Enzi Hizo S02

Salama wakuu.....Leo tupitiepitie baadhi ya nyimbo za Nguza Vicking,kwa kuanzia tunze na wimbo wa Kadiri ka Nsimba

Uaminifu wa mapendo ee naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,
Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga

Nilikutimizia mahitaji yako ee ee mama,nilikulindia heshima yako ee ee mama,

Ooooo nikupe nini sasa we mama,Ooooo nifanye nini sasa we mama,
Ooooo sasa tuko wapi oooo,Kadiri ka Nsimba unieleze ukweli wako mama...

Oooooo nikupe nini sasa we mama,Ooooooo nifanye nini sasa we mama,
Oooooo sasa tuko wapi oooo,Kadiri ka Nsimba unieleze ukweli wako mama...

Kwa mara ya kwanza nimekuona,nimekusamehe,mara ya pili tena umenidanganya eti mjomba wako,

Oooo Kadiri tumetoka mbali mimi na wewe,Oooooo Kadiri tumetoka mbali mimi na wewe,

Ooooo nikupe nini sasa we mama,Ooooo nifanye nini sasa we mama,
Ooooo sasa tuko wapi oooo,Kadiri ka Nsimba unieleze ukweli wako mama...

Oooooo nikupe nini sasa we mama,Ooooooo nifanye nini sasa we mama,
Oooooo sasa tuko wapi oooo,Kadiri ka Nsimba unieleze ukweli wako mama...

Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga
Uaminifu wangu mama naonekana zoba,uminifu wangu mie naonekana mjinga,
nifanye nini sasa sheri sema nijue mama,nikupe nini sasa mie sema nijue mama,
Mama Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,mama Kadiri ka Nsimba naonekana zoba

Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,
Iringa Chunya Mwanza kote nimekwenda,Iringa Chunya Kigoma kote nimefika,
nifanye nini sasa sheri mapenzi yangu kwako ni bure,nikupe nini sasa mie mapenzi yangu kwako ni bure,
Mama Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,mama Kadiri ka Nsimba naonekana *****

Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,
Iringa Chunya Tangaa kote nimekwenda,Iringa Chunya Arusha kote nimefika,
nifanye nini sasa sheri mapenzi yangu kwako ni bure,nikupe nini sasa mie mapenzi yangu kwako ni bure,
Mama Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,mama Kadiri ka Nsimba naonekana *****

Kadiri ka Nsimba (Mama Kadiri) naonekana mjinga,Kadiri ka Nsimba naonekana mjinga,

E kanyungunyungu nyungulula,E kanyungunyungu e nyungulula,

Kisha kuna huu hapa mwingine wa Nguza Vicking

Karubandika toleo la pili(Remix)

Kama wewe umenipenda kwa nini kunidanganya bwana wee,
Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe,

Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna ee,
Unazurura mchana kutwa ee,kupita kurandaranda mitaani,

Kumbe hukuwa na uwezo wa kunioa ila kuniharibia maisha,
Heri unaimbie ukweli ulivyo kuliko kunidanganya,

Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa

Bridge: (Nguza) Karubandika..........Kumbe wewe tapeli

Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaa,
Nikuelewe vipi ee babu ee unaminifu wako uko wapi ee,babaaaaaaaaaaaa

Usinione ***** baba,usinione ***** baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

(Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....

Usinione ***** baba(Karubandika yoo),usinione ***** baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

(Nguza); Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia,akiingia kwenye bia kazi yake kuomba baa,hana hata aibu ee,sigara pia anaomba,hana hata aibu wee na supu pia anabomu,mitaani na kwenye masoko kujitangazia kuwa yeye ni mkurugenzi wa kampuni fulani,kumbe sio hivyo..

Usinione ***** baba(Karubandika aaa),usinione ***** baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....

(Nguza); Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie,kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka,pa kulala hana analala kwenye stendi ya basi,pa kulala hana anakesha kwenye kituo cha City,Karubandika yoyo,acha vituko we baba....

Usinione ***** baba(Karubandika aaa),usinione ***** baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
Usinione ***** baba,usinione ***** baba,kwa kukubali wito wako Karubandika,kwa kukubali wito wako Karubandika ee,
Hayo yote ni matatizo ya dunia baba,hayo yote ni matatizo ya dunia baba....
 
Halafu pia kuna huu pia wa Nguza Vicking,wimbo huu kauimba kwa kushirikiana na Issa Nundu na Makumbule Lulembo 'Parash'......Hakika ya kale ni dhahabu wakuu wangu,dah...

Ufitina(Sumu ya mapenzi)

Ufitina na upelelezi ni sumu ya mapenzi,

Mimi kupendwa na yeye,nyinyi mwakerwa na nini,
Tumependana wawili bila nyinyi kujua,
Sasa mwaona mwaanza kuleta matatizo,
Mimi kupendwa na yeye,nyinyi mwakerwa na nini

Yeye kanipenda nami nampenda,nyinyi mwakerwa na nini,nyinyi mwakerwa na nini eeee

Nasi twazidi kuimarisha mapenzi yetu,
Dunia tumekuja wawili wawili,
Kusaidiana ndiyo raha ya dunia
Nyinyi mwakerwa na nini yeyeee

Yeye kanipenda nami nampenda,nyinyi mwakerwa na nini,nyinyi mwakerwa na nini eeee
Yeye kanipenda nami nampenda,nyinyi mwakerwa na nini,nyinyi mwakerwa na nini eeee

Uuuuuu.......uuuuu......uuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Habari za leo wakuu...Ni wikiend nyingine tena....Leo ngoja tumuangalie Le Supreme Hayati Freddy Ndala Kasheba akiwa na kundi lake la ZAITA MUSICA wana Zuke(Zuke) Muselebende.Tuanze na kibao hiki:

Nimlilie nani........Hii ni remix aliyoitoa mwaka 2001.......I love this song jamani,hasa lile gitaa la solo linavyokung'utwa....dah...

Nimlilie nani jamani anipe mawazo,
Nimpende nani mie wangu anipende nami,
Kila ninaye mpenda mama yangu hampendi,
Yeyote anayenipenda baba yangu hamtaki,
Nikikaa nyumbani nakandamizwaza na maneno,
Eti wenzangu wameolewa mimi bado niko ndani,
Nikipunga hewa jioni naitwa mimi jobless,
Sielewi sielewi hawa kweli ni wazazi wangu auu si wangu....

Bridge..

Jibu nitapata wapi jibu litoke wapi,anuani yangu nawaambieni jina langu ni shida Posta moja mbili tatu Temeke mtaa wa matatizo,namba moja kwenye kona nisaidieni jamani ee eee

Mikono juu,mikono juu,mikono juu.........Operesheni Kilombero kata miwa kata.....kata...kata..kata....kata....kata

Wewe mtoto wa kike(enhee) acha umbea mbea,wewe mtoto wa kike(enhee) acha umbea mbea,wewe mtoto wa kike(enhee) acha umbea mbeaaaaaaaaaaaaaa

Ntakusemea,ntakusemea,ntakusemeaa......Sio siri....Sema basi

Zuke zuke zuke Muselebende......Muselebende
 
Marashi ya Pemba

Alfajiri upepo wa bahari umenukia,nitaona nyota ya kanda ya mashariki,
Kuishi visiwani mama kuna utamu wake,Unguja Pemba Zanzibar Visiwa vya kwetu,
Siku nitafika Pemba binti Sultan Khalfani, siku nitafika Pemba binti Sultan Khalfani,
Siku nitafika Pemba binti Sultani Khalfani,nitembeze sehemu zote hadi mwisho,
Kuishi visiwani mama kuna utamu wake,Unguja Pemba Zanzibar Visiwa vya kwetu eeee.

Marashi ya Pembaaa.....Zanzibar

Wallah sitabaki naenda Pemba ndege inaruka, wallah sitabaki naenda Pemba ndege inaruka,
Nasikia ni kuzuri,jioni kuna upepo,eti unanukia marashi ya karafuu,
Nipae angani nikatishe bahari,juu kwa juu nione halafu nitue Pemba,marashi nipokee Pemba oo Pembaa.

Nasikia ni kuzuri,jioni kuna upepo,eti unanukia marashi ya karafuu
Bridge....

