Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Kwa mnaosafiri Kwa ajili ya Mapumziko ya Mwisho wa Mwaka, ni jambo kuzingatia mambo haya:
1. Hakikisha gari iko vizuri
2. Ukiwa unaendesha na si mzoefu wa safari ndefu ni vizuri kusafiri mchana tu
3. Waza kufika salama na si saa ngapi
4. Epuka mafuta ya vichochoroni
5. Kama kwenu mbali yaani KM 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6. Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho
7. Kuwa makini unapoanza safari na unapokaribia kufika
8. Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9. Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10. Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11. Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12. Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13. Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14. Hakikisha upepo wa matairi uko sahihi wakati wote
15. Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16. Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu, chukua namba kisha mpishe aende
17. Kama sio mzoefu kuendesha safari ndefu hata kama umenunua gari lako jipya chukua dereva….kijijini watajua tu ni lako hata kama sio wewe umeenda unaendesha.