Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Wanabodi,

Kwanza tupeane pole kwa msiba huu mkubwa wa member mwenzetu Regia Mtema!.

Najua jinsi wengi tulivyoguswa na msiba huu wa ghafla, hivyo huu pia ni wakati wa kufarijiana.

Nilimfahamu Regia Mtema wakati wa harakati za uchaguzi mkuu wa 2010 kupitia posti fulani ya Mzee Mwanakijiji. Nilikuja kukutana naye rasmi Bungeni Dodoma na nilipomuona, ndipo nikamtambua ni mtu wa aina gani!. Kusema ukweli ni miongoni mwa wanawake wachache majasiri ambayo wanajiamini kusimama na kile walichoamini.

Nakiri kukwaruzana naye humu jukwaani haswa kwenye post zangu zinazo criticise Chadema, ila tukikutana, tulizimaliza tofauti zetu.

Ni mwezi Desemba 2011 ndipo aliponikumbusha kumuona, kumbe Regia Mtema ni kile kibinti kidogo tulichokuwa tunakiona pale nyumbani kwa Priva Mtema, kikisoma primary, wakati sisi tukiwa chuo cha uandishi wa habari miaka ya 90!.

Sasa Regia, hatunaye!. Ila kiukweli ni hatunaye kidunia tuu!. Regia Mtema is dead and she is no more!. Lakini kiroho, Regia Mtema is still alive not only in our hearts, but she is alive indeed, spiritually!.

Binadamu ana sehemu kuu mbili, ya kwanza ni mwili (body) na roho (spirit).
Mwili ndio phisical body, huu tunaouona kwa macho, huu unaotazamika, kushikika, unaoonekana, na ndio mwili huu unaokufa na kuzikwa na kugeuka no more!.

Mwili wa pili ni mwili wa kiroho, spiritual body, astral body, ambao haufi, unaishi milele!. Hivyo kwa Regia Mtema, kilichokufa ni ile phisical body yake tuu, lakini spiritual body yake iko hai na saa hizi anashuhudia kila kinachoendelea kuanzia kwenye familia yake mpaka jf!. Kwa waumini wa Kikiristo, roho yake inakwenda kwenye pumziko la muda, ikisubiri ile siku ya ufufuo wa wafu na uzima wa milele ambapo roho za wote waliokufa, zitafufuliwa kwa hukumu ya mwisho zikiwa kwenye miili mipya na nchi mpya!.

Hivyo wapendwa, pamoja na huzuni zetu kuondokewa na mwenzetu huyu Regia Mtema, nawaombeni tujifariji kuwa Regia hatunaye kimwili tuu, lakini bado yuko nasi kiroho na sisi ambao ni waumini wa "life after life", tunaamini licha ya kutokuwepo kimwili, lakini bado atasimamia yale aliyo yaasamini!.

Kipindi hiki chote ambacho mwili wake bado haujawekwa kwenye pumziko la milele, japo the body is dead body, astral body yake is still attached to the body, anaona na kusikia kila kinachoendelea mpaka after several hours, be it 24, 48 up to 72! ndipo astral body ina get detached na kuacha physical body iki decompose huku astaral body au ikiendelea wondering as "wondering spirit", au iki seek refuge in a new body na to continue with "after life'!.

Kwa vile hiki ni kipindi cha majonzi, nawaombeni sana, msiniulize maswali yoyote kuhusu "life before life, na "life after life"!, ila baada ya shughuli za msiba kukamilika, nitakuja na thread kuhusu maisha in such a way, mtagundua death is only a transformation of life, but life goes on!.

Dada Yetu Regia, May Your Soul Rest in Eternal Peace!

Amen.

Pasco.
 
Daima milele tutakukumbuka Regia kwa mambo mengi tu kwa kweli sina hata cha kuongeza i'm just speechless..
 
...Sikuwahi kumfahamu Regia personally lakini nilikuwa navutiwa na jinsi alivyokuwa humble na Geniune (I could see it kwenye post zake) ....Post yake ya Mwisho says it all na ukiisoma (na jinsi alivyokuwa anarespond kwe neye posts zilizofuatia)

RIP Regia
 
Yaani leo imekuwa siku ngumu sana kwangu!
Nalazimika kukubali kwamba the young vibrant politician has gone indeed. Our memory will always remember you and I hope as a personal I have to demote my life more in community services as a remembrance of our beloved sister
 
ewe mpiganaji
leo umekuwa maji
ghafla umekata chaji
ulistahili taji

watanzania wanachadema
Tumekupoteza Mtema
ulituorodheshea mema
Mola akulaze pema

wengi tumepigwa butwaa
Ulipozima kama taa
Mara chini tukakaa
Tukaanza kushangaa

Jukwaa litakukosa
Mawazo yatatutesa
Haya yote tisa
Kumi taifa umelitikisa
 
Hivyo wapendwa, pamoja na huzuni zetu kuondokewa na mwenzetu huyu Regia Mtema, nawaombeni tujifariji kuwa Regia hatunaye kimwili tuu, lakini bado yuko nasi kiroho na sisi ambao ni waumini wa "life after life", tunaamini licha ya kutokuwepo kimwili, lakini bado atasimamia yale aliyo yaasamini!.

