Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

kijanamakini

Senior Member
Nov 2, 2010
116
13
1G ni simu za kizazi cha kwanza kabisa katika teknolojia ya mawasiliano katika mfumo wa bila waya (wireless). Wakati huu ndio simu za mkononi (zikiwa kubwa kwelikweli enzi hizo) zilianza kutengenezwa na kununuliwa. Hii ilikuwa katika miaka ya 1980, na moja ya simu maarufu enzi hizo kuanza ni Motorola DynaTAC. Hakukuwa na huduma ya intaneti katika mfumo huu wa teknolojia. Kulikuwa na modemu kwa ajili ya intaneti kwa ajili ya kutumika kwenye kompyuta, ila zilikuwa zinatumia teknolojia ya 'Dial up', yaani kwenye mipangilio (settings) unakuwa kama unapiga simu hivi ndio unakuwa unaunganishwa katika huduma ya intaneti. Na gharama ilikuwa unalipia kulingana na muda ambao umekuwa umeunganishwa kwenye intaneti, yaani kama vile dakika za maongezi.
Kuja na uwezo wa kujiunga mara zote bila ata ya kutumia teknolojia ya Dial Up ndio kulizaa teknolojia ya 2G kwa kuanzia na GPRS.
Teknolojia za 2G;

GPRS

GPRS ndiyo teknolojia ya kwanza kwenye simu iliyoleta uwezo wa kutumia data, yaani intaneti. Teknolojia hii ipo katika familia ya teknolojia za 2G, yaani '2nd Generation'. Kirefu cha GPRS ni 'General Packet Radio Service', kiasi kikubwa zaidi cha kasi ya intaneti ndani ya teknolojia hii ni hadi kufikia kati ya kb 35 hadi 171 kwa sekunde. Lakini mara nyingi huwa chini ya hapo.Katika kutumia teknolojia hii ndio utaweza kufungua mtandao wowote au ata kutuma barua pepe kwenye simu yako, tatizo ni moja tuu..itachukua muda mrefu sana mtandao kufunguka au ata hiyo barua pepe kwenda.
Hapa mfano wa kasi yake ni kama vile mwendo wa kutembea kwa miguu..
EDGE

Kibongo bongo, yaani Tanzania utakuwa umeona sana alama ya E au EDGE ikiwa imekamilika katika simu yako. Ukiona E, ujue ni EDGE na kirefu chake kimombo ni 'Enhanced Data rates for GSM Evolution). Kwa kiasi kikubwa teknolojia hii ilitengenezwa kama maboresho ya teknolojia ya GPRS, hapa uwezo uliongezwa zaidi katika suala la kasi ya uhamishaji wa data katika huduma ya intaneti.Teknolojia hii huwa inategemewa kuweza kuwa na kasi ya hadi kufikia kb 120 hadi 384 kwa sekunde, lakini mara nyingi huwa chini ya hapo. Teknolojia hii ipo juu zaidi ya GPRS lakini ni ya chini sana ukilinganisha na 3G. Wataalamu wengine huwa wanaiona EDGE kama ni 2.5G au 2.75G kutokana na kuwa kasi zaidi ya GPRS.
Hapa mfano wa kasi yake tunaweza fananisha na kamwendo ka kwenda kwa baiskeli. Unajitahidi kidogo ila si kasi sana.
3G - pia HSPA n.k

Teknolojia ya 3G ilitengenezwa kwa ajili ya kutoa maboresho mapya ukilinganisha na teknolojia nzima ya 2G. Teknolojia hii iliingia sokoni rasmi mwaka 2001, na mitandao mingi ya simu ikaanza kuitumia mara moja katika maeneo yenye ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti. Kuja kwake kulikuwa maarufu sana hadi baadhi ya makampuni ya kutengeneza simu kama vile Apple waliamua kuita baadhi ya simu zao '3G', kuna iPhone 3G na iPhone 3GS zilitoka kipindi hicho, hii yote ni kutaka kufahamika ya kwamba simu hizo zitaweza kupata intaneti ya kasi zaidi.Kasi kubwa zaidi inayoweza kupatikana ndani ya mitandao ya 3G ni hadi kufikia Kb 384 hadi MB 2 kwa sekunde.Je HSPA, HSPA+, EVDO, HSDPA n.k ni nini?
Hizi ni teknolojia za maboresho zaidi ya 3G na zimefanikiwa kukuza kasi ya intaneti ya 3G kufikia hadi zaidi ya MB 100 kwa baadhi yake, kasi hii si kwa watumiaji wadogo kupitia simu kama mimi na wewe. Lakini bado kwa watumiaji wadogo, mimi na wewe kasi inakuwa ndogo, lakini bado utaona utofauti kulinganisha na 3G hasili. Maboresho haya ndiyo yanaleta majina mengine kama vile 3.5G, 3.75G n.k.
Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema apa una mwendokasi wa pikipiki. Ni maendeleo makubwa sana kutoka kwa utumiaji wa basikeli, yaani EDGE.
4G!

