Elimu kuhusu Kifafa cha Mimba: Fahamu Chanzo, Dalili, Tiba na Tahadhari

kwenye blue matunda yanaongezea nini katika kukinga, na je vipi akiwa mjamzito kwa mara ya pili apunguze hicho kiasi cha matunda? naomba unifahamishe kiundani hapa madau.

Pia kwa kuongezea ni muhimu mama mjamzito kujitahidi kupunguza kiwango cha chumvi anayotumia, na hasa chumvi ya kuongezea mezani (raw salt)na pia kuongeza kiasi cha matunda anachokula. Kwa mimba ya kwanza, ni vizuri kufanya utaratibu wa kujifungulia hospitali kubwa just incase (badala ya zahanati).

Kuna kituo hapo kabla ya issue ya mimba ya kwanza ndugu. Kujibu suala lako, matunda yatasaidia katika ku-balance diet, na hivyo kupunguza uwezekano wa presha, ambayo ndo underlying cause ya kifafa cha mimba. Pia wakati mjamzito anakuwa anatamani kula kila wakati, akijitahidi kula matunda kwa wing itasaidia pia kutokuwa na uzito wa kupita kiasi.Mimba ya kwanza inahitaji uangalizi zaidi na dharura zaweza tokea, ikiwemo hii ya kifafa cha mimba. All in all, ushauri wa daktari unahitajika, as no two people/patients are the same.
 
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions). Sababu kamili za ugonjwa huu hazijukani. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu zikiwemo:-
(i) Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.
(ii) Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.
(iii) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.
(iv) Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

Hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa huu, bali nguvu huelekezwa katika kuchukua hatua za kuepuka tatizo hili kwa kuwashauri wanawake wasibebe mimba katika umri mdogo au mkubwa sana. Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi. Kifafa cha mimba kikisha tokea nguvu huelekezwa katika kupunguza madhara yatokanayo na kifafa hicho. Kwa mfano kuzuia degedege isirudie rudie kwa kutoa dawa za kuzuia degedege. Kutoa dawa za kuteremsha msukumo wa damu, iwapo uko juu, na vile vile kumsaidia mama ajifungue mapema mara itakapoonekana mtoto amefikia umri wa kuzaliwa

Asante sana mama mdogo.
 
Tatizo la kifafa cha mimba limekuwa comon sana kwa mda huu, kwa hapa tanzania kati ya wanawake 100 wanaojfungua 20 husumbuliwa na kifafa cha mimba ambapo watano hupoteza maisha(my research done in BUKOMBE District ths year)

kwa sababu hyo basi leo na ningependa kdogo nitoe elimu kuhusu hl tatzo.

NI AKINA NANI HUPATWA NA HILI TATIZO.

1. Wanawake wote wenye mimba za kwanza
2. Mimba za mapema kabla ya 20
3. Wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao
4. Wanawake walev hasa wakiwa wajawazito
5. Wavutaj wa sigara
6. Wanawake wenye visukar
7. Wanawake wenye presha
8. Mimba za uzeeni baada ya miaka 35
9. Wanawake wenye tabia ya kubadlisha badlisha wanaume
10. Wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata
11. Mimba za mapacha
12. Kuzaa mara nyingi

Mwanamke mwenye kuwa na moja ya mambo hayo ana hatar kubwa ya jupata presha au hatar wakat wa kujifungua. hvyo lazma wawe makini.

Tuonane tena next tyme tujfunze dalili, je utajuaje kama nina hatar ni dalil zp wakat wa ujauzto huashria kifafa cha mimba. KAMA UNA SWALI KUHUSU MAMBO HAYO JUU ULIZA HAPA UJIBIWE.
 
Nampongeza mtoa mada maana ni muhimu hasa kwa sababu tatizo hili linaongezeka,wakati tukisubiri mwendelezo wa somo kama alivyo ahidi mtoa mada,napenda wana jf wajua kinachosabibisha tatizo hili hakijulikani.Point zilizotajwa hapo juu ni mambo yanayoweza kuchangia tu mama kupata tatizo hili,si kwamba mama ukiona point moja inakuhusu eti uhofu huenda ukapata tatizo hili.