kwa sasa ni ngumu sana kuamini na kukubali kilichotokea........
mimi binafsi bado nipo kwenye usingizi mzito wenye njozi ya majonzi....
hadi hapo nitakapoamka ndipo nitaamini.....
 
Sikuwahi kumuona marehemu live, lakini alikuwa anani-insipire sana. Pamoja na hali yake marehemu hakubweteka bali alijichanganya na kila watu na kila tukio.

Pichani ni marehemu (wa pili kutoka kulia) na mh Sugu wakishiriki show ya ant virus ustawi wa jamii...

375494_10151160980885716_705885715_22747561_1264128946_n.jpg
 
What a shoking report. Regia namfahamu vema, mpiganaji wa kweli. Tutakukumbuka daima
 
Nitakulilia siku zote Regia! Ulikuwa mwepesi wa kuja JF haraka pale wadau wanapoomba kiongozi yeyote wa CHADEMA aje kufafanua jambo. Aaaaaaaah! Huzuni sana huzuni kubwa umetuachia. Tunalia na hatuna la kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu tu.

Binafsi naahidi kutimiza wajibu wangu ili kuleta mabadiliko ili kuifikia Tanzania tunayoitaka! Aaaaaaa pumzika Regia.
 
Sikupata bahati ya kukutana na Regia lakini kupitia huu mtandao nilijiona kama namfahamu kabisa. Regia was trully one of us humu JF, na najisikia kama nimepoteza ndugu wa karibu. Kama kuna matukio yanayomfanya mwanadamu atake mazungumzo ya ana kwa ana na mungu basi ni msiba kama huu wa Regia. Na ombi kubwa kwa mungu lingekuwa kutuachia Regia. Kifo chake kimenihuzunisha beyond words. I am so sad.
 
Hivyo wapendwa, pamoja na huzuni zetu kuondokewa na mwenzetu huyu Regia Mtema, nawaombeni tujifariji kuwa Regia hatunaye kimwili tuu, lakini bado yuko nasi kiroho na sisi ambao ni waumini wa "life after life", tunaamini licha ya kutokuwepo kimwili, lakini bado atasimamia yale aliyo yaasamini!.

Kipindi hiki chote ambacho mwili wake bado haujawekwa kwenye pumziko la milele, japo the body is dead body, astral body yake is still attached to the body, anaona na kusikia kila kinachoendelea mpaka after several hours, be it 24, 48 up to 72! ndipo astral body ina get detached na kuacha physical body iki decompose huku astaral body au ikiendelea wondering as "wondering spirit", au iki seek refuge in a new body na to continue with "after life'!.

Kwa vile hiki ni kipindi cha majonzi, nawaombeni sana, msiniulize maswali yoyote kuhusu "life before life, na "life after life"!, ila baada ya shughuli za msiba kukamilika, nitakuja na thread kuhusu maisha in such a way, mtagundua death is only a transformation of life, but life goes on!.

Dada Yetu Regia, May Your Soul Rest in Eternal Peace!

Amen.

Pasco.

Ah! Asante Pasco kwa ufariji ila ni ngumu sana kukubali.
 
Mauti yamemfika, uhai umemponyoka.
Huzuni imetawala Regia kututoka. .
Mioyo imesinyaa kwa mapema ye kuondoka. . .
Amani iwe nae, apumzike salama.

Pengo aliloacha, hakika ni la kipekee. .
Kwa wote alowaacha pole zangu mpokee. . .
Tutazidi kumuenzi, kumbukumbu zake zisipotee. .
Amani iwe nae, apumzike salama.
 
Japo ni vigumu kumwuliza Mungu, lkn kwa hili nina haki ya kumwuliza Mungu kwanini amemchukua Regia wakati bado ni Tumaini la wengi? Nakuuliza Mungu kuwa ni nani sasa atakayekwea badala yake kupigana na adui zetu? Kazi yako Mungu haina Makosa, natumaini utatupatia atakayeziba pengo lake. Amen!
 
Nasikitika kumkosa. Sitasahau siku alipokua akitoa Live updates katika show ya Vinega kupitia JamiiForums
 
Back
Top Bottom