Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Ameondoka wakati tunamuhitaji sana. Hakika tutakukosa sana muheshimiwa. Pole tena kwa wanafamilia na wanaharakati wa haki za watz.
 
Msichana aliyeonyesha ujasiri na uthubutu katika siasa..... kugombea ubunge kwa mara ya kwanza katika jimbo. Alionyesha mfano wa kuigwa na vijana na hasa dada zetu.
 
So young to go now! But we can't change anything! I believe as time evolves she could reach her potential as a prominent politician and for that I have a reason to cry. Indeed she was just setting her feet on ground, ready to start long political journey of this country.
 
bado natafakari la kusema juu yake......aaaaaaagh! basi tena, vizuri havikawii kutoweka duniani, watu wazuri kwa jamii wanaondoka inabaki mijaza dunia.
 
Inasikitisha sana.

Bado najiuliza, hii juhudi yangu yote, tamaa isiyokwisha ya kutaka mafanikio zaidi na zaidi, mipango ya kesho, miaka 5/10/15 nk ijayo kumbe yaweza kuwa bure kabisa tena kwa dakika moja tu.

Fundisho: Wakuu tukumbuke kuna kufa siku moja, tusiishi kwa kujisahau sana as if ndiyo tumefika hapa duniani.

Pumzika kwa amani dada
 
Mwenyezi Mungu Ipokee Roho ya Marehemu Regia Mtema. Apumzike kwa Amani.
Regia tutakukumbuka sana na kampeni zako za K4C.
Poleni sana watanzania, Poleni sana wana Kilombero na wapenda maendeleo wote. Naamini Mwenyezi Mungu atamwinua mtu mwingine atakayesimamia K4C ili kuikomboa wilaya yenye rasilimali nyingi lakini maskini.
 
Basi tena ishatokea na hatuna jinsi,Mungu amlaze Regia mahala pepa peponi

Amen!daima tutakukumbuka.
 
Binafsi sikupata nafasi ya kuonana naye ana kwa ana ila niliweza kuongea na Regia mara nyingi sana kwenye simu. Tuliaongea mengi wakati wa kampeni za uchaguzi ili kumpa sapoti.

Nilihamisika sana kuona kijana mdogo kama yeye (achilia mbali jinsia na ulemavu wake), aliamua kugombea ubunge wa jimbo tofauti na wanawake wengi wanaokimbilia kwenye viti maalumu ili kukwepa changamoto na mikiki mikiki ya kupitia majimboni. Hili kwangu lilikuwa jambo zito sana na lilinifanya nimwone Regia kama mtu ambaye amezaliwa na kipaji muhimu sana cha kutoogopa changamoto. Hili ni funzo kubwa kwetu.

Na funzo jingine ni la kujitoa hata pale ambapo watu wengine wanaona ni pagumu na hatari sana. Kwa mazoea ya Watanzania wengi hasa vijana, siyo jambo la kawaida kugombe ubunge kupitia upinzani. Nina marafiki zangu wengi sana ambao tumepishana mno kuhusu jambo hili. Katika hili, Regia hakuogopa lolote na hata alipokuwa mbunge wa viti maalumu, ameonesha ushupavu wa hali ya juu sana. Ni changamoto kwetu tuliobaki, kupima na kutafakali michango yetu katika jamii. Pia tutumie uwezo wetu na fursa tulizozipata kutoa michango yetu katika kuwakomboa wenzetu wa hali ya chini ambao wanatuhitaji sana!

Kitendo cha Regia kuutafuta uwakilishi ili awe mtetezi wa wananchi wenzake wa Kilombero, litutie nguvu na kutuandoa woga ili tutamani nasi kutoa mchongo wetu hata kama ni mdogo. Hili litasaia sana katika kuleta ukombozi wa Watanzania wenzetu ambao hawakupata fursa kama tulizobahatika kuzipata.

Mungu ailaze roho ya marehemu Regia Mtema mahali pema peponi, Amina.
 
Misingi ya mambo aliyoanzisha yaitaishi milele! Yalikuwa na ubinadamu na thamani isiyopitwa na MUDA!!

R I P Regia!!!
 
Ni masikitiko makubwa kwa watanzania,ingawa kufa ni lazima lakini ni ngumu kukubali kwa binti mdogo kama huyu hata hivyo itoshe tu kuwa mapenzi ya Mungu yametimia.Upumzike kwa amani-Amen!
 