Cha msingi ni muhimu kwenda klinic upatapo mimba maana watakupima blood pressure kila unapokwenda ni rahisi kugundua kama kuna dalili za BP kuanza kupanda tofauti na mwanzo na wataweza kudhibiti mapema maana hiyo ni moja ya dalili za kwanza.
 
Nampongeza mtoa mada maana ni muhimu hasa kwa sababu tatizo hili linaongezeka,wakati tukisubiri mwendelezo wa somo kama alivyo ahidi mtoa mada,napenda wana jf wajua kinachosabibisha tatizo hili hakijulikani.Point zilizotajwa hapo juu ni mambo yanayoweza kuchangia tu mama kupata tatizo hili,si kwamba mama ukiona point moja inakuhusu eti uhofu huenda ukapata tatizo hili.

Cha msingi ni muhimu kwenda klinic upatapo mimba maana watakupima blood pressure kila unapokwenda ni rahisi kugundua kama kuna dalili za BP kuanza kupanda tofauti na mwanzo na wataweza kudhibiti mapema maana hiyo ni moja ya dalili za kwanza.

Vizur mama akienda clinic atleast mara 5-8 inasaidia kugundua hzo risk facoq tayari kwa kuchukua action.
 
Na vipi mwenye presha ya kushuka anaweza kukutwa na tatizo hilo akiwa mjamzito?
 
Tatizo la kifafa cha mimba limekuwa comon sana kwa mda huu, kwa hapa tanzania kati ya wanawake 100 wanaojfungua 20 husumbuliwa na kifafa cha mimba ambapo watano hupoteza maisha(my research done in BUKOMBE District ths year)

kwa sababu hyo basi leo na ningependa kdogo nitoe elimu kuhusu hl tatzo.

NI AKINA NANI HUPATWA NA HILI TATIZO.

1. Wanawake wote wenye mimba za kwanza
2. Mimba za mapema kabla ya 20
3. Wanawake ambao wazaz,bib au ndg zao wa karbu waliwah kupatwa na matatzo ya kifafa katka mimba zao
4. Wanawake walev hasa wakiwa wajawazito
5. Wavutaj wa sigara
6. Wanawake wenye visukar
7. Wanawake wenye presha
8. Wimba za uzeeni baada ya miaka 35
9. Wanawake wenye tabia ya kubadbadlishalisha wanaume
10. Wanawake waliopatwa na kfafa mimba zao za kwanza kuna hatar kukpata kifafa tena mimba znazofuata
11. Mimba za mapacha
12. Kuzaa mara nyingi

Mwanamke mwenye kuwa na moja ya mambo hayo ana hatar kubwa ya jupata presha au hatar wakat wa kujifungua. hvyo lazma wawe makini.

Tuonane tena next tyme tujfunze dalili, je utajuaje kama nina hatar ni dalil zp wakat wa ujauzto huashria kifafa cha mimba. KAMA UNA SWALI KUHUSU MAMBO HAYO JUU ULIZA HAPA UJIBIWE.

RK nashukuru sana kwa hili darasa huru ambalo umeamua kutupa, nimepitia post yako na inaonekana ina mapungufu makubwa sana hasa kwenye sehemu hizo nilizo highlight!

Approach uliotumia kuelezea hili tatizo sio sahihi kabisa; huwezi kuanza kuelezea tatizo kwa kutuelezea risk, kabla hujaeleza tatitizo ni nini? mambo mengi hayako sawa mfano; Kuna tofauti gani kati ya kifafa cha mimba (eclampsia) na Kifafa cha kawaida (epilepsy).

Kumbuka hapa unaongea na watu wa kawaida (lay people) na sio ma doctor wenzako. Hata huo utafiti ulio ufanya Bukombe tungependa utuelezee, objectives na methodology zake na kwanini unahisi ni representative ya Tanzania yote (20% ya wanawake husumbuliwa na kifafa cha mimba?) kwa takwimu zilizopo ni wanawake 6 hadi 100 kati ya 10,000 ndio hupatwa na tatizo hili. Tungependa u publish hizo finding zako zinaweza kusaidia hata WHO kutengeneza guidelines mpya.