Nasikia ni kuzuri,jioni kuna upepo,eti unanukia marashi ya karafuu
 
Kesi ya Khanga(Monica)-ZAITA Musica

Mama nipe nauli nikamfuate Monika ee,amekimbilia Zambia na treni ya mizigo ee,kisa cha kukimbia madeni yamemzidi doti kumi za khanga alizokopa hajalipa ee,anatafutwa na Polisi popote hapatikani,na mimi rafiki yake nipo nje kwa mdhamana ee,nililala rumande siku mbili kituoni,usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha ee

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh

Mwanaidi

Nimetokea kumpenda binti Mwanaidi

nimeridhishwa na tabia yake
nikaamua tufunge nae pingu za maisha
urithi ulioacha baba niliutumia
ili kuneemesha ukoo wake
nilianza kuuza mifugo
hatimaye shamba
ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh

baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi
..... .. kuwa yeye hanitaki tena
tena hawezi kuolewa na mimi

(wote)
mimi najuta eh najuta mama
gharama nilizogharamia
ameona bure
sijui la kufanya .. nasikitika oh
sababu yako ....... Mwanaidi x 3

Mkuu umenikumbusha mbali sana, enzi hizo niko primary school! Ila kumbu kumbu yangu inanionyesha kuwa huu wimbo (siku hizi wanasema nyimbo hii), ulipigwa na bendi iliyoitwa ORCHESTRA TOMA TOMA na mtindo wao wa TAMBA TAMBA, na si DR> REMMY! Ni wakati ule Kasaloo Kyanga na nduguye Kyanga Songa wametokea Orchestra Matimila. Inasemekana ulikuwa kijembe kwa DR. pamoja na wimbo mwingine sikumbuki uliitwaje lakini ulikuwa na maneno kama.....Undugu ni taka ya ngozi hata usafishe vipi hautaweza kusafishika! anayekumbuka mashairi ya nyimbo hizi atuwekee!!
 
Salama wakuu?......Naona kimya sana,mmeamua kuupotezea muziki wetu mtamu wa Enzi hizo....

Haya ni weekend nyingine tena,Ijumaa ya leo naomba tuwaangalie wana Orchestra Marquis Original wana Zembwela na baadae Sendema....Kundi hili lilikuwa linaundwa na wakali kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Audax na wakali wengine kibao.....Hawa jamaa walikuwa ni noma wakuu.......

Kwa leo tuanze kuangalia kitu Ngalula utunzi wake 'Mutoto Muzuri' Tshimanga Kalala Assosa.....Wanamuziki walioshiriki kuimba na kupiga vifaa/vyombo vya wimbo huu ni hawa wafuatao(I stand to be corrected wakuu maana ni muda umepita)...

Waimbaji: Tshimanga Kalala Assosa, Mukumbule Lulembo 'Parash', Kabeya Badu, Mutombo Audax, na Issa Nundu,
Gitaa la solo lilipigwa na 'Vumbi' Dekula Kahanga na second solo alipiga Mbwana Kocks,
Gitaa la Rhythm alipiga William Maselenge,
Gitaa la bass alipiga Banza Mchafu,
Kinanda alipiga Mbuya Makonga 'Adios',
Trumpet zilipulizwa na Kaumba Kalemba akishirikiana na Ngoyi Mubenga,
Saxaphone zilipulizwa na Mukuna Roy akishirikiana na Bery Kankonde,
Tumba zilipigwa na Seif Said,
Drums zilicharazwa na Matei Joseph.

Tuuangalie wimbo wenyewe wa Ngalula sasa(I like the song wakuu wangu):

Kinachonifanya nishindwe kuamua ee mama ee....ee najua mwenyewe,ee mama...
Pamoja na vituko vyake mama ee,bado namuhitaji masihani ee,ee najua ee Ngalula,ee nimekuzoea ee,shanganga Ngalula,ananielewa vizuri mama ee kuliko mtu yeyote ee mama,shida na raha zangu Ngalula anazielewa,jamani Ngalula nimekusamehe mama,jamani Ngalula nitamvumilia nione mwisho wake,ee mama aa,ee mama aa........aaaaaaaaa Vumbi......Kahanga.

