Esoteric: Uhusiano wa Zitto, JK, Salim A.S, Ridhwan, Omar Ilyas & then some Islams?

Status
Not open for further replies.
Zito amesema anangoja adhabu. Hi maana yake nini? Soma katikati ya mistari. huyu jamaa naona anataka kuwa kumbikumbi, ataliwa na kunguru sasa hivi.


Zito alisema atagombea Urais Mwaka 2015. Anachotafuta ni sababu ya kuondoka aende NCCR ili agombee urais.
 
udini- sitaki kujisemea.
Mentor-salim ahmed salim ni mentor wangu kama mtanzanzania bila kujali u ccm wake. Jaji warioba is my mentor pia. Ninapokuwa na hawa wazee siwaoni kama ccm bali statemen. I am very proud kuwa karibu nao na napata ushauri wao muda wowote. Nina mentors nje ya tanzania na pia marafiki wengine viögozi ktk serkali zao na wengine ex. Kgm imepata antention ya serkali wakati wa jk. Watu wa kgm wanajua


Mheshimiwa is this statement in red from your own mouth? Do you realy believe in fragmented development strategies driven by political motives? Unachokifanya ni dhambi kubwa kwa wasomi na vijana wa leo wa Tanzania; kwahiyo leo unataka kutuambia jambazi mmoja akisaidia kukujengea shule kwenye jimbo lako na wewe kama mbunge ukigundua huyo mtu nijambazi basi kwavile zile pesa alizitumia kujengea raia wema shule basi wewe kumwajibisha siyo sahihi? Au mwanao akikupa zawadi ya gari na baadaye ukagundua kahongwa utashindwa kumuadabisha kwavile gari alilohongwa kakupa ww baba yake kama zawadi? (By this I dont mean rais ni jamabazi au ni muhuni just take the context) unapomrekebisha mtu haijalishi alishawahi kukupa nini unachotakiwa nikuona ukweli wa kosa kutendeka au la; kama ungesema kwakweli CDM wanadanganya katika madai yao kuhusu tume ya uchaguzi etc then kila mmoja angesimama kukutetea maana hapo ungetoa hoja na sisi tukazipima. Such opportunistic behaviour should be left to those who are not confident and capable lakini kwa msomi kijana mwenye qualification kama wewe kwakweli huitendei haki jamii!

Na mimi nakuhakikishia kwavile watu wanakosa majibu ya hiyo statement ndiyo maana wanaanza kuspeculate labda udini, labda pesa etc pengine maskini you are not such ways.

To be frank as a CDM leader the timing for your description was not right at all. You are a political leader and not a spiritual leader na every statement you make counts a lot. If at all you can not identify the proper audiences, timing and places then why should you be a political leader? Unless you tell the public you have your own agenda!

Na sisi tunakulaumu kwasababu tunaitumia hii platform ya CDM kupeleka agenda zetu za tume huru na katiba all ove the sudden brigedia wetu mmoja unauza brigedi tukufanyeje?

Naomba unisamehe kwakua ww ni mkweli na mm nimejaribu kusema yakwangu ya moyoni kabisa!
 
Zitto kwenye ili uliwakera watu wengi... Kwenye vikao vingi viwe vya kichama, harusi, kiserikali huwa kuna mijadala mizito inayopinginga... kwa sisi tunaofuata demokrasia ya wengi wape hukuwa na sababu kuongelea msimamo wako hadharini ili mradi kila mtu ajue kumbe kuna mfarakano ndani ya Chadema.

Viongozi wengi walianguka kisiasa kwa makosa madogo madogo kama yako. Husipoangalia huu unaweza ukawa mwanzo wa mwisho wako kisiasa.... Kubwa Omba radhi yaishe

Zitto aombe radhi kwa kusimami misimamo yake au aombe radhi kwa kukera watu. Kama kiongozi huwezi kumfurahisha kila mtu kwa maamuzi ambayo unayaona kuwa ni sahihi. Au unataka Zitto aombe radhi halafu mtake advantage kummaliza kisiasa what a crap!!!
 