Kama mmoja wa wachangiaji walivyosema hapo juu, sababu hasa ya kiifafa cha mimba haijulikani, na hiyo orodha uliyoitoa ni ya risk tu, na hivyo kusema "nani hupatwa na tatizo hili" sio sahihi labda ungesema walio kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili. Hata hivyo inaonekana kidogo umetuchenga hapo kwa sababu kuna kitu kinachoitwa pre eclampsia (kabla ya kifafa) na eclampsia ( kifafa) sio lazima mtu mwenye pre eclampsia aende kwenye eclampsia.

Sitaki kuzichambua hizo risks mojamoja, kwa ujumla sikubaliani na jinsi ulivyo mu address mwanamke hapa, as if yeye ndo chanzo cha matatizo yote, hiyo si kweli, naomba ukazipitie theories zote 12 za pregnancy induced hypertension utaona kuwa mama, baba na mtoto aliyeko tumboni wote wanahusika katika hili.

Unaposema mimba za uzeeni unamaana gani? mwanake mzee ni nani? au unamaana mwanamke mzee ni yule aliye koma hedhi ambaye tunajua hawezi tena kubeba mimba kwa njia ya kawaida. Pitia hizo highlight hapo nadhani mwenyewe utaona mapungufu yake. Nashauri ujipange tena vizuri utuletee darasa lilikamilika.
 
RK nashukuru sana kwa hili darasa huru ambalo umeamua kutupa, nimepitia post yako na inaonekana ina mapungufu makubwa sana hasa kwenye sehemu hizo nilizo highlight!
Approach uliotumia kuelezea hili tatizo sio sahihi kabisa; huwezi kuanza kuelezea tatizo kwa kutuelezea risk, kabla hujaeleza tatitizo ni nini? mambo mengi hayako sawa mfano ;Kuna tofauti gani kati ya kifafa cha mimba (eclampsia) na Kifafa cha kawaida (epilepsy).

Kumbuka hapa unaongea na watu wa kawaida (lay people) na sio ma doctor wenzako. Hata huo utafiti ulio ufanya Bukombe tungependa utuelezee, objectives na methodology zake na kwanini unahisi ni representative ya Tanzania yote (20% ya wanawake husumbuliwa na kifafa cha mimba?) kwa takwimu zilizopo ni wanawake 6 hadi 100 kati ya 10,000 ndio hupatwa na tatizo hili. Tungependa u publish hizo finding zako zinaweza kusaidia hata WHO kutengeneza guidelines mpya.

Kama mmoja wa wachangiaji walivyosema hapo juu, sababu hasa ya kiifafa cha mimba haijulikani, na hiyo orodha uliyoitoa ni ya risk tu, na hivyo kusema "nani hupatwa na tatizo hili" sio sahihi labda ungesema walio kwenye hatari zaidi ya kupatwa na tatizo hili.

Hata hivyo inaonekana kidogo umetuchenga hapo kwa sababu kuna kitu kinachoitwa pre eclampsia (kabla ya kifafa) na eclampsia ( kifafa) sio lazima mtu mwenye pre eclampsia aende kwenye eclampsia.

Sitaki kuzichambua hizo risks mojamoja, kwa ujumla sikubaliani na jinsi ulivyo mu address mwanamke hapa, as if yeye ndo chanzo cha matatizo yote, hiyo si kweli, naomba ukazipitie theories zote 12 za pregnancy induced hypertension utaona kuwa mama, baba na mtoto aliyeko tumboni wote wanahusika katika hili.

Unaposema mimba za uzeeni unamaana gani? Mwanake mzee ni nani? au unamaana mwanamke mzee ni yule aliye koma hedhi ambaye tunajua hawezi tena kubeba mimba kwa njia ya kawaida. Pitia hizo highlight hapo nadhani mwenyewe utaona mapungufu yake. Nashauri ujipange tena vizuri utuletee darasa lilikamilika.

Kwa kweli naungana kabisa na maelezo aliyotoa discoverer,hata mimi niliona kwa jinsi mada ilivyopresentiwa ni kama inawatisha sana akina mama wasio na uelewa wa ugonjwa huu, ndo maana niliona vile mleta mada ataendelea may be atakuja kujibu vema hoja alizoanisha discoverer.
 
Ni nini tiba ya tatizo la kifafa ha mimba? Na je, kune aina ngapi za vifafa vya mimba?
 
Mke wangu alipopata ujauzito kwa mara ya kwanza mwaka jana alikuwa na kifafa cha mimba mara tu mimba yake ilipofikia miezi 6 na kiliendelea hadi mimba ilipofikia miez 8 (mwezi Oktoba) alifanyiwa operation mtoto aliishi siku nane akafariki.Sasa ana mimba tena had sasa ni ya mwezi mmoja na nusu je ule ugonjwa huwa unajirudia? maana niliambiwa always huwa ni kwa mimba ya kwanza kwa sababu ya stress. Msaada plz wakuu.
 
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza. Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsions). Sababu kamili za ugonjwa huu hazijukani. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu zikiwemo:-

(i) Mimba ya kwanza, hususan katika umri mdogo chini ya miaka 20 na umri mkubwa zaidi ya miaka 35.
(ii) Wenye mimba ya mapacha hupata zaidi kuliko mimba ya mtoto mmoja.
(iii) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.
(iv) Kuwa na ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

Hakuna chanjo wala tiba ya kuzuia ugonjwa huu, bali nguvu huelekezwa katika kuchukua hatua za kuepuka tatizo hili kwa kuwashauri wanawake wasibebe mimba katika umri mdogo au mkubwa sana. Aidha mama wajawazito wanatakiwa kuwahi kliniki ambako watafuatiliwa maendeleo yao ili kubaini dalili za mwanzo za kifafa cha mimba na kushauriwa kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.

Kifafa cha mimba kikisha tokea nguvu huelekezwa katika kupunguza madhara yatokanayo na kifafa hicho. Kwa mfano kuzuia degedege isirudie rudie kwa kutoa dawa za kuzuia degedege. Kutoa dawa za kuteremsha msukumo wa damu, iwapo uko juu, na vile vile kumsaidia mama ajifungue mapema mara itakapoonekana mtoto amefikia umri wa kuzaliwa

chanzo.
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/207741-kifafa-cha-mimba.html
 
DAWA YA MARADHI YA MARADHI YA KIFAFA:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1:
Chukua udi swalib (udi sulb) kijiko kimoja cha chai (5ml),chukua na kijiko kimoja cha chakula (10ml) cha mbegu za habbat Sawda.

Twanga pamoja halafu changanya na Asali safi ya nyuki kijiko kimoja (10ml).
Tumia mchanganyiko huu kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa miezi mitatu hata mwaka mmoja (miezi 3-miezi12).

TIBA 2:

Kunywa maji yaliyochemshwa na Harmal.Kisha baada ya kunywa ujipake kifuani Mafuta ya Habat Sawda na unywe kijiko kimoja (10ml) cha mafuta hayo.

Treating epilepsy through herbal

Pomegranate+leaves+can+help+curing+epilepsy+as+per+indian+traditional+medicines+ayurveda.JPG

Epilepsy* is an ailment that can be cured but the patient and his/her family members need to take certain precautions. As far as natural and herbal ways of treatment are concerned, here are a few remedies:

1. Give onion juice (around 3 ounce) daily mixed with small quantity of water in the morning. It has to be given regularly for at least 40 days.

2. If the patient is given slight 'heeng' (Asafoetida) along with lemon to chew, it will be helpful to the epileptic. The patient shouldn't immediately gobble it up, rather let it in the mouth and chew slowly.

3. Bake garlic (light broiling) for a while in oil and administer it to the person suffering from epilepsy on a regular basis.

4. Take 60 gms 'henna' (mehndi) juice along with 250 gm milk. It cures the condition as per ayurveda.

4. A wonderful remedy in Indian ayurvedic medicinal system is to boil pomegranate leaves (100 grammes) in 500 gramme water. When just a quarter water remains, filter it and add 60 gramme 'ghee' and an equal amount of sugar. Give it to patient twice in day, in the morning and in the evening. Mostly it works.

Tumia Dawa kisha uje unipe Feedback.By MziziMkavu.
 
