Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

Duuuh.... Eli79!! Sina maneno mengine zaidi ya kusema POLE SANA
 
Last edited by a moderator:
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Ili tuweze kuufahamu vizuri ugonjwa wa kifafa cha mimba (eclampsia), ni vyema nikaanza kuelezea kuhusu PRE-ECLAMPSIA: kwa sababu kifafa cha mimba (eclampsia) kwa kawaida huanza kama presha ya damu kuwa juu wakati wa ujauzito (pre eclampsia), na hali ikizidi kuwa mbaya ndo inakuwa kifafa cha mimba (eclampsia-fikiria kama muendelezo wa ugonjwa huo huo, ambapo katika upande wa mwanzo kuna presha kuwa juu**pre-eclampsia** na upande wa mwisho kuna kifafa cha mimba**eclampsia**).

Pre eclampsia ni pale ambapo mgandamizo wa damu (blood pressure) kwa mama mjamzito unakuwa juu kuliko kawaida !!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 140/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction).

Mgandamizo wa damu ukiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila imatibabu, mama pia hupata degedege/kifafa, na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama. Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.

Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.

KIFAFA CHA MIMBA HUSABABISHWA NA NINI?

Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.

Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.

Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA

Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA/KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KIFAFA CHA MIMBA

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu(kama yalivyotajwa hapo juu) wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

Pia, ni muhimu kwa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapofahamu kuwa wameshika mimba, na kuendelea kuhudhuria kliniki kwa kadri wanavyopangiwa. Pia ni muhimu kwenda kituo cha afya/ hospitali pale tu mjamzito anapoona dalili za hatari (kuumwa na kichwa sana, kutokwa na damu sehemu za siri, mapigo ya mtoto kupungua,kupoteza fahamu).

Cc charminglady Heaven Sent The Boss Elli
 
dangers-of-pre-eclampsia.jpg

KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Ili tuweze kuufahamu vizuri ugonjwa wa kifafa cha mimba (eclampsia), ni vyema nikaanza kuelezea kuhusu PRE-ECLAMPSIA: kwa sababu kifafa cha mimba (eclampsia) kwa kawaida huanza kama presha ya damu kuwa juu wakati wa ujauzito (pre eclampsia), na hali ikizidi kuwa mbaya ndo inakuwa kifafa cha mimba (eclampsia-fikiria kama muendelezo wa ugonjwa huo huo, ambapo katika upande wa mwanzo kuna presha kuwa juu**pre-eclampsia** na upande wa mwisho kuna kifafa cha mimba**eclampsia**).

Pre eclampsia ni pale ambapo mgandamizo wa damu (blood pressure) kwa mama mjamzito unakuwa juu kuliko kawaida !!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 140/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction).

Mgandamizo wa damu ukiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila imatibabu, mama pia hupata degedege/kifafa, na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.

Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.

KIFAFA CHA MIMBA HUSABABISHWA NA NINI?

Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.

Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.

Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA

Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA/KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KIFAFA CHA MIMBA

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu(kama yalivyotajwa hapo juu) wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

Pia, ni muhimu kwa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapofahamu kuwa wameshika mimba, na kuendelea kuhudhuria kliniki kwa kadri wanavyopangiwa. Pia ni muhimu kwenda kituo cha afya/ hospitali pale tu mjamzito anapoona dalili za hatari (kuumwa na kichwa sana, kutokwa na damu sehemu za siri, mapigo ya mtoto kupungua,kupoteza fahamu).

Cc charminglady Heaven Sent The Boss Elli
Barikiwa mpendwa ktk bwana!!!
 
Magonjwa yakielezewa zaidi ndipo na uoga unaongezeka lakini ni vyema kujua haya mambo ili kujua cha kufanya.Shukrani kwa wote mnaojitolea kutupa elimu kuhusu magonjwa mbalimbali.
 
MSc yangu ilihusu pre/eclampsia na Cytokines profile. Wamama wanakufa hakika na ni ugonjwa hatari.
 
hebu hapa tuambiane ukweli na wala tusimung'unye maneno! tusiishie kutaja tu dalili. hebu madoctor tuwe wakweli kuhusu kifafa cha mimba. Nijuavyo mimi kifafa cha mimba hutokea kwa mwanamke ambaye amepewa mimba na mwanaume ambaye hajawahi kuzaa naye. ni mzio wa mbegu ngeni za kiume!
kifafa cha mimba hutokea kwa mama ktk ujauzito wake wa kwanza. kama kikitokea ktk ujauzito wa pili au zaidi basi huo ujauzito si wa mwanaume wa kwanza!
ukitaka amini hivyo la hutaki achaa! lkn huo ndo ukweli ingawa unakera sana!
 
Napi

Napingana na wewe. Nilishapata pre eclampsia mara mbili na sio nimezaa na wanaume tofauti. So kwa maelezo yako mbegu za mume wangu zinanipa mzio?
 
hebu hapa tuambiane ukweli na wala tusimung'unye maneno! tusiishie kutaja tu dalili. hebu madoctor tuwe wakweli kuhusu kifafa cha mimba. Nijuavyo mimi kifafa cha mimba hutokea kwa mwanamke ambaye amepewa mimba na mwanaume ambaye hajawahi kuzaa naye. ni mzio wa mbegu ngeni za kiume!
kifafa cha mimba hutokea kwa mama ktk ujauzito wake wa kwanza. kama kikitokea ktk ujauzito wa pili au zaidi basi huo ujauzito si wa mwanaume wa kwanza!
ukitaka amini hivyo la hutaki achaa! lkn huo ndo ukweli ingawa unakera sana!
Kila familia ina watoto wa nje ya ndoa, si ingekuwa balaa,
Huu ushauri wako ni sawa na nguvu za giza.
 
Jamani nami nauliza hichi kifafa cha mimba kinatokea wakati w ujauzito tu mtu akijifungua hakiendelei maana nini mama yangu mdogo Ana mwaka wa sita Sasa yupo kitandani na wanasema anakifafa Cha mimba msaada please
 
Lkn pia inaaminika mjamzito akiwa anakula kwa wing viaz vtamu vilivyoçhemshwa basi ni ngumu kwake kukumbwa na kifafa cha mimba
 
Back
Top Bottom