Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Gone too SOON!
We love you and....
We'll miss you dearly!

Roho wa faraja awape faraja yake, Familia yake kwanza na sisi pia! AMEN!!!
 
Japo ni vigumu kumwuliza Mungu, lkn kwa hili nina haki ya kumwuliza Mungu kwanini amemchukua Regia wakati bado ni Tumaini la wengi? ... Amen!

Nyota iliyozimika ghafla.
ni mlemavu ambae alisimama imara ktk mstari wa mbele wa mapambano,...

Kwaheri kamanda umetutangulia nasi tuko nyuma tunakuja, sina namna ya kuelezea msiba huu...Mungu awape moyo wa subira

the good die young..!!!

Wakati mwingine najiuliza "Why Regia?". Kwa nini Mungu kakuchagua Regia? Mbnona ndo kwanza ulianza kukusanya kero zetu kupitia humu mtandaoni [...] Why now?.


"Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake libarikiwe"
Ameen.

Jamani jamani,why had she to go when we need her so much, ...machozi

Kazi ya Mungu haina makosa.Regia sijui niseme nini [...] Niseme nini basi! Maneno yameniishia na machozi yananilengalenga. Oh Mungu wangu.Pumzika kwa amani Regia.Tutakutana Paradiso siku hiyo!


Nyota Imezimika

Ni kweli Nyota ya Regia imezimika Duniani, inasikitisha na inauma sana!

Hatutaitenda haki Tanzania kama hatutaweka ukweli na kujifunza kutokana na makosa hili tusiendele kupoteza na kuzima taa ambazo tunazitegemea kama hii ya Regia kwa kuendeleza tabia na mila yetu ya kusifu na kukwepa ukweli kwa kuwa kwetu sisi Watanzania kukwepa ukweli na kuishi kama bendera fuata upepo ndio uungwana!

Wakati kifo cha Regia kinauma na kunisikitisha hakika roho yangu inanituma kuuliza kwanini alikuwa anajiendesha mwenyewe katika Barabara za Tanzania, tena Long Safari na tena barabara ya Dar - Moro?! Huku kodi yetu ikikatwa kwa ajili ya madereva wa Wabunge wetu wapendwa, ukiachilia mbali maumbile ya Regia na kazi ya Ubunge inavyohitaji kufikiri na kuwaza kila wakati kama siyo kila dakika!

Najuwa kwa mila na uwezo wetu wengi mtashangaa haya maswali yangu, ila "smart people learn from others mistakes" kama hatutaki kuendelea kuwapoteza wapendwa wetu lazima tuwaambie ukweli na kuwaepusha na mazingira hatarishi. Wabunge waache kujiendesha wenyewe, hasa katika safari ndefu, na pale afya zao zisipowahurusu pia waheshimu hilo.

Regia tulikupenda sana, umetutoka wakati bado tunakupenda mwenyezi Mungu akurehemu.
 
I mean, ni kwa namna gani unaweza kukielezea kifo cha role model kama Regia?

Kifo hiki kidoogo kifanane na cha Nyerere, tofauti kuu ni moja tu yaani viongozi wa CCM hawakulia kwa Nyerere ila kwa Regia wamelia chozi ....anayebisha hilo namwomba alete picha ya kiongozi yeyote wa CCM aliyelia wakati wa mazishi ya Nyerere
 
Ni masikitiko makubwa kupoteza kiongozi kijana,na hii imedhihirisha wazi kuwa Kijana akipewa nafasi anaweza kuongoza.Ningependa kuwashauri viongozi wa Chadema,Wanachama na wapenzi wa Chadema ili kumuenzi dada huyu aliyeonyesha ujasiri wa hali ya juu pamoja na ulemavu aliokuwa nao basi wangeanzisha mfuko wa Regia (Regia Foundation) ambayo itawagroom vijana wenye uwezo wa uongozi bila kujali itikadi na kuweka Tanzania mpya itakayokuwa na viongozi watakaomuogopa Mungu na wenye mapenzi na Nchi yao.
Mungu ametoa Mungu ametwaa jina lake litukuzwe.Amina
 
mungu ni zaid ya mipango yetu, tulikupenda JEMBE, tulikupenda sana
Tunaamini umetutoka hapa duniani ila harakati utaziendeleza huko ulikoenda,
REST IN PEACE
 
Nami kama mgeni niliyejiunga na jukwaa hili natoa pole yangu ya dhati kwa wanajukwaa ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu. Regia Mtema, kutoka uvunguni mwa moyo wangu nakiri kuwa posts za Marehemu. Regia ni mojawapo wa vitu vilivyonisababisha kujiunga na jukwaa hili, rest in peace our fallen heroine.
 
Kama watu wakifa hua wanaona waliobaki huku wanareact vipi kwa kuondoka kwao basi atakua anatabasamu sasa hivi huku machozi yakimtoka.

RIP RM.

