Eng Stella Manyanya: CHADEMA Wanahusika na mgomo wa madaktari; amfananisha Ulimboka na Hitler

Mbunge stella amesema wazi chadema wanahusika na migomo ya madaktari, pia amesema mungu amemuepusha ulimboka kwa kupata kipigo maana ni kama hiltler wa tanzania kwa kuendesha migomo yenye kuumiza wananchi. Pia amesisitiza waliompiga ulimboka walikuwa na jezi "magwanda" kama ya chadema.

Tumshukuru huyu mama kwa kubainisha.

Kutoka mpinaji feki wa ufisadi sasa anaonyesha rangi yake halisi. Vyeo vyote vya kupendelewa tu. Viti maalum mpaka leo, akagombee na sijui kwao ni wapi
 
Hii ni kauli ya mabumba kwa mheshimiwa mnyika.kabla ya kulipuka kwa chemba la ma.i,,,,,,,,,,
 
ni nafsi gan tena hanaitaka huyu mama!ubunge kapewa,uku wa mkoa kapewa.....!gan tena hanataka?
 
Not at all Eliza, ndiyo maana nasema mwisho wa siku watu mnaweza kutwangana ngumi. Maana kuna watu hawataweza kuvumilia hizo biases za waziwazi kiasi hicho.

Teh teh, nimeona Mnyika anamtaka Manyanya atangaze kwamba Polisi ni wa CHADEMA!!

Si ndio hapo! Hata hivyo imekula kwao kwa kuwa Ulimboka kashawaumbua
 
Mie hasira sina. Najua kesho ataomba radhi akidai alinukuliwa vibaya. Maji marefu alionyesha njia!
 
Hivi ikijakupatikana ukweli kwamba UWT wamehusika huyu Eng.Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma atajificha wapi? Nio bora kutumia busara kuliko alivyoongea haikufurahisha kwa mtu mwenye ubongo uliotimia.Pili Mungu hawezi kumfanyia hayo mtu au kutuma mtu amfanyie binadamu aliyemuumba Mungu mwenyewe kwa mkono unyama huu.Ninavyoelewa mimi Mungu wetu ni Mungu wa upendo siyo mungu wa visasi na hawezi kuharibu alichokiumba,hivyo Mh.Stella Manyama anatakiwa kuomba radhi.Ila nimemdharau ni afadhali asingeenda shule tungejua moja.
 
Wakati anachangia Stella Manyanya alihusisha Chadema na mgomo wa Madaktari ndipo John Mnyika alipotoa taarifa kuwa yeya akiwa Kiongozi wa CDM anasimama na kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni za uongo na....yaani kutokea hapo ikawa valuvalu mara naye Mwigulu akasimama na kutoa madai ya uongo eti CDM kwenye hotuba yao kuna ushahidi wa kutoa sapoti ya mgomo huo...
Manyanya naye akaendelea kuchangia kuwa eti waliomvamia Ulimboka walikuwa wamevaa magwanda ya CDM....Mwenyekiti naye akawa anawaunga mkono, wabunge wakaanza kupiga kelele, Machali akatolewa nje...

Huo ndio ukweli hakuna uongo hata chembe hapo, ukweli Leo umewauma sana sana cdm, niliisha wahi sema cdm ni kikundi cha wahuni, si mmeona sasa mnataka kumuua ulimboka
 
Mabumba kiboko, mpaka Mnyika ilibidi akae huku anacheka, maana kila akiambiwa kaa, yeye alikuwa mara anakaa mara anayanyuka, mara anakaa mara ananyanyuka.

Mwenyekiti ikamtoka "unawashawashwa"?

Bunge la Tanzania ni more than entertainment, lina kila comedy, lina suspense, lina thriller, lina horror, lina "vituko".
 
Mbunge stella amesema wazi chadema wanahusika na migomo ya madaktari, pia amesema mungu amemuepusha ulimboka kwa kupata kipigo maana ni kama hiltler wa tanzania kwa kuendesha migomo yenye kuumiza wananchi. Pia amesisitiza waliompiga ulimboka walikuwa na jezi "magwanda" kama ya chadema.

Tumshukuru huyu mama kwa kubainisha.



Kwanza pole kwa kumtumia Stella Manyanya kama source wako, unajua kudiriki kumnukuu mwanasiasa hopeless kama Manyanya ni suala linalohitaji ujasiri wa kujitoa mhanga. Pole tena.

oleni wakubwa kwa kufikiria kinyume nyume. Ninyi mtarudi nyuma, wananchi wanafikiria kwenda mbele. They know their enemy. Mnahangaika kweli kutafuta pa-kutokea. Mnatafuta kila upenyo.

Unajua ujinga ukizidi unakaanga...watu mna serikali, mna dola, mnaenda kutuhumu bungeni, badala ya kukamata.

Naona Mnyika kawashughulisha kweli kweli. Mwigulu Nchemba ambaye ameshaathirika kabisa na CHADEMA-phobia na kubakia mifupa tu, akashindwa hata kutofautisha tofauti ya msimamo wa CHADEMA kuunga mkono wafanyakazi wa kada zote kupigania haki na kuhusika na mgomo. Sasa kama akili ya Katibu wa Fedha na Uchumi na Mbunge haiwezi kutofautisha jambo ndogo kama hilo, nini utarajie hapo.

Jamaa anajenga hoja kwa jazba huyo, duh! Atapona lini gonjwa baya la CHADEMA-phobia. Mapovu yanafoka kutoka kila pembe ya mdomo na matundu mengine. Moja ya dalili kubwa. Aede akamsome Shivji, kwenye Intellectuals at the Hill, Argue don't shout.

Kama bado mnafikiri mna uwezo wa kuendesha nchi hii, basi kubalini ile Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mgogoro wa madaktari na serikali, ambayo imetokana na kusikilizwa pande zote mbili, itolewe bungeni na ijadiliwe.

Katika kudhihirisha kuwa mmekuwa dhaifu to thje extreme, leo ni siku tano sasa, hakuna hata mtu mmoja amekamatwa kwa kutuhumiwa. No even a single suspect! Halafu mnashinda mkipiga porojo na propaganda uchochoroni, hivi nani atawaelewa!!!
 
kinacho nishangaza mkuu hapa ni kwamba kuwa walisema swala la migomo liko mahakama na wao ccm ndo wamelianzsha why?
sasa yeye ana ushahidi gan kusema waliomtesa ulimboka walikuwa wamevaa
magwanda!? Kama sio uvumi
na kama uvumi Mnyika kasema vyombo vya habar vimendika pamoja na wamemrekod Ulimboka mwenyewe kuwa waliomtesa ni police! Why?
Ikabdi wamkalishe kwa ubabe wao!


Stella Manyanya amenistua mno na kauli yake bungeni.

1. Police wameuwa Nyamongo na kutupa maiti barabarani - hakuna hata mtu mmoja amekamatwa.
2. Police wameuwa raia Arusha wakati wa maandamano - hakuna mtu amekamatwa
3. Mauji yametokea Igunga, Arumeru, hakuna yoyote aliyekamatwa
4. Wabunge wa CCM wamevamiwa na kujeruhiwa vibaya - hakuna yoyote aliyekamatwa
5. Doctor Ulimboka amekamatwa, amepigwa usiku mzima, ameng'elewa meno, kucha, kavunjwa taya and left for the dead, mungu kamuepusha na kifo na sasa yuko nje ya nchi kwa matibabu. Lakini siku 5 zimepita sasa hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na kuhojiwa licha ya Dr Ulimboka kutaja majina!

Sasa, leo Mbunge wa CCM na mkuu wa mkoa ambaye amepata ubunge kwa njia na sababu anazojua yeye mwenyewe anasimama mbele ya bunge na kumuita huyu mhanga wa mateso ya kupindukia Hitler! Wazazi wa Dr Ulimboka na wananchi wa Mbeya wakianza kupaza sauti kweli watakuwa wamekosea?

Inakuwaje serikali iwe na uwezo wa kukamata majambazi yaliyomuua mzungu in just 2 days lakini washindwe kusaka watu waliomfanyia Unyama Dr Ulimboka? Tena huku akiwa ametaja majina?

Wananchi bado tuendelee kuiamini serikali ya chama anachotoka Stella Manyanya kwamba watatupa ulinzi? Nani atakeyamini kuwa sasa polisi hawana 'plaizi' za kung'oa watu meno na kucha? Nani atakayeamini police watu hawana riffle za kutupiga? Usalama wa watanzania uko wapi? Stella Manyanya anaweza kutupa majibu? Na tukayaamini?

Nimefedheheshwa mno na ukatili aliouonesha huyu mama!
 
Kamwambia Mnyika anawashwa washwa pia anatafuta umaarufu.

Jamaa anafaa kuongoza bunge
 
Huyu mama vyeo alivyopewa na JK ndo vinamzuzua.......hala lolote, Nimemshangaa sana kusema Ulimboka amepewa hiyo adhabu ya kipigo na mwenyenzi Mungu, Huyu mama kachangalikiwa. Mungu endelea kuwapiga upofu. Ukombozi is around the corner.
kwa hiyo MUNGU ndo alimpeleka dr uli Mabwepande akamng'oa kucha na meno?kwakweli watu wanamdhihaki Mungu na adhabu juu yao itakua kali sana
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom