Familia ya Nyerere yaikana CHADEMA

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
habari zilizoripotiwa na gazeti la habari leo ni kuwa mmoja wa wanafamilia ya Nyerere ametoa tamko la kuikana chadema na kusema kwamba chama hicho kisitumie jina na kaburi la hayati Nyerere kujipatia umaharufu wa kisiasa! pia amesisitiza kwamba wao kama familia hawaungi mkono maandamano ya chadema na hawana uhusino wowote na chadema.
TAHARIFA RASMI NI HII;

WAKATI Watanzania wakizidi kujitokeza kulaani maandamano ya kichochezi ya Chadema, familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imeelezea kushangazwa na uongo wa viongozi wa chama hicho, kwamba familia hiyo inakiunga mkono.

Mbali na kuelezea kilichotokea wakati viongozi wa chama hicho walipotembelea familia hiyo hivi karibuni, pia imekemea mbinu za kutumia kaburi la Baba wa Taifa kujipatia umaarufu.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia hiyo, tofauti na ilivyotangazwa na vyombo vya habari vinavyoshabikia maandamano hayo, familia hiyo haikuunga mkono maandamano hayo na badala yake ilisisitiza umuhimu wa kuzingatia utaratibu wa Serikali na kudumisha utulivu.

Akitoa taarifa hiyo jana, mmoja wa wanafamilia hiyo, Makongoro Nyerere, aliweka bayana kwamba familia hiyo haijaunga mkono Chadema kwa mambo inayoendelea nayo sasa, ikiwamo maandamano yaliyoendeshwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba chama hicho kimepata baraka na kuombewa dua yenye lengo la kuungwa mkono na mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria na familia yake kwa lengo la kukitabiria ushindi.

Makongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM ya Mkoa kilichoshirikisha wajumbe na wabunge wa CCM wa mkoa huo, alisema kilichofanyika Butiama ni utaratibu wa kawaida wa kupokea wageni wanaotembelea kaburi la Mwalimu.
 
Ujumbe wao "orojino" tuliusikia...Waliifagilia cdm sana sik ile, sasa wamebanwa kidogo wanabadilika na kuzikana kauli zao!....Tena yule mtoto wa mwalimu wa kiume alisema 2015 lazima cdm ikamate dola!...Waache kutubabaisha nao hawa, kama ni allowance za kujikimu watapewa tu bana!
 
habari zilizoripotiwa na gazeti la habari leo ni kuwa mmoja wa wanafamilia ya Nyerere ametoa tamko la kuikana chadema na kusema kwamba chama hicho kisitumie jina na kaburi la hayati Nyerere kujipatia umaharufu wa kisiasa! pia amesisitiza kwamba wao kama familia hawaungi mkono maandamano ya chadema na hawana uhusino wowote na chadema.

Nyerere si ni baba wa Taifa , wote CCM .CDM na wewe ni familia ya nyerere....
Huyo ni mtazamo wake, jina la nyerere kama mwasisi wa tafa hili litatumika daima kukumbuka na kuelezea mazuri kama nchi inaenda kusiko!
 
Ni nani huyo msemaji wa familia?? Hana jina??

Makongoro Charles Nyerere amabaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara....natuarally ameshinikizwa kutoa kauli hii Lakini familia ilishaikubali CHADEMA wakati wa ziara yao majuzi....too late CCM
 
Makongoro Charles Nyerere amabaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara....natuarally ameshinikizwa kutoa kauli hii Lakini familia ilishaikubali CHADEMA wakati wa ziara yao majuzi....too late CCM

Ndio maana kaitwa makongoro na sio Julius (baba wa TAIFA) ni haki yake ya kikatiba kusema chochote.
Na kama ni ccm bac hana budi kuunga mkono mambo ya ccm kwa njia yoyote.
 
Hivi siasa za CHADEMA zinaongozwa na familia za watu mashuhuri au sera za chama chao. Au uhalali wa CHADEMA unategemea familia ya Mwalimu, au umaarufu wa CHADEMA unategemea kuungwa mkono na familia. Nadhani ni hoja ambazo CHADEMA wanaziweka kwa wananchi wakazichambua ndizo zinazowafanya waungwe mkono na watu (kama wanaumgwa mkono anyway, SIJUI) . NI HATARI CHAMA KUTEGEMEA NGUVU ZA FAMILIA ZA WATU MASHUHURI BILA KUWA NA HOJA HALALI (MAANA KUNA HOJA ZISIZO HALALI HATA KAMA ZINAUNGWA MKONO NA WANANCHI) ZINAZOKUBALIKA KWA WANANCHI, sidhani kama CHADEMA wako hivyo.
 
