Free and Independent Zanzibar

jana samweli sitta kasema mnadaiwa hela kibao za umeme,tunaombeni hela zatu nyie waunguja!!mmeona vimafuta vitapatikana ndio mnaanza kelele zenu wala nguru wakubwa

hizo hela zikilipwa, mtaondoa wanajeshi wenu walioko zanzibar? Watu wanaelewa kanuni ya mtawala ni kumpandikizia deni anae mtawala... We shall overcome ...we shall overcome ... We shall overcome !!!
 
POUND 600.000 YA MİAKA YA 60s , SIO SAWA NA POUND 600,000 YA MWAKA 2011... ACHENI UNAFIKI NA UPOTOSHAJI...

Takashi,

600,000 pounds. £1 pound ya miaka ya 1940-1960 ni sawa na £45-£40 ya sasa. Kwasababu hiyo :-
600,000 x 45 = £27,000,000

£27,000,000 ndio initial capital iliyotumbukizwa BOT.

Tukicompound for 50 years ya muungano (muungano sasa ni 47 years).

FV = 27,000, 0000 ((1 +0.071)(Tbills yields by January 2011))^50= £833,368,931.674 (Tuchukulie wazanzibar hawachangii BOT zaidi ya initial capital invested).

Tukiweka na michango yao BOT kila mwaka kutoka kwenye mauzo ya karafuu na utalii na kodi tunaweza kufikia kiwango cha £ Billion kadhaa.

Chenge hataweza kulipa na wala Serikali ya Tanzania haiwezi kulipa. Narudia tena Muungano ujadiliwe kwa busara na hekima wakuu na sio dharau na kebehi uchumi wa nchi hii unaweza kucollapse.
 
huko usa mnafanya nini???kubeba magunia??njooni msaidie ndugu zenu kuvua samaki!
labda hizo gunia anazobeba ndio zinafanya ndugu zake wapate pesa za kununua vyombo bora vya kuvua samaki na kuwapeleka ndugu zake shule. Si kweli kwamba ambae yupo nchini ndio anafanya more for his/her country kuliko aliye nje, huenda tena ambae yupo ndani ndio fisadi mkubwa kodi halipi na kila kukicha anauza nchi
 
Takashi,

600,000 pounds. £1 pound ya miaka ya 1940-1960 ni sawa na £45-£40 ya sasa. Kwasababu hiyo :-
600,000 x 45 = £27,000,000

£27,000,000 ndio initial capital iliyotumbukizwa BOT.

Tukicompound for 50 years ya muungano (muungano sasa ni 47 years).

FV = 27,000, 0000 ((1 +0.071)(Tbills yields by January 2011))^50= £833,368,931.674 (Tuchukulie wazanzibar hawachangii BOT zaidi ya initial capital invested).

Tukiweka na michango yao BOT kila mwaka kutoka kwenye mauzo ya karafuu na utalii na kodi tunaweza kufikia kiwango cha £ Billion kadhaa.

Chenge hataweza kulipa na wala Serikali ya Tanzania haiwezi kulipa. Narudia tena Muungano ujadiliwe kwa busara na hekima wakuu na sio dharau na kebehi uchumi wa nchi hii unaweza kucollapse.
Ni mtu mpumbavu tu anayeweza amini vitu kama hivi(note mpumbavu hafundishiki).
Na hizo hela zilikuwa zikitika Unguja , wakati waunguja wamelala usingizi au ilikuwaje?
Acheni uvivu wa kimwili na wa kufikiri.
Halafu kwa ujinga wenu hivi BOT ilikuwepo 1964?
OVYO!!!
 
kuwa na adabu na heshima
kama zamani walikuwa taifa huru
wana haki ya kutaka kuwa huru tena

matusi yako yanaongeza hasira
nahisi umetumwa labda,kuwatukana na kuwachokoza wazanzibari
Same mistake buddy,
Kwanza,hivi unapoambiwa umewaibia wazenj wewe unachekelea tu.
Kama hilo si tusi la kuambiwa wewe ni mwizi basi sielewi maana ya neno tusi.
Pili, inaeleleka we ni kama wale watu wanaotumiwa as a face nappy au tissue.
Hawa haja yoa ilikuwa nini katika kuingia muungano in the first place, walichotaka wamepata? hilo nikuulize weye mkubwa
 
