Elimu bure iondolewe, watu waanze kulipa Ada

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,523
52,188
ELIMU BURE IONDOLEWE, WATU WAANZE KULIPA ADA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Hakunaga kitu cha bure kikawa na thamani, sijawahi kuona popote pale tangu nimezaliwa; hivyo ndivyo naweza anza makala hii.
Kitu cha thamani lazima kigharamiwe, na uthamani wa kitu upo kwenye gharama. Kusema elimu iwe bure kwa kweli ni kujidanganya, ni kushusha thamani ya elimu. Vitu vya bure vinatoka kwa Mungu pekee, lakini kwa sisi binadamu kwa kweli hakuna cha bure. Kama unataka cha bure mwambie aliyekuumba akupe, sisi binadamu hatunaga vya bure. Nikikupa lazima ulipie, ukinipa hakikisha nalipia, mambo ya bure yapo kwa Mungu tuu.

Kitu cha bure hakithaminiwi huo ndio ukweli, hakuna kitu cha bure kikathaminiwa labda kitoke kwa Mungu, lakini vya binadamu sio kweli.

Kwanza kwa nini iwe bure?
Utanijibu ni umasikini, ikiwa umejibu hivyo basi wewe ni mjinga, kwa hiyo kwa vile mtu watu/jamii ni masikini ndio maana utoe elimu bure, alafu unajiona umetoa umeisaidia jamii? Badala ungetengeneza mazingira ya kuuondoa umasikini ndani ya jamii watu waweze kulipa ada, ati wewe unaondoa ada, ajabu sana hii. Hivi utaondoa vingapi? mwishowe utaondoa nauli watu wasafiri bure, watu watibiwe bure mahospitalini, utaondoa Zaka watu wasali bure misikitini na makanisani, bure! bure! bure!

Kwa nini iwe bure? Mtu yeyote mwenye akili timamu lazima ajiulize swali hili; Kwa nini bure? Ukipewa bure inamaana wewe ni wa bure. Upewe bure imekuwa Zawadi? Zawadi ndio huwa bure na sio zaidi ya hapo.

Kwa nini iwe bure? Kwa nini serikali isitengeneze mazingira ya watu kuweza kulipa ada na sio kuondoa ada. Unaondoa ada alafu waalimu wanalia mishahara, hii ni akili ya wapi asee?

Unatoa ada alafu shule haina maabara, na maabara zikiwepo hazina apparatus. Unatoa Ada alafu shule hazina maktaba, na kama maktaba zipo basi hazina Mkutubi, hazina vitabu zaidi ya majarida ya Fema,hii ni akili ya wapi ndugu zangu. Unatoa ada alafu shule haina madawati, hii imekaaje?

Alafu waliotoa ada ukiwasikiliza wanavyojieleza utabaki mdomo wazi, kuna mmoja nilimsikia akisema; tumetoa ada na elimu ni bure ili kusaidia Kaya Masikini, badala wasaidie kuutoa umasikini watu waweze kulipa ada wao wanaondoa Ada, nani alisema umasikini unaletwa na watu kulipa Ada? Oooh! unajua hawawezi kulipa ada hawa sasa hawatasoma ukiiweka" Hivi mtu anashindajwe kulipa 20,000 au 50,000 kwa mwaka? Au ndio kufundishana uvivu na kulemazana.

Haya unaondoa Ada, alafu unashindwa kuongeza mishahara ya waalimu, unafikiri watawafundisha vizuri hao wanafunzi? Elimu ya bure huzalisha wanafunzi wa bure vichwa vikiwa bure kabisa.

Haya usiongeze mishahara ya waalimu, basi kuwepo na Posho, napo hakuna. Unatoa Ada alafu walimu haumpi Posho, ajabu sana hii. Alafu matokeo yakitoka watoto wamefeli unakuwa wakwanza kuwalaumu walimu, ajabu sana hii!

Kuna Member mmoja wa Jf Anaitwa FaizaFoxy hupenda kusema, huko shule mmeenda kusomea ujinga. Bure huzalisha ujinga ujinga. Sio ajabu vijana wa siku hizi wengi akili zao ni bure bure, hufuatilia mambo ya bure bure, udaku udaku kwa sababu udaku hauna gharama, ni bure kabisa.

Watu walipe Ada
Serikali ifanye utafiti ione ni kiasi gani cha Ada iwekwe kwa ajili ya watu kulipia ada kwa watoto wao.

Napendekeza kwa shule ya msingi Ada iwe 20,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 10,000 na muhula wa pili 10,000
Shule ya sekondari (O' Level) iwe 50,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 25,000 muhula wa pili 25,000
Shule ya sekondari ya juu (A'Level) Iwe 100,000 kwa mwaka. Muhula wa kwanza 50,000, muhula wa pili 50,000
Vyuoni kubaki kama kulivyo, watu wapewe mikopo ya riba nafuu.

Sasa wewe unajijua kabisa ni fukara, alafu unajitia kuzaa kama kuku ili uonewe huruma na serikali, ajabu sana hii. Ati sina uwezo wa kusomesha lakini una uwezo wa kuzaa, ajabu sana hii. Kama unauwezo wa kuzaa basi ongeza nguvu ya kuzalisha upate pesa