ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Tulimpenda sana, na tulipenda awe sehemu ya familia yetu, nilifurahi wakati ule ambapo ndugu yangu wa damu alipokuja kuniarifu kuwa amekwisha mpa ujauzito ...na wanatarajia kuoana. Hata hivyo, baada ya kujifungua tu, mama yake ambaye ana kipato cha wastani kuzidi familia yetu alishindwa kukubali kuona mwanae anaolewa kwetu, akaanza mizengwe yenye kishindo. Baaada ya misukosuko mingi, ndugu yangu akabwaga manyanga, binti akatangaza kuolewa na mwanaume mwingine wakafunga pingu za maisha baada ya miezi kadhaa tayari wamepata mtoto . Ni miaka mitatu tu imepita, binti ameanza kumtafuta ndugu yangu akitaka ikiwezekana amsaidie kuachana na munmewe wa ndoa kwa kuwa amebaini si chaguo lake na tayari amepoteza muda kwake, anataka waachane kabisa ili amrejee ndugu yangu ikibidi wafunge hata ndoa ya Kiserikali (Bomani) au ya Kimila, anasema alimpenda sana ndugu yangu anataka waishi pamoja walee mtoto waliomzaa.
Tupo kwenye maandalizi ya harusi ya ndugu yangu, kama zilivyo ndoa za zama hivi, tayari nae alikwishapata mwenza na kama itampendeza Mwenye enzi apandenae katika madhabau takatifu, basi itakuwa ni kwenda kuhalalisha dhambi (sio kiubariki ndoa) kwani tayari mwenza huyo mpya nae yu mjamzito... ndugu yangu nae anaonekana kama yu njia panda katika maamuzi...mtaani anasikika akimsifia huyo wake wa zamani kuwa angemfaa..anatamani kuwa nae.