Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
Kifafa.jpg

Una experience yoyote ya mgonjwa aliyeshawahi patwa na huo ugonjwa?

Nishasikia hadithi za kusikitisha na kukatisha tamaa jinsi wakunga wetu Bongo walivyo wazembe kuwasaidia kina mama wanaoshikwa na kifafa cha mimba.

- Kifafa cha mimba ni nini?
- Nini inasababisha kifafa cha mimba?
- Dalili zake na ushauri wa haraka iwapo mama mjamzito atakumbana na hali hiyo?

MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU UGONJWA HUU
Ndugu wana JF, naomba kujuzwa kifafa cha mimba ninini, kinatokeaje, kinasababishwa na nini, nini dalili zake na jinsi ya kukizuia, mana nimeuliza wamesema sio epileps but ni eclampsia sasa kisogo inanichanganya, ninandugu yangu amefanyiwa oparation mimba ikiwa na miezi nane kamili na mtoto amekufa kisa eti alipata dalili zote za kifafa cha mimba, yeye haongeai hadi sasa.
Nina maswali kuhusu huu ugonjwa uwapatao wanawake wajawazito, kifafa cha mimba:

1. Ni nini chanzo cha ugonjwa huu?
2. Zipi dalili za huu ugonjwa?
3. Je, inawezekana kuwa nao na bado ukaendelea kulea mimba na kujifungua bila tatizo lolote?

I just lost my baby today, I was so dejected nilipoambiwa my wife had "kifafa cha mimba" and there's no way to keep the baby-to-be, just a month to go azaliwe. Imeniuma coz sikujua kuhusu huu ugonjwa.

MAELEZO YA KITABIBU

KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).

Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

MADHARA YAKE

Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.

Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.

Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.

Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.

SABABU ZA KUTOKEA

Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.

Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.

Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi hayo yaliyoyotajwa hapo juu kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

TIBA YAKE
Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.

Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.

Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa ch mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.

Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.

Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Kwa sababu ugonjwa wa kifafa cha mimba huongeza uwezekano wa damu kuganda mwilini, daktari anaweza kushauri mgonjwa atumie dawa ya kuzuia damu kuganda.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

MICHANGO YA WADAU KUHUSU UGONJWA HUU
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Ili tuweze kuufahamu vizuri ugonjwa wa kifafa cha mimba (eclampsia), ni vyema nikaanza kuelezea kuhusu PRE-ECLAMPSIA: kwa sababu kifafa cha mimba (eclampsia) kwa kawaida huanza kama presha ya damu kuwa juu wakati wa ujauzito (pre eclampsia), na hali ikizidi kuwa mbaya ndo inakuwa kifafa cha mimba (eclampsia-fikiria kama muendelezo wa ugonjwa huo huo, ambapo katika upande wa mwanzo kuna presha kuwa juu**pre-eclampsia** na upande wa mwisho kuna kifafa cha mimba**eclampsia**).

Pre eclampsia ni pale ambapo mgandamizo wa damu (blood pressure) kwa mama mjamzito unakuwa juu kuliko kawaida !!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 140/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction).

Mgandamizo wa damu ukiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila imatibabu, mama pia hupata degedege/kifafa, na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.

Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.

KIFAFA CHA MIMBA HUSABABISHWA NA NINI?

Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.

Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.

Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA

Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.

Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.

Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA/KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KIFAFA CHA MIMBA

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu(kama yalivyotajwa hapo juu) wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

Pia, ni muhimu kwa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapofahamu kuwa wameshika mimba, na kuendelea kuhudhuria kliniki kwa kadri wanavyopangiwa. Pia ni muhimu kwenda kituo cha afya/ hospitali pale tu mjamzito anapoona dalili za hatari (kuumwa na kichwa sana, kutokwa na damu sehemu za siri, mapigo ya mtoto kupungua, kupoteza fahamu).

Cc charminglady Heaven Sent The Boss Elli
RISK FACTORS ZA UGONJWA HUU

Kwanza pole sana mkuu.

