Escrow yazidi kuvimba: CHADEMA wampatia kibarua kizito Rais Kikwete kuelekea Hotuba yake kesho

Hapa hakuna wanahabari hili jukwaa la siasa.Pelekeni upuuzi wenu Tanzania daima.
sawa kabisa Hotuba ipo palepale Diamond Jubilee,
na Rais ataelewesha ni nani mweye uhalali wa pesa za ESCROW km alizalisha umeme akalipwa na alipe Kodi TRA au sasa asilipwe tena zirudishwe ziwe za umma, km hasara iwe kwao waliotupatia umeme
 
@kenonke

Hapo hakuna wa kulaumiwa. Wa kulaumiwa ni wale wanaotunza siri za ufisadi kwenye makabati yaliyoko kwenye ofisi za umma. Ofisi hizo si za kutunzia ufisadi. Zinapaswa kutunza maslahi ya wananchi. Period.

Mkuu Tumaini Makene naona post yangu imefutwa sijui kwanini Alinda na EMT waliomba zile document zilizoletwa na Kurugenzi ya Habari na kufutwa

Kama mnaamini hizi document ni za UKWELI WEWE basi chukua jukumu la kuziweka PUBLIC sisi tuliowai kuzinyakuwa kabla ya kufuta tukiweka zitaFUTWA NA kupigwa BAN
 
RAIS Jakaya Kikwete, amepanga kulinda na kutetea watuhumiwa wakuu katika ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ndani ya Benki Kuu ya Taifa (BoT), ----------- Online limeelezwa.
Taarifa kutoka ndani ya serikali na Ikulu jijini Dar es Salaam zinasema, Rais Kikwete amepanga kuwatetea kwa nguvu zake zote, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi.
“Prof. Muhongo na Maswi, hawawezi kuondoka ndani ya serikali hii. Hawa watu wanamtandao mkubwa sana ndani ya serikali na katika Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ambao unafanya kazi kubwa ya kuwatetea,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.
Amesema, “Mtu pekee ambaye anataka kutolewa kafara na ambaye kwa hakika, hakuhusika kwa namna yoyote ile na miamala iliyofanyika, ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.”
Kuvuja kwa taarifa kuwa Rais Kikwete amepanga kutetea wizi katika Akaunti ya Escrow, kumekuja siku tatu baada ya Prof. Tibaijuka kuhutubia mkutano na waandishi wa habari ambapo alieleza kusikitishwa kwake na njama za kumuhusisha katika kashfa hiyo.
Prof. Tibaijuka amekiri kupokea kiasi cha Sh. 1.6 bilioni kutoka kwa James Rugemalira, ambaye ni mmoja wa wanahisa katika kampuni ya kufua umeme wa dhaurura ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Hata hivyo, mbunge huyo wa Muleba Kusini amesema, fedha hizo hazikuwa zake; zilitolewa kama mchango kwa shule ya Sekondari ya Barbro Johansson ya jijini Dar es Salaam na Kajumulo Girls High School, iliyoko Bukoba.
Amesema, yeye aliupokea mchango huo na kuufikisha kunakohitajika. Wala hakujua kuwa fedha zilizotolewa na Rugemalira, zimetoka kwenye Akaunti ya Escrow, wala hakujua kama fedha hizo ni uharamu.
“Alichoniambia nikafungue akaunti ya kupokea fedha hizo katika benki ya Mkombozi. Nami nikafanya kama ambavyo mwenye fedha alinielekeza. Katika hili, sioni kosa langu na hivyo, siwezi kujiuzulu,” ameeleza Prof. Tibaijuka.
 
EMT

Asante Mkuu EMT kwa kunogesha mnakasha huu kwa kuweka hiyo nakala ya hukumu ya mahakama ambayo inafichua makubwa yasiyozungumzwa sana, kama ilivyosema hiyo press statement hapo juu.
Mkuu Tumaini Makene hiyo si hukumu bali ni makubaliano kati ya wahusika kwenye shauri.
 