Kinachonifanya nishindwe kuamua ee mama ee....ee najua mwenyewe,ee mama...
Pamoja na vituko vyake mama ee,bado namuhitaji masihani ee,ee najua ee Ngalula,ee nimekuzoea ee,shanganga Ngalula,ananielewa vizuri mama ee kuliko mtu yeyote ee mama,shida na raha zangu Ngalula anazielewa,jamani Ngalula nimekusamehe mama,jamani Ngalula nitamvumilia nione mwisho wake,ee mama aa,ee mama aa.

Bridge

Ngalula mama,Ngalula wangu mama ee,Ngalula mama,ziba masikio,
Ngalula mama,Ngalula wangu mama ee,ni maji ya moto mama,yatapoa mama.

Yeeeeeeeee,ewalaaaaaaa,
Yeeeeeeeee,ewalaaaaaaa,
Yeeeeeeeee,ewalaaaaaaa

Zembwela.....Zembwela....Vumbi......Vumbi.....Vumb i.....Sendema,Sendema.....Vumbi

Vumbi.....Vumbi.....Sendema,Sendema.....Vumbi
 
Last edited by a moderator:
Sasa tuangalie kitu Makumbele namba 1

Makumbele nimevumilia mengi,sijakutendea kosa mpenzi wee,
Nimevumilia mengi mpenzi wangu baba watoto Makumbele,

Lakini leo,nimefika mwisho,kwa kweli mpenzi si kawaida yangu,

Nitarudi kwa baba na mama mawazo yangu yote ni kwa watoto Makumbele,
Mazoea pia yana tabu yake,nitajitahidi mpenzi nitayasahau,mazoea pia yana tabu yake,nitajitahidi mpenzi nitayasahau.

Rudi ee rudi mama watoto,umetoroka nyumbani bila taarifa yoyote mama,

Kama nilikukosea ungesubiri mpenzi ee,kma nilikukosea naomba msamaha,

.................Yaaaaaaaaaa...........Zembwelaaaa aaaaa
.................Yaaaaaaaaaa...........Zembwelaaaa aaaaa
.................Yaaaaaaaaaa...........Zembwelaaaa aaaaa
 
Last edited by a moderator:
Kwa leo naomba nimalizie na kitu Mpenzi Luta utunzi wake Mutombo Audax

Mpenzi Luta nasikitika Sheri ee,yoyoyo kuishi tena na wewe,
Mama wee,vituko vyako vimezidi,vimenichosha ooh mpenzi,
Nashindwa hata la kufanya,nilikuwa nikikuonya hukutaka kunisikia,
Najuta,yoyoyoyooo,kuishi na wewe,masikini mie mamaa,kwa kweli sina raha....

Mpenzi Luta nasikitika Sheri ee,yoyoyo kuishi tena na wewe,
Mama yoo,vituko vyako vimezidi,vimenichosha ooh mpenzi,
Nashindwa hata la kufanya,nilikuwa nikikuonya hukutaka kunisikia,
Najuta,yoyoyoyooo,kuishi na wewe,masikini mie mamaa,kwa kweli sina raha....

Sasa umeipatapata hiyoo mama Luta ee,tizama sasa maisha yako,yamebadilika,
Ubishi wako mpenzi wangu ukweli umekuponza,hukutaka kusikia cha mume sasa yamekukuta,
Dunia ya leo Luta,nenda polepole.

Luta eeeeeeeeeee mpenzi wangu maaaaaaaaaa
Luta eeeeeeeeeee mpenzi wangu maaaaaaaaaa
Luta eeeeeeeeeee mpenzi wangu maaaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,habari za siku ....Leo naomba tuwaangalie Vijana Jazz Band wana Air Pambamoto awamu ya pili kwa vibao vyake Maria(Hemed Maneti), V.I.P(Jerry Nashon 'Dudumizi'), Aza(Hemed Maneti) pamoja na Penzi haligawanyiki namba 2/Wifi zangu(Kida Waziri)........Pia tutamuangalia hayati Nico Zengekala akiwa na JUWATA Jazz Band na nyimbo zake Solemba na Jacky......

Tuanze na Vijana Jazz Band na kitu chao Maria...

Maria ee...........Mere....Sikiliza miziki ya awamu ya pili Maria,
Inavyolalamika juu yako,sina raha Maria,wala sitamani kula Maria,
Ngano anasafiri Tanga Moshi Arusha Sumbawanga,nakufikiria wewe Maria,
Sijapenda namna hii wala sitopenda mpaka siku ya kufa........hahaaaaaa....
Maria eeeeeee.............adios

Bridge

Kwa kweli sasa nimenasa,sina ujanja eeee,sina ujanja eeee,
Kupenda sawa na ajali haina kinga eeeee,haina kinga eeee,

Nilivyomhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliwe,
Na wala sitopenda mpaka nife mpaka nife mama Mary ooooh,
Nilivyomhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliwe eeeeeh,
Na wala sitopenda mpaka nife mpaka nife mama Mary ooooh,

Kiitikio;
Nasononeka aaaa mamaaa,nasononeka eeeeeee,nasononeka aaaa mamaa,nasononeka eeeeee,
Ninateseka aaaa mamaaa,ninateseka eeeeee,ninateseka aaaa mamaa,ninateseka eeeeeee,
Aaaaa nimezama kwenye dimbwi oooo la mapenzi,aaaa nimezama kwenye dimbwi oooo la mapenzi,

Ayayaya Maria wangu,ayayaya Maria wangu,ayayaya ooo Maria,ayayaya ooo Mariaaaaa

(Maneti) Ni wewe Maria,Maria wangu,ni wewe wakufa na kuzikana,hakuna mwingine zaidi yako,angalia Pendo langu kwako ooo,utakuwa
wa milele Maria aaa,nakuomba ulitunze Pendo oooo,ni wewe Maria,Maria wangu ayayaaa

Ayayaya Maria wangu,ayayaya Maria wangu,ayayaya ooo Maria,ayayaya ooo Mariaaaaa

(Maneti) Ni wewe Maria wa kunisibu,ni wewe wa kufa na kuzikana,hakuna mwingine zaidi yako,angalia Pendo langu kwako ooo,akili
zimeniruka Maneti iii,nakuomba ulitunze Pendo oooo,ni wewe Maria,Maria wangu ayayaaa.

Ayayaya Maria wangu(oooo Maria mama),ayayaya Maria wangu(oooo Maria wangu),ayayaya ooo Maria(I love you),ayayaya ooo Mariaaaaa(awamu ya pili)

Ayayaya Maria wangu,ayayaya Maria wangu,ayayaya Maria wangu,ayayaya Maria wanguuuuuuuuuuu
 
Aza(Hemed Maneti)

Aza ee umelikatili pendo langu,(Maneti) Aza Aza mbona nilikwisha kuamini,ahadi ya kwetu,ahadi ya ndoa vipi sasa Aza eeh

Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo Azamela naumia(rudia tena)

Barua yako Aza eeh ilinishangaza hasa ulipoeleza umevunja mipango ya ndoa,lakini Aza ni kipi kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

Ningelikwisha oa toka siku za nyuma,lakini ilibidi nisubiri ahadi,umalizie kozi,ya masomo Tabora

Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee,Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee

(Maneti)Matarajio yangu Aza ee,ni kushi pamoja vipi leo Aza ee umenigeuka

(Maneti)Aza wangu mama ee unanishangaza Aza ee,vip leo Aza ee umenigeuka

Penzi haligawanyiki namba 2(Wifi zangu)-Kida Waziri

(Wote) Vituko na matusi ndani,matusi na maneno nyumbani iii
Vituko na matusi ndani,matusi na maneno nyumbani iii

Kwa kweli ni jambo la kushangaza mtu na wifize kugombana aaa,
Tunachogombea sikijui,hivyo yanibidi niyavumilie mimi

Pengine ni mavazi jamani,pengine jumamosi tunavyotoka,pengine ni mavazi jamani,pengine jumamosi tunavyotoka,
Lakini jamani yakizidi,itanibidi mimi niondoke eee,sababu ni kwamba sipendelei na wifi zangu tugombane eeee
Lakini jamani yakizidi,itanibidi mimi niondoke eee,sababu ni kwamba sipendelei na wifi zangu tugombane jamani eeee

(Kida Waziri): Kuwasema naogopa,kwani nitagombanisha,wifi zangu mna mambo,mambo yenu ya ajabu,
Jamani nifanye nifanye nini oooo nifanye nini,jamani nifanye nini ooo nifanye nini.

(Wote): Naelewa mazoea aa,yana tabu lakini nitajitahidi kusahau,naelewa mazoea aa,yana tabu lakini nitajitahidi kusahau.

(Kida Waziri): Kwanza mngejiuliza,kipi ananipendea(Maneti nacheka-hahaaaa),mnadhani ni miti shamba,na mapenzi hayana dawa,
Jamani nifanye nifanye nini oooo nifanye nini,jamani nifanye nini ooo nifanye nini.

(Wote): Naelewa mazoea aa,yana tabu lakini nitajitahidi kusahau,naelewa mazoea aa,yana tabu lakini nitajitahidi kusahau.

Bridge

Kida Waziri: Aaaah wifi yangu angalieni,nitamuacha kaka yenu kwenye mataa.....itampa shida
 
V.I.P-Jerry Nashon 'Dudumizi"

(Wote): Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo,

(Dudumizi): Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe VIP,
Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,VIP
Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa,na kisirani cha kufokewa na boss,
Nahitaji VIP wa kunibembeleza,nakutaka wewe mama,unibembeleze,
Si kwa maneno ila kunitomasatomasa,kwa mikono yako laini yenye bangili,
Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP).

Unipe busu mwanana la kunipumbaza wee (VIP)

Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,
Ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo.

Dudumizi: VIP sogea karibu,ubipe busu mwanana mama

(Wote): Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka.
Binadamu hanunuliwi kama nguoo VIP,ungekuwa Dukani ningekununua nikuweke ndani,lakini nikikununua bila mapenzi yako
Utanitoroka

Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP,
Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwako,kwa uzuri ulionao VIP
Natamani penzi live sio penzi la ndotoni,nakuomba uwe wangu VIP,
Tafadhali nakusihi, ili niondokane na ndoto za mapenzi.

Tafadhali nakusihi, maaa mamaa,maaa....maaa yoooo,maa mamamaaaaaaaaaaaaaaa,

Dudumizi: Ukinikubali VIP,mimi niko tayari,kubadili dini,
Ukinikubaliii VIP mimi niko tayari,kubadili dini,
Hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba)
nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa

Ukinikubalii VIP,mimi niko tayari kubadili dini,
Ukinikubalii VIP,nitatoa mahaliii ya mbuzi saba,
Hata kama sina VIP,nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe na wewe
sambamba.

Wimbo huu ndio ulibeba jina la albamu ya VIP ambayo ilikuwa na nyimbo kama Mfitini(John Kitime),Thereza(Jerry Nashon),Mama Chichi(Suleiman Mbwembwe) na Bahari imechafuka(Benno Villa Anthony),

Waimbaji katika albamu hii walikuwa ni Jerry Nashon,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Suleiman Mbwembwe,Said Hamis 'Misukosuko' na Rahma Shally.

Wapiga magitaa walikuwa ni Shabani Yohana 'Wanted'-Solo,Shabani Dogodogo-second solo,Aggrey Ndumbalo-Rhythm na Bakari Semhando-Bass.

Drums-Ally Jamwaka

Kinanda-Mhando
 
Jacky-Nico Zengekala-JUWATA Jazz Band

Mtoto Jackiee,mtoto wa Nirobi
Ingawa ni mara ya kwanza mimi nawe Jackiee
Tulipokutana palee Kampala kwenda Nairobi
Tulifurahiana sana kama tuliishi mwaka
Tabia yako njema kweli sitoisahau.

Mtotoo Jackie,mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi ukielekea Nairobi nyumbani eeh
Lakini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi,ukielekea Nairobi nyumbani eeh
LAkini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Kiitikio:

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau lakini nashindwa
Hasa ni ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Nimejaribu kukusahau lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua eeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Sauti yako nyororo inaniua sana na mwendo wako wa maringo unanikondesha mamaaah,ayoleli mwanamama nakuwinda sana Jackie yeyeyeeeh mwanamamaah aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Mvumilivu hula mbivu,Jacki yeyeeeh,mvumilivu hula mbivu Jackie yeyeeeh
Jaribu kuvumilia yeeh tutaonana mamaah kama sio Kampala ni Tanzania mamaa
Jackie yeyeyeeh mwanamama aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Nitakuja Nairobi eeh nikuone mamaah
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Tutafurahi pamoja mi na wewe mama yeeh
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Jackie yeyeyeeh Maneno sema na yeye
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
 
Solemba-Nico Zengekala& JUWATA Jazz Band

Solemba solemba solemba aaaaaaaaaah

Sitakuwa nikifika nyumbani kwako,aibu nilopata ni kubwa sana,
Ahadi nilopewa ilivunjwa oooh ooooh hata bila kosa,
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi oooh ooh na dharau tele,

Ungenieleza ukweli Solemba,kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi oooh ambayo si ya kweli,

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Ulinikana mbele za watu ati hunifahamu,
Ndugu zako na marafiki walianza kutoka nje,
Waliponiona ni mimi,walishangaa sana mama,
Mbona hivyo solemba mama eee

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Nilikuuliza mbona ulinitendea hivyo Solemba,
Ulisema mimi hujipendekeza kwako tena sana,
Na kuwa hunipendi,nakusumbua bure mamaa,
Mola yupo Solemba,Eloi yupo mamaa.

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba,Sababu ya kukungoja wewe
Kumbe ulikuwa ndani,unachungulia dirishani,
Huna huruma Solemba,I shall never forget you mamaa,

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Sikutaki tena,sina haja nawe,
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,nimeshituka solemba.

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba

Zengekala: Lalala lalala lalala lalalalala
Nimeshapata mwingine anayenipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakayembabaisha kama mimi,
Nimeshituka Solemba,lololo lolololo mama lo

(Wote): Nilikupenda kimapenzi Solemba ee,Ila dharau uliweka mbele Solemba
 
Ogopa Tapeli-Vijana Jazz utunzi wake hayati Adam Bakari 'Sauti ya zege'

Adam Bakari: Ogopa Tapeli.......Vipi Vwewe bwana mangushi naona umechanganyikiwa.
Wote: Yaliyonikuta mwenzangu,ni mambo makubwa
Adam Bakari: Vipi Vwewe bwana mangushi naona umechanganyikiwa.
Wote: Yaliyonikuta mwenzangu,ni mambo makubwa

Adam Bakari: Hata duka umelifunga,hatuelewi sababu
Wote: Yaliyonikuta mwenzangu,nitakueleza

Wote: Natamani kunywa sumu au hata kujinyonga ee bwana ee,nimechukuliwa pesa zangu....milioni mili,nimeuziwa nyumba hati zake
kumbe za bandia.
Natamani kunywa sumu au hata kujinyonga ee bwana ee,nimechukuliwa pesa zangu....milioni mili,nimeuziwa nyumba hati zake
kumbe za bandia

Kiitikio: Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai wanaitwa matapeli ee,wanaitwa matapeli ee
Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai(ni walaghai ee) wanaitwa matapeli ee(ee wanaitwa tapeli baba),
wanaitwa matapeli ee.

Eddy Sheggy: Watu hao wameenea sana kila pembe hapa mjini kazi yao kuibia watu jina lao matapeli,

Kiitikio: Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai wanaitwa matapeli ee,wanaitwa matapeli ee
Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai(ni walaghai ee) wanaitwa matapeli ee(ee wanaitwa tapeli baba),
wanaitwa matapeli ee.

Eddy Sheegy: Huuzia watu mashamba,majumba hata mashamba hivyo vyote ni vya bandia ogopa sana tapeli,

Kiitikio: Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai wanaitwa matapeli ee,wanaitwa matapeli ee
Bwana Mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai(ni walaghai ee) wanaitwa matapeli ee(ee wanaitwa tapeli baba),
wanaitwa matapeli ee.

Kibwagizo: Nawe nami,bara mpaka pwani,pambamoto,shambuliaaaaa,
Nawe nami,bara mpaka pwani,pambamoto,shambuliaaaaa,
Nawe nami,bara mpaka pwani,pambamoto,shambuliaaaaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom