Mbunge Eng. Stella Manyanya aridhishwa na Kasi ya Ukuaji Utalii Nyasa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Nyasa Mhe. Eng. Stella Manyanya ameeleza kuridhishwa kwake na Kasi ya ukuaji wa Utalii katika Wilaya ya Nyasa baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuanza kusimamia vivutio vya Utalii katika Wilaya hiyo.

Ameyasema hayo Juni 5, 2023 akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa Mwaka wa fedha 2022/23 katika Mkutano wa 11 kikao cha 39 cha bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma

".. Sasa hivi Wilaya ya Nyasa inakuwa vizuri kiutalii lakini tumehamasishwa Kwa muda mrefu, wadau wamekuwa hawajitokezi sana, sasa hivi wametokea TAWA ambao wameichukua mlima mbambabay. tumbi na kile kisiwa cha Lundo" amesema

" tunashukuru wameanza kazi nzuri na tayari boti limeshaenda kupeleka watalii Lundo" amesisitiza

Aidha ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA iendelee kuelekeza nguvu zake katika Wilaya ya Nyasa Ili kuhakikisha Utalii unakua zaidi.

maxresdefaultSDERERT5.jpg
 
Back
Top Bottom