Last edited by a moderator:
IPTL mpaka ESCROW ni higher level of deception ni mpango uliosukwa kwa ustadi mkubwa
ukiwa mjinga majinga kama Lusinde, Kisanji au Mshama huwezi kushitukia.
Kwanza JK alitengeneza tatizo bandia la umeme kisha kwa kumshirikisha Rugemalira wakaja na suluisho wakamuuzia mzee Ruksa akakubali nchi ikaingia mikataba ya kijingajinga na unajua mikataba nchi hii ni siri ya serikali, ukatengenezwa mpango wa kukusanya hela kupitia ESCROW baada ya JK kubakiza miezi michache atoke ikulu wakaamua kugawana kilichopatikana kupitia kwa yule boya wa kihindi na kesi feki ya Ruge.
Hapa nakukubalia Mkuu tena kulitafuta Kampuni hili huko Malaysia alitumwa Kigoda, (pia alikuwa mweka hazina wa CCM) JK akiwa naibu waziri wa Nishati na Mwandosya pale Nishati na Madini
sasa Watanzania wote tumeingizwa mkenge tumedhulumiwa na umeibiwa kwa kupandishiwa bei za umeme na Tarrif zake
Je baada ya kuzalisha umeme hawa wezi malipo ya madai yao ni halali? au wazirudishe fedha zote?
au JK na Chama chake na Serikali vihusihsweje?
ni hayo tu Mkuu
 
Chadema ina potosha watu kwa kutafuta umaarufu, au sijui wanataka kumuudhi Rais asifanye kazi yake, Nchi nzima iko masikio wazi kungoja atakachofanya, ni vizuri kuweka historia wazi na kwa ukweli CHAMA CHA KWANZA kupinga ufisadi huo na kutaka wote waliopokea hizo pesa wawajibishwe, ni Katibu Mkuu Kinana ndiye wakwanza kuto wito huo, Leo CDM inatafuta kila namna ya kumchafua kinana, mumeanza na Machine za Laundry, Meno ya Tembo na sasa mnataka kumuingiza kwa nguvu kwenye escrow.

CDM mnapoteza wakati , Kinana hatapunguza mwendo kukijenga chama, na tunasikitishwa sana kwani laiti Raisi angechukua uamuzi kitambo, basi ccm ingafanya vizuri zaidi kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa.

Jee napenda kuwauliza nyie washabiki wa cdm, kama kila mtu anavyojua Bilcanes inamilikiwa na Mbowe, na pale ni pahali maarufu pa watu kubeba wanawake Malaya , makuwadi ni wafanya kazi wa pale na pia panauzwa Bangi na madawa ya kulevya na wahuni wakishirikiana na wafanyikazi na walinzi wa hapo. jee tutasema Mbowe pia anahusika????????????????. Mimi ninavyo jua mbowe ni mmliki na hafaidiki na hayo maovu.

Kinana alikuwa board member Stanbic , lakini kwa muda sasa hayumo na hawezi kujihusisha na upumbavu kama huo, he is a true nationalistic and a great leader.
 
Inaelekea wafadhili wanamawasiliano ya moja kwamoja na ukawa. Inamaana ukawa wataulizwa kwanza kama wameridhika na kama hawajaridhika mbinyo uendelee. Lakini raisi wetu namwamini atawanyoa wote anaweza kuwaambia siwanyoi ila kwenye baraza la wazee ananyoa kipara
 
Wewe mpuuzi wacha kuandika story ndefu utter nonsense

nashukuru mimi mpuuzi, lakini kuna ukweli ktk hii ya wazee.

Hebu tujaribu ku-narrow down hii mission ya wizi.katika mashirika au taasisi za umma accounltable officers ktk masala ya fedha mara nyingi ni Ceo, mkurugenzi wa fedha, chief finance manager na bursar/cashier.
sasa tunachoongelea hapa ni waziri wa fedha, katibu mkuu, na governor.Matatizo yeyote ya kifedha yanapotokea hao ni wawajikaji wa kwanza, kitendo cha kuwaacha hao eti hawahusiki utaonekana wa ajabu.

sorry Waziri, katibu mkuu na governor mchoro mnaujua.
 