Teknolojia ya 4G ina kiwango cha kuwezesha hadi kasi ya intaneti ya GB 1 kwa sekunde kwa maunganisho ya kiwaya, yana 'fiber', na kwa eneo la kimawasiliano ya simu inatakiwa kuwa na kasi ya MB 100 kwa sekunde. Kumbuka mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yamefanyika kuwezesha kasi hizi kubwa za intaneti, mfano teknolojia za 2G na 3G zote zilikuwa zinapatikana katika mifumo ya GSM (mitandao yetu mingi inatumia mfumo huu) na CDMA (mfumo unaotumiwa na TTCL), lakini 4G inapatikana katika mifumo mipya ya LTE (Long Term Evolution) na WiMAX.Ingawa kiteknolojia WiMAX inatakiwa kutoa intaneti ya hadi ya kasi ya MB 40 kwa sekunde na LTE hadi kasi ya MB 100 kwa sekunde mara nyingi hali inakuwa tofauti unapokuja kwa watoa huduma za intaneti katika teknolojia hizo. Kiutumiaji wa kawaida tegemea kasi ya kati ya MB 4 hadi MB 30 kwa sekunde, na hii ni kasi kubwa tuu ukilinganisha na kile unachoweza kupata ukiwa unatumia 3G. Kiuhalisia pia ni kwamba ili uweze kufurahia kasi hizi kifaa chako pia kinatakiwa kiwe na uwezo wa kupokea intaneti ya kasi hiyo.
Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema katika teknolojia hii unasafiri kwa ndege, utawahi kufika sana kulinganisha na teknolojia za nyuma.
5G?

Tayari nguvu zimewekwa katika kujenga teknolojia ya 5G ingawa ata hii 4G bado haijaweza kusambaa zaidi kama 3G. Na ni kampuni ya Samsung ndio wamejikita katika kuleta teknolojia wanayofikiria itaweza kuwa hadi mara 100 haraka zaidi ya 4G!

CHANZO:
http://teknokona.com/2015/04/27/fahamu-tofauti-kuu-kati-ya-teknolojia-za-2g-3g-4g-n-k/
 
DC-HSPA+ ndo kilele cha 3G speed mpaka 42Mbps
Hivo unaposema 3G unaweza pata mpaka speed ya 16Mbps i.e 2MB/sec kadiri ya maelezo yako nafikiri unakua haujafika kilele cha 3G ambacho ni 42Mbps japo practically sijui kama kuna nchi ime implement hiyo kitu...Binafsi siku moja nipo Ilala chuo cha DSJ nilipata 24Mbps

Hii DC-HSPA+ kwa hapa Dar inasoma kwa Airtel tu na Tigo baadhi ya maeneo
 
Safi ndugu kwa kutufahamisha maana kuna vitu huwa vinachanganya, unapo kwenda sehem una dawnload kitu chenye 4mb unapewa time remain 99>mn mpaka unajiuliza cm si itaishiwa chaji!
 
kampuni ya Samsung ndio wamejikita katika kuleta teknolojia wanayofikiria itaweza kuwa hadi mara 100 haraka zaidi ya 4G!

Ni kama unasema cocacola kajikita kumpiku tanga cement.
Samsung role yake ni kutengeneza modem za 5g za simu au vifaa vitakavyotumia 5g nk

Makampuni makubwa ya telecom ni
-ericsson
-huawei
-nokia
-alcatel lucent
-zte

Ukiskia 5g imetoka ujue mmoja wapo hapo juu au wote ndio wamegundua
 
Kuna campuni moja ya simu inaitwa smile inauza internet (line na vocha ya interner) 4 G.. LTE sasa endapo simu yangu ni (0‡8) 2.5 G ITAKUWAJE HAPO
 
Ni kama unasema cocacola kajikita kumpiku tanga cement.
Samsung role yake ni kutengeneza modem za 5g za simu au vifaa vitakavyotumia 5g nk

Makampuni makubwa ya telecom ni
-ericsson
-huawei
-nokia
-alcatel lucent
-zte

Ukiskia 5g imetoka ujue mmoja wapo hapo juu au wote ndio wamegundua

Kaka kuuza simu ni moja ya department kubwa ya Samsung. Makampuni yote makubwa yanafanya Research n development ktk teknolojia. Na hili ni la kweli. Korea Kusini, makao makuu ya Samsung ni moja ya nchi yenye kasi kubwa kabisa ya internet...
 
kaka usisahau kwamba mitandao yote mitatu ya korea kusini wanatumia technology ya nokia.

Korea kuna mitandao hii
-sk telecom
-kore telecom freetel
-lg telecom

mitandao yote mitatu inatumia technology za nokia
sk telecom
SK Telecom names Nokia Siemens Networks as its 100G optical supplier - FierceTelecom

lg telecom
LG U+ selects Nokia Siemens Networks for LTE roll out in Korea | Nokia Networks

even kibongo bongo ukiskia sjui smile wana lte haimaanishi wao ndio wameigundua bali wametoa hela then wanafungiwa technology. mfano lte ya smile hapa tz inatoka kwa alcatel lucent

Alcatel-Lucent wins Tanzania LTE | Global Telecoms Business
 
Sikutaka mabishano, tunaongelea 5G TECHNOLOGY... Soma zaidi hapa kuhusu technology ya 5G na role ambayo Samsung wanaplay... http://www.pcworld.com/article/2834072/samsung-claims-data-speed-test-30-times-faster-than-lte.html note: 30 times faster than LTE....
 
kaka usisahau kwamba mitandao yote mitatu ya korea kusini wanatumia technology ya nokia.

Korea kuna mitandao hii
-sk telecom
-kore telecom freetel
-lg telecom

mitandao yote mitatu inatumia technology za nokia
sk telecom
SK Telecom names Nokia Siemens Networks as its 100G optical supplier - FierceTelecom

lg telecom
LG U+ selects Nokia Siemens Networks for LTE roll out in Korea | Nokia Networks

even kibongo bongo ukiskia sjui smile wana lte haimaanishi wao ndio wameigundua bali wametoa hela then wanafungiwa technology. mfano lte ya smile hapa tz inatoka kwa alcatel lucent

Alcatel-Lucent wins Tanzania LTE | Global Telecoms Business

Soma hapa pia http://www.zdnet.com/article/samsung-boasts-7-5gbps-mobile-speed-record-in-5g-trial/ i hope hii topic ipo closed now..
 
kaka usisahau kwamba mitandao yote mitatu ya korea kusini wanatumia technology ya nokia.

Korea kuna mitandao hii
-sk telecom
-kore telecom freetel
-lg telecom

mitandao yote mitatu inatumia technology za nokia
sk telecom
SK Telecom names Nokia Siemens Networks as its 100G optical supplier - FierceTelecom

lg telecom
LG U+ selects Nokia Siemens Networks for LTE roll out in Korea | Nokia Networks

even kibongo bongo ukiskia sjui smile wana lte haimaanishi wao ndio wameigundua bali wametoa hela then wanafungiwa technology. mfano lte ya smile hapa tz inatoka kwa alcatel lucent

Alcatel-Lucent wins Tanzania LTE | Global Telecoms Business

SIJUI KILA KITU BUT PIA HUWA SITOI FACT BILA RESEARCH.... I hope now umejua kipya pia, ya kwamba Samsung ni zaidi ya kutengeneza na kuuza simu na tv..
 
Bango kama hizi ndio zinafaa, yaani giving back to the community, kuna vijana wapo wanataka kuingia kwenye huu ulimwengu wa technologia lakini wanashindwa kuelewa tofauti ya hii mifumo. Akina Kimweri wanaojiita wataalamu halafu wamejifungia maofisini wanafaa kuona jinsi jamaa ameamua kutafsiri mfumo wote kwa lugha ya Kiswahili.
 
Last edited by a moderator:

Nitake radhi, mimi sio blogger.na vitu vilivyoandikwa humo ni daraja la kawaida kabisa kwa mie kupoteza muda kuvielezea.
Wenye muda wa kutosha kufanya tafsiri na wafanye,kuna vitu watumiaji wa kawaida wanatakiwa kujua vile wanavyoambiwa na maafisa masoko,inatosha. Maana maleezo yakiwa mengi, unaweza kujikuta unakosa wateja. fikiria unapomueleza mtu kuwa spidi ya juu ni 2048Kbps lakini wewe daima utakuwa unapata spidi ya 250Kbps mwisho unategemea kuwe na amani hapo?
Kama mtu anataka kujua zaidi kuhusu teknolojia na mifumo ya kihandisi, aanze kujifunza hesabu na fizikia, ili somo likifika katikati asitoke mbio na kumpotezea muda mwelekezaji.

Natoa pongezi za dhati kwa walioamua kuwasilisha teknolojia hizi nyepesi kwa lugha rahisi na inayoeleweka.
 
Back
Top Bottom