Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Nimemjua Regia kupitia JF ndio nikaanza kumfuatilia nikagundua nilichelewa kujua nasaha zake na busara alizokuwa nazo.

Mungu amempenda zaidi. Tumuenzi kwa kutekeleza na kuyatenda yale aliyoyatenda kwa manufaa ya uma bila kuwa waoga kama yeye. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Regia Mtema.
 
"Hakuna namna yoyote ya maneno itakayotosha kumpamba Regia.......

Kwangu mimi Regia ni mdogo wangu, Rafiki yangu, Dada yangu na kupita yote ni kiongozi wangu. Nimezungumza mara kadhaa na Regia ni miongoni mwa Viongozi wachache wanaokubali kukosolewa pale wanapokosea, alikuwa mnyenyekevu na mwepesi kujifunza na ni mtu wa kuheshimu watu wa Matabaka yote!...

Pengo lake ni zito mno kuzibwa..... Mwenyezi Mungu amemuita mapema...... Kumuenzi Regia tufuatilie yale yote aliyoyaanzisha na tujali kila mtu kwa nafasi yake.....

Mwenyezi Mungu amlaze Mahali pema Peponi,Bado tupo nawe Regia......Tutakutana!

Amen!"
 
Ni mara chache tunapata wawakilishi wanawake wanaojielewa na kuelewa majukumu yao wakiwa wamejaa "Uzalendo" katika mioyo na vitendo vyao. Nimemfahamu Rejia E. Mtema (May she Rest In Peace) hapa JF tokana na baadhi ya threads zake na mchango wake katika Siasa... She was an impressive lady.... Post na hoja zake ndizo zilizonijengea heshima juu yake, kua kathubutu kutumia jina lake.. kathubutu kusimamia ambalo anaamini na pia kathubutu kuonesha na kutuwakilisha wanawake katika Uongozi tena akiwa ni mdada mdogo saana kulingana na kazi alokua akifanya.

Tokana na nafasi na kasi yake katika Siasa ni mengi yataongelewa, yatakua comprehended, yatazushwa.... Lakini hakuna hata moja ambalo litafanya machungu yapungue ama kuweza mrudisha hai tena. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yoote, na nawaombea wafiwa, wakaribu wa marehem, ndugu na jamaa wawe na mioyo jasiri... Sio rahisi na ndiio maaana nawaombea wawe na Imani na Amani waweze maliza shughuli nzima ya Mazishi na msiba huu mkubwa salama.

Rejia E. Mtema... May your soul Rest in Eternal peace.

Ameeen.
 
Truely we have lost a jewel, a personality that can never be replaced by anyone. I knew you in person and for the few times we met I always admired your ambition and I can say you were such a loving, caring, down, to earth kind of a person that anyone would wish to be you.

No words can explain how it feels to lose someone that you know and on top of it all, a friend.

May the Lord Almighty grant you eternal peace dada Rejia. Condolences to her twin sister Regina and all the family members.
 
Sisi ni ndugu zenu si watani,HAKUNA UTANI KATI YA NURU NA GIZA kama ilivyo mbali kati ya mashariki na magharibi
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Kila nikiandika najikuta nafuta, nakosa kauli
Maxence Melo.... I wish I had words za kukufariji lakini sina. Nakuombea kwa Maanan akuzidishie nguvu katika shughuli nzima ya Msiba na mazishi. Just brace yourself for you are still needed out there.

Poleni Saana na Msiba.
 
Rest in peace Regia. We will always remember you. You have been an inspiration to majority of people in Tanzania but i think God loved you than us. I know God has a plan on you and us and thats why he has called you to his kingdom. Its so sad but we will always live in hope....:disapointed:
 
Inasikitisha sana.

Bado najiuliza, hii juhudi yangu yote, tamaa isiyokwisha ya kutaka mafanikio zaidi na zaidi, mipango ya kesho, miaka 5/10/15 nk ijayo kumbe yaweza kuwa bure kabisa tena kwa dakika moja tu.

Fundisho: Wakuu tukumbuke kuna kufa siku moja, tusiishi kwa kujisahau sana as if ndiyo tumefika hapa duniani.

Pumzika kwa amani dada

Hapana mkuu! Inaumiza sana!

Ila tumeambiwa tuitumikie dunia kama vile tutaishi miliele pasi na kusahau kujishirikisha na akhera kama vile tutakufa kesho!

Tuyape nafasi maisha yaendelee kama kawaida. Ila ki ukweli binafsi kifo cha huyu sister leo kimeniumiza sana sana! Sijui kwa nini?
 
REGIA, you had all good leader deserves, CDM should be stable at this sorrowful period, real the party has lost the fighter. RIP Regia
 
Binafsi namshukuru sana Mungu kunipa nafasi ya kumfahamu Regia.

Hakuna siku niliyozungumza nae au kufanya nae jambo likaishia katikati, hakuwa wa kukata tamaa wala kuyumba,alikuwa akiamua na kuanza jambo analimaliza kwa ubora wake...!

Kweli ni mfano wa kuigwa na wanawake wa Tanzania,hakupenda short cut wala mambo rahisi, alifanya lile lililo ndani ya uwezo wake.
Tutakukumbuka Regia, umetuacha mapema sana...katika yote, kazi njema uliyoianza katika maisha ya watanzania, Mungu mwema ataiendeleza kupitia sisi uliotuacha na ataimaliza....!

Hauko nasi kimwili lakini kiroho u pamoja nasi. Pumzika kwa amani rafiki mzuri na kiongozi mwanamke shupavu.
 
Jaman naomba msinifikirie vibaya ila acha nsema sina lengo la kuchulia,ila itanbid nseme
NAAMIN KUNA VIONGOZI WAKIFA NI HASARA KWA TAIFA mfano REGIA,Pia naamin kuna viongozi wakifa ni FAIDA KWA TAIFA mfano........,dada Regia pumzika kwa amani.
 
Sijui niandike nini
Maana machungu ni makubwa mno
Kuondokewa na mpendwa wetu
Mpambanaji ambaye hakuchoka kupambana
Uendako Mungu akuweke mahali pema
Upumzike kwa amani
Tuliobaki tutakukumbuka kwa mengi ambayo ulituonyesha njia
Tutakukumbuka kwa moyo wako wa kutokuchoka kupambana na kuamini katika kile ambacho unakipigania
Tutakukumbuka kwa kutokuchoka kupigania haki
Moyo uliouonyesha uwe ndio mfano wetu
Kuenzi mapambano na kupambana katika kuyafanya maisha ya kila mmoja wetu kuwa maisha bora
Ulale mahali pema peponi mpambanaji wetu ambaye hukuchoka kupambana na kupigania haki
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yako mahali pema peponi
Upumzike kwa amani na mwanga wa milele ukumulikie mpendwa wetu
 
Wakuu wangu Mwanakijiji,Pasco na wakuu wengine.................kwa kweli post zenu zimenitia uchungu lakini ukizisoma tena na tena zinafariji sana.Mwenyezi Mungu awabariki sana.
 
kwa sasa ni ngumu sana kuamini na kukubali kilichotokea........
mimi binafsi bado nipo kwenye usingizi mzito wenye njozi ya majonzi....
hadi hapo nitakapoamka ndipo nitaamini.....

Amini tu Preta!Ndo imeshatokea hivyo mpendwa!Hakuna jinsi.
 
Back
Top Bottom