Kumbukeni-uraisi wangu hauna ubia na mtu-Mh Raisi

Nikiwajibishwa nchi itatikisika -Muhongo

Nijiuzulu kwa kufanikiwa kupata pesa?-Mama T

SINGASINGA ALIANGUSHA kanu-kafulila

mI NSHACHOKA-ZITTO kABWE
nITAKUWA MGENI WA NANI-mAKINDA
WAZIRI MKUU UWE MKALI-MBOWE

TUJIPIME SISI WATAZAMAJI MAANA HAWA HATUWAWEZI UTATA MTUPU.MUNGU KATUFICHA WATU WAZIMA KAWAFUNULIA WATOTO .INABIDI URUDI UTOTONI UYAELEWE HAYA
 
sijawahi kuona rais mzembe kama jk! mheshimiwa amerogwa? yaani kelele zote hivi ikulu mnajiona mna amani! mnawatengenezea maisha magumu wake zenu na watoto wenu! kweli Biblia inasema wanamacho lakini hawaoni, wanamasiokio lakini hawasiki, wana mikono lakini haifanyi kazi! jk alishaonyesha mapungufu tangia kwenye mabilion yake. pale alipokili kuwa kuna wajanja wameyala. hivi kunamjanja gani ndani ya nchi zaidi ya rais? majeshi yote yapo chini yake kitu gani kinamfanya ashindwe kuwachukulia hatua hao anaowaita wajanja? kama na yeye hashiriki ktk huo ujanja? haimgii akilini jk anahusika kwenye matukio yote.
 
Chadema ina potosha watu kwa kutafuta umaarufu, au sijui wanataka kumuudhi Rais asifanye kazi yake, Nchi nzima iko masikio wazi kungoja atakachofanya, ni vizuri kuweka historia wazi na kwa ukweli CHAMA CHA KWANZA kupinga ufisadi huo na kutaka wote waliopokea hizo pesa wawajibishwe, ni Katibu Mkuu Kinana ndiye wakwanza kuto wito huo, Leo CDM inatafuta kila namna ya kumchafua kinana, mumeanza na Machine za Laundry, Meno ya Tembo na sasa mnataka kumuingiza kwa nguvu kwenye escrow.

CDM mnapoteza wakati , Kinana hatapunguza mwendo kukijenga chama, na tunasikitishwa sana kwani laiti Raisi angechukua uamuzi kitambo, basi ccm ingafanya vizuri zaidi kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa.

Jee napenda kuwauliza nyie washabiki wa cdm, kama kila mtu anavyojua Bilcanes inamilikiwa na Mbowe, na pale ni pahali maarufu pa watu kubeba wanawake Malaya , makuwadi ni wafanya kazi wa pale na pia panauzwa Bangi na madawa ya kulevya na wahuni wakishirikiana na wafanyikazi na walinzi wa hapo. jee tutasema Mbowe pia anahusika????????????????. Mimi ninavyo jua mbowe ni mmliki na hafaidiki na hayo maovu.

Kinana alikuwa board member Stanbic , lakini kwa muda sasa hayumo na hawezi kujihusisha na upumbavu kama huo, he is a true nationalistic and a great leader.

hapo kwenye nyekundu kama mwendo wewnyewe wa kujenga chama ndio huo amabao matokeo kwa ccm kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni mabovu toka kuanzishwa kwake mwa 1977 basi tunaomba aongeze spidi ili mwakani ccm ipotee kabisa hapa nchini.
 
Ifahamike tu wazi kuwa aliyetajwa hapo kama Albert Marwa ameoa mtoto wa Kikwete. Kwa maneno mengine ni mkwewe wa Kikwete.
ni mtoto wa kufikia wa General Marwa alimuokota kule uganda wakati wa vita ya uganda baada ya mama yake kumuacha kwake.... sio mtz ni mganda ila kwa sbb alikuja mdogo kakulia hapa ni mtz kwa sasa.....
 
hapo kwenye nyekundu kama mwendo wewnyewe wa kujenga chama ndio huo amabao matokeo kwa ccm kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni mabovu toka kuanzishwa kwake mwa 1977 basi tunaomba aongeze spidi ili mwakani ccm ipotee kabisa hapa nchini.

Ccm sawa na wale wajenzi wa mnara wa Babeli.
 
Back
Top Bottom