Mkuu wangu sana Mwanakijiji,yaani ni kama ndoto......

Regia ameondoka mapema mnoo wakati Taifa likimhitaji....Kwa kweli alikuwa ni binti jasiri,mwenye uthubutu wa kufanya jambo na alikuwa tayari kujishusha na kujifunza kila uchao......Hakika hili ni pigo kwa Tanzania, CHADEMA na vijana wapenda maendeleo na mabadiliko nchini Tanzania...

Kwangu mimi Regia alikuwa ni zaidi ya Mbunge/Mwanasiasa ndani ya JF.......Alikuwa ni mtu maalum hasa......Hakika nimeumizwa sana na taarifa hizi na hata nilipopigiwa simu kuelezwa kwamba mpendwa wangu Regia amefariki sikuamini,nilikataa katakata.....Ameondoka mapema sana Regia wetu....

Regia pamoja na kupata ubunge hakuitenga/kuiacha JF......Daima alikuwa nasi katika shida na raha na alijitahidi kuutumia muda mchache anaoupata kuja humu kutujuza mambo mbalimbali yanayojiri bungeni na katika medani za siasa kwa ujumla......She was born for JF na JF tutamlilia daima....


Yeye ni tofauti sana na wanasiasa wengine ambao waliitumia JF kama daraja la mafanikio yao kisiasa na mara baada ya kufanikiwa kisiasa wanaacha kabisa kuingia JF,Regiia/GS hakuwa hivyo........Yeye daima tulikuwa nae JF,hakuchagua jukwaa....Jukwaa la siasa utamkuta,MMU kama kawa, kule kwetu kwenye Michezo na Burudani kulikuwa kwake pia.....Chit Chat ndo usiseme, yaani alikuwa anaingia kila jukwaa tofauti na wanasiasa wengine ambao wao kila siku ni SIASA tuuuu.....

Kwangu mimi Regia alikuwa zaidi ya ndugu,sikujuana na Regia tangu utotoni wala sehemu yoyote nyingine, nimekutana nae JF na tangu tumefahamiana nae tumekuwa zaidi ya ndugu.......Kwa hakika hili ni pigo,sisi tumempenda lakini Mungu amempenda zaidi....

Kwa hakika nilikosa la kusema mara baada ya kupata taarifa kwamba mpendwa wetu/kamanda wetu na mpiganaji wetu Gender Sensitive amefariki........
Upumzike kwa amani rafiki yangu,dada yangu na kiongozi wetu mpendwa...

Umeondoka katika kipindi ambacho Tanzania inakuhitaji hasa....

Kwa heri rafiki.......Umetangulia nasi tuko njiani...

Pole kwa familia, Pole kwa CHADEMA, Pole kwa vijana wote wa Tanzania, Pole kwa wana Kilombero, Pole kwa watanzania kwa jumla...

Hakika hili ni PIGO kwa watanzania........Bala na JF Tutakukumbuka daima dada yetu Gender Sensitive/Regia Mtema

Raha ya milele umpe mpendwa wetu Regia ee bwana, na Mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani......Amina.

 
Last edited by a moderator:
Regia ni mbunge wa Tanzania wala si wa chadema,

Bado na umri mdogo kuweza kutoa mchango,

Alikuwa kioo kwa wale wenye ulemavu na inspiration kwao,

Kwangu mimi alikuwa mpinzani asiyogopa kupingwa japo kwa maudhi,

Alifahamu sote ni watanzania hata kama tunapingana,

Hakukata tamaa hata kama akipondwa, mwepesi kukubali anapoona amekosa..

Umri wake, mafanikio yake, ushiriki wake katika mambo ya jamii utakuwa simanzi kwangu siku zote

R.I.P
 
Poleni sana & mno wana JF, ndugu wapiganaji, makamanda, CHADEMA na watanzanzania wote.
Nimefarijika sana na namna utawala wa JF na wadau tunavyoshiriki kwa staha katikati ya huzuni ya msiba huu mkubwa. MMM hongera kwa utenzi. Kazi tulonayo ni kuendeleza mapambano dhidi ya aina zote za udhalimu, kusimamia haki, kujitoa kwa ajili ya wengine na kuwa tayari muda wowote.

RIP Mh: Dada yetu mpendwa sana Regia!
 
bwana ametoa na bwana ametwaa.
Jina lake lihimidiwe.
Umeondoka mapema mno kamanda.pumzika kwa amani.
Tutakukumbuka daima.
 
Back
Top Bottom