Ndugu wana JF, naomba kujuzwa kifafa cha mimba ninini, kinatokeaje, kinasababishwa na nini, nini dalili zake na jinsi ya kukizuia, mana nimeuliza wamesema sio epileps but ni eclampsia sasa kisogo inanichanganya, ninandugu yangu amefanyiwa oparation mimba ikiwa na miezi nane kamili na mtoto amekufa kisa eti alipata dalili zote za kifafa cha mimba, yeye haongeai hadi sasa.
 
Mke wangu alipopata ujauzito kwa mara ya kwanza mwaka jana alikuwa na kifafa cha mimba mara tu mimba yake ilipofikia miezi 6 na kiliendelea hadi mimba ilipofikia miez 8 (mwenz oktoba) alifanyiwa operation mtoto aliishi siku nane akafariki.Sasa ana mimba tena had sasa ni ya mwezi mmoja na nusu je ule ugonjwa huwa unajirudia? maana niliambiwa always huwa ni kwa mimba ya kwanza kwa sababu ya stress. Msaada plz wakuu.

Nivo uliza uliza wanasema maranyingi huwa kinarudia, chakushauri akipata kifafa cha mimba miezi ya sita wamtoe mtoto miezi saba au wiki kati ya 28-30 huwa wanaishi yani akifika wiki ya 32 -33 huwa hawaishi walau 34 kidogo factor sijui
 
1. JF Doctor naomba msaada kuhusu KIFAFA CHA MIMBA...

- Nini dalili za awali za kifafa cha mimba?
- Kifafa cha mimba kinasababishwa na nini?
- Kinatokea mimba ikiwa na miezi mingapi

2.
Habarini wapendwa,
Nina maswali kuhusu huu ugonjwa uwapatao wanawake wajawazito, kifafa cha mimba:

1. Ni nini chanzo cha ugonjwa huu?
2. Zipi dalili za huu ugonjwa?
3. Je, inawezekana kuwa nao na bado ukaendelea kulea mimba na kujifungua bila tatizo lolote?

I just lost my baby today, I was so dejected nilipoambiwa my wife had "kifafa cha mimba" and there's no way to keep the baby-to-be, just a month to go azaliwe. Imeniuma coz sikujua kuhusu huu ugonjwa.

Michango kutoka kwa WanaJF

dangers-of-pre-eclampsia.jpg

KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Ili tuweze kuufahamu vizuri ugonjwa wa kifafa cha mimba (eclampsia), ni vyema nikaanza kuelezea kuhusu PRE-ECLAMPSIA: kwa sababu kifafa cha mimba (eclampsia) kwa kawaida huanza kama presha ya damu kuwa juu wakati wa ujauzito (pre eclampsia), na hali ikizidi kuwa mbaya ndo inakuwa kifafa cha mimba (eclampsia-fikiria kama muendelezo wa ugonjwa huo huo, ambapo katika upande wa mwanzo kuna presha kuwa juu**pre-eclampsia** na upande wa mwisho kuna kifafa cha mimba**eclampsia**).

Pre eclampsia ni pale ambapo mgandamizo wa damu (blood pressure) kwa mama mjamzito unakuwa juu kuliko kawaida !!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 140/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction).

Mgandamizo wa damu ukiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila imatibabu, mama pia hupata degedege/kifafa, na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.

Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.

Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.
Kila mjamzito mwenye dalili hizi ni muhimu aonwe na mtaalam wa afya ili apimwe na kupewa ushauri.

KIFAFA CHA MIMBA HUSABABISHWA NA NINI?

Sababu ya ugonjwa huu kutokea hazijulikani mpaka sasa ingawa zipo nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea kutokea kwake. Mojawapo ya nadharia hizo inaelezea kuwa ugonjwa huu hutokana na matatizo ya ukuaji wa kondo la nyuma (placenta). Mishipa ya damu inayounda placenta ikikosea jinsi ya kujikita kwenye ukuta wa kifuko cha uzazi husababisha mishipa hiyo kuwa na tabia tofauti na ile ya kawaida na kusababisha mjazito kupata msukumo mkubwa wa damu na kifafa cha mimba. Kwa vile ugonjwa huu huonekana kutokea zaidi kwenye familia fulani kuliko nyingine, inaaminika kuwa urithi pia huchangia kupata ugonjwa huu. Hii inamaanisha mjamzito ambaye mama yake aliwahi kupata kifafa cha mimba ana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba.