Same mistake buddy,
Kwanza,hivi unapoambiwa umewaibia wazenj wewe unachekelea tu.
Kama hilo si tusi la kuambiwa wewe ni mwizi basi sielewi maana ya neno tusi.
Pili, inaeleleka we ni kama wale watu wanaotumiwa as a face nappy au tissue.
Hawa haja yoa ilikuwa nini katika kuingia muungano in the first place, walichotaka wamepata? hilo nikuulize weye mkubwa
Majoja, huna sababu ya kuwashushia heshima kiasi hiki wenzako. Kwanza ukubali, Zanzibar ilikuwa ni nchi huru au la? Kama ilikuwa ni nchi huru na yenye rais wake, mnachoona shida kuturudishia tena ule uhuru wetu tuendelee na hamsini zetu wakati nyie mkiendelea na za kwenu ni nini? Tulumbane kwa hoja na si kwa kuwafananisha wengine na tissue. Hii ni dharau kubwa sana mkuu. Tambua kwamba wazanzibari ni watu kama wewe na katu hawapaswi kubezwa pale wanapoomba haki yao ya msingi ya kuwa huru.
 
View attachment 33609 Bendera ya tanganyika
View attachment 33610Ya tanzania ina tofauti gani na tanganyika ?
View attachment 33611Nembo ya tanganyika hii sasa ona ya tanzania
View attachment 33612hii sasa imekuwa ya tanzania

View attachment 33613Wakiambizana kuwa zanzibar ni nchi ndogo sana hawatushughulishi,hii ndio ccm,hata ule wimbo wa taifa wa tanganyika umekuwa wa tanzania,huu ni utapeli wa kutupwa,hizo rangi za kanisa ndio zimetukaba watanzania na wazanzbari.

Muungano lazima tuuvunje,hatuutaki umetukaa rohoni,mkubwa mnyanyasa mdogo
imewakilisha
 
Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure. Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu. Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.
free zbr. Mimi ni mtanganyika na sipendezwi na serikal yangu kuendelea kunyima zbr uhuru. Wazanzibar fanyeni mapinduz mengine. Shamhuna awe kiongoz wa serikal maana yeye pekee sio mnafik ktk suala hilo. Ccm iache upumbavu wa kulazmisha watu limuungano ambalo hawalitaki. Sitaki muungano, nataka nchi yangu TANGANYIKA.
 
Wazanzibar kwa asilimia kubwa sana mlichagua serikali ya mseto na CCM, sasa hivi kelele za kutokuwa huru zinatoka wapi wakati hata mwaka hamjamaliza ktk ndoa yenu?
 
Pasco, kuhusu uhuru nafikiri somewhere tumeargue pia na mwanakijiji. Wazanzibari tunaujua lakini hatuutambui uhuru wa 1963, ambao alikabidhiwa Sultani. Ule haukuwa uhuru wetu sisi, kwani wewe Pasco ulishawahi kuona Zanzibar wanasherehekea uhuru wa December 1963? Sisi uhuru kamili tuliupata 12/01/1964 pale tulipofanikiwa kuifanya nchi kuwa mali yetu wazanzibar weusi wazalendo. Nafikiri Pasco kama umefuatili kwa karibu historia ya Zanzibar utakuwa unajua kabisa ni namna gani ambavyo ushindi wa Chama cha ASP ulikuwa unaporwa na waarabu, hadi kufikia kuifanya ASP kutumia nguvu kurudisha utawala mikononi mwa wazanzibar. Kwetu sisi uhuru ni ule wa mapinduzi ya zanzibar na ndiyo maana tutayaenzi mapinduzi daima.

Naona umeongea sana kuhusu umoja ni nguvu na habari za sisi kuuana sisi kwa sisi. Nafikiri Pasco kuna kitu hapa umeamua kujifanya hukielewi au kwa makusudi umeamua kuupotosha umma wa watanzania kuhusu zanzibar. Hivyo visa na visasi vya mwaka 1964, kama vingeendelea kuwepo, kwa hakika tusingeshindwa kuuana hata kama tupo ndani ya muungano. Muungano umesaidia nini kuzuia watu wasilipane visasi vya mauaji yale? Na unafikiri muungano ukivunjika, nini kitasababisha watu wakumbuke machungu ya mapinduzi? Hapa Pasco sikubaliani na wewe hata kidogo.

Na kwa upande mwingine unaongelea habari ya umoja ni nguvu, yes hakuna anayekataa hilo, lakini hakuna haja ya kuwa katika umoja ambao hauna faida. Tunaweza kuvunja muungano, Zanzibar ikawa nchi huru na yet tukaungana kama federation. Wote tukawa washirika katika East Africa Federation. Kwanini nyinyi mnataka sisi tuwe nchi moja na nyie wakati mna mamlaka yenu na maamuzi yenu, ambayo mengi yao wazanzibar hatuhusishwi?

