Fedha ya kugharamia elimu bure ilipitishwa na Bunge gani na ni kutoka fungu gani la Bajeti?

Mkuu wakati wa kampeni umeisha wewe kila wakati unakuja na uzi wa kupingana na kasi ya Dr.Magufuli.

Umeishajiuliza kiongozi wako Lowassa alivyokuwa anatoa ahadi kuwa akichukuwa dola elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Vipi ulihoji pesa zitatoka wapi au Lowassa akisema marufuku kuhoji.

umegonga kwenyewe
 
Kabla hatujaendelea na huo mjadala wake kuhusu Dkt Magufuli...hemu atueleze yeye, Je Lowassa angeshinda urais hiyo pesa ya elimu bure hadi chuo kikuu ingetoka wapi!?

Fungua Uzi mwingine,hapa tujadili hoja husika!Huyo unayetaka tumjadili sio Rais wa Tanzania!Je,kikatiba ni sahih kutumia fedha serikali iliyokusanya kupeleka kwenye wizara ya elimu bila bunge kuidhinisha?
 
Mkuu huyu ni mfuasi wa ccm ila amechanga na kasi ya magufuli.

Mkuu wakati wa kampeni umeisha wewe kila wakati unakuja na uzi wa kupingana na kasi ya Dr.Magufuli.

Umeishajiuliza kiongozi wako Lowassa alivyokuwa anatoa ahadi kuwa akichukuwa dola elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Vipi ulihoji pesa zitatoka wapi au Lowassa akisema marufuku kuhoji.

Hata kama ni mfuasi wa ccm, mda mwingine ni lazima kujipa changamoto kama hizi. Kama Huyu kafikiria hv ujue wapo wengine wengi wanao fikiria hvyo pia
 
Watanzania watu wa ajabu sana..hoja nzito mnazijibu juu juu tu na ushabiki kwa sana...mambo yakienda kombo nyie nyie mtarudi kuponda...tunahitaji sustainability kwenye hili jambo je mnadhani msingi wa elimu bure ushajengwa kwa hela za bandari tu... je kwenye afya..barabara..reli na mengine kibao!??tufikirie kwa upana zaidi na sio ushabiki.
 
Unafiki ni kitu kibaya sana, hizi ngonjera za kutoa elimu bure zilinadiwa na asilimia kubwa ya wagombea kwenye kampeni, tulijipa upofu na kushabikia na wapo waliahidi mpaka chuo itakuwa bure, ni nani alihoji nafasi ya bunge ktk ahadi zile? Tulijivisha unafiki kwa maslahi ya vyama vyetu huko tukijua kuna bunge. Ukiona watu wanajibu kirahisi hivi ujue mada yenyewe ni ya kinafiki na mtoa mada alitakiwa kwanza akiri kuwa yeye alikuwa bendera fata upepo kipindi kile cha hizi ahadi
 
Jibu swali acha kuruka ruka kama nguchiro Lowassa, alivyokuwa anatoa ahadi zake kwenye kampeni kuwa tukimchagua elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu pesa angetoa wapi???

Uliambiwa Lowasa ataanzia January ?? hata hivyo Magufuli anachofanya saa hizi n sahihi kabisa , nchi hii tulifikia uhitaji wa utawala wa aina hii ...Show that things can be done
 
Pamoja na dhamira hii njema ya Raisi Magufuli na chama chake, lakini bado swali hili linanijia kila kukicha na kama kuna mwenye jibu/ufafanuzi naomba anisaidie hapa.

Bunge lijalo litaanza tarehe 27 mwezi January na bila shaka shule za serikali zitakuwa teyari zimefunguliwa kabla ya tarehe hio.Sasa hapa itakuwaje?Je,itabidi mwakani shule zifunguliwe mwezi February?Au itabidi serikali iwakope wazabuni?Je, ni sahihi kwa serikali kuwakopa wazubuni huku ikitegemea kuwalipa kwa hela ambayo Bunge halijaipitisha?Je,tutarajie Bunge la dharura kwa ajili ya swala hili tu?

Je,si busara kwa hawa wenzetu kukiri kuwa walisukumwa tu na pressure na mihemko ya uchaguzi kiasi cha kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake hauwezi kuanza sasa na kisha kuwaomba radhi wananchi?

Jamani si mliapa kuilinda katiba ya nchi?

Maswali ni mengi kuliko majibu!

Kweli cha kuazima hakisitiri maungo.

Hatimae nimejikuta nakumbuka ule uzi wa Pasco uliongelea swala la "Presidential decree".

unajuaa watanzaniaa hamna jema, hatabungee likipitisha hiyo bajeti huwa inatekelezwaa?? bajeti yenyewe ipo kifisaadi sana, mwacheni magufuli afanye inavowezekana kuleta heshima ya mtanzaniaa.
 
Last edited by a moderator:
Rejea jopo ambalo JPM aliunda kumshauli moja ya terms of reference ni namna gani shule bure itaanza bila kaudhili budget.
Ndo maana mkuu akaanza na austerity measures ndani ya mwezi kpata 997 billions baada ya hayo maelezo una swali
 
Pamoja na dhamira hii njema ya Raisi Magufuli na chama chake, lakini bado swali hili linanijia kila kukicha na kama kuna mwenye jibu/ufafanuzi naomba anisaidie hapa.

Bunge lijalo litaanza tarehe 27 mwezi January na bila shaka shule za serikali zitakuwa teyari zimefunguliwa kabla ya tarehe hio.Sasa hapa itakuwaje?Je,itabidi mwakani shule zifunguliwe mwezi February?Au itabidi serikali iwakope wazabuni?Je, ni sahihi kwa serikali kuwakopa wazubuni huku ikitegemea kuwalipa kwa hela ambayo Bunge halijaipitisha?Je,tutarajie Bunge la dharura kwa ajili ya swala hili tu?

Je,si busara kwa hawa wenzetu kukiri kuwa walisukumwa tu na pressure na mihemko ya uchaguzi kiasi cha kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake hauwezi kuanza sasa na kisha kuwaomba radhi wananchi?

Jamani si mliapa kuilinda katiba ya nchi?

Maswali ni mengi kuliko majibu!

Kweli cha kuazima hakisitiri maungo.

Hatimae nimejikuta nakumbuka ule uzi wa Pasco uliongelea swala la "Presidential decree".

Mkuu hiyo ndio tanzania yetu maneno ni mengi kuliko vitendo
 
Last edited by a moderator:
Jibu swali acha kuruka ruka kama nguchiro Lowassa, alivyokuwa anatoa ahadi zake kwenye kampeni kuwa tukimchagua elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu pesa angetoa wapi???

Hivi bado upo?
 
Hiyo ni pesa ya serikali,inatakiwa iidhinishwe na bunge kuwa itaenda kwenye elimu

Mkuu ngoja kwanza zile za posho ya wabunge zikatwe kwanza ndo tupange vizuri zipi ziende wapi, sasa hivi lengo ni kupata fedha kwanza kumwezesha Magufuli kutimiza aliyowahidi watanzania
 
Mkuu hongera kwa kumjibu SALARY SLIP.Wengi wameleta siasa zisizo na maana.Unaweza kuwa na jibu la kipumbavu lakini usiwe na swali la kipumbavu.
Siasa za kivyama hazitusaidii wakati huu.Swali kama huna jibu nalo bora ukae kimya kuliko kum-degrade mtu kwa ajili ya tofauti za kimitazamo ya kisiasa.

Tatizo wengi humu wanajibu kwa mihemuko ya kisiasa mkuu
 
Pamoja na dhamira hii njema ya Raisi Magufuli na chama chake, lakini bado swali hili linanijia kila kukicha na kama kuna mwenye jibu/ufafanuzi naomba anisaidie hapa.

Bunge lijalo litaanza tarehe 27 mwezi January na bila shaka shule za serikali zitakuwa teyari zimefunguliwa kabla ya tarehe hio.Sasa hapa itakuwaje?Je,itabidi mwakani shule zifunguliwe mwezi February?Au itabidi serikali iwakope wazabuni?Je, ni sahihi kwa serikali kuwakopa wazubuni huku ikitegemea kuwalipa kwa hela ambayo Bunge halijaipitisha?Je,tutarajie Bunge la dharura kwa ajili ya swala hili tu?

Je,si busara kwa hawa wenzetu kukiri kuwa walisukumwa tu na pressure na mihemko ya uchaguzi kiasi cha kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake hauwezi kuanza sasa na kisha kuwaomba radhi wananchi?

Jamani si mliapa kuilinda katiba ya nchi?

Maswali ni mengi kuliko majibu!

Kweli cha kuazima hakisitiri maungo.

Hatimae nimejikuta nakumbuka ule uzi wa Pasco uliongelea swala la "Presidential decree".

Huo ni ujuha. Mtu mzima unajitoa ufahamu? hakuna jema kwako kila wakati kupinga anachofanya Magufuli.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wakati wa kampeni umeisha wewe kila wakati unakuja na uzi wa kupingana na kasi ya Dr.Magufuli.

Umeishajiuliza kiongozi wako Lowassa alivyokuwa anatoa ahadi kuwa akichukuwa dola elimu itakuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Vipi ulihoji pesa zitatoka wapi au Lowassa akisema marufuku kuhoji.

Hahaaaaa, aliambiwa itatoka vitalu vya gesi, sijui bunge gani lilikaa na ama kupitisha
 
Kama tunavojua kuwa hostel si program ya wizara au shule kwa wanafunzi wa kutwa.je,wazaz wataendelea kuwahudumia au srkl
 
Hili nalo ni moja ya vitu vinavyoumiza kichwa kwani Hostel hizi ni huduma itolewayo shuleni na lazima watoto wanaoishi hapo wale na lazima kuwe na mpishi wa kumlipa na lazima kuwe na muuguzi aka matroni wa kumlipa
 
Back
Top Bottom