Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,846
Una experience yoyote ya mgonjwa aliyeshawahi patwa na huo ugonjwa?
Nishasikia hadithi za kusikitisha na kukatisha tamaa jinsi wakunga wetu Bongo walivyo wazembe kuwasaidia kina mama wanaoshikwa na kifafa cha mimba.
- Kifafa cha mimba ni nini?
- Nini inasababisha kifafa cha mimba?
- Dalili zake na ushauri wa haraka iwapo mama mjamzito atakumbana na hali hiyo?
MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU UGONJWA HUU
Ndugu wana JF, naomba kujuzwa kifafa cha mimba ninini, kinatokeaje, kinasababishwa na nini, nini dalili zake na jinsi ya kukizuia, mana nimeuliza wamesema sio epileps but ni eclampsia sasa kisogo inanichanganya, ninandugu yangu amefanyiwa oparation mimba ikiwa na miezi nane kamili na mtoto amekufa kisa eti alipata dalili zote za kifafa cha mimba, yeye haongeai hadi sasa.
Nina maswali kuhusu huu ugonjwa uwapatao wanawake wajawazito, kifafa cha mimba:
1. Ni nini chanzo cha ugonjwa huu?
2. Zipi dalili za huu ugonjwa?
3. Je, inawezekana kuwa nao na bado ukaendelea kulea mimba na kujifungua bila tatizo lolote?
I just lost my baby today, I was so dejected nilipoambiwa my wife had "kifafa cha mimba" and there's no way to keep the baby-to-be, just a month to go azaliwe. Imeniuma coz sikujua kuhusu huu ugonjwa.
MAELEZO YA KITABIBU
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).
Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.
MADHARA YAKE
Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.
Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.
Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.
SABABU ZA KUTOKEA
Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.
Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.
Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.
Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.
Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.
Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi hayo yaliyoyotajwa hapo juu kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.
TIBA YAKE
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.
Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.
Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.
Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa ch mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.
Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.
Kwa sababu ugonjwa wa kifafa cha mimba huongeza uwezekano wa damu kuganda mwilini, daktari anaweza kushauri mgonjwa atumie dawa ya kuzuia damu kuganda.
Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.
Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.
MICHANGO YA WADAU KUHUSU UGONJWA HUU
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?
Ili tuweze kuufahamu vizuri ugonjwa wa kifafa cha mimba (eclampsia), ni vyema nikaanza kuelezea kuhusu PRE-ECLAMPSIA: kwa sababu kifafa cha mimba (eclampsia) kwa kawaida huanza kama presha ya damu kuwa juu wakati wa ujauzito (pre eclampsia), na hali ikizidi kuwa mbaya ndo inakuwa kifafa cha mimba (eclampsia-fikiria kama muendelezo wa ugonjwa huo huo, ambapo katika upande wa mwanzo kuna presha kuwa juu**pre-eclampsia** na upande wa mwisho kuna kifafa cha mimba**eclampsia**).
Pre eclampsia ni pale ambapo mgandamizo wa damu (blood pressure) kwa mama mjamzito unakuwa juu kuliko kawaida !!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 140/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction).
Mgandamizo wa damu ukiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.
Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila imatibabu, mama pia hupata degedege/kifafa, na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).
Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.
Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.
Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.
Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.
KIFAFA CHA MIMBA HUSABABISHWA NA NINI?
Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.
Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.
Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.
Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.
Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.
TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.
Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.
Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.
Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.
Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.
Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.
Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.
JINSI YA KUJIKINGA/KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KIFAFA CHA MIMBA
Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu(kama yalivyotajwa hapo juu) wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.
Pia, ni muhimu kwa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapofahamu kuwa wameshika mimba, na kuendelea kuhudhuria kliniki kwa kadri wanavyopangiwa. Pia ni muhimu kwenda kituo cha afya/ hospitali pale tu mjamzito anapoona dalili za hatari (kuumwa na kichwa sana, kutokwa na damu sehemu za siri, mapigo ya mtoto kupungua, kupoteza fahamu).
Cc charminglady Heaven Sent The Boss Elli
RISK FACTORS ZA UGONJWA HUU
Kwanza pole sana mkuu.
Kifafa cha mimba kitaalamu hujulikana kama ECLAMPSIA. Ni kati ya magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wamama wajawazito katika 3rd world countries, Tanzania included.
Chanzo cha ECLAMPSIA:
Kiukweli, hakuna kitu kimoja ambacho kinafahamika kuwa ndio kisababishi cha ugonjwa huo, yaani chanzo bado hakijafahamika, lakini kuna risk factors (visababishi) nyingi nyingi ambazo ziko associated na eclampsia.
Pia ziko theory nyingi sana zinazojaribu kuelezea ni kitu gani hasa kinatokea wakati wa eclampsia (watu wengine huuita eclampsia kama 'a disease of theories' kwa sababu hii). Baadhi ya risk factors za eclampsia ni kama zifuatazo:
1. Kama ni mimba ya kwanza kwa mama.
2. Kama kuna historia ya eclampsia kwa mama yako/ndugu yako.
3. Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.
4. Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.
5. Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).
6. Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.
7. Mimba ya mapacha.
8. Kama baba wa ujauzito huo ni a new partner kwa mama.
Dalili za tatizo hili: Naomba kwanza nikueleze kuhusu PRE-ECLAMPSIA ninapokuelezea kuhusu dalili za eclampsia: kwa sababu eclampsia kwa kawaida huanza kama pre eclampsia, na ikiwa very severe ndo inakuwa eclampsia(think of this like a spectrum, where by at the low end you have pre eclampsia, and at the high end you have eclampsia).
Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida!!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 150/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)...
Pressure ikiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.
Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila intervention yoyote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).
Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.
Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.
Kwa bahati mbaya sana, matibabu ya ECLAMPSIA ni termination of the pregnancy!! bila kujali wiki za ujauzito!!
Lakini, kama mama akiwa na dalili za pre eclampsia(kabla hajapata seizures/degedege ambapo na jina la ugonjwa litabadilika pia).
Kulingana na dalili za mama na wiki za ujauzito, madaktari wanaweza kujaribu kushusha presha yake kwa dawa na kumfanyia a close monitoring na kuangalia kama wanaweza ku push huo ujauzito ili awezee kudeliver, na hapa care kubwa ni kumantain blood pressure ili isiwe juu na kusababisha ECLAMPSIA.
I hope I have tried to explain vizuri, huu ni ugonjwa ambao ni complex na una mambo mengi, nimejaribu kutumia lugha ya kawaida; na samahanini sana kwa kuchanganya lugha, kama kuna kitu hakijaeleweka mnaweza kuuliza for more explanations. Eli79
DALILI NYINGINE ZA UGONJWA HUU
Kuongezea maelezo ya Dr hapo, ukisikia Pre eclampsia si chochote kigumu ila ni hali ya kupatwa na preha kwa mama mjamzito ambaye si mgonjwa wa presha kwa hali ya kawaida na inatokea mimba ikifika wiki 20 na kuendelea hali ambayo inaambatana na kuchuja kwa protini kwenye mkojo.(Kiwango maalum cha protini na presha pia kinatumika ku classify hili kama ni mild pre eclampsia au ni severe).
Pili, Eclampsia sasa(dalili zimeshatajwa na Dr hapo juu) huwa ina tabia ya kuwapata kina mama ambao wana/ wameingia kwenye "severe pre eclampsia" ambaye ni presha kali wakati wa ujauzito. Hii inamweka huyu mama katika hatari kubwa ya kuingia kwenye kifafa sasa au eclampsia yenyewe, shetani mkuu mwenyewe.
Kwa wale wenye presha kali na wanaonyesha dalili za hatari I.e. kizungu zungu, kichwa kuuma sana, maumivu juu ya kitovu hasa upande wa kulia, kushindwa kuona vizuri (features of impending eclampsia) wana kua managed kwa aggressive blood pressure control na pia dawa ya kumkinga na kifafa (MgSo 4 prophylaxis) ikifanikiwa kushuka anaangaliwa kwa karibu kujaribu ku delay tarehe ya kujifungua, depending on the mother's gestation age.
Akiingia kwenye eclampsia sasa anapewa dawa za kumtuliza na kuzalishwa baada ya hapo.
Unfortunately kuna kuaga na risk kubwa ya kumpoteza mtoto kutokana na kutozingatia matumizi ya dawa kwa wakina mama husika au hata hiyo presha yenyewe inaweza leta hiyo shida.
Kikubwa hapa ni kuhudhuria kliniki mapema na mara kwa mara na pia "kuzingatia matumizi ya dawa za presha" ni muhimu sana.
Mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifungua ni tarehe salama pia ya kujifungua endapo atawahiwa kabla heart rate ya mtoto haijaanza kubadilika. Kwasababu kikubwa tunachohofia hapa ni maturity ya mapafu ya mtoto ambayo ni ya mwisho ku mature mtoto asije zaliwa na Respiratory Distress Syndrome. Huwa Tunatoa dawa ya kuharakisha hii process kwa kina mama wenye risk ya kujifungua kabla ya term.
CC Eli79
UZOEFU WA MDAU
Pole sana kwa kupoteza mtoto.
Nina rafiki yangu aliambiwa ana kifafa cha mimba mimba ikiwa na miezi 7 (kama nakumbuka).
Nchi za wenzetu wanagundua kwa kuwapima wanawake wakati wa clinic hata kabla dalili hazijaonekana kwa macho.
Walichofanya ni walimzalisha kabla ya muda na mtoto akabaki hospital mpaka akakomaa...
Wahaya hili tatizo hawanaga tofauti na baadhi ya makabila ambayo mama alikuwa ananitajia kama mifano ambao kwao hili tatizo ni kama sugu... sababu (according to my mum) ni wahaya wanatumia mitishamba sana wakati wa ujauzito kama njia ya ku prevent hili tatizo na matatizo mengine.
Nakumbuka mama yangu alikuwa ananambia wewe acha kunywa hizi dawa uone kama hujapata kifafa cha uzazi.
Ni kibaya sana, unakuta mzazi anajing'ata wakati wa kujifungua. Wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuua watoto..nadhani kinaathiri ubongo pia.