Kwa kuongezea, katika jimbo la Zitto la Kigoma Kaskazini, Dr. Slaa alipata asilimia 30.7 ya kura zilizopigwa dhidi ya asilimia 63.0 za Kikwete; wakati jimbo jirani la Manyovu, ambako hiyo barabara ya lami na kwenyewe imefika, (na huo ndio mradi pekee anaohubiri Zitto), tena ambako mbunge ni wa CCM, Dr. Slaa alipata asilimia 57.8 dhidi ya asilimia 36.6 za Kikwete. Kwa hakika Zitto amempigia kampeni Kikwete. AENDE CCM HARAKA SANA
Lemme speak it loud we don't need them rats in CHADEMA, Zitto nenda zako CCM utasambaratisha chama chetu Chonde Chonde....
 
aliahidiwa kigoma kuwa kama dubai

ndo maana analowanisha msimamo wa chama .
hana maana
 
Hivi ni mgombea gani wa Ubunge awe wa CCM ama Chadema aliyeshiriki katika kampeni za chama chake kwa mapana yake kama Zitto?. Hivi sio Zitto aliyetoka hadi Mtwara, Shinyanga na mikoa mingine kuwapigia kampeni wagombea wa chama chake" Hivi Mwenyekiti wake Mbowe zaidi ya zile activity tatu zilizokuwa na LIVE COVERAGE mlimuona sehemu nyingine yeyote.....Hivi Dr Slaa amewahi kwenda jimbo lolote na kutembezwa na mgombea mbunge katika kata zote kama ilivyokuwa Kigoma Kaskazini? Hivi kuna mgombea ubunge yeyote aliyetumia muda wake kuwatafutia/kufundraise fedha za uchaguzi wagombea wenzake wa ubunge na udiwani kama alivyofanya Zitto? Hivi kuna mgombea yeyote wa CHADEMA ambaye amejitolea hata kumtengenezea posters/mabango ya kampeni mgombea mwenzake yeyote kama alivyofanya Zitto kwa wagombea zaidi ya 20 na huku kwake akiwa hana uhakika hata wa fedha za kuwalipa mawakala wake??

Acheni kumuonea Zitto ama kwa kutojua ukweli au chuki zenu binafsi.......

Japo nakubaliana na wewe kuhusu mambo aliyofanya Zitto kwenye kampeni katika kusaidia chama na kusaidia wagombea wengine, ishu ni kuwa Zitto anaonekana ana-potential kubwa sana ya kuleta mageuzi tunayoyataka hapa Tz. Tatizo lake amekuwa akiwatenda wanamagezi vibaya na kusababisha watu tusimwamini kabisa. Hutumwonei tunataka arudi kwenye mstari aua aende ccm,cuf,nccr,tlp, ijulikane moja.
 
nilisema a fraction ya yaliyotokea. Kuhusu kura tu na mie msimamo wangu ulikuwa wapi. Unataka niwe na msimamo kisha nifiche? Huo ni unafiki. Unataka niseme kisiri siri? Siwezi. Kulikuwa kuna ulazima? Ndio na hapana. Kisiasa hapana. Kisiasa za maadili na kuwa wakweli mbele ya umma na hasa jimbo la uchaguzi, ilikuwa lazima msimamo wa kila mmoja uwe wazi.

Hata wakati wa DOWANS ulikuja na majibu rahisi rahisi hivi hivi. Kutoa msimamo wako TBC ulikuwa unamnufaisha nani? Msimamo? Msimamo gani ulionao wewe Zitto! Binadamu anakuwa mkamilifu pale anapofanya yale yaliyokamilika. Huwezi kuniambia hata mkeo akitaka unyumba na wewe ukawa hutaki kumpa unyumba kesho yake utakwenda TBC kusema "Mke wangu alitaka unyumba na mimi nimemkatalia na huo ndio msimamo wangu" Acha bana! Zitto mimi nilishaandika humu jamvini kuwa wewe hufai, hufai, hufai kabisa! Ni busara tu ya Wazee wa CDM ndio inafanya wewe uendelee kuwepo pale. Sio wewe ulitangaza kwenye mikutano yako ya Kampeni kuwa mwaka 2015 utakwenda kwenye Jimbo lako kuomba kura lakini safari hii ukiomba Kura za Urais na si Ubunge? Nani alikuhakikishia kuwa utavuka michakato yote hadi kuwa mgombea wa Urais. Kwa kutamka maneno hayo kwa wapiga kura wako huoni kama ulikuwa unamharibia Mgombea wa Chama chako mwaka huu kwa kuwambia Wananchi huyu Slaa 'wenu' hashindi ng'o'

