Fahamu haya kuhusu matairi ya gari lako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,707
Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari lako).......Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote.

Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (2603) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa.

Kwa mfano 2603 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au 2699 inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE......hapo ndio inapotokea tairi mpya umenunua juzi kisha baada ya Wiki moja ya matumizi inapasuka puu ukiwa kwenye mwendo na kuanza kutafuta chanzo na usikione kuumbe lilisha Expire ivo ni vema kuchukua tahadhari.

Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi Kama ifuatavyo.

CODE. SPIDI
F========80
G ========90
J ========100
K ========110
L ========120
M ========130
N ========140
P ========150
Q ========160
R ========170
S ========180
T ========190
H ========200

Huandikwa hivi
280/R/70/13/560/S
hiyo herufi ya mwisho ndio speed ya mwisho ya tair kama
Hapo herufi S inawakilisha Spidi,180.
 
Back
Top Bottom