Binadamu yeyote,lazima aonje mauti,biblia inasema kuwa na mavumbini mtarudi,na sio binadamu tu hata kiumbe chochote,kilicho baki hapa ni kutenda matendo mazuri ya kumpendeza mwenyezi Mungu,hatujui siku wala saa ya kufa ndiyo maana bibli inasema muwe Tayari wakati wote,Binadamu ni sawa na kuku anayejiokotea chakula bila kujua lolote lakini ghafula anachinjwa pindi ajapo mgeni,sisi makao yetu hayapo hapa duniaini kuna makao ya kudumu huko Mbinguni kwa baba sisi ni wapitaji tu ndugu yangu
kwaheri Mbunge wangu Regia.
 
Naamsha vidole vyangu kuandika haya nikiwa na masikitiko makubwa na moyo mzito wenye majonzi yasiyotamkika. Majonzi ya kupotelewa na rafiki wa karibu, kiongozi mnyoofu na kipenzi cha watanzania wanyonge.

Taarifa za ajali iliyopoteza maisha ya Regia niliipata kupitia kwa afisa wa polisi ambaye sitamtaja, majira ya saa sita ikiwa ni nusu saa tuu tangu kutokea kwa ajali hiyo . Ghafla masikio yangu yakawa mazito kuendelea kusikiliza na macho yangu kupoteza nuru, kwa hakika nilipatwa na ganzi ya simanzi na moyo wangu ulizimia kwa kitambo.

Akiwa kama rafiki niliyefahamiana naye tangu chuoni SUA miaka ya 2003-2006, Regia alikuwa mtu asiye na makuu, mcheshi na mwenye moyo wa unyenyekevu. Japokuwa hakuwa akishiriki kwa kasi siasa za vyuoni bali alionekana kuwa kiongozi katika kundi lolote la watu aliloshiriki.

Kuanzia miaka ya 2008 nilianza kuliona jina la Rejia katika medani za siasa, wakati huu nikiwa mfanyakazi wa serikali mjini Ifakara ambako ndipo nilipo hata sasa. Kwa hivyo, Rejia akawa mbunge wangu akiwakilisha jimbo ninaloishi bungeni. Kwa bahati mbaya nilikuwa nje ya nchi wakati Rejia akifanya kampeni za ubunge jimbo la Kilombero 2010, na wakati huo tulikuwa tukiwasiliana kwa facebook na emails juu ya rundo la kero na changamoto za maendeleo jimboni hapa pamoja na mbio za uchaguzi, Tulipeana moyo kwamba ushindi utapatikana......Hata baada ya kuwa mbunge wa viti maalum tuliendelea kuwasiliana na mara zote aliwakilisha vema kero za wananchi wake. binafsi amenisaidia sana katika masuala fulani ya kikazi.

Mara ya mwisho kuwasiliana na Rejia ilikuwa ni tar 19 Dec. 2011, tulichat kwa muda na akaniahidi tungeweza kuonana nyakati za Chris-mass hapa Ifakara. Kwa bahati mbaya hatukuweza kuonana mpaka mauti ilipomfika mpendwa wetu. Inabaki kuwa kumbukumbu nzuri kwamba tulikuwa tunaishi na mtu wa kipekee na mwenye kila sifa za ubinadamu wema. Kwangu inakuwa kama ndoto, yote niliyoyaona na kuyasikia katika mazishi ya Rejia hujirudia mara kwa mara akilini mwangu. Hakika tulikupenda sana kwa kadri ulivyotupenda pia....lakini yupo aliyekupenda na anayekupenda zaidi hata sasa, huyo alikuleta duniani, na huyo amekuchukua mbinguni, JINA LAKE MUNGU AISHIYE NA KUMILIKI LIHIMIDIWE DAIMA. Mungu anabaki kuwa Mungu hata kama hakujibu kama tuombavyo na kutamani.

Binafsi nitakuenzi Rejia na kushiriki kuendeleza yote uliyoamini na kupigania. Mungu aipe nguvu familia ya Mtema na hasa pacha wake Remija katika wakati huu mgumu mno kwao. Poleni ndugu na marafiki wa Rejia, poleni wananchi wote wa Ifakara, poleni wanachama na wapenzi wa CHADEMA, Poleni watanzania wote.

Mungu aiweke roho ya mpendwa wetu Rejia Mtema Mahali pema peponi, Amen!
 
Ninawapa pole wote walioguswa na msiba huu wa mpendwa wetu Regia. Ingawa sikumfahamu kibinafsi, ninajua kwamba Taifa limepoteza mtu muhimu. Si Chadema tu au watu wa Morogoro tu. Mchango wake ulikuwa wa manufaa kwa taifa zima. Kwa jinsi ambavyo hakuchagua wala kubagua kwa misingi ya kiitikadi au iwayo yoyote ile, ameacha fundisho kwa kila mmoja wetu. Alisimamia alichokiamini na utu wake ukabaki pale pale. Tumuenzi kwa kufuata mazuri aliyotuachia. Buriani mpendwa Regia. Mungu ailaze pema roho yako.
 
Back
Top Bottom