Ibambasi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2007
- 9,277
- 4,683
Wakuu wachangia mada,
MKJJ,FMES,KM,na wengine wote,
Mi nadhani kwamba mjadala kuhusu Nyerere na destiny ya Tanzania ni sawa na ule wa mwanzo wa ulimwengu (dunia) kati ya divinity and science,yaani nani wako sahihi divinti or science.Vivyo hivyo kwa Nyerere kuna makundi mawili mabayo yako opposed to each other,sasa inategemea kila mtu anaargue kutoka angle ipi.Kwa wale wanaopenda utafutaji na utumiaji (kwa maana ya a material life) Nyerere sio mfano wa kuigwa na ni karibu na shetani kabisa,hawa ndo watapinga siku zote mazuri yale aliyoyafanya au aliyojaribu kuyafanya (mf. kutoa elimu bure,matibabu,ujamaa,kutenganisha siasa/uongozi na biashara,njia za uchumi kuwa chini ya serikali,etc)kundi hili litajaribu siku zote kuhighlite failure za Nyerere katika mambo haya (ingawa katika ulimwengu halisi kila attempt lazima iwe na upande wa pili,yaani kufail),watataka kudiscredit yote aliyoyafanya Nyerere.Pia watu hawa wanajifanya kwa makusudi kuignore kabisa falsafa binafsi ya Nyerere ambayo ni kutopenda maisha ya juu na/au kufaidika kupitia mali ya umma.Kundi la pili ni lile ambalo linamuunga mkono Nyerere,watu hawa ni wale wanaopenda maisha kwa maana ya usawa (kwa maana yoyote ile) kwa binadamu wote,watu ambao huumia wanapoona mwenzao mmoja kashndwa kulipia dawa hospitali,watu ambao siku zote utawakuta hawana raha na maisha wanapoona injustice inayoendelea hapa duniani.Hawa siku zote watapingana na wale wanaojilimbikizia (sina neno zuri zaidi) mali kwa kisingizio cha utafutaji (rejea Mkapa na mtaji wa masikini au Sumaye:Ukitaka mfanyabiashara mambo yako yakinyookee),kundi hili siku zote litaonesha ubaya wa watu binafsi kumiliki njia kuu za uchumi (hata kama kuna faida kwa jamii nzima).Huku ndiko utakuta watu kama kina Shivji na wenzake wengi.
Hivyo basi mjadala huu kuhusu legacy ya Nyerere hautakwisha kamwe kwa sababu unareflect hali halisi ua ukinzani wa falsafa mbili kuu katika maisha ya mwandamu ambao kina Karl Marx na wenzake walikiwsha kuyaona na kuyajadili almost two centuries ago.Matabaka katika jamii ndo mjadala husika,Nyerere is just being used as a battle ground katika swala hili.
Kwangu mimi ndo naona mjadala huu umesimama hapa.Ni jukumu la kila mwanabodi kujiangalia yeye yuko upande gani ndo ataweza kuchangia mjadala huu kwa ukweli wake.
Mimi niko upande wa Nyerere kwa maana ya usawa wa maisha kwa binadamu wote (ambayo kimsingi ndiyo mafundisho ya karibu dini zote hapa chini ya jua).
Naomba kuwasilisha mada.