Ulipokuwa mbunge mteule haraka haraka ukaja na ajenda ya kutaka kugombea kuwa kiongozi wa upinzani Bungeni? Hivi ulishajua chama chako kitatumia njia gani kumpata mgombea? Zitto kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa wewe ni 'agent' wa watu fulani au kundi fulani na labda bila kutafuna maneno wewe ni 'agent' wa Mafisadi na tuliliona hili wakati ule wa DOWANS! Wewe ondoka tuachie CDM yetu, akina Hiza Tambwe wanakusubiri pale Ofisi ndogo ya CCM.
 
udini- sitaki kujisemea.
Mentor-salim ahmed salim ni mentor wangu kama mtanzanzania bila kujali u ccm wake. Jaji warioba is my mentor pia. Ninapokuwa na hawa wazee siwaoni kama ccm bali statemen. I am very proud kuwa karibu nao na napata ushauri wao muda wowote. Nina mentors nje ya tanzania na pia marafiki wengine viögozi ktk serkali zao na wengine ex. Kgm imepata antention ya serkali wakati wa jk. Watu wa kgm wanajua

Zito usijishushie hadhi kigoma imepata hadhi sababu yako wewe Zitto.
 
Kwenye Swala la Udini, mhhhhh hili naweza kukutetea hata mie. Nimesoma habari zako nyingi na kwa hili nina uhakika wa asilimia kubwa sana kuwa huhusiano nalo. Na uendelee hivyo...... Jamaa yako Omar ni MDINI haswaaa na hilo hawezi kujificha. Nimeshamuambia hata yeye moja kwa moja kwenye majadiliano humu JF. Hutetea kila hoja ambayo Muislaam ameshambuliwa. Ukisema fulani Mwizi yeye atakuja na kuandika "tunamshambulia kwa sababu yeye ni Muislaam...." Siku hizi hata kumsoma sitaki..

Then kama hii ndio tafsiri ya UDINI then nipo tayari kuitwa mdini. Hawezi kuja mtu hapa anajaribu kuhusisha mapungufu ya kiongozi fulani na dini yake, awe mkristo ama muislamu hala mimi ninyamze eti kwa kuogopa kuitw mdini.....Kama unanijua vizuri u will never say this kwani ungeliua wazi kuwa siogopi tafsiri ya mtu pale ninaposimamia kitu ambacho naamini ni cha haki.....

Nijuavyo ni kuwa ni kweli miongoni mwa jamii yetu wapo wenye kutowaamini, kuwashambulia na kuwachukia wengine wawe viongozi ama sio, wawe waislamu ama wakristo...hili ni tatizo la kijamii ambalo kukosa uthubutu wa kulisemea ndio kumelifikisha kuanza kuwa tatizo la kitaifa ambalo naamini ni jukumu langu na wengine kusimama kulisemea, kulionya, kulikaripia whatever the price I will pay......
 
cheap popularity kupingana na wenzako? Hapana, ulikuwa ni uamuzi na niliuelezea kwenye kikao. Sikukubaliana na strategy. Nkrumah once said, one struggle many fronts. Strategy ya kutoka rais akihutubia sikukubaliana nayo na ndio mana sikwenda ukumbini kwani ningeenda nisingetoka kabisa. Nikaona bora kuji absent kuliko kutotoka wakati wenzangu wanatoka.

Kuna Mshauri alishauri ukikaa kimya itakusaidia. How many times do you need to react to issues of thousands........ use proper forum to react to sensitive issues if need be. How is your stay in Thai? Ask your mentors on how to respond to issues of this nature - they are delicate they can take you down just like that.

" SILENCE CAN NOT BE MISQUOTED"
 
unaridhika na hayo majibu? Dont ever undermine my readings of Nyerere. He was unpredictable on Biafra. Can you imagine mwalimu kuwa timu moja na Boigny wa ivory coast? Unajua hakwenda OAU Summit ya egypt iliyojadili biafra akampeleka Kawawa na kukawa moto timu ya Tanzania ikakimbia? On mwadui, tanzania had 50% shares. Makaburu waliruhusiwa kufanya biashara Tanzania wakati hapakuwa na ruksa kufanya biashara. Unakumbuka ppt zetu hata ilitajwa SA marufuku? Unasema mwl was predictable!
...hata zile simu alizokuwa anazipokea MTATIRO,JULIUS wakati wa kampeni zilikuwa very UNPREDICTABLE
 
Japo nakubaliana na wewe kuhusu mambo aliyofanya Zitto kwenye kampeni katika kusaidia chama na kusaidia wagombea wengine, ishu ni kuwa Zitto anaonekana ana-potential kubwa sana ya kuleta mageuzi tunayoyataka hapa Tz. Tatizo lake amekuwa akiwatenda wanamagezi vibaya na kusababisha watu tusimwamini kabisa. Hutumwonei tunataka arudi kwenye mstari aua aende ccm,cuf,nccr,tlp, ijulikane moja.