Kifafa cha mimba kitaalamu hujulikana kama ECLAMPSIA. Ni kati ya magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wamama wajawazito katika 3rd world countries, Tanzania included.

Chanzo cha ECLAMPSIA:

Kiukweli, hakuna kitu kimoja ambacho kinafahamika kuwa ndio kisababishi cha ugonjwa huo, yaani chanzo bado hakijafahamika, lakini kuna risk factors (visababishi) nyingi nyingi ambazo ziko associated na eclampsia.

Pia ziko theory nyingi sana zinazojaribu kuelezea ni kitu gani hasa kinatokea wakati wa eclampsia (watu wengine huuita eclampsia kama 'a disease of theories' kwa sababu hii). Baadhi ya risk factors za eclampsia ni kama zifuatazo:

1. Kama ni mimba ya kwanza kwa mama.

2. Kama kuna historia ya eclampsia kwa mama yako/ndugu yako.

3. Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.

4. Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.

5. Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).

6. Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.

7. Mimba ya mapacha.

8. Kama baba wa ujauzito huo ni a new partner kwa mama.

Dalili za tatizo hili: Naomba kwanza nikueleze kuhusu PRE-ECLAMPSIA ninapokuelezea kuhusu dalili za eclampsia: kwa sababu eclampsia kwa kawaida huanza kama pre eclampsia, na ikiwa very severe ndo inakuwa eclampsia(think of this like a spectrum, where by at the low end you have pre eclampsia, and at the high end you have eclampsia).

Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida!!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 150/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)...

Pressure ikiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila intervention yoyote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Kwa bahati mbaya sana, matibabu ya ECLAMPSIA ni termination of the pregnancy!! bila kujali wiki za ujauzito!!
Lakini, kama mama akiwa na dalili za pre eclampsia(kabla hajapata seizures/degedege ambapo na jina la ugonjwa litabadilika pia).

Kulingana na dalili za mama na wiki za ujauzito, madaktari wanaweza kujaribu kushusha presha yake kwa dawa na kumfanyia a close monitoring na kuangalia kama wanaweza ku push huo ujauzito ili awezee kudeliver, na hapa care kubwa ni kumantain blood pressure ili isiwe juu na kusababisha ECLAMPSIA.

I hope I have tried to explain vizuri, huu ni ugonjwa ambao ni complex na una mambo mengi, nimejaribu kutumia lugha ya kawaida; na samahanini sana kwa kuchanganya lugha, kama kuna kitu hakijaeleweka mnaweza kuuliza for more explanations. Eli79

DALILI NYINGINE ZA UGONJWA HUU

Kuongezea maelezo ya Dr hapo, ukisikia Pre eclampsia si chochote kigumu ila ni hali ya kupatwa na preha kwa mama mjamzito ambaye si mgonjwa wa presha kwa hali ya kawaida na inatokea mimba ikifika wiki 20 na kuendelea hali ambayo inaambatana na kuchuja kwa protini kwenye mkojo.(Kiwango maalum cha protini na presha pia kinatumika ku classify hili kama ni mild pre eclampsia au ni severe).

Pili, Eclampsia sasa(dalili zimeshatajwa na Dr hapo juu) huwa ina tabia ya kuwapata kina mama ambao wana/ wameingia kwenye "severe pre eclampsia" ambaye ni presha kali wakati wa ujauzito. Hii inamweka huyu mama katika hatari kubwa ya kuingia kwenye kifafa sasa au eclampsia yenyewe, shetani mkuu mwenyewe.

Kwa wale wenye presha kali na wanaonyesha dalili za hatari I.e. kizungu zungu, kichwa kuuma sana, maumivu juu ya kitovu hasa upande wa kulia, kushindwa kuona vizuri (features of impending eclampsia) wana kua managed kwa aggressive blood pressure control na pia dawa ya kumkinga na kifafa (MgSo 4 prophylaxis) ikifanikiwa kushuka anaangaliwa kwa karibu kujaribu ku delay tarehe ya kujifungua, depending on the mother's gestation age.

