Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
- Thread starter
- #21
Mkuu unatisha,
Mariam wangu unanikumbusha Tanga.
Asante mkuu....Karibu kwa kuchangia mkuu,si unajua ya 'kale ni dhahabu'...............lete mashairi mkuu
Mkuu unatisha,
Mariam wangu unanikumbusha Tanga.
naomba mwenye mashairi ya wimbo wa milima ya kwetu atuwekee hapa au kama kuna mp3 yake
.......umekuwa kama helkopta ndege isiyochagua mahala pakutua eeh.......
na kama kuna mwenye wimbo washakaza I na II atuwekee hapa maana sijapata hata mp3 zake
Nasikitika
Nasikitika yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema....mmmmmmmmmmm
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Ningeelewa walimwengu ni wachina,mimi nisingekubali kuzaliwa,nsingekubali kuzaliwa ee,lakini nimedanganyika,wakati nalikuwa mdogo,nalikuwa nabebwa,nalikuwa nabembelezwa,nalikuwa nalishwa ee,sikutegemea kama leo nitakuwa hivi,eeeeeeee...
Ulimwengu uwanja wa mapambano,kila mtu kujitafutia,kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida....
Ilimwengu umejaa maovu,walimwengu tumezingirwa,magonjwa chungu nzima,hata ukijifanya wewe mlevi wa Gongo jirani yako anawagombanisha mke wako na watoto wako anawapika bila sababu kwa tabu,hata ukijifanya wewe mpenda mabibi mabwana hamsini lakini ujihadhari na Ukimwi utapata ukavu kwa tabu......
Ulimwengu imani imekwisha,imani imekwisha,imani imekwisha,watu wameota mapembe,hata watoto zetu heshima hawana tena,imani imekwisha,imani imekwisha,imani imekwisha....
Ulimwengu hakuna raha,hata ukiwa na mapesa ulimwenguni,porini hawakujui,mnyama hakujui,nyoka hakunujui,hasa mbu hakujui,hata ukiwa mheshimiwa ulimwenguni,majani haikujui,porini haikujui...
Ulimwengu uwanja wa mapambano,kila mtu kujitafutia,kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida....
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.....
Nasikitika yeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema
Nasikitika eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee..............Maisha yamenijia magumu,nashindwa la kusema........mmmmm........eeeeeeee
Nasikitika eeeee....kula kwa tabu,kuvaa kwa tabu,kila kitu kwa shida.......eeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,mmmmmmmmmmmmmmm
Muziki Asili yake wapi
Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.
Muziki alivyo na nguvu ulimwenguni kote,
Hata makanisani wanaimba kwaya kwa kumuomba Mungu,kumuabudu Mungu,kwa kumsifu Mungu,
Hata kukiwa sherehe za serikali,mbele ya Mwenyekiti kuhutubia,ni Muziki unaanza kuwakusanya watu;
Kumbuka Paulo na Sila waliimba gerezani Mungu amewasikia,
Kumbuka Mussa aliimba Muziki wa aina yake,kuwakomboa wana wa Israel waliopo utumwani katika nchi ya Misri..
Kukiwa na sherehe utaimba nyimbo za furaha,kukiwa na tabu utaimba nyimbo za masikitiko;
Ukifa leo utapelekwa kaburini na nyimbo za maombolezo;
Ni mzuiki pekee ulio na nguvu,utawakusanya wabaya na wazurimsiku ya mwisho Mungu akitoa hukumu.
Muziki sio uhuni,kama muziki ni uhuni kwa nini unanunua kaseti;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unaomba nyimbo redioni;
Kama muziki ni uhuni kwa nini kwa nini unanunua rekodi;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unacheza muziki weeee;
Kama muziki ni uhuni kwa nini unafanya top ten show...
Kumbuka siku ya mwisho ikifika,kutakuwa mlio mmoja wa parapanda utawakusanya wateule wote,
walioteuliwa katika pembe nne za dunia siku ya mwisho mungu akitoa hukumu,hukumu,hukumu.
Hata kwa Mungu malaika wanaimba oooooooooooooooooooo
Muziki asili yake wapi eeeeee,Muziki ni wa nani eeeeeeeeeeeee,
Muziki hakuna mwenyewe,Muziki ni mwito,
Muziki ni fundisho,Muzi maombolezo kilio
Usinione nikiimba,ukadhani ninayo furaha,kumbe ninayo huzuni moyoni.
Nalilia mtoto
Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2
Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2
Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,
Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,
Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto
Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!
Mola Mola, Mola eeeh....
Mariamu
ataka yote akosa yote
apita ahangaika asijue la kufanya ... asijue la kufanya
mshika mawili yote yamponyoka
apita akebakeba asijiue la kujitetea
mmmhhh mapenzi yawaka moto
naitika nilikukosea sasa nihurumie
si ninafikiri zaidi kuliko wewe
nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo
nilalapo nakuota mchana kutwa sili
moyo wanichechemea mwili damu hukauka
penzii eh ..... mmmh penzi eh x 2
nasumbuka kwako unionavyo moyo wangu
wewe ndio dawa yangu
Maraimu wangu
Tanga mbali
waja leo wondoka leoo
waja leo warudi leo
Mariamu bibi
mwenzenu sina pumuzi kujizuwia siwezi ohhh
mwanaume barabara kazi ya mume kwa mke
neno ya mke chumvi kwa mumewe
neno ya muke kachumbari kwa mumewe
penzi oh penzi likamung'uma he heh heh
likamung'uma hen heh heh .... mmhhhh
mdundiko, mdundiko ........ waaaaaa
mdundiko ...... waaaa
Tembea Ujionee
Natembea popote unapokwenda,
iwe usiku ama mchana mbele yetu kuna mwanga wa maisha,
Natembea popote lakini wajua pa kula pa kulala,
maisha ya mtu tumefautiana na tumezaliwa mahali mbali mbali,
Mtu anaweza kufanana na nduguye sio shangazi wala mjomba,
labda pengine rafiki yake,
mkifanana kwa sura mwendo tofauti,
mkifanana kwa mwendo sura tofauti,
mawazo mbali mbali,
tabia mbali mbali,
mavalio mbali mbali,
Tumefikiria kuimba hivi kutokana na kutembea sehemu mbali mbali,
kutofautisha tabia na vitendo vya huyu vipi na kile vipi,
huyu bwana vipi na yule bibi vipi,
Hii shati vipi na suruwali vipi,
hii soksi vipi na kiatu vipi,
Kila mtu na kila sehemu vinatofautiana,
hauwezi kufananisha Morogoro na Darisalama,
tembea ujionee usingoje kuambiwa,
(chorus ya akina Skassy kasambaula na wenzake)
Tembea ujionee usingoje kuambiwa,
Duniani kuna mengi yote yanakusubiri x2
(Dr Remmy)
Tembea mama tembea bibi ii,
Tembea uone mambo,
tembea ushangae,
tembea upande mabasi,
tembea tembea tembea mama tembea bibi oo x2
oo tembea oo mama,
tembea oo mama
(oo tembea bibi oo)
tembea oo bibi oo
(oo tembea uone mambo)
tembea uone mambo
embea oo mama
Najaribu tu mkuu, kuweka lyrics na muziki... Umetukumbusha mbali mkuu thanx very much....Tupo pamoja kaka.Ubarikiwe sana mkuu wangu X-PASTER
Lete vitu zaidi