Una uhakika gani kuwa hao wanamageuzi hawamtendei Zitto vibaya? Kwa nini ni lazima Zitto afanye wanayofanya wanamageuzi hata kama wako wrong?


Na kwa wale wanaomwona Zitto opportunist, wanapiganaji wa kweli kwenu ni kama kina Shibuda, etc, sio maoprtunist. Huyu asingeingia CCM kama kura za maoni zingempitisha.

Acheni kukibomoa chama chenu mtandaoni, tumieni muda huu kukijenga.

Salamu kwako Rutashubanyuma.
 
aliahidiwa kigoma kuwa kama dubai. ndo maana analowanisha msimamo wa chama .hana maana

Na unadhani ahadi hii wangepewa wa mikoa mingine na sio Kigoma........No wander hata Dr Slaa akafanya kosa la kukejeli ahadi hii huku akiaahidi Treni ya masaa matatu kutoka Mwanza hadi Dar Es Salaam....Mwanza akapata kura nyingi, Kigoma ngome ya Chama chake akaanguka.....Ingawa kabla ya tamko lake hilo alikuwa akiongoza katika opinion polls zote kwa upande wa Kigoma....ofcourse na HAI pia

Kigoma nao wana haki ya kuwa na ndoto za kuwa Dubai kama wa Arusha walvyo na ndoto za kuwa Geneva......
 
Hivi ni mgombea gani wa Ubunge awe wa CCM ama Chadema aliyeshiriki katika kampeni za chama chake kwa mapana yake kama Zitto?. Hivi sio Zitto aliyetoka hadi Mtwara, Shinyanga na mikoa mingine kuwapigia kampeni wagombea wa chama chake" Hivi Mwenyekiti wake Mbowe zaidi ya zile activity tatu zilizokuwa na LIVE COVERAGE mlimuona sehemu nyingine yeyote.....Hivi Dr Slaa amewahi kwenda jimbo lolote na kutembezwa na mgombea mbunge katika kata zote kama ilivyokuwa Kigoma Kaskazini? Hivi kuna mgombea ubunge yeyote aliyetumia muda wake kuwatafutia/kufundraise fedha za uchaguzi wagombea wenzake wa ubunge na udiwani kama alivyofanya Zitto? Hivi kuna mgombea yeyote wa CHADEMA ambaye amejitolea hata kumtengenezea posters/mabango ya kampeni mgombea mwenzake yeyote kama alivyofanya Zitto kwa wagombea zaidi ya 20 na huku kwake akiwa hana uhakika hata wa fedha za kuwalipa mawakala wake??

Acheni kumuonea Zitto ama kwa kutojua ukweli au chuki zenu binafsi.......

Ilyas acha jazba brother,nafaham zitto ni Swahiba ila ndo hivyo watu wanahoji.Mwache achambue mchele na Pumba then Mwisho wa yote tutafaham nini ni nini!Zitto kajitolea mambo mengi sana ndani ya chama,hili halimfanyi kutokuwa na mapungufu,maana hakuna kimoja kinacho substitute kingine iwe baya ama jema!Baya na lijulikane baya na jema na lifahamike kuwa jema!Ukifanya mtihani ukawa wa kwanza wakati huu na ukaja kufanya mtihani ukafeli,haikufanyi kuwa wewe ulifaulu kwa sababu ulishawahi kufaulu huko nyuma!Binafsi naamini katika uhuru wa mawazo,ila naamin pamoja na kuwa mi si mwana siasa kama Zitto, Zitto aliteleza si katika hilo tu la kuripoti TBC1,bali pia nakumbuka siku kama 3 au 5 nyuma yake alishawahi kuweka post kuwa CUF hawakumpigia kura Marando kwa ushahidi wa idadi ya kula walizopiga.Kama Zitto anaamini katika maamuzi binafsi asingetakiwa kwenda kauandika katika profile yake ya facebook kwamba CUF hawakuipigia kura CDM kwa sababu ya hadhi yake na utata wa taarifa yenyewe pamoja na ukweli kuwa kitu alichokizungumza hakikuwa na Ushahidi pia lazima aamini hata CDM wengine hawakumpigia kura Marando,maana si lazima kumpigia kura marando ingawa ndio ulikuwa msimamo wa chama.Binafsi napenda nione Zitto akifanikiwa.Siamini katika "Perfection" but "completeness".Hata siku moja Zitto na binadamu mwingine yeyote hawezi kuwa Perfect,but i agree one day he can be a complete Politician.Aepuke makosa ya kuepukika,aamini ktk Team work hata kama pengine isiwe katika akili yake ila isiwe na nia mbaya kwa maslahi ya taifa.Sioni shida kama angekaa kimya na kumwacha nguruwe akapita kwa kujifanya hana mkuki'
 
