Anataka nizae naye watoto

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Aug 22, 2014
516
890
Huyu dada nafahamiana nae kwa mda wa mwaka na miezi kadhaa hivi. Tulikutana katika mishe mishe za maisha tukajenga urafiki wa kawaida. Binafsi nafurahia sana urafiki wetu, ni dada flan ivi ana akili sana ya maisha.

Wiki iliyoisha amenipigia simu anahitaji kuongea nami lakini si kwa simu. Tukakutana sehem ndo akanambia lengo lake, kua anapenda sana kuwa na watoto umri, uwezo anao lakini hana mpango wa kuolewa. Akawasilisha ombi lake la kutaka kuzaa na mimi.

Wakuu mimi nina mke na watoto wawili, naipenda familia yangu. Japokua uyu dada anasema jukumu la kulea, shule na malezi kwa ujumla litakua juu yake. Amenda mbali anasema kama nikitaka watoto wanaweza wasitumie jina langu.

Nimeshindwa kumpa jibu nimemwambia acha nifikirie kwanza sijataka kuumiza moyo wake kwa mda ule.

Nimejikuta nawaza sana ivi naanzaje kuzaa nje ya ndoa? Ikitokea nimezaa nae uyu dada nitawezaje kuwaficha watoto wangu kwa ndugu na marafiki? Bila kujali watoto wamepatikana katika mazingira gani kwa hili sio sahihi kabisa nitakuwa siwatendei haki watoto. Kama ikitokea watoto wasitumie jina langu ivi nitaendelea kuishi vipi apa duniani hali ya kua najua nina damu sehem flan ambao wanatumia jina la mtu mwingine. Mwisho kabisa mke wangu akijua nina watoto nje ya ndoa anaweza kutaka tuachane. Sipo tayari kuachana na mke wangu na familia yangu. Nimetoka nae mbali.

Ombi la uyu dada limenifikirisha sana. Ivi nini kimempata uyu dada adi kuja na ombi kama hili tena kwa mme wa mtu! Hii dunia inaelekea pabaya sana!
 
Huyu dada nafahamiana nae kwa mda wa mwaka na miezi kadhaa hivi. Tulikutana katika mishe mishe za maisha tukajenga urafiki wa kawaida. Binafsi nafurahia sana urafiki wetu...
Pole mkuu, kimbia usigeuke nyuma huyo anataka akuharibie maisha kama yeye alivyojikatia tamaa. Kalipenda ua anataka alikate ana upendo wa kishetani huyo.

Okoa damu yako okoa ndoa yako okoa heshima yako.

Kama anataka ukuni tu aseme ila habar za watoto uongo, ebu ongea na mkeo akikubali wao wote wawili ndipo umzalishe.
 
giphy (1).gif


KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Wakuu mimi nina mke na watoto wawili, naipenda familia yangu. Japokua uyu dada anasema jukumu la kulea, shule na malezi kwa ujumla litakua juu yake. Amenda mbali anasema kama nikitaka watoto wanaweza wasitumie jina langu.
Hahahaaaa.....imebidi nicheke.

Jaribu uone utakavyojuta.

Akiwa na mimba tu utakimbia Nchi.

Inaonekana huyo mwanamke anakuzidi akili, kipato na ufahamu
 
Back
Top Bottom