Akiingia kwenye eclampsia sasa anapewa dawa za kumtuliza na kuzalishwa baada ya hapo.

Unfortunately kuna kuaga na risk kubwa ya kumpoteza mtoto kutokana na kutozingatia matumizi ya dawa kwa wakina mama husika au hata hiyo presha yenyewe inaweza leta hiyo shida.

Kikubwa hapa ni kuhudhuria kliniki mapema na mara kwa mara na pia "kuzingatia matumizi ya dawa za presha" ni muhimu sana.

Mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifungua ni tarehe salama pia ya kujifungua endapo atawahiwa kabla heart rate ya mtoto haijaanza kubadilika. Kwasababu kikubwa tunachohofia hapa ni maturity ya mapafu ya mtoto ambayo ni ya mwisho ku mature mtoto asije zaliwa na Respiratory Distress Syndrome. Huwa Tunatoa dawa ya kuharakisha hii process kwa kina mama wenye risk ya kujifungua kabla ya term.

CC Eli79
UZOEFU WA MDAU

Pole sana kwa kupoteza mtoto.

Nina rafiki yangu aliambiwa ana kifafa cha mimba mimba ikiwa na miezi 7 (kama nakumbuka).

Nchi za wenzetu wanagundua kwa kuwapima wanawake wakati wa clinic hata kabla dalili hazijaonekana kwa macho.

Walichofanya ni walimzalisha kabla ya muda na mtoto akabaki hospital mpaka akakomaa...

Wahaya hili tatizo hawanaga tofauti na baadhi ya makabila ambayo mama alikuwa ananitajia kama mifano ambao kwao hili tatizo ni kama sugu... sababu (according to my mum) ni wahaya wanatumia mitishamba sana wakati wa ujauzito kama njia ya ku prevent hili tatizo na matatizo mengine.

Nakumbuka mama yangu alikuwa ananambia wewe acha kunywa hizi dawa uone kama hujapata kifafa cha uzazi.
Ni kibaya sana, unakuta mzazi anajing'ata wakati wa kujifungua. Wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuua watoto..nadhani kinaathiri ubongo pia.
 
  • Thanks
Reactions: RR
Mbu, nimepata hii article from internet. I will be back. I have experienced hii kitu.

Kifafa cha mimba (eclampsia)
Overview

Eclampsia, a life-threatening complication of pregnancy, results when a pregnant woman previously diagnosed with preeclampsia (high blood pressure and protein in the urine) develops seizures or coma. In some cases, seizures or coma may be the first recognizable sign that a pregnant woman has preeclampsia.

There has never been any evidence suggesting an orderly progression of disease beginning with mild preeclampsia progressing to severe preeclampsia and then on to eclampsia. The disease process can begin mild and stay mild, or can be initially diagnosed as eclampsia without prior warning.

Preeclampsia usually occurs in a woman's first pregnancy but may occur for the first time in a subsequent pregnancy.

Causes
No one knows what exactly causes preeclampsia or eclampsia.

Since we don't know what causes preeclampsia or eclampsia, we don't have any effective tests to predict when preeclampsia or eclampsia will occur, or treatments to prevent preeclampsia or eclampsia from occurring (or recurring).

Preeclampsia usually occurs with first pregnancies. However, preeclampsia may be seen with twins (or multiple pregnancies), in women older than 35 years, in women with high blood pressure before pregnancy, in women with diabetes, and in women with other medical problems (such as connective tissue disease and kidney disease).

Preeclampsia may run in families, although the reason for this is unknown.

Preeclampsia is also associated with problems with the placenta, such as too much placenta, too little placenta, or how the placenta attaches to the wall of the uterus. Preeclampsia is also associated with hydatidiform mole pregnancies, in which no normal placenta and no normal baby are present.

There is nothing that any woman can do to prevent preeclampsia or eclampsia from occurring.

Symptoms (Dalili)
The hallmark of eclampsia is seizures. Similar to preeclampsia, other changes and symptoms may be present and vary according to the organ system or systems that are affected. These changes can affect the mother only, baby only, or more commonly affect both mother and baby. Some of these symptoms give the woman warning signs, but most do not.

The most common symptom and hallmark of preeclampsia is high blood pressure. This may be the first or only symptom. Blood pressure may be only minimally elevated initially or can be dangerously high; symptoms may or may not be present. A common belief is that the risk of eclampsia rises as blood pressure increases above 160/110 mm Hg.

The kidneys are unable to efficiently filter the blood (as they normally do). This may cause an increase in protein to be present in the urine. The first sign of excess protein is commonly seen on a urine sample obtained in your provider's office. Rarely does a woman note any changes or symptoms associated with excess protein in the urine. In extreme cases affecting the kidneys, the amount of urine produced decreases greatly.

Nervous system changes can include blurred vision, seeing spots, severe headaches, convulsions, and even occasionally blindness. Any of these symptoms require immediate medical attention.
 
Last edited by a moderator:
ECLAMPSIA (kifafa cha mimba) ni matokeo ya mwisho au complication ya PRE-ECLAMPSIA (EPH gestosis), si kila mjamzito mwenye PRE-ECLAMPSIA anaishia na ECLAMPSIA, hallmark ya PRE-ECLAMPSIA ni dalili tatu, ambazo ni HIGH BLOOD PRESSURE (hYPERTENSION), EDEMA (kuvimba miguu au mwili mzima) na PROTENURIA (mkojo unakuwa na protein nyingi).

PREECLAMPIA inagundulika kirahisi kwa kutumia elimu kidogo hata katika zahanati, kama mama anahudhuria kiliniki akiwa mjamzito (>90% ya akina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki Tanzania), mama mwenye hali hiyo huwa lazima apelekwe kwa mganga/dakitari kwa ufuatiliaji zaidi na anashauriwa kuhudhuria kiliniki mara nyingi kuliko wajawazito wengine, na hupewa dawa za kupunguza pressure (HYPERTENSION).

Daktari hutakiwa kufanya grading ya hiyo hali (EPH gestosisi scoring/grading),ambapo kuna makundi matatu ya ukali wa EPH (Mild EPH, Moderate na Severe) mwenye Severe EPH htakiwa kulazwa/hupewa rufaa kwenda ktk hospitali yenye watalaamu na facilities za kutosha kwa uangalizi wa karibu, anaweza asiruhusiwe kurudi nyumbani mpaka MWISHO WA MIMBA.

KUTIBU ECLAMPSIA NI SHUGULI PEVU, ni EMERGENCY na inahititaji skilled hands, Kama mama ata-develop ECLAMPSIA (Kifafa cha Mimba) juhudi zinafanyika kumwokoa mama na si vinginevyo, ambapo ni kutibu kifafa na ku-terminate mimba kwa haraka sana bila kujali umri wa mimba hiyo, kama mtoto ata-survive ni bahati yake, lakini wanakuwa na complications nyingi na wachache wana-survive, sometimes with life long sequelae.

Mimba inaweza kuwa-terminated kwa njia ya operation (caeserian section) au kama hali inaruhusu ni ku-speed up process ya kuzaa kwa madawa yanayoongeza uchungu (oxytocic drugs)

ECLAMPSIA inaogopwa sana na ukienda kila wodi ya maternity utakuta ukutani kumebadikwa kanuni/GUIDELINES za ku-deal na ECLAMPSIA.

Mimba ikishakuwa terminated huwa ndiyo mwisho wa KIFAFA CHA MIMBA na dalili zote zinapotea, lakini hali hii inaweza kurudia kwa mimba inayofuata.

Hakuna ujanja au Tekinologia ya kujua kuwa mama akipata ujauzito utaweza kupata PRE- ECLAMPIA na ECLAPSIA

Kuhudhuria kiliniki (antenatal clinc) ni muhimu sana ili kuweza kufanya screening ya matatizo kama haya, na ikigundulika mapema inasaidia kupunguza madhara mengi ya hali hiyo.
 
Triplets Thank very much for this post it is real nice Mama watoto the next 10 days Inshallah anaweza kujifungua na muomba mungu asipate hayo matatizo.
 
Triplets Thank very much for this post it is real nice Mama watoto the next 10 days Inshallah anaweza kujifungua na muomba mungu asipate hayo matatizo.

Ee Mungu mwepushe mke wangu na tatizo hili, aje ajifungue vizuri watoto wetu. thank you.

Mwenyezi Mungu atawavusha salama.

Mgogoro unakuja pale 17% ya vifo vya kina mama Tanzania vinatokana na kifafa cha mimba.

Katika sababu mojawapo inayosababisha vifo vya kina mama kutokana na kifafa cha mimba ni Uzembe, dharau, na ujuzi mdogo wa wauguzi :(:(:(

Really sad, inabidi siku ya siku kumshikisha muuguzi/wauguzi 'kitu kidogo', la sivyo unaweza mpoteza mama na mwana hivi hivi unaangalia

Hali inatisha kwa kweli.
 
Ni kweli mwa maoni yako mchongoma lakini si wauguzi woote kuwa ni wazembe mara nyingi unakuta mama yupo mabali na health facilities as the results anakuja katika advanced stage ambapo inakuwa shida sana mtu kumsaidia, mbali na hiyo look on our health facilities, disp nyingi hazina dawa za kutosha kuweka ku manage mama amabaye anakuwa na hali kama hii ya kifafa cham mimba hata hiyo wanayoita Lytic coctatai drugs kwa ajili ya ku control fits and spasm inakuwa hakuna hivyo lazima ana end with death.

Nimekuwa nikishuhudia zaidi ya akina mama 10 ndani ya miaka 8 ambao wamekuwa wakipata mauti kwa sababau tu Nurses hawana la kufanya,na hata hiyvo ndugu zanguni coverage ya trained health staff katika nchi hii is only 32% of the required staff, unafikiri ni lini hili gap litazibika, serikari inabidi ifanye jitihada za pamoja kuweza kuwa na health trained staff wa kutosha ili maternal mortality iweze kushuka.

Mbali na hiyo kuna wenzangu wamechangia suala la rushwa, ni kweli kabisa rushwa ipo lakini pia unajua health staff wamekuwa wanadharaulika sana na policy makers, mtu kama Nurse anaomwa kama specimen lakini ni mtu muhimu sana katika secta ya afya, look Nurse anayefanya kazi USA au hapa jirani tu Emirate kipato chake kikoje lakini Nurse wa kibongo ni choka mbaya!!!!!!!! kwa hiyo hata kama ningekuwa ni mimi lakima ningevuta huo moto tu!!! how can I make like kwa mshahara wa 280,000 wakati nna watoto na nipo katika nyumba ya kupanga.

Ok ndugu zanguni cha muhimu ni kumuwaisha mama hosp anapokuwa mjamzito na hivyo let us join all to advocate maternal mortality to the govermant so that extra funding can be re- allocated to the responsible ministry/firm.

Ndimi,

Muvimba
 
Ni kweli mwa maoni yako mchongoma lakini si wauguzi woote kuwa ni wazembe mara nyingi unakuta mama yupo mabali na health facilities as the results anakuja katika advanced stage ambapo inakuwa shida sana mtu kumsaidia,

Ufafanuzi mzuri sana ndugu Muvimba, lakini vile vile kwa dhana hiyo hiyo ya UMBALI na health facilities ingeingia vichwani mwa baadhi ya wauguzi na kuacha DHARAU y
ao ya "...ndio mkome, kwanini mmemchelewesha mjamzito!"

mbali na hiyo look on our health facilities, disp nyingi hazina dawa za kutosha kuweka ku manage mama amabaye anakuwa na hali kama hii ya kifafa cham mimba hata hiyo wanayoita Lytic coctatai drugs kwa ajili ya ku control fits and spasm inakuwa hakuna hivyo lazima ana end with death.
Nimekuwa nikishuhudia zaidi ya akina mama 10 ndani ya miaka 8 ambao wamekuwa wakipata mauti kwa sababau tu Nurses hawana la kufanya

Hivi kuna uwezekano wa ku control hizo spasm na fits kabla hazijatokea? Au some nurses mistook it with labour pains? It is scarry and cruel watching your spouse/mama mjamzito going thru this kwakweli!

Na hata hiyvo ndugu zanguni coverage ya trained health staff katika nchi hii is only 32% of the required staff, unafikiri ni lini hili gap litazibika, serikari inabidi ifanye jitihada za pamoja kuweza kuwa na health trained staff wa kutosha ili maternal mortality iweze kushuka.

Ok ndugu zanguni cha muhimu ni kumuwaisha mama hosp anapokuwa mjamzito na hivyo let us join all to advocate maternal mortality to the govermant so that extra funding can be re- allocated to the responsible ministry/firm.

Ndimi,

Muvimba

When nature is taking place, hizo labour pains ni kitendawili, hasa mama anapokuwa ana experirnce 1st pregnancy, false alarms kibao hata kama siku zinahesabika. Ndugu Muvimba, ubarikiwe sana kwa mchango wako.

Shukran.
 
Positive thinker, nakutakia kila la kheri ktk kumkaribisha mwanao, shaka na wasiwasi ondoa kabisaeverything will be alright with Gods help.

Ilivyotokea kwangu mimi ni kwamba blood pressure ilianza kupanda gradually kwa kama wiki mbili, wakapima routine urine protein kwa nyakati mbili tofauti hakupata kitu, kwa vile nilikuwa naexpect twins waliniweka kwenye group la wenye uwezekano mkubwa kupata hili tatizo (high risk group)wakacheki 24 hrs urine protein wakakuta iko juu.

Hapo hapo nikalazwa na kuanza kutibiwa, wakati huo huo wakiniandaa kwa operationany way I was operated and at last we ended up with two health babies.

Utaona kwamba blood pressure ikiwa juu halafu urine protein kuwa negative kwenye routine check up haimaanishi kwamba huna pre eclampisia. Nafikiri kitu cha muhimu walichofanya ilikuwa ni ile kucheki 24 hrs urine protein, hii ni tofauti na ile test wanayofanya as routine tukienda clinic.
 
To JF Doctor!

Mke wangu yupo wiki ya 32 na amekuwa diagnosed kuwa na kifafa cha mimba, amebeba mapacha. Naomba ushauri na maoni ya kitaalamu kumsaidia yeye na watoto.

Asante
 
To JF Doctor!

Mke wangu yupo wiki ya 32 na amekuwa diagnosed kuwa na kifafa cha mimba, amebeba mapacha!! Naomba ushauri na maoni ya kitaalamu kumsaidia yeye na watoto.

Asante

Semesozi, kifafa cha mimba, au kwa lugha ya kitaalamu preeclampsia/eclampsia ni medical emergency. Nina imani kuwa mkeo sasa hivi atakuwa chini ya observation ya madaktari muda wote. Kama bado basi fanya hima uhakikishe kuwa anapata hiyo attention.

Sidhani kama kuna ushauri wa maana utapata zaidi ya kuhakikisha kuwa mkeo anapata full time attention ya madaktari (Gynaecologist) hadi atapojifungua.

Under normal circumstances, mwanamke mwenye preeclampsia anatakiwa awe chini ya uangalizi wa madaktari ambao watajitahidi ku-control BP yake na kuhakikisha (kwa njia za kitaalamu) kuwa hafikii kupata eclampsia.

Pole kwa kuuguza na nawatakieni kila la kheri.
 
Nani anafahamu ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga nao. Ni vyema kujikinga kuliko kutibu. Karibuni
 
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions).

Sababu kamili za ugonjwa huu hazijukani. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu zikiwemo:-

(i) Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.
(ii) Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.
(iii) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.
(iv) Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

Hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa huu, bali nguvu huelekezwa katika kuchukua hatua za kuepuka tatizo hili kwa kuwashauri wanawake wasibebe mimba katika umri mdogo au mkubwa sana.

Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.

Kifafa cha mimba kikisha tokea nguvu huelekezwa katika kupunguza madhara yatokanayo na kifafa hicho. Kwa mfano kuzuia degedege isirudie rudie kwa kutoa dawa za kuzuia degedege. Kutoa dawa za kuteremsha msukumo wa damu, iwapo uko juu, na vile vile kumsaidia mama ajifungue mapema mara itakapoonekana mtoto amefikia umri wa kuzaliwa..
 
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions). Sababu kamili za ugonjwa huu hazijukani. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu zikiwemo:-

(i) Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.

(ii) Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.

(iii) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.

(iv) Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

Hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa huu, bali nguvu huelekezwa katika kuchukua hatua za kuepuka tatizo hili kwa kuwashauri wanawake wasibebe mimba katika umri mdogo au mkubwa sana. Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi. Kifafa cha mimba kikisha tokea nguvu huelekezwa katika kupunguza madhara yatokanayo na kifafa hicho. Kwa mfano kuzuia degedege isirudie rudie kwa kutoa dawa za kuzuia degedege. Kutoa dawa za kuteremsha msukumo wa damu, iwapo uko juu, na vile vile kumsaidia mama ajifungue mapema mara itakapoonekana mtoto amefikia umri wa kuzaliwa

Thanks mamdo kwa ushauri mzuri.
 
Asante MamaMdogo
 
Asante Mama Mdogo. Pia kwa kuongezea ni muhimu mama mjamzito kujitahidi kupunguza kiwango cha chumvi anayotumia, na hasa chumvi ya kuongezea mezani (raw salt) na pia kuongeza kiasi cha matunda anachokula. Kwa mimba ya kwanza, ni vizuri kufanya utaratibu wa kujifungulia hospitali kubwa just incase (badala ya zahanati). Ni muhimu kupata matibabu sahihi mara dalili za kifafa cha mimba zinapojitokeza.
 
Asante MamaMdogo. Pia kwa kuongezea ni muhimu mama mjamzito kujitahidi kupunguza kiwango cha chumvi anayotumia, na hasa chumvi ya kuongezea mezani (raw salt)na pia kuongeza kiasi cha matunda anachokula. Kwa mimba ya kwanza, ni vizuri kufanya utaratibu wa kujifungulia hospitali kubwa just incase( badala ya zahanati). Ni muhimu kupata matibabu sahihi mara dalili za kifafa cha mimba zinapojitokeza.
Walioko vijijini ndani wanapata sana shida kutokana na hili tatizo.
 
Asante MamaMdogo. Pia kwa kuongezea ni muhimu mama mjamzito kujitahidi kupunguza kiwango cha chumvi anayotumia, na hasa chumvi ya kuongezea mezani (raw salt)na pia kuongeza kiasi cha matunda anachokula. Kwa mimba ya kwanza, ni vizuri kufanya utaratibu wa kujifungulia hospitali kubwa just incase( badala ya zahanati). Ni muhimu kupata matibabu sahihi mara dalili za kifafa cha mimba zinapojitokeza.

Kwenye blue matunda yanaongezea nini katika kukinga, na je vipi akiwa mjamzito kwa mara ya pili apunguze hicho kiasi cha matunda? Naomba unifahamishe kiundani hapa madau.
 
Kwenye blue matunda yanaongezea nini katika kukinga, na je vipi akiwa mjamzito kwa mara ya pili apunguze hicho kiasi cha matunda? Naomba unifahamishe kiundani hapa madau.
Matunda ya aina gani? Inawezekana yote lakini kuna ambayo ni muhimu zaidi.
 
Back
Top Bottom