Na mwisho nataka ieleweke kwamba hakuna ushahidi wowote beyond reasonable doubt unaoonyesha kwamba Tanganyika inaibeba Zanzibar. Mna nini cha ziada nyie watanganyika ambacho zanzibar hatuna? Wakati tunaamua kuutafuta uhuru na hata kumpiga sultani tulijua kwamba tunaouwezo wa kujitegemea na tulijua kwamba tunaweza kuiendesha zanzibar huru kwa nguvu zetu wenyewe. Sasa kusema kwamba tunabebwa ni dharau kwa wazanzibar ambao walimwaga damu wakati wa mapinduzi ya 1964.

Umeongelea habari ya waingereza kutia nanga mombasa tayari kwa kuirudisha zanzibar kwa sultani wa oman. Nadhani katika hili pia umeamua kuupotosha umma. Ninakumbuka vizuri sana taarifa zilizoenea wakati huo juu ya kurudi kwa waingereza,tulikaa mafichoni kwa zaidi ya wiki kama tatu baada ya mapinduzi, tukila mtunda na madafu kwa kuhofia machafuko mengine yatokanayo na ujio mpya wa waingereza. Je unajua kwanini waingereza hawakuivamia Zanzibar ili kuirudisha kwa Sultani? Unaweza kuuhakikishia umma kwamba waingereza hawakuivamia zanzibar kwa sababu ya muungano? Mimi naomba nisiseme kitu juu ya hilo, manake naweza onekana mchochezi. Lakini kwa taarifa yako millions of Arabs were already dead. Huyo Sultan angerudi aje awaongoze akina nani? Fuatilia vizuri mkuu uelewe kwanini uvamizi wa waingereza hakufanyika. Kwamba hawakuvamia kwa kisingizio cha muungano, nafikiri tutakuwa tunapotosha.

Lakini pia nashukuru kwamba umenirekebisha mahali fulani kwamba kwa sababu tulishapata uhuru mara ya kwanza sasa tuombe restoration ya sovereignty ya wazanzibari na si uhuru. Hilo nakubaliana na wewe. Maana tayari tuna kila kitu kinachotupa haki ya kuwa nchi, isipokuwa uhuru wetu umebakwa na watanganyika. So turudishieni ule uhuru muliotuibia men.
Msema hovyo, kusema ukweli, kutokushukuru kwa lolote kuhusu muungano, ni ukosefu wa shukrani.
Panapo majaaliwa 2015 nitapenyesha karata yangu pahali, nikifanikiwa nitakuwa miongoni mwa nitakao waunga mkono mpate mnachotaka. Tukiendelea hivi, sio tena kuhusu kero za muungano, sasa ni kero za wanaotaka kuuvunja muungano, ili isiwe kero, mtakipata tuu mnachokitafuta. Naamini, atufutae, hachoki, na akichoka, kesha pata.

Hii hoja yako ya "kwa taarifa yako millions of Arabs were already dead", haina mashiko, japo ni kweli maelfu walikufa, nilisoma mahali population ya Zanzibar ilikuwa around laki 6-8. Waliokufa ni 86,000, sasa hao millions walitoka wapi?.
 
Hakiii, Munanifurahisha sana kwa comments zenu. Nina washangaa watu wazima wanasema maneno ya kitoto sana. Hizo 50 billion ni pesa za tanzania. Hivo katika fikra zenu kuwa hiyo ndio itakayotuzuia kutetea UHURU wetu?. Fanyeni hesabu za haraka haraka.

Mid-market rates: 2011-07-11 00:07 UTC
50,000,000,000.00 TZS = 31,397,177.40 US

hizi ndio vijisenti wanavyotudai. hahahahahahahaha. Eti Zanzibar inadaiwa na tanesco yaguju. Chukueni mutuachie nchi yetu mumesahau mulioiba karafuu. Mumesahau kama BOT ni pesa za Zanzibar. Amir Jamal amekufa lakini wenzake wengi bado wapo hai. Ile Dhahabu tani 600 ya zanzibar muliipeleka wapi?. Nyinyi muna vichwa vibovu sana tukianza kuwadai, ziwa tanganyika litakauka. "Lake tanganyika will cease (dry up)"
 
Wazanzibar kwa asilimia kubwa sana mlichagua serikali ya mseto na CCM, sasa hivi kelele za kutokuwa huru zinatoka wapi wakati hata mwaka hamjamaliza ktk ndoa yenu?

Napenda nikujuze kuwa Mseto ule ni wa Znz kwa Znz na wala hauwezi kabisa kuhusisha wa Tanganyika. Mseto ule umewekwa kwa ajili ya maslahi ya Znz na kwa waZanzibar. na wala si kwa WaTanganyika.

Lakini hapa kinachoongelewa ni Muungano na uhuru wa Znz kujikomboa dhidi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom