Eti kufanya Engine Overhaul kunaondoa engine katika ubora na ufanisi daima?

Makobus

Senior Member
Jul 30, 2012
161
103
Engine ya gari yangu inanizingua kwa kunywa oil. Mafundi wanasema kubadili spare za kwenye engine ni kazi bure. Bora kufanya overhaul kabisa.

Lakini mafundi wengine wananitahadharisha kuwa nikifanya overhaul ndiyo nitakuwa nimeiua engine na itanitesa zaidi.

Wanashauri bora ninunue engine nyingine tu. Hili limekaaje wataalam?
 
Engine ya gari yangu inanizingua kwa kunywa oil. Mafundi wanasema kubadili spare za kwenye engine ni kazi bure. Bora kufanya overhaul kabisa. Lakini mafundi wengine wananitahadharisha kuwa nikifanya overhaul ndiyo nitakuwa nimeiua engine na itanitesa zaidi. Wanashauri bora ninunue engine nyingine tu. Hili limekaaje wataalam?
Nafikiri inategemea na Aina ya engine mkuu.. ngoja wataalam waje
 
Weka vifaa OG... na fundi mzuri tu.

Overhaul chuma inakuwa Mpya. Nimefanya juzi ktk Patrol TD42, Inamlio wa tapping ktk Cylinder head inatakiw kupimwa tena.. hilo ndio tatizo dogo tu.. maana hakupima vzr.

Pia uwekaji wa Gasket nzuri, Usafi wa Ufundi na kuweka vimiminika Bora.

OVERHAUL haitaki UBAHILI.

pia jipange unaweza ambiwa hii OVERHAUL yake maybe 1.2M ila utashangaa inakutafuna mpk 2.0M
 
Engine ya gari yangu inanizingua kwa kunywa oil. Mafundi wanasema kubadili spare za kwenye engine ni kazi bure. Bora kufanya overhaul kabisa. Lakini mafundi wengine wananitahadharisha kuwa nikifanya overhaul ndiyo nitakuwa nimeiua engine na itanitesa zaidi. Wanashauri bora ninunue engine nyingine tu. Hili limekaaje wataalam?

Kwa mafundi wetu tia maji, overhaul inapunguza ubora...

Mara chache sana inakuwa imenyoka ikipata fundi very competent.
 
Engine ya gari yangu inanizingua kwa kunywa oil. Mafundi wanasema kubadili spare za kwenye engine ni kazi bure. Bora kufanya overhaul kabisa.

Lakini mafundi wengine wananitahadharisha kuwa nikifanya overhaul ndiyo nitakuwa nimeiua engine na itanitesa zaidi.

Wanashauri bora ninunue engine nyingine tu. Hili limekaaje wataalam?
nunua mswaki tuu umalize kazi, tatizo la overhaul fundi kama hayupo vzr na spea zikawa sio genuine baada ya muda mfupi sana matatizo yanaanza kuibuka tena
 
Engine ya gari yangu inanizingua kwa kunywa oil. Mafundi wanasema kubadili spare za kwenye engine ni kazi bure. Bora kufanya overhaul kabisa.

Lakini mafundi wengine wananitahadharisha kuwa nikifanya overhaul ndiyo nitakuwa nimeiua engine na itanitesa zaidi.

Wanashauri bora ninunue engine nyingine tu. Hili limekaaje wataalam?
Kamilisha maelezo upate ushauri mzuri.
-Gari gani?
-Engine aina gani?
Sio kweli kuwa ukifanya overhaul itapoteza ufanisi maana kufanya hivyo ndiko kutafuta huo ufanisi, bali ukiiacha bila kufanya hivyo ndio kupoteza ufanisi.
Angalia garama za matengenezo/ maintenance kisha linganisha na garama za kubadili engine/ replacement. Baada ya hapo jipime kisha fanya maamuzi.
Engine nzuri kwa overhaul ni Castic Iron kuliko Alluminnium Iron.
NB. Hakuna engine itakayorudi ktk upya kwa kufanya overhaul kwa 7bu kila ukiweka engine oil mpya/safi, ukitoa inakua chafu, jiulize kinacho ichafua huwa ni nini? Overhaul hupunguza tatizo la ulaji wa oil na sio kuondoa maana engine inakula oil tangu siku inatoka kiwandani. Soma spacefikation za engine yako kutoka ktk manu ya gari lako utagundua.
 
Gari ni Succeed, Engine ni 1NZ. Zidi kunishushia nondo boss wangu.
 
-Angalia gharama.
-1NZ ni alumminium block. Ukipata fundi mzuri wa overhaul hilo tatizo litaondoka, ila mlio hautarudi kama ulivyokua, utaongezeka. Na asije mtu akakuambia vifaa vilivyowekwa na fundi wako ni feki ukaifungua tena, hapo ndio utakua umeiua kabisa.
Alminiam ni nyepesi, hivyo unapofunga zile bolt silinda head-block huwa hazikazi kama awali, ukisema uzifungue tena, ukifunga ndio zinapwerepweta kabisaaa na hapo ndipo oili italiwa.
Pia 1NZ engine maisha yake ni kilomita laki mmbili (200,000,km)life spane. Ikifika km 150,000 majanga yataanza kama kula oil, ku vibrate, kutoa mlio wa kugonga nk, hapo utabadili hadi taimingchain na tanshiner yake, gasket karibu zote, rings, kisha itaishi kwa km 50,000. Hapo utoe engine. Sasa angalia gari yako ina km ngapi.
 
Gari ni Succeed, Engine ni 1NZ. Zidi kunishushia nondo boss wangu.
Kwa ushauri wangu, tafuta injini nyingine, iwe 'mswaki' au injini kamili. Nilishawahi kuhangaika na overhaul ya 1ZZ, uwezo haukurudi kama ilivyokuwa awali. Gari nilikuja kuiuza miaka 4 baadae. Mara zote hizo, iligharimu sh 1mil. Kilichonifanya nikae nayo muda mrefu ilikuwa ni bei ghali ya injini nyingine. Ikiwa safi kabisa, ni hadi milioni 3. Ila 1NZ ni cheap.
 
Back
Top Bottom