CHADEMA ilikuwepo hata kabla ya kaburi la Baba wa Taifa hivyo kaburi si kigezo cha CDM kuendelea mbele. Ila kama wanafikiri Nyerere ni baba yao peke yao tu basi waseme hadharani kwamba Mwalimu J.K Nyerere si baba wa Taifa ni baba wa Makongoro tu basi na sisi tutamuenzi muasisi huyu kwa njia nyingine ambayo tunaona inastahili.

CDM 4EVER.
 
Mimi nilimsikia mama maria nyerere kwenye TBC jana akisema serikali itatue kero za wananchi, maneno mengine sikuweza kuyasikia habari ilikuwa inakatakata, nadhani walikuwa wanachakachua baadhi ya maneno mengine
 
WAKATI Watanzania wakizidi kujitokeza kulaani maandamano ya kichochezi ya Chadema,.

Hee hivi kuna Watanzania wamejitokeza kupinga maandamano? zaidi ya Mwenyekiti wa C.C.M na wenda wazimu wengine kama KASHA GA?
 
Ujumbe wao "orojino" tuliusikia...Waliifagilia cdm sana sik ile, sasa wamebanwa kidogo wanabadilika na kuzikana kauli zao!....Tena yule mtoto wa mwalimu wa kiume alisema 2015 lazima cdm ikamate dola!...Waache kutubabaisha nao hawa, kama ni allowance za kujikimu watapewa tu bana!
Hawajabadilika hata kidogo isipokuwa wanabadilishiwa maneno wanawekewa vinywani mwao bila wao kupenda. Wanaipenda CHADEMA kwa vitendo huku wakiigiribu CCM kwa maneno ndiyo maana familia hiyo ina wabunge wawili wote kwa tiketi ya ..... wenye akili zetu!
 
Ni vema tukajiepusha na kupost habari za ubabaishaji hapa, maana ni mahali pa watu makini. Mimi nijuavyo hakuna mahali popote ambapo ilisemwa kwamba katika safari yao huko kanda ya ziwa CDM ilikutana na familia ya Nyerere; kilichosemwa ni kwamba viongozi wa CDM walikutana na baadhi ya watu kwenye familia ile, na wala siyo familia nzima. Aidha CDM haijawahi kutoa tamko lolote kuhusu mazungumzo yao na wanafamilia hao; kama hivyo ndivyo hili suala la kuikana CDM linakujaje?
 
Huyo ni Makongoro, hamumjui, tunapoteza muda kujadili kauli zake, mama yake anamjua Baba wa taifa kuliko yeye, akisema mama Maria labda, lakini si huyu aliefulia Makongoro.
 
Ni vema tukajiepusha na kupost habari za ubabaishaji hapa, maana ni mahali pa watu makini. Mimi nijuavyo hakuna mahali popote ambapo ilisemwa kwamba katika safari yao huko kanda ya ziwa CDM ilikutana na familia ya Nyerere; kilichosemwa ni kwamba viongozi wa CDM walikutana na baadhi ya watu kwenye familia ile, na wala siyo familia nzima. Aidha CDM haijawahi kutoa tamko lolote kuhusu mazungumzo yao na wanafamilia hao; kama hivyo ndivyo hili suala la kuikana CDM linakujaje?

nina wasiwasi na uelewa wako mkuu,maelezo yako yanajikanganya sana,umesema hawajakutana na familia ya nyerere,then unasema wamekutana na baadhi ya watu wa familia ile(i take it to be wanafamilia) kwahiyo wewe ulitaka ukusanywe ukoo wote ndo cdm waseme walikutana na familia? hata kama wangekutana na mke na mtoto mmoja tayari hiyo ni familia na ni waakilishi wa familia! usiwe unakurupuka kucomment tuu bila kufikiria ndugu utakuja kuaibika mbele ya kadamnasi
 
Back
Top Bottom