Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

Endelea na dawa bila kukosa, utajifungua salama, kikubwa ku control presha vizuri. Hospitalini wanatoa kinga ya kifafa cha mimba kwa wale wenye presha ya juu sana, ila wata kulaza wakiona ipo juu sana ili waweze kuishusha na kukupa hiyo kinga ambayo ni ya sindano.

CC ringson
 
Pole sana Eli79 Nadhani @dr wansegamila kaelezea vizuri hapo juu. Management ya enclampsia ni muhimu sana ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia kama mama yupo na uzito mkubwa tafadhali hebu kuwa nae bega kwa bega aanze kupunguza uzito kwa njia sahihi na anapokuwa mjamzito aepuke kugain weight zaidi ya ambao upo recommended kulingana na uzito wake before conception.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kwann nimeingia huu uzi nimejikuta naogopa...mtoto wa kwanza nilipata kifafa cha mimba nashukuru mungu nilipona mimi na mtoto. Kwa sasa nina mimba ipo miez ya mwishon ila tangu last week natumia dawa za kushusha presha maana ilikua juu sana, sina raha naogopa mnooo

Pole sana pamoja na kutumia dawa jitahid sana ufanye mazoezi mepesi kama kutembea na pia usizid kuongezeka uzito kama uzito upo juu.
 
Pole sana Eli79... Nadhani @dr wansegamila kaelezea vizuri hapo juu.. Management ya enclampsia ni muhimu sana ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.. Pia kama mama yupo na uzito mkubwa tafadhali hebu kuwa nae bega kwa bega aanze kupunguza uzito kwa njia sahihi na anapokuwa mjamzito aepuke kugain weight zaidi ya ambao upo recommended kulingana na uzito wake before conception
Asante sana Dr. Lakini mbona uzito wake, kulinganisha na urefu ni wa kawaida tu na wala haukuongezeka kupitiliza? Na hata hilo shinikizo la damu (pressure) hakuwa nalo, tulijaribu sana kupima pressure kila siku kwa hiyo hakuwa na shida hiyo.
Ninachojiuliza, mbona kabla ya kupata hizo complications hakuwa na tatizo lolote? Yani hata kusikia tumbo kuuma hakusikia, mbona ilitokea tu ghafla?
 
Pole sana pamoja na kutumia dawa jitahid sana ufanye mazoezi mepesi kama kutembea na pia usizid kuongezeka uzito kama uzito upo juu

Endelea na dawa bila kukosa, utajifungua salama, kikubwa ku control presha vizuri. Hospitalini wanatoa kinga ya kifafa cha mimba kwa wale wenye presha ya juu sana, ila wata kulaza wakiona ipo juu sana ili waweze kuishusha na kukupa hiyo kinga ambayo ni ya sindano.

CC ringson

Asanten nyote kwa ushauri, nimejifungua salama mtoto wa kiume week iliyopita. Mbarikiwe
 
Asante sana Dr. Lakini mbona uzito wake, kulinganisha na urefu ni wa kawaida tu na wala haukuongezeka kupitiliza? Na hata hilo shinikizo la damu (pressure) hakuwa nalo, tulijaribu sana kupima pressure kila siku kwa hiyo hakuwa na shida hiyo.
Ninachojiuliza, mbona kabla ya kupata hizo complications hakuwa na tatizo lolote? Yani hata kusikia tumbo kuuma hakusikia, mbona ilitokea tu ghafla?

Pole sana Eli79.

Una uhakika hata kichwa hakikuwahi kumuuma? Maana sio lazima tumbo liume. Mtu anaweza akapata baadhi tu ya dalili ama zote kuendana na stage ugonjwa (Pre-eclampsia, eclampsia au severe eclampsia). Mi mtoto wangu wa kwanza nilipata hilo tatizo nikiwa na mimba ya miezi saba. Ndani ya wiki nilivimba vimba miguu nikachukulia poa, maumivu ya kichwa sikuyapa uzito, kuumwa tumbo nikafikiria labda ndo kawaida.

Yani sikwenda hosp mpaka siku niliyokuwa nimeandikiwa kwaajili ya kuangalia maendeleo yangu na mtoto. Baada ya kuniona kitu cha kwanza dr alichotaka ni kupima mkojo na alivyoona majibu akaniambia lazima nibaki hosp. Kama ningechelewa hata siku moja ingeshakula kwetu. Kwahiyo dalili sio lazima zionekane muda mrefu ama maumivu yawe makali sana kwasababu inapokuwa kwenye level ya chini viashiria vyake navyo haviwi vikali.

Kuwa mjamzito ni delicate sana. Yani kila kitu,no matter how small COUNTS. Kutokujua kunafanya mtu anadhani labda hiki au kile ni hali ya kawaida tu kwenye ujauzito wakati inatakiwa muda wowote ukiona kitu cha tofauti ufuatilie. Kama nyie pengine mngewahi siku moja kabla mambo yangekuwa tofauti. Anyway, hopefully wifi yetu akipata tena mimba haitomsumbua maana bado uwezekano wa kuwa na 'smooth pregnancy' upo kama ilivyokuwa kwangu mimba ya pili.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza pole sana mkuu.

Kifafa cha mimba kitaalamu hujulikana kama ECLAMPSIA. Ni kati ya magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wamama wajawazito katika 3rd world countries, Tanzania included.

Chanzo cha ECLAMPSIA:

Kiukweli, hakuna kitu kimoja ambacho kinafahamika kuwa ndio kisababishi cha ugonjwa huo, yaani chanzo bado hakijafahamika, lakini kuna risk factors (visababishi) nyingi nyingi ambazo ziko associated na eclampsia.

Pia ziko theory nyingi sana zinazojaribu kuelezea ni kitu gani hasa kinatokea wakati wa eclampsia(watu wengine huuita eclampsia kama 'a disease of theories' kwa sababu hii). Baadhi ya risk factors za eclampsia ni kama zifuatazo:

1.Kama ni mimba ya kwanza kwa mama.

2.Kama kuna historia ya eclampsia kwa mama yako/ndugu yako.

3.Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.

4.Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.

5.Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).

6.Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.

7.Mimba ya mapacha.

8. Kama baba wa ujauzito huo ni a new partner kwa mama.

Dalili za tatizo hili: Naomba kwanza nikueleze kuhusu PRE-ECLAMPSIA ninapokuelezea kuhusu dalili za eclampsia: kwa sababu eclampsia kwa kawaida huanza kama pre eclampsia, na ikiwa very severe ndo inakuwa eclampsia(think of this like a spectrum, where by at the low end you have pre eclampsia, and at the high end you have eclampsia).

Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida!!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 150/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)...

Pressure ikiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila intervention yoyote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Kwa bahati mbaya sana, matibabu ya ECLAMPSIA ni termination of the pregnancy!! bila kujali wiki za ujauzito!!
Lakini, kama mama akiwa na dalili za pre eclampsia(kabla hajapata seizures/degedege ambapo na jina la ugonjwa litabadilika pia).

Kulingana na dalili za mama na wiki za ujauzito, madaktari wanaweza kujaribu kushusha presha yake kwa dawa na kumfanyia a close monitoring na kuangalia kama wanaweza ku push huo ujauzito ili awezee kudeliver, na hapa care kubwa ni kumantain blood pressure ili isiwe juu na kusababisha ECLAMPSIA.

I hope I have tried to explain vizuri, huu ni ugonjwa ambao ni complex na una mambo mengi, nimejaribu kutumia lugha ya kawaida; na samahanini sana kwa kuchanganya lugha, kama kuna kitu hakijaeleweka mnaweza kuuliza for more explanations. Eli79


Dr. Hiki Kifafa cha Mimba ni kwa Mimba ya kwanza au Mimba yoyote ile.Mfano Mtu Mimba ya Kwanza amajifungua salama je ya pili au ya tatu anaweza kupata kifafa
 
Pole sana Eli79.

Una uhakika hata kichwa hakikuwahi kumuuma? Maana sio lazima tumbo liume. Mtu anaweza akapata baadhi tu ya dalili ama zote kuendana na stage ugonjwa (Pre-eclampsia, eclampsia au severe eclampsia). Mi mtoto wangu wa kwanza nilipata hilo tatizo nikiwa na mimba ya miezi saba. Ndani ya wiki nilivimba vimba miguu nikachukulia poa, maumivu ya kichwa sikuyapa uzito, kuumwa tumbo nikafikiria labda ndo kawaida. Yani sikwenda hosp mpaka siku niliyokuwa nimeandikiwa kwaajili ya kuangalia maendeleo yangu na mtoto. Baada ya kuniona kitu cha kwanza dr alichotaka ni kupima mkojo na alivyoona majibu akaniambia lazima nibaki hosp. Kama ningechelewa hata siku moja ingeshakula kwetu. Kwahiyo dalili sio lazima zionekane muda mrefu ama maumivu yawe makali sana kwasababu inapokuwa kwenye level ya chini viashiria vyake navyo haviwi vikali.

Kuwa mjamzito ni delicate sana. Yani kila kitu,no matter how small COUNTS. Kutokujua kunafanya mtu anadhani labda hiki au kile ni hali ya kawaida tu kwenye ujauzito wakati inatakiwa muda wowote ukiona kitu cha tofauti ufuatilie. Kama nyie pengine mngewahi siku moja kabla mambo yangekuwa tofauti. Anyway, hopefully wifi yetu akipata tena mimba haitomsumbua maana bado uwezekano wa kuwa na 'smooth pregnancy' upo kama ilivyokuwa kwangu mimba ya pili.

Asante sana Lizzy, tumepoa tayari!
Tutajitahidi Mungu akitujalia tena tuwe makini zaidi. Naamini next time ujauzito utakuwa smooth tu.

Ni kweli alivimba miguu kidogo, lakini kama ilivyokuwa kawaida, na sisi tuliona ni kawaida tu..na imagine tulienda clinic siku mbili kabla..kwa hiyo haikupangwa tu.
 
Last edited by a moderator:
Pole Mimi nilipata tatizo hilo mwaka Jana, pre eclampsia dalili za awali za kifafa cha mimba, wakaniambia hamna jinsi Ni kumtoa mtoto tu. Yani pb alikuwa juu, epigastric pain, na Protein ikawa juu. Pia nlikuwa nimevimba sana.
 
Eli79

Pole sana. Sisi Leo tuko msibani kwa jirani yetu aliyefariki kwa kifafa cha mimba. Alikuwa na Mimba ya ya miezi 9. Sijui hii kitu jinasababishwa na nini.
 
Last edited by a moderator:
Pole Mimi nilipata tatizo hilo mwaka Jana, pre eclampsia dalili za awali za kifafa cha mimba, wakaniambia hamna jinsi Ni kumtoa mtoto tu. Yani pb alikuwa juu, epigastric pain, na Protein ikawa juu. Pia nlikuwa nimevimba sana .
Pole sana, haya ndiyo maisha ya mwanadamu. Hope utajaribu tena mwaka huu.
 
Eli79

Pole sana. Sisi Leo tuko msibani kwa jirani yetu aliyefariki kwa kifafa cha mimba. Alikuwa na Mimba ya ya miezi 9. Sijui hii kitu jinasababishwa na nini.
Dah acha kabisa mkuu, mke akiwa na mimba unashukuru na kuomba dua coz hizi mimba nazo zaweza kuwa balaa. Poleni sana.
 
Kwanza napenda ninashukuru mleta mada! Pili ninashukuru Dr kwa Elimu aliotoa na sababu zinazopelekea KIFAFA CHA MIMBA,somo zuri sana
 
Back
Top Bottom