Benin bila shaka itapata uamarufu nchini China kutokana na ubora wake, na kufungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa kilimo na biashara kati ya nchi hizo mbili.
 
Back
Top Bottom