Eti anataka kurudi...

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
927
Tulimpenda sana, na tulipenda awe sehemu ya familia yetu, nilifurahi wakati ule ambapo ndugu yangu wa damu alipokuja kuniarifu kuwa amekwisha mpa ujauzito ...na wanatarajia kuoana. Hata hivyo, baada ya kujifungua tu, mama yake ambaye ana kipato cha wastani kuzidi familia yetu alishindwa kukubali kuona mwanae anaolewa kwetu, akaanza mizengwe yenye kishindo. Baaada ya misukosuko mingi, ndugu yangu akabwaga manyanga, binti akatangaza kuolewa na mwanaume mwingine wakafunga pingu za maisha baada ya miezi kadhaa tayari wamepata mtoto . Ni miaka mitatu tu imepita, binti ameanza kumtafuta ndugu yangu akitaka ikiwezekana amsaidie kuachana na munmewe wa ndoa kwa kuwa amebaini si chaguo lake na tayari amepoteza muda kwake, anataka waachane kabisa ili amrejee ndugu yangu ikibidi wafunge hata ndoa ya Kiserikali (Bomani) au ya Kimila, anasema alimpenda sana ndugu yangu anataka waishi pamoja walee mtoto waliomzaa.

Tupo kwenye maandalizi ya harusi ya ndugu yangu, kama zilivyo ndoa za zama hivi, tayari nae alikwishapata mwenza na kama itampendeza Mwenye enzi apandenae katika madhabau takatifu, basi itakuwa ni kwenda kuhalalisha dhambi (sio kiubariki ndoa) kwani tayari mwenza huyo mpya nae yu mjamzito... ndugu yangu nae anaonekana kama yu njia panda katika maamuzi...mtaani anasikika akimsifia huyo wake wa zamani kuwa angemfaa..anatamani kuwa nae.
 
unajuana inakuja wakati katika maisha abapo inabidi ufanya uamuzi na inakula kwako kwa upande mwengine. sasa kwa huyu jamaa yeye aendelee tuu na huyo dada aliyepang kufunga nae ndoa na yule wengine aliyemtosaga sio wakusetle nae becoz tayari aeshaonyesha kuwa hawezi simama kideti na kile anachokipenda!!!
 
huyo ndugu yako amesahau kuwa huyo wa zamani hana maamuzi anaamuliwa na mama yake? ama mama sio kikwazo tena?
 
Tulimpenda sana, na tulipenda awe sehemu ya familia yetu, nilifurahi wakati ule ambapo ndugu yangu wa damu alipokuja kuniarifu kuwa amekwisha mpa ujauzito ...na wanatarajia kuoana. Hata hivyo, baada ya kujifungua tu, mama yake ambaye ana kipato cha wastani kuzidi familia yetu alishindwa kukubali kuona mwanae anaolewa kwetu, akaanza mizengwe yenye kishindo. Baaada ya misukosuko mingi, ndugu yangu akabwaga manyanga, binti akatangaza kuolewa na mwanaume mwingine wakafunga pingu za maisha baada ya miezi kadhaa tayari wamepata mtoto . Ni miaka mitatu tu imepita, binti ameanza kumtafuta ndugu yangu akitaka ikiwezekana amsaidie kuachana na munmewe wa ndoa kwa kuwa amebaini si chaguo lake na tayari amepoteza muda kwake, anataka waachane kabisa ili amrejee ndugu yangu ikibidi wafunge hata ndoa ya Kiserikali (Bomani) au ya Kimila, anasema alimpenda sana ndugu yangu anataka waishi pamoja walee mtoto waliomzaa.

Tupo kwenye maandalizi ya harusi ya ndugu yangu, kama zilivyo ndoa za zama hivi, tayari nae alikwishapata mwenza na kama itampendeza Mwenye enzi apandenae katika madhabau takatifu, basi itakuwa ni kwenda kuhalalisha dhambi (sio kiubariki ndoa) kwani tayari mwenza huyo mpya nae yu mjamzito... ndugu yangu nae anaonekana kama yu njia panda katika maamuzi...mtaani anasikika akimsifia huyo wake wa zamani kuwa angemfaa..anatamani kuwa nae.

Kulamba matapishi si kinyaa?
 
Mungu atusaidie
us.jpg
 
its hard na afanye maamuzi haraka kwani inavyoonekana hajampenda mpenzi wake wa sasa ..kitakachoendelea ni uhawara na kuwatesa wenzi wao
 
Too late!Aachane na mipango ya kuvuruga mahusiano ya sasa ili kurejesha enzi!Enzi zikipita hazirudi kamwe!
 
Isitoshe huyo wa zamani ni mke wa mtu ana ndoa kwahiyo ni sumu kwake, iliyoko abaki na huyo wa sasa ambae ni halali kwake ili hata mbele ya Mungu ampendeze
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom