SoC03 Elimu ya Kidato cha Tano na Sita iondolewe

Stories of Change - 2023 Competition

Mkoba wa Mama

Senior Member
May 5, 2021
113
45
Kulingana na utaratibu uliopo hivi sasa, mwanafunzi anapo hitimu elimu ya sekondari (kidato cha nne) na kufikisha alama zinazohitajika anaweza kuchaguliwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita/kujiunga na vyuo vya kati (astashahada/stashahada)

1. Mwanafunzi atakayechaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita, akihitimu kidato cha sita na kufikisha alama zinazohitajika, atajiunga na elimu ya chuo kikuu (shahada). Na ikitokea mwanafunzi amehitimu kidato cha sita na hajafikisha alama zinazohitajika ili ajiunge na elimu ya chuo kikuu, itambidi arudi nyuma atumie cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aweze kutuma maombi ya kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).
Kwa maana hiyo mwanafunzi huyo atakuwa amepoteza miaka miwili aliyosoma kidato cha tano na sita, lakini pia wazazi wanakuwa wameingia gharama pamoja na serikali kugharamia elimu kwa mda wa miaka miwili ambayo haina manufaa wala matokeo chanya kwa mwanafunzi mwenyewe, kwa wazazi na taifa kwa ujumla, kwa sababu mwanafunzi huyo anakuwa bado hana ujuzi katika fani yoyote ile utakao muwezesha yeye kuajiriwa ama kujiajiri.

2. Kwa mwanafunzi atakaye chaguliwa/kuchagua mwenyewe kujiunga na vyuo vya kati, atakapo hitimu anaweza kuchagua kuendelea na elimu ya chuo kikuu/kuajiriwa/kujiajiri mwenyewe kwa sababu tayari anakuwa na ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana na fani aliyosoma.

Napendekeza kuondolewa kwa elimu ya kidato cha tano na sita kwa sababu, ni njia inayopoteza mda kwa wanafunzi na kuingiza gharama kubwa wazazi na serikali kugharamia elimu ambayo mwisho wa siku mwanafunzi itambidi arudi tena kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili kujiunga na vyuo vya kati.

Sasa kwa nini mwanafunzi huyu asitumie cheti cha elimu ya sekondari mara tu anapohitimu kidato cha nne na kujiunga moja kwa moja na elimu ya vyuo vya kati kulingana na masomo aliyofaulu au fani atakayo ichagua yeye.

Nitoe mfano mmoja hapa:
Unatakiwa kufika kituo D (elimu ya juu/maisha ya kujiajiri/ kuajiriwa) ukitokea kituo C (kidato cha nne), kuna njia mbili za kukuwezesha kufika kituo D, ambazo ni elimu ya kidato cha tano na sita (njia A) au vyuo vya kati (njia B).

Njia A ni fupi (miaka miwili ya kidato cha tano na sita) lakini inakatiza mtoni, na njia B ni ndefu (miaka mitatu ya stashahada) lakini haikatizi mtoni.

Endapo utaenda na njia A unakuwa hauna uhakika wa moja kwa moja wa kufika kituo D maana kuna uwezekano ukakuta mto umefurika maji na usiweze kuvuka, kwa hiyo itakulazimu urudi tena nyuma uanze safari upya kwa kutumia njia B ambayo haikatizi mtoni ili ikufikishe kituo D.

Ikitokea hivyo, unakua umetumia jumla ya miaka mitano kwa safari ambayo kama ungelichagua njia B tangu mwanzo ingelikugharimu mda wa miaka mitatu tu kufika kituo D.

Mfano huu namaanisha nini:
Elimu ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anapohitimu na kushindwa kufikisha alama za kumuwezesha kujiunga na elimu ya chuo kikuu, itamlazimu arudi tena nyuma kutumia cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha nne) ili aombe kujiunga na elimu ya vyuo vya kati (astashahada/stashahada).

Lakini mwanafunzi aliyehitimu elimu ya vyuo vya kati, tayari anakuwa na ujuzi wa kutosha kumuwezesha yeye kujiajiri/kuajiriwa mahali popote kulingana na fani aliyoisoma na anakuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu kama atahitaji kufanya hivyo.

Elimu ya vyuo vya kati inatolewa kwa kiasi kikubwa ikijikita katika ujuzi na kwa vitendo kwa sababu wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo na wakiwa huko wanasimamiwa na kukaguliwa ni tofauti na elimu ya kidato cha tano na sita ambapo wanafunzi wanatumia mda mwingi kukaa darasani kukariri masomo ya nadharia na hata wakiingia maabara, majaribio wanayoyafanya hayana uhalisia kwa asilimia 100 na maisha watakayo kutana nayo baada ya shule aidha ni katika kujiajiri/kuajiriwa.

Elimu ya kidato cha tano na sita kwa sasa haina umuhimu kwa nchi yetu, ni lazima tuchague njia moja iliyo bora zaidi, maana mtu anahitimu kidato cha sita akiwa hana ujuzi wowote ule tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ni kwa nini serikali iendelee kuingia gharama kugharamia suala ambalo tunaweza kuachana nalo na kujikita katika njia moja na gharama hizo zote kuelekezwa katika kuboresha mazingira na miundombinu (hasa katika suala la teknolojia) ya kujifunzia na kufundishia katika vyuo vya kati ili viwe bora zaidi na vizalishe wataalamu mahili wenye ujuzi na ubora unaohitajika.

Ni maarifa gani/ujuzi gani wa ziada anaoupata mwanafunzi aliyepita elimu ya kidato cha tano na sita utakao msaidia yeye katika ulimwengu wa sasa. Ama ni kitu gani cha ziada chenye manufaa watakikosa wanafunzi iwapo elimu ya kidato cha tano na sita itaondolewa na kubakia na elimu ya vyuo vya kati tu.

Naomba wadau, wizara ya elimu na serikali kwa ujumla ilitazame suala hili, tusiendelee kuwa na mifumo ya elimu kwa sababu ilikuwepo tangu mwanzo, kwa sasa inatakiwa tutazame zaidi mabadiliko yaliyopo, ulimwengu umekuwa wa sayansi na teknolojia na unahitaji watu wenye ujuzi zaidi (ili kuwawezesha aidha kujiajiri ama kuwa na sifa za kuajiriwa na kuwa wabunifu zaidi katika nyanja mbalimbali) kitu ambacho elimu ya kidato cha tano na sita haiwezi kutupatia jibu la suala hilo, zaidi ya wanafunzi kukariri vitu ili waje wajibu mitihani wafaulu, tofauti na elimu ya vyuo vya kati, ambapo mwanafunzi anapata mda wa kutosha wa kufanya mafunzo kwa vitendo na tena katika uhalisia, hivyo kumuwezesha kuwa na maarifa, ujuzi wa kutosha, uwezo mkubwa wa ubunifu na utatuzi wa changamoto zinazoikabili dunia katika fani aliyoisomea.

Hivyo itumike elimu ya vyuo vya kati mara tu mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne. Hii itasaidia vijana wengi kuwa na ujuzi mapema zaidi na kuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kujiajiri na sio kutegemea kuajiriwa tu.

Serikali iweke utaratibu maalum mwanafunzi anapohitimu kidato cha nne aangaliwe ni masomo gani alikuwa akifanya vizuri zaidi tangu mwanzo na sio mtihani wa mwisho tu, ili aende kusomea fani inayoendana na masomo hayo, au mwanafunzi achague mwenyewe fani anayoona anaimudu na anauwezo wa kuisoma na baadae kuwa na ujuzi wa kutosha katika fani hiyo.

Ahsanteni.
 
Huku Afrika kipaumbele ni ufaulu upate cheti na sio uelimike ndo maana leo hii ni kawaida kuona ufaulu mkubwa sana form six tofauti na miaka ya nyuma point ni kwamba shule nyingin Tanzania zinampa-mbinu mwanafunzi afaulu tu kama kipaumbele na sio kuelimika

Ni rahis sana mtu kukwambia A level ifutwe ukweli ni kwamba sisi ni watu ambao tunatafuta short-cut always ndo maana tuko kama tulivyo maskin sana wanatu ni ma-proffesor ila hawana maajabu au output yeyote

Dhana ya elimu kwa mwafrika na mzungu ni vitu viwili tofauti
Ni kweli kabisa Mfano halisi Michael faraday alitumia miaka sita kugundua law of electromagnet induction. Mbele kidogo Rutherford akaja akasema hatuna Cha kumlipa faraday kwa jinsi uvumbuzi huo ulivyo Kuwa muhimu. Lakini Sasa njoo bongo sasa utaskia sisomi electromagnetism Kwa vile Kuna swali la kuchagua kwenye mtihani. Mwingine ndio kama huyu eti advance ifutwe yaani ni noma tupu mkuu
 
Nimeona watu wengi Wana judge advanced level bila kujua Nia ya hiyo level...
1.advanced level ni muhimu sana kuliko ata ordinary level katika kutengeneza misingi ya taaluma mf sayansi ,Sanaa au biashara mtu let's say akitokea o level akaenda co ni ngumu kuwa na uelewa mpana juu ya associate fields mechanics behind medical tools ambazo atazitumia yeye atafundishwa tuu jinsi ya kuzitumia mwishowe ndo mambo ya x ray ya kifua kuonyesha mende na mgonjwa kupelekwa India bila kuwaza shida inaweza kua katika mitambo
2. Ukisoma a level una uwanda mpana wa machaguzi ya career ipi u pursue ukifika at university, mfano pcb unaweza kuwa dr,nurse,dentist,radiologist,pharmacist and all medical fields furthermore unaeza kua physicist,chemists, biologist,mwalimu, na hata baadhi ya engineering courses ata pia biashara na arts mind you all these are in Batchelor level
3.elimu ya advance ni sehemu sahihi ya kupata mwanga halisi juu ya career unayotaka kuiendea how will it look like. mfano unatamani kusoma pharmacy lakini ukiitizama organic chemistry ilivyokulemea unajua tuu kabisa pharmacy unaipenda ila hutaiweza. Unataka kuwa mechanical engineer ila mechanics form five imekupiga chenga kabisa kuifafanua unajua mm si wa kuwa hivyo vitu...tofauti na alietoka o level anauelewa mwembamba mno juu ya vitu vinavyohusiana na career anayotaka kuiendea
4. Gharama utayolipa kufikia Naoto zako kupitia advanced level ni ndogo sana ukilinganisha na kupitia diploma,,,let's say unataka kuwa MD ,ukipita pcb utahitajika si zaidi ya fedha laki tano kwa mwaka serikalini na msuli wa maana kwa miaka miwili...ukichomoka ni MD ambayo ukienda serikalini gharama si zaidi ya 3M kwa mwaka....unlike atayeenda Co, Kwanzaa kupata serikalini Co lazima uwe ulipita advance Kwanzaa la sivyo ukitikea o level uwe na one single digit(kutokana na competition) ambapo hapo utalipia gharama sawasawa na MD serikalini about 3M katika kila kitu(tuition fee,vifaa vyote hostels na chakula chako) iyo ni kwa miaka mitatu inakua almost 9M na msuli mzito kama kawaida. Then uende University ukaanze tena MD . Gharama hizi zinaongezeka to an Average about 3M to 5M total kwa a level na 10M to 15M total kwa wataoenda CO katika private kwa muda wote wamasomo,,So ukilinganisha cost wise A livel is cheap.
5. Uwepo wa infarmalities nyingi katika mfumo wa vyuo vya kati ukilinganisha na necta. Vyuo vingi vina ubabaishaji na wanafunzi wengi wanakumbana na maswaibu ya supplementary, carry zisizo halali in the name of , kwakua vyuoni wanainfluence kubwa katika matokeo ya mwisho,Rushwa pia imetatiza Nia kuu ya Ivi vyuo
6. Inefficiency ya professionals wanaotokea a level ukilinganisha na wa diploma kwenda vyuo vikuuu ni swala la vyuo vikuu husika na sio a level aliyesoma..otherwise experience is a good teacher

Kiujumla vyuo vya Kati ni muhimu pia kama backup kwa wale wengi wanaoshindwa kutoboa a level au waliotokea certificate programmes mbalimbali . Ikiwa ni kusema restructuring of our education systems huge changes are needed from pre unit level ,primary up to University na sio kusema eti ukafute tu a level apo utakua unaharibu zaidi
 
Ni kweli mkuu japo Kuna hivi vyuo vya ufundi Kama dit vinadai vyenyewe vina toa degree ya Engineering Kwa aliyepita diploma lakini ukimwangalia engineer mwenyewe hajui hesabu Hajui physics Sasa huwa nashindwa kuelewa ni engineer ukimlinganisha na standard ipi.
Kwani pale DIT hawafundishi physics?!
 
Wanafundisha ila wana brush tu brush huwezi sema eti mtu unafundisha physics, math, masomo ya fani na mengine hapohapo hafu umtoe msomi wa degree
Sio kwamba sayansi ni pana sana na wao wanajitahidi kufocus na sayansi ya uhandisi wanaoufundisha nabsio sayansi ya kila kitu?! Yaani topic za magnetism, light, projectile motion, rotations na nyinginezo hazitoguswa na mtu wa Civil. Hali kadhalika mtu wa umeme hatosoma masomo ya uhandisi ya Civil. Just kwa DIT na vyuo vingine vinavyotoa diploma za engineering.
 
Sio kwamba sayansi ni pana sana na wao wanajitahidi kufocus na sayansi ya uhandisi wanaoufundisha nabsio sayansi ya kila kitu?! Yaani topic za magnetism, light, projectile motion, rotations na nyinginezo hazitoguswa na mtu wa Civil. Hali kadhalika mtu wa umeme hatosoma masomo ya uhandisi ya Civil. Just kwa DIT na vyuo vingine vinavyotoa diploma za engineering.
Ni sahihi Ila Kwa nchi yetu bado sana kutengeneza watu aina hiyo yaani watu wanaona jua kitu kimoja bado sana utatengeneza bomu tu. Nchi inahitaji watu wanaojua vitu vingi vingi sana kutokana na mazingira yaalivyo Sector binafsi Zinazo deal na haya mambo ni chache sana Kwa hiyo Inabiidi elimu itengeneze watu watukuwa multiple purpose. Yaani mtu apite O level na A level Hadi chuo + experience za mtaani hapa unapata mtu ambaye hata akikosa ajira anaweza akajimudu somehow
 
Ni sahihi Ila Kwa nchi yetu bado sana kutengeneza watu aina hiyo yaani watu wanaona jua kitu kimoja bado sana utatengeneza bomu tu. Nchi inahitaji watu wanaojua vitu vingi vingi sana kutokana na mazingira yaalivyo Sector binafsi Zinazo deal na haya mambo ni chache sana Kwa hiyo Inabiidi elimu itengeneze watu watukuwa multiple purpose. Yaani mtu apite O level na A level Hadi chuo + experience za mtaani hapa unapata mtu ambaye hata akikosa ajira anaweza akajimudu somehow
Atajimudu vipi mtaani na elimu aliyonayo haina vitendo ina nadharia peke yake?!
 
Kwa maoni yangu, kidato cha tano na sita vinafundisha basics wakati vyuo vyote vya kati vinajiegemeza zaidi kwenye applied subjects. Kwa mfano, hakuna chuo cha kati kitajikita kwenye basic biology kwa mapana kama utakavyofundishwa A-level. Madhara yake ni nini? Tutajikuta tunatengeneza wasomi wanaokosa essential foundations. Vinginevyo, mitaala ya vyuo vya kati ibadilishwe.
 
Bado sio ya nadharia kushinda A-level, si ndio?!
Elimu ya vyuo vya kati haileweki yaani theory ni legelege practical ndio kabisa mpaka field. Bora Advance kama ni theory ni theory kweli ukitoka hapo hayo mambo sijui ya mechanical na electrical kama kugusa tu. Pia inakupa uwanja wa kujipatia maarifa mengi Mfano nitajitolea mwenyewe hapo baadaye
 
Back
Top Bottom