Wanawake ambao wana tatizo la msukumo wa damu, kisukari, unene kupita kiasi, ugonjwa wa figo kabla ya ujauzito wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata kifafa cha mimba. Kwa sababu hii, wanawake wote wenye matatizo haya wanashauriwa kufuatiliwa kwa karibu na mtaalam katika kipindi chote cha ujauzito.

Mjamzito aliyepata kifafa cha mimba kwenye ujauzito uliopita, ana uwezekano mkubwa wa kupata tena.

Imegundulika kuwa iwapo mwanamke anazaa na mwanaume mwingine tofauti na aliyezaa naye awali, uwezekano wa kupata kifafa cha mimba huongezeka.

Ujauzito kwa mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 40 huongeza uwezekano wa kupata kifafa cha mimba.

TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA

Tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu ugonjwa huu husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyumba ndani ya kifuko cha uzazi. Bila kutoa kondo la nyuma mgonjwa hawezi kupona.

Iwapo ugonjwa huu utagundulika kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzalishwa.
Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kumzalisha huweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya mama na mtoto kuathirika iwapo ujauzito utaendelea.
Mojawapo ya hatari inayoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa kendelea ni mtoto kufia tumboni, kupoteza fahamu kwa mjamzito na kupata dalili za “degedege“, damu kupoteza uwezo wa kuganda na kusababusha mjamzito kupoteza damu nyingi, damu kuganda mwilini na kuziba mishipa, kondo la nyuma kujitenga na kifuko cha uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa, figo za mjamzito kushindwa kabisa kufanya kazi, mjamzito kupata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.
Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.
Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani. Hii hutegemea na uwepo na nafasi ya kulaza wagonjwa kwenye hospitali.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

JINSI YA KUJIKINGA/KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA KIFAFA CHA MIMBA

Ingawa hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba, wanawake walio kwenye makundi ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu(kama yalivyotajwa hapo juu) wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

Pia, ni muhimu kwa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapofahamu kuwa wameshika mimba, na kuendelea kuhudhuria kliniki kwa kadri wanavyopangiwa. Pia ni muhimu kwenda kituo cha afya/ hospitali pale tu mjamzito anapoona dalili za hatari (kuumwa na kichwa sana, kutokwa na damu sehemu za siri, mapigo ya mtoto kupungua,kupoteza fahamu).

Cc charminglady Heaven Sent The Boss Elli

Kwanza pole sana mkuu.

Kifafa cha mimba kitaalamu hujulikana kama ECLAMPSIA. Ni kati ya magonjwa ambayo yanaongoza katika kusababisha vifo vya wamama wajawazito katika 3rd world countries, Tanzania included.

Chanzo cha ECLAMPSIA:

Kiukweli, hakuna kitu kimoja ambacho kinafahamika kuwa ndio kisababishi cha ugonjwa huo, yaani chanzo bado hakijafahamika, lakini kuna risk factors (visababishi) nyingi nyingi ambazo ziko associated na eclampsia.

Pia ziko theory nyingi sana zinazojaribu kuelezea ni kitu gani hasa kinatokea wakati wa eclampsia(watu wengine huuita eclampsia kama 'a disease of theories' kwa sababu hii). Baadhi ya risk factors za eclampsia ni kama zifuatazo:

1.Kama ni mimba ya kwanza kwa mama.

2.Kama kuna historia ya eclampsia kwa mama yako/ndugu yako.

3.Kama una chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wakati wa ujauzito.

4.Kama ulikuwa na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.

5.Kama uzito wako ni mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).

6.Kama una historia ya eclampsia mimba iliyopita.

7.Mimba ya mapacha.

8. Kama baba wa ujauzito huo ni a new partner kwa mama.

Dalili za tatizo hili: Naomba kwanza nikueleze kuhusu PRE-ECLAMPSIA ninapokuelezea kuhusu dalili za eclampsia: kwa sababu eclampsia kwa kawaida huanza kama pre eclampsia, na ikiwa very severe ndo inakuwa eclampsia(think of this like a spectrum, where by at the low end you have pre eclampsia, and at the high end you have eclampsia).

