SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

Senior Member
May 5, 2021
113
45
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Ashumu kwamba ameenda Advance na akafaulu kwenda Chuo Kikuu, huoni ni kwamba kuna faida kubwa hapo
 
Nakujibu kwa kifupi, na kama una maswali zaidi nakukaribisha uulize.
Ni hivi; career options za mtu aliyeishia form four ni chache kuliko za yule aliyeishia form six na kufaulu.
 
Hawezi kabisa

Ndio maana kipindi cha waziri Ndalichako aliwaambia vyuo vikuu wasidshili kabisa mtu mwenye diploma baadaye wakalegeza kidogo lakini hata hapa nchini mtu wa Diploma kupata nafasi ya vyuo bora sio rahisi kabisa
Hahahaha, Njoo kwenye ajira sasa hichi unachoongea ni tofauti kabisa
 
mfano medicine ukipitia form four ni njia ngumu sana sababu unahitaji miaka angalau 5 ili uwe eligible kusoma degree ya medicine tofauti na aliyepitia form six akifauli tu njia yake ni rahis sana same kwa kozi nyingi za engineering

In short course za science karibia zote anayepitia form six anatumia njia fupi kuliko hata anayepitia diploma

Kwa diploma ni nzuri kwa course za biashara na arts ila sio science
Mkuu Course za Engineering kwanza Best Ni Kupita Diploma, Leo uniletee Dogo Amepata One form four akapamgwa Arusha,mbeya au Dar Tech then akasoma Miaka mitatu diploma afu akaendelea mitatu degree mtu huyo ni bora sana Kuliko alitoka six Akaingia Mlimani 4 yrs degree, Upande wa Medicine nakubaliana na wewe kuwa Njia ya six ni bora zaidi kuliko Kusoma CO then MD
 
mfano medicine ukipitia form four ni njia ngumu sana sababu unahitaji miaka angalau 5 ili uwe eligible kusoma degree ya medicine tofauti na aliyepitia form six akifauli tu njia yake ni rahis sana same kwa kozi nyingi za engineering

In short course za science karibia zote anayepitia form six anatumia njia fupi kuliko hata anayepitia diploma

Kwa diploma ni nzuri kwa course za biashara na arts ila sio science
Unamaanisha aliyesoma diploma hawezi kuunga moja kwa moja degree, sio kweli. Labda unazungumzia aliye maliza diploma then akaajiriwa, na huyo sio mpaka miaka mi5.
 
Nakujibu kwa kifupi, na kama una maswali zaidi nakukaribisha uulize.
Ni hivi; career options za mtu aliyeishia form four ni chache kuliko za yule aliyeishia form six na kufaulu.
Naomba uniorodheshee hizo career options za aliyemaliza fm4 na aliyemaliza fm6 na wote wakafaulu, ili nione huo uchache wake kwa huyo wa fm4
 
Elimu ya advance ni ya watu serious,diploma ni ya wavivu,na ni ghali zaidi hasa kwa waliolengwa kunufaika na HESLB na imechakachuliwa sana siku hizi,,,mind u that unaweza ukaenda diploma pia ukafeli usihitimu
 
Wavivu ukiwa na maana gani? Mbona hiyo advance unayoisema ni ya walio serious baada ya hapo hao walio serious wanaenda tena kusoma diploma unayoiita ya wavivu?
 
Ukifeli ukarudi diploma maana yake wewe ni mvivu au hukua serious huko advance niamini mimi....huwezi faulu form four ukashindwa kufaulu advance unless kuwe na tatizo mahali
 
Unamaanisha aliyesoma diploma hawezi kuunga moja kwa moja degree, sio kweli. Labda unazungumzia aliye maliza diploma then akaajiriwa, na huyo sio mpaka miaka mi5.
Unajua ni miaka mingapi unatumia mpaka upate hiyo diploma ni miaka isiyopungua minne kama umeishia form four

Unaanza degree mwenzako akiwa anaingia mwaka wa tatu kwa aliyemaliza form six
Kwa medicine njia ya diploma ni long way ukitaka short cut pambana ufaulu form six
 
Ninachofahamu mimi diploma ni miaka mitatu, sasa wewe hiyo miaka isiyopungua minne sijui ni diploma ya wapi.
 
kwa mtizamo wangu nnachoona diploma n shortcut nzuri to professionalism bt advance n shortcut ya kwenda chuo ..since utatumia miaka miwl tu kufanikiwa uingie chuo then ukabase na proffessional uko na dream nayo...
so zote ni best kulingana na mtu anachotaka n nn
 
Back
Top Bottom