Free and Independent Zanzibar

Msema hovyo, itakuwa ulizaliwa baada ya mapinduzi matikufu ya Januari 64 ndio maana inasema hovyo. Uhuru gani huo unaouulizia. Zanzibar si ilipata uhuru wake Desemba 1963?, sasa uhuru gani tena mnaoutaka.

Muungano wetu ni ndoa ya ukweli ya mkeka iliyoongiwa kwa convenience. Ndoa ni ndoa hata ikiingiwa kwa hiari ni binding na haiwezi kuvunjika kwa hiari hata kama mmoja wa wanandoa hakuingia kwa hiyari na kesha ichoka ndoa yanyewe, bado haiwezi kuvunjika.

Ukiona mke amekuchoka na kuanza kukufanyia visa, ujue kesha pata bwana mwingine hivyo anafanya visa ili apewe talaka akajinafasi. Bara tumeshalibaini hilo, tena bwana mwenyewe ni mafuta ambayo hayajai hata kwenye kinibu!. Visa fanyeni, talaka kamwe hatutoi na ndoa itadumu daima. Muungano Milele!

Mungu ibariki Tanzania.

Pasco.

Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure.

Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu.

Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.
 
hivi mnaonaje ikiwa kila mkoa ikiwa ni nchi inayojitegemea halafu tuwe kwenye shirikisho? nadhani ufisadi utapungua.
 
Sudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati
 
Na wao walipeni pound 600,000 walizoanzishia benki kuu ya Tanzania 1960s na US dollar zao zilizotumika katika vita vya kagera kutoka kwenye mauzo ya karafuu yaliyopita.

Dharau mkuu hazitaleta mwafaka wala kuelewana hekima na demokrasia ndio solution ya muungano huu. Serikali 3 au muungano kuvunjika kabisa kwa ustaarabu.

jamani hizo paundi laki sita zinaweza kulipwa na chenge tu peke yake; hivi mnajua bajeti nzima ya Zanzibar ni sawa na bajeti ya Wizara moja tu ya Muungano!?
 
Kaka umesema kweli visiwa vingi ni matajiri wakubwa sana, zanji wamekuwa masikini kwa sababu walikosea sana kukubali kuungana na magamba we si unaona wapemba wanaenda kasi?

Sudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati
 
hivi mnaonaje ikiwa kila mkoa ikiwa ni nchi inayojitegemea halafu tuwe kwenye shirikisho? nadhani ufisadi utapungua.
Duh, Zumbemkuu!!! nafikiri hapa hujaitendea haki thread yangu? Kwani ni mkoa gani mwingine ambao ulipigania uhuru wake binafsi, ukawa na bendera yake, na alama zote za taifa halafu ghafla huo uhuru ukanyang'anywa? Ukumbuke Zanzibar ni nchi ambayo ilipigania uhuru wake na ikajitawala kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kunyang'anywa huo uhuru na Nyerere.
 
jamani hizo paundi laki sita zinaweza kulipwa na chenge tu peke yake; hivi mnajua bajeti nzima ya Zanzibar ni sawa na bajeti ya Wizara moja tu ya Muungano!?
Si na ndiyo maana tunasema tuachieni nchi yetu, maana tunachokizalisha Zanzibar kinatutosha kabisa, maana hatuhitaji vikubwa kama ninyi. Sasa kitendo cha kuwa kwenye muungano kila kitu mnatupangia, kiasi cha kwamba tunashindwa kufanya maendeleo yetu binafsi. Tunabaki tumeconcentrate kwenye issue za muungano ambazo hazitusaidii kwa lolote.
 
Duh, Zumbemkuu!!! nafikiri hapa hujaitendea haki thread yangu? Kwani ni mkoa gani mwingine ambao ulipigania uhuru wake binafsi, ukawa na bendera yake, na alama zote za taifa halafu ghafla huo uhuru ukanyang'anywa? Ukumbuke Zanzibar ni nchi ambayo ilipigania uhuru wake na ikajitawala kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kunyang'anywa huo uhuru na Nyerere.

sorry! mkuu. mawazo tu, sio kuwa nimekosoa thread yako.
 
hilo deni wala hata wasilipe litaingia magambani tu na umeme wenyewe ndo hivyo tena kimeo siku zote. sasa hivi ni kumwaga ugali/wali tu ndo kilichobaki maana magamba walishamwaga mboga yote.

Lipeni kwanza deni la Bilioni 50 kwa kuwapatieni umeme, halafu mnasepa tu.
 
Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure.

Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu.

Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.

sidhani kama unajua kilichotokea siku ya mapinduzi; mmeaminishwa soga mkaziamini. Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwa kuhusu Uhuru, Zanzibar ilikuwa tayari huru by the time mapinduzi yanafanyika.
 
Sudani ya kusini wameweza , tunataka kuwasikia na wanzanibar nao as soon as possible.hivi kwa nini zanzibar ni maskini? why?kile ni kisiwa theres a lot of tourists attraction and so many things to with fishing . Think twice..ukoloni na mambo ya ndio mzee yalishaisha na kupitwa na wakati

Kule serikali na watumishi wana chakachukua mno mapesa ya wananchi .Umesikia kwenye mkutano wa kafu wa juzi ? Pesa zimeliwa kishenzi nako kuna waka moto .
 
na wala haitakuwa kazi kubwa, ni kuchukua hatua ya kuachia madaraka yote yanayohusu muungano then warudi kwao.
Fine, lakini mkumbuke kwamba ni lazima iwe declared before international acts kwamba sasa imekuwa ni nchi halali. Ndiyo maana tunasema tunataka uhuru wetu. Mkubali kwamba mnatuacha tuishi na kujijenga kama nchi, mdeclare mbele ya sheria zote za kimataifa zitakazoitambua zanzibar kama nchi, na si kirahisi rahisi hivyo kusema eti tuachie madaraka tuende zetu! Halafu tukifanya hivyo? Nani atakayetutambua kwamba ni nchi?

Mchakato uanze sasa, mturuhusu wananchi wa zanzibar tupige kura ya bila kampeni kama tunataka muungano or not? Hii kura ndiyo kitakuwa kigezo mhimu cha kuitangaza zanzibar kama nchi huru. Hivi sasa watanganyika mmejitahidi sana kuzuia mijadala yote inayohusu muungano kwa kuhofia kwamba zanzibar itajitenga. Lakini someni alama za nyakati. Tayari watanganyika wanachomewa maduka zanzibar na tayari makanisa, mabaa na mabucha ya nguruwe yanasambaratishwa kule. Ni dalili tosha kwamba hatuwahitaji wageni tena. Tunataka nchi yetu huru.
 
mie nashangaa mpaka leo hamjafanya tu MAPINDUZI ya kumrudisha sultan! daini nchi yenuuu mtazidi kuonewa mpaka lini? km sisi wa bara hatunufaiki na huu muungano na nyie hamuutaki ni nani sasa anaetaka kubebeshwa zigo la misumari? si kmeona sudan ya kusini? changamkeni mapeeema
 
Kama kuna mtu kaisikiliza hotuba ya KAFU hadi mwisho ambayo link iliwekwa hapa mtandaoni basi atakuwa amesikia onyo alilopewa Pinda .Wamesema asiwatishe na asijidanganye yeye na wenzake .Wamesema kauli zake zinaudhi na hawako tayari kuvumilia .Wamesema mjadala ya Muungano uwepo na marekebisho waliyo mpa Sitta .Wakasema kama hawatafuata ushauri wao wako tayari kuvua koti maana linawabana sasa wanataka koti size yao .Pinda kaambiwa hajui siasa an historia ya Nchi ya Zanzibar .CCM kimya , JK kimya , Wabunge wa CCM kimya , haya inakuwaje hapo ?
 
sidhani kama unajua kilichotokea siku ya mapinduzi; mmeaminishwa soga mkaziamini. Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwa kuhusu Uhuru, Zanzibar ilikuwa tayari huru by the time mapinduzi yanafanyika.
Tunajua fika ukweli huo kwamba uhuru wa zanzibar ulipatikana mwaka 1963, hilo halina ubishi, lakini waarabu ndo waliokuwa wamekabidhiwa huo uhuru, na mapinduzi ya 1964, yalilenga kumpa utawala mzanzibari mzalendo. Bila shaka mwanakijiji una kumbukumbu nzuri ni mara ngapi ASP ilinyang'anywa ushindi wake na waarabu kiasi cha kuamua kuopt mapinduzi kama njia mbadala ya kurudisha utawala kwa wazalendo. Lakini hayo hayakufanyika ili kutoa mwanya kwa Tanganyika kututawala, bali wazanzibari wazalendo kujitawala wenyewe.
 
Zanzibar's issue go way beyond Muungano. Zanzibar seceding from the union will not change their economic situation contrary to what they want to believe. Wajitenge kwa sababu zingine ila si uchumi.
 
Siku Zanzibar ikijiondoa tukabaki na Tanganyika yetu nitalia sana, machozi ya furaha kwani hatimae nitakuwa najihisi ninabelong kwenye nchi fulani. Siyo sasa, huu ni upuuzi mtupu, kwanini wapendelewe wao kwa kila kitu?

Huku bara, Mbezi Beach ndani ya wiki tunakosa umeme masaa zaidi ya 12 kwa siku 6, majuzi nimeenda Zanzibar hata hawajui kama kuna mgao. To hell with them, where is G55? Please lets do something, liberate Tanganyika from Kupe,
 
Back
Top Bottom