Waberoya

Nafikiri tulikuwa wote kwenye sakata la kipindi kile. Nafikiri ukitulia ukatafakari yale yaliyotokea kipindi kile utagundua kabisa uamuzi alioufanya Zitto ndio uamuzi muafaka. Nafikiri unachotakiwa kufanyia uchunguzi kabla ya yote ni je ma- HARDLINE wa chadema wanapenda maendeleo ya Zitto ama move zao ni kumwangamiza?

Nionavyo mimi, Zitto maadui wake wakubwa ni hao wachadema, hawapendezwi naye kama ambavyo alivyokuwa CHACHA, KAFULILA n.k, Wenda pale Zitto yupo na wenda kaupata ubunge kwa nguvu zake akiwa ametelekezwa na chama ili amalizike. KWa mtaji huo huo move yoyote inayochukuliwa na chama lazima naye awe na move yake ya kujinasua. Nigumu kuliona hilo kama tayri una majawabu tayari yanayokuongoza.
 
mimi nilisafiri toka hedaland oslo norway had mwanza pale nyamagana

kwa lengo la kupiga kura, na niliiipigia chadema, tulikesha pale na kuomba matokeo yetu hadi wakatoa na jimbo tukachukua.

haiwezekani wewe leo upingane na chama chak......kama mlipiga kura na wengi wakashinda ugumu uko wapi?
umetuaibisha sana wana chadema huna adabu kabisa na hovyo sana wewe!
ubinafsi utakuua kaka..... kama vipi mfate kafulila kule aliko then utupishe.....

leo nakwambia ukweli kaka umetia kinyaa sana kwa hili ulilofanya...... halafu kwa nini uliongea na waandishi wa habari? unataka sifa sana wewe ....kwenda zako nccr fasta utupishe na chama chetu..


JIFUNZE ADABU NA HESHIMA...... halafu unasema jk ndo amefanya kigoma ijulikane?!!! unaona ulivyo na akili fupi wewe!! huna maana kabisa.

narudia kwa sauti ya juu.. ONDOKA CHADEMA
 
hapakuwa na kikao cha siri.

mkuu naona bado hujajifunza kitu kwa hao unao waita mentor wa ccm mbona wao huwa hawatoki kwenye media kusema kile walicho jadiliana iwe siri au sio siri hata kama hawakuafiki maamuzi mbona wanabaki kimyaa na msimamo wa chama wanaudumisha naona hujajifunza bado.
 
Una uhakika gani kuwa hao wanamageuzi hawamtendei Zitto vibaya? Kwa nini ni lazima Zitto afanye wanayofanya wanamageuzi hata kama wako wrong?


Na kwa wale wanaomwona Zitto opportunist, wanapiganaji wa kweli kwenu ni kama kina Shibuda, etc, sio maoprtunist. Huyu asingeingia CCM kama kura za maoni zingempitisha.

Acheni kukibomoa chama chenu mtandaoni, tumieni muda huu kukijenga.

Salamu kwako Rutashubanyuma.

Kwao wao Populists ndio Patriots, Wajanjawajanja ndio MAKINI.....Sishangai kutomuelewa na hata kumshuku Zitto kwani wamelewa na Siasa za master COPY .....Wanamageuzi wenye kuamini katika ESTABLISHED RULES OF THE GAME....na sio wenye uthubutu wa kuzibadilisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom