Falsafa ya CHADEMA ni hii, ya CCM iko wapi?

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Falsafa ya Chama​

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.


Nimemsikia Nape Akiongea Star TV, Kuhusu uchaguzi wa CCM, Swali wamewachagua Wajamaa au Mabepari? Wakulima na Wafanyakazi (Maofisa waandamizi) wanaruhusiwa kugombea? (Nyundo na Jembe)


Mwingine anaweza kukuona mbaya, hata unapojaibu kumsaidia. Nyerere aliwaambia "mnaondoa Azimio la Arusha na mambo yake yote, mnaweka nini badala yake", nadhani hawakumwelewa kabisa "kwamba wametema falsafa na wanahitaji mbadala". Aliwaambia chukueni mazuri muache mabaya, tena akawaambia ninyi mnachukua mabaya na kuacha mazuri. Kama wangetumia akili kidogo, kesho yake wangefanya retreat. Haya jamani CCM. Sasa looo! wanaimba ujamaa.
 
Kolimba alishasema zamani sana kuwa hawa jamaa wameshapoteza dira

Una maana hawana kabisa, duh:embarassed2:

Ujenzi wa ujamaa si lelemama bali ni mapambano, mapambano ya kudumu dhidi ya ubepari na unyonyaji, dhidi ya wapinga maendeleo na wababaishaji wa kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi, wezi, wazururaji na wazembe. Msimamo sahihi wa mapambano unaotokana na nadharia sahihi ya ujamaa ungelituepusha na maamuzi na vitendo ambavyo vimerahisisha kuoteshwa kwa
mizizi ya ubepari, kinyume cha msimao wa mapambano dhidi ya ubepari. Leo ubepari, una vishawishi vingi zaidi nchini kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao, ubepari umefaulu kujipanua na
kujipenyeza hata ndai ya sekta yenyewe ya Umma. Na ndiyo maana ubepari sasa unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu ujamaa, kubabaisha baadhi ya viongozi na kututaka tubadilishe siasa yetu.​


Hii inanichanganya saidia wana JF.
 
Naomba kuuliza swali moja tu, hivi hii imesomwa na wale wasomi waliopo kwenye pay roll yenu kama akina baregu na Kitilla? hivi hata maana ya falsa nayo mfundishwe?
 
Naomba kuuliza swali moja tu, hivi hii imesomwa na wale wasomi waliopo kwenye pay roll yenu kama akina baregu na Kitilla? hivi hata maana ya falsa nayo mfundishwe?

Hebu fundisha basi, labda tutaelewa kama CCM:juggle:
 
sasa kazi za akina Kitila huko kwenu ni nini? au kuweka vigezo vya kujaza wabunge wa viti maalum kwenye ukoo wa Mtei?

Lete falsafa za CCM sio za kwako tafadhali. Hapa kama hamna basi kolimba alikuwa wa kweli. Hivi Kolimba nae ni ukoo wa Mtei: focus:
 
Lete falsafa za CCM sio za kwako tafadhali. Hapa kama hamna basi kolimba alikuwa wa kweli. Hivi kolimba nae ni ukoo wa mtei:focus:

Unapaswa kuwa umekufa au haujawahi kuishi Tanzania ndio uwe hauifahamu Falsa ya CCM, maana hata ukilitaja jina hili kwa kirefu utapata majibu.
 
CCM hawana vision wala falsafa wao wana mision moja tu kutwaa madaraka kwa ajili ya kuwanyonya watz, kulindana na kufanya kazi kwa maslahi ya viongozi, maswaiba wao na vitegemezi vyao hawana tofauti na mkoloni ambaye alikuwa hana vision bali mission
 
unapaswa kuwa umekufa au haujawahi kuishi Tanzania ndio uwe hauifahamu Falsa ya CCM, maana hata ukilitaja jina hili kwa kirefu utapata majibu.

Chama cha kijamaa kama
CCM ni chombo cha kuongoza mapambano ya ujamaa nchini. Ni kweli kuwa
ujamaa kimsingi ni siasa ya Wakulima na Wafanyakazi na kwamba utajengwa na
wafanyakazi katika umoja wao wa kitabaka. Lakini ni kweli pia kwamba bila ya
wapiganaji ujamaa wa mstari wa mbele, bila kikosi cha askari wa mstari wa
mbele kujenga ujamaa haliwezi kufikiwa. Kikosi hicho cha wapiganiaji ujamaa
wa mstari wa mbele ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Hapa panasomeka kweli:juggle:
 
Chama cha kijamaa kama
CCM ni chombo cha kuongoza mapambano ya ujamaa nchini. Ni kweli kuwa
ujamaa kimsingi ni siasa ya Wakulima na Wafanyakazi na kwamba utajengwa na
wafanyakazi katika umoja wao wa kitabaka. Lakini ni kweli pia kwamba bila ya
wapiganaji ujamaa wa mstari wa mbele, bila kikosi cha askari wa mstari wa
mbele kujenga ujamaa haliwezi kufikiwa. Kikosi hicho cha wapiganiaji ujamaa
wa mstari wa mbele ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Hapa panasomeka kweli:juggle:

Asante kwa kuufungua moyo wako sasa.
 
Asante kwa kuufungua moyo wako sasa.

Ujamaa ni nini?:lol: Na azimio la Arusha bado lipo, maana nipo mbali na Tanzania.

Hebu some hapa chini:

Chama chetu ni miongoni mwa vyama vichache katika Afrika ambavyo vimefaulu kubuni nadharia ya ujamaa iliyo sahihi, wazi na ya kiwango cha juu. Nadharia hiyo ya Chama inajidhihirisha yenyewe katika Katiba, Azimio la Arusha, Mwongozo na maandishi mengine muhimu ya Chama. Nadharia hii ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea imetujengea msingi wa uelewano, umoja na ushirikiano wa aina mpya katika ujenzi wa taifa na kutufanya tueleweke na wengi kimataifa, jambo ambalo limetupa sifa na heshima duniani kote.​
 
Una maana hawana kabisa, duh
[/FONT]

Si kuwa hawana... walikuwa nayo lakini along the way wamepoteza mwelekeo. Viongozi wengi wa CCM hivi sasa sidhani kama wanaelewa kwa undani falsafa ya chama chao ni nini na ndio mwaana wanaonekana kutekeleza kitu ambacho ni topfauti kabisa na hiyo falsafa. na ndio msingi wa Kolimba kuwapasha ukweli
 
Ujamaa ni nini?:lol: Na azimio la Arusha bado lipo, maana nipo mbali na Tanzania.

Azimio la Arusha halikuwa ndio msingi wa falsafa ya chama ila falsa ya chama ndio iliyozaa azimio la Arusha, kuwepo au kutokuwepo kwa azimio la Arusha hakuwezi kuwa ndio msingi wa kuwepo kwa falsa ya chama. Na kwa kuwa chama kina uhai kama ilivyo kwa jamii mabadiliko yanatokea na kila yanapotokea ni lazima athari zake ziakisiwe katika sera, mipango na maazimio ya chama.
 
Azimio la Arusha halikuwa ndio msingi wa falsafa ya chama ila falsa ya chama ndio iliyozaa azimio la arusha, kuwepo au kutokuwepo kwa azimio la arusha hakuwezi kuwa ndio msingi wa kuwepo kwa falsa ya chama. Na kwa kuwa chama kina uhai kama ilivyo kwa jamii mabadiliko yanatokea na kila yanapotokea ni lazima athari zake ziakisiwe katika sera, mipango na maazimio ya chama.

Ahaa in maana kinabadilika, sasa kwa sasa falsafa yake ni ipi. Maana ukisoma miongozo bado inazungumzia azimio la Arusha, pale nafiki chama kilikomaa. Na azimio lilikipa chama mboresho wa falsafa.

Kolimba alikuwa anaongelea dira ipi?:lol:
 
Ahaa in maana kinabadilika, sasa kwa sasa falsafa yake ni ipi. Maana ukisoma miongozo bado inazungunzi azimio la arusha, pale nafiki chama kilikomaa. Na azimio lilikipa chama mboresho wa falsafa.

Kolimba alikuwa anaongelea dira ipi?:lol:

Sijasema falsafa imebadilika, labda ukisema miongozo inayozungumzia azimio la Arusha unamaanisha ipi specifically? Kuhusu Kolimba sina kumbukumbu haswa alikuwa ana refer kitu gani haswa kwa hivyo siwezi kuongelea sana, lakini naweza tu kukuambia chama kimeendelea kushinda uchaguzi mara tatu tangu Kolimba amefariki 1997, na hali ilivyo kitashinda tena 2015.
 
Eeheeee, mambo si ndio hayo bwana!!!! Kwa kweli CHADEMA you uniquely STAND OUT OF THE CROWD of political parties in Tanzania in many well-thought ways.

Nijuavyo mimi ni kwamba Chama Cha Siasa bila Falsafa inayoongoza mienendo yake yote katika shughuli zake za kila siku si tu kwamba chastahili kusemwa kwamba KIMEKOSA DIRA kama ambavyo Mzee wetu Marehemu Horace Kolimba alivyowahi kutubainishia huko nyuma bali ni kwamba Cha hicho ni sawa tu na abiria aliyefungasha mizigo hadi stendi Ubungo bila hata kujua haswa ni wapi kimeinuiya kwenda ndipo kiweze kukaribisha watu uanachama katika safari ya kwenda huko.

Ni masikitiko yangu makubwa sana hadi najiunga CHADEMA miaka michache iliopita, huko nyuma sikuwa na uhakika kama chama changu cha zamani CCM kilikua kinaendeleza bado falsafa yake ya miaka hiyo ya kuamini katika ujamaa na kujitegemea au kwa sasa siasa zake hufuata falsafa mpya ambayo kwa wenye akili huonekana kama vile kusema 'Taifa hujengwa na Wenye Moyo, Hutafunwa na Wenye Meno'.

Hakika, tangu azungumze Mzee Kolimba watani zetu CCM bado waonekana kiaibu kabisa kung'angania tena kwa sana tu falsafa ya 'Uvuguvugu, Moto na Baridi zote kwa pamoja'.

Hakika dereva asipojua njia anakoenda, mafuta akanyagayo kwenye gari lake ni kazi kure sawa na kuzunguka tu mbuyu pale barabara ya Ali Hassan Mwinyi Road - Masaki.
 
Eeheeee, mambo si ndio hayo bwana!!!! Kwa kweli CHADEMA you uniquely STAND OUT OF THE CROWD of political in Tanzania in many well-thought ways.

Nijuavyo mimi ni kwamba Chama Cha Siasa bila Falsafa inayoongoza mienendo yake yote katika shughuli zake za kila siku si tu kwamba chastahili kusemwa kwamba KIMEKOSA DIRA kama ambavyo Mzee wetu Marehemu Horace Kolimba alivyowahi kutubainishia huko nyuma bali ni kwamba Cha hicho ni sawa tu na abiria aliyefungasha mizigo hadi stendi Ubungo bila hata kujua haswa ni wapi kimeinuiya kwenda ndipo kiweze kukaribisha watu uanachama katika safari ya kwenda huko.

Ni masikitiko yangu makubwa sana hadi najiunga CHADEMA miaka michache iliopita, huko nyuma sikuwa na uhakika kama chama changu cha zamani CCM kilikua kinaendeleza bado falsafa yake ya miaka hiyo ya kuamini katika ujamaa na kujitegemea au siasa hivi falsafa yao huenda ikawa ni ile ya 'Taifa hujengwa na Wenye Moyo, Hutafunwa na Wenye Meno' au tangu azungumze Mzee Kolimba watani zetu bado 'Wato ya maji ya moto na ya baridi kama kawaida yao maika yote?????????????

Kwa kweli wan JF mimi naona CCM haina falsafa, kama ipo hebu mtu asummarise. Nafikiri itasaidia kuelewa hali halisi na chanzo cha matatizo ndani ya CCM.:lol:
 
Back
Top Bottom