Eng Stella Manyanya: CHADEMA Wanahusika na mgomo wa madaktari; amfananisha Ulimboka na Hitler

Mwenyekiti kituko.leo nimsikitishwa na uendeshaji wa bunge....mbayaaa
 
Something must be done................hasira ninayosikia right now, i'm literally shaking

Hi Betty.. please keep cool... hawa jamaa wako hivyo. byproducts za maji machafu... Nakushauri just mobilise watu 20 wajinga wa mfumo ulipo. Kama nao watafanya hivo kwa wangine itakuwa multiplier effect babu kubwa. dont get mad

Good thing its happening before our eyes nakwambia impact yake ni kubwa sana
 
Stella Manyanya amenistua mno na kauli yake bungeni.

1. Police wameuwa Nyamongo na kutupa maiti barabarani - hakuna hata mtu mmoja amekamatwa.
2. Police wameuwa raia Arusha wakati wa maandamano - hakuna mtu amekamatwa
3. Mauji yametokea Igunga, Arumeru, hakuna yoyote aliyekamatwa
4. Wabunge wa CCM wamevamiwa na kujeruhiwa vibaya - hakuna yoyote aliyekamatwa
5. Doctor Ulimboka amekamatwa, amepigwa usiku mzima, ameng'elewa meno, kucha, kavunjwa taya and left for the dead, mungu kamuepusha na kifo na sasa yuko nje ya nchi kwa matibabu. Lakini siku 5 zimepita sasa hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na kuhojiwa licha ya Dr Ulimboka kutaja majina!

Sasa, leo Mbunge wa CCM na mkuu wa mkoa ambaye amepata ubunge kwa njia na sababu anazojua yeye mwenyewe anasimama mbele ya bunge na kumuita huyu mhanga wa mateso ya kupindukia Hitler! Wazazi wa Dr Ulimboka na wananchi wa Mbeya wakianza kupaza sauti kweli watakuwa wamekosea?

Inakuwaje serikali iwe na uwezo wa kukamata majambazi yaliyomuua mzungu in just 2 days lakini washindwe kusaka watu waliomfanyia Unyama Dr Ulimboka? Tena huku akiwa ametaja majina?

Wananchi bado tuendelee kuiamini serikali ya chama anachotoka Stella Manyanya kwamba watatupa ulinzi? Nani atakeyamini kuwa sasa polisi hawana 'plaizi' za kung'oa watu meno na kucha? Nani atakayeamini police watu hawana riffle za kutupiga? Usalama wa watanzania uko wapi? Stella Manyanya anaweza kutupa majibu? Na tukayaamini?

Nimefedheheshwa mno na ukatili aliouonesha huyu mama!

Her head is full of "manyanya" What else would you have expected from a head of tomatoes. Remember the plural for nyanya is nyanya. They are called manyanya only when they are rotten and possibly in the dustbin.
 
"who are you what is this "- futuhi a.k.a Bunge la jamhuri ya muungano wa wadanganyika
 
Mbunge stella amesema wazi chadema wanahusika na migomo ya madaktari, pia amesema mungu amemuepusha ulimboka kwa kupata kipigo maana ni kama hiltler wa tanzania kwa kuendesha migomo yenye kuumiza wananchi. Pia amesisitiza waliompiga ulimboka walikuwa na jezi "magwanda" kama ya chadema.