Pre eclampsia ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida!!(MARA NYINGI CUT OFF POINT NI 150/90). Hii huendana na dalili zingine kama maumivu makali ya kichwa,kuvimba miguu,maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),kushindwa kuona vizuri(blurred vision),mapigo ya mtoto kushuka,mtoto kutokukua vizuri tumboni(intra uterine growth restriction)...

Pressure ikiendelea kupanda zaidi huweza kupata kondo la mtoto kuachia kabla ya muda(abruptio placenta), mtoto kufia tumboni, figo kufeli, seli chembe-sahani za mama kupungua (hizi ndio husaidia damu kuganda pale unapopata jeraha) na kusababisha mama kutoka damu sana na hata kufariki.

Sasa, kama pressure ikiendelea kupanda bila intervention yoyote, mama pia hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa), na pia kuchanganyikiwa(confusion), na hata kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Kwa hiyo basi dalili za eclampsia ni zile zote za pre eclampsia kujumlisha kifafa/degedege.

Pre eclampsia na eclampsia hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Kwa bahati mbaya sana, matibabu ya ECLAMPSIA ni termination of the pregnancy!! bila kujali wiki za ujauzito!!
Lakini, kama mama akiwa na dalili za pre eclampsia(kabla hajapata seizures/degedege ambapo na jina la ugonjwa litabadilika pia).

Kulingana na dalili za mama na wiki za ujauzito, madaktari wanaweza kujaribu kushusha presha yake kwa dawa na kumfanyia a close monitoring na kuangalia kama wanaweza ku push huo ujauzito ili awezee kudeliver, na hapa care kubwa ni kumantain blood pressure ili isiwe juu na kusababisha ECLAMPSIA.

I hope I have tried to explain vizuri, huu ni ugonjwa ambao ni complex na una mambo mengi, nimejaribu kutumia lugha ya kawaida; na samahanini sana kwa kuchanganya lugha, kama kuna kitu hakijaeleweka mnaweza kuuliza for more explanations. Eli79

Kuongezea maelezo ya Dr hapo, ukisikia Pre eclampsia si chochote kigumu ila ni hali ya kupatwa na preha kwa mama mjamzito ambaye si mgonjwa wa presha kwa hali ya kawaida na inatokea mimba ikifika wiki 20 na kuendelea hali ambayo inaambatana na kuchuja kwa protini kwenye mkojo.(Kiwango maalum cha protini na presha pia kinatumika ku classify hili kama ni mild pre eclampsia au ni severe).

Pili, Eclampsia sasa(dalili zimeshatajwa na Dr hapo juu) huwa ina tabia ya kuwapata kina mama ambao wana/ wameingia kwenye "severe pre eclampsia" ambaye ni presha kali wakati wa ujauzito. Hii inamweka huyu mama katika hatari kubwa ya kuingia kwenye kifafa sasa au eclampsia yenyewe, shetani mkuu mwenyewe.

Kwa wale wenye presha kali na wanaonyesha dalili za hatari I.e. kizungu zungu, kichwa kuuma sana, maumivu juu ya kitovu hasa upande wa kulia, kushindwa kuona vizuri (features of impending eclampsia) wana kua managed kwa aggressive blood pressure control na pia dawa ya kumkinga na kifafa (MgSo 4 prophylaxis) ikifanikiwa kushuka anaangaliwa kwa karibu kujaribu ku delay tarehe ya kujifungua, depending on the mother's gestation age.

Akiingia kwenye eclampsia sasa anapewa dawa za kumtuliza na kuzalishwa baada ya hapo.

Unfortunately kuna kuaga na risk kubwa ya kumpoteza mtoto kutokana na kutozingatia matumizi ya dawa kwa wakina mama husika au hata hiyo presha yenyewe inaweza leta hiyo shida.

Kikubwa hapa ni kuhudhuria kliniki mapema na mara kwa mara na pia "kuzingatia matumizi ya dawa za presha" ni muhimu sana.

Mwezi mmoja tu kabla ya tarehe ya matarajio ya kujifungua ni tarehe salama pia ya kujifungua endapo atawahiwa kabla heart rate ya mtoto haijaanza kubadilika. Kwasababu kikubwa tunachohofia hapa ni maturity ya mapafu ya mtoto ambayo ni ya mwisho ku mature mtoto asije zaliwa na Respiratory Distress Syndrome. Huwa Tunatoa dawa ya kuharakisha hii process kwa kina mama wenye risk ya kujifungua kabla ya term.

CC Eli79

Pole sana kwa kupoteza mtoto.

Nina rafiki yangu aliambiwa ana kifafa cha mimba mimba ikiwa na miezi 7 (kama nakumbuka).

Nchi za wenzetu wanagundua kwa kuwapima wanawake wakati wa clinic hata kabla dalili hazijaonekana kwa macho.

Walichofanya ni walimzalisha kabla ya muda na mtoto akabaki hospital mpaka akakomaa...

Wahaya hili tatizo hawanaga tofauti na baadhi ya makabila ambayo mama alikuwa ananitajia kama mifano ambao kwao hili tatizo ni kama sugu... sababu (according to my mum) ni wahaya wanatumia mitishamba sana wakati wa ujauzito kama njia ya ku prevent hili tatizo na matatizo mengine.

Nakumbuka mama yangu alikuwa ananambia wewe acha kunywa hizi dawa uone kama hujapata kifafa cha uzazi.

Ni kibaya sana, unakuta mzazi anajing'ata wakati wa kujifungua...wengine wanakuwa vichaa kabisa na kuua watoto..nadhani kinaathiri ubongo pia...
 
kifafa cha mimba.png

KUHUSU KIFAFA CHA UZAZI(MIMBA)

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini. Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua.

SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.

Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili (Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na

1. Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes.
2. Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.

DALILI.
1. Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).
2. Shinikizo la damu kupanda.
3. Kuwa na protein katika mkojo.
4. Kizunguzungu na macho kuoana giza.
5. KUPATWA NA KIFAFA.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.

1. Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.
2. Kuzaa mtoto mfu.
3. Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)
4. Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)
5. Kuzaa mtoto mwenye uzito
pungufu.

NINI KIFANYIKE?

1. Kujifungulia katika kituo cha afya.
2. Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.
3. Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda.


Ukiwa na Swalila ziada unaweza kunitafuta kwa kubonyeza hapa.
 
355px-NWTND_pab_Page_16-1.png


KUHUSU KIFAFA CHA UZAZI(MIMBA)

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo
yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.
Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada
ya kujifungua.

SABABU ZINAZO PELEKEA TATIZO HILO.

Sababu la tatizo bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua. Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili
(Predisposi ng factors). Baadhi ni pamoja na


1.Mwanamke kuwa na wenza wengi hali inayopelekea muingiliano wa Chromosomes.
2.Sehemu moja ya ubongo kuwa na damu nyingi kuliko nyingine na kupelekea shinikizo la damu kuwa kubwa katika ubongo.

DALILI.

1.Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).

2.Shinikizo la damu kupanda.

3.Kuwa na protein katika mkojo.

4.Kizunguzungu na macho kuoana giza.

5.KUPATWA NA KIFAFA.

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.

1.Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.

2.Kuzaa mtoto mfu.

3.Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)

4.Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)

5.Kuzaa mtoto mwenye uzito
pungufu.

NINI KIFANYIKE?

1.Kujifungulia katika kituo cha afya.

2.Kuhudhuria Klinik wakati wa ujauzito.

3.Kumuona daktari unapokuwa na viashiria vya hatari wakati wa ujauzito kama kuvimba miguu au shinikizo la damu kupanda.


Ukiwa na Swalila ziada unaweza kunitafuta kwa kubonyeza hapa.
Shukrani MZIZIMKAVU, ilimpata wife,ikichanganyika na marelia,ilikuwa mbaya sana, kwa bahati alikuwa anafaniya krinik MUhimbili,nilipoona dalili tu,haraka nilimwahisha na kufanyiwa operation.
 
Back
Top Bottom