Tumshukuru huyu mama kwa kubainisha.

tushukuru Mungu ulimboka mzima!na kwa maneno yake mwenyewe ametamka kuwa waliomteka ni polisi na amewataja kwa majina!ss hao cdm wanahusikaje hapo? By 'Mnyika'.....hyu mwanamke haoni hata aibu,hivi vyeo vya kupewa ni tatizo!kilichomfanya akimbilie kwny siasa ni nn?c angeenda kufanya kazi aliyosomea km kuna maslahi
 
Hakuna kitu kama hicho basi huyo aliyeenda hospital Ulimboka akamtambua ilikuwaje. Alafu kitu kingine cha kushangaza ivi hao viongozi wetu wanajua kwamba sisi sio wale wa 1960 hatunganyiki yaani tunasema Kikwete na serikali yake ndo wamemfanyia Ulimboka hivyo. Nilikuwa naongea na mgeni mmoja kutoka Europe yeye mwenyewe anasema he hate chama cha mapinduzi kwanza kabisa kwa rushwa iliyokufuru wananchi wanaendelea kufa kwa kukosa mahitaji muhimu. Isitoshe wameripot eti madaktari wamegoma kwa sababu ya mshahara laa hasha watu wanakufa madaktari hawawezi kuvumilia kuona watu wanafia mikononi mwao wakati wana ujuzi wa kutosha. CCM inahesabu siku ngoja tuu mtaona yatakayotokea Tz hawa viongozi wasipochapwa kidogo wanajisahau na kujiona Miungu mtu hasa huyu Kikwete anaangamiza watu wengi hivyo kwa kutojali umuhimu wa madaktari. Siku zake zinahesabika
 
Mbunge stella amesema wazi chadema wanahusika na migomo ya madaktari, pia amesema mungu amemuepusha ulimboka kwa kupata kipigo maana ni kama hiltler wa tanzania kwa kuendesha migomo yenye kuumiza wananchi. Pia amesisitiza waliompiga ulimboka walikuwa na jezi "magwanda" kama ya chadema.

Tumshukuru huyu mama kwa kubainisha.
Mtu mwenye busara hawezi kushukuru au kushabikia upuuzi huu. Kauri za yule mama ni za hatari sana ktk jamii yetu. Wala asidhani anaisaidia CCM ila anazidi kuibomoa kulikoni.
 
Kila anayedai haki katumwa na chadema.

Unknowingly giving CHADEMA a good label worth it, kupigania na kuunganisha umma wa Watanzania wote, which CCM and its allies don't possess!

Who in the earth with unpolluted mind doesn't know that HAKI is a cornerstone for everlasting peace na sustainable democracy, ambapo kila mmoja atatumia fursa zilizopo kujitafutia maendeleo yake mwenyewe na taifa lake.

Ukiona manyoya ujue kaliwa.
 
Wakati anachangia Stella Manyanya alihusisha Chadema na mgomo wa Madaktari ndipo John Mnyika alipotoa taarifa kuwa yeya akiwa Kiongozi wa CDM anasimama na kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na....yaani kutokea hapo ikawa valuvalu mara naye Mwigulu akasimama na kutoa madai ya uongo eti CDM kwenye hotuba yao kuna ushahidi wa kutoa sapoti ya mgomo huo...
Manyanya naye akaendelea kuchangia kuwa eti waliomvamia Ulimboka walikuwa wamevaa magwanda ya CDM....Mwenyekiti naye akawa anawaunga mkono, wabunge wakaanza kupiga kelele, Machali akatolewa nje...

Kwa hiyo Stella Manyanya anawajua hao watu walimpiga Dr Ulimboka? anajuwa walikuwa wamevaa nguo gani? kwa nini polisi wanachunguza wakati kuna wakina Stella Manyanya wanaojua issue yote ilivyokwenda?
 
Viongozi wetu wanavijimamabo imetoka Lilwalo na liwe imekuja unawashwawashwa.Mimi nadhani hili bunge letu lingefaa kuitwa something to do with comedians maana kwa kweli hawana tofauti.
 
Ushahidi apeleke kwa kova unahitajika atapata promotion kwani tunahitaji kujua aliyetenda kwa uli? Mbona anajulikana? Mbona anahangaika kujisafisha? Mbona anahangaika kuchafua wasiokuwepo? Kwann asikae kimya hana amani? Vx moko sawa na mashine ya utra sound moja, inchi zima hospitali za govt hazina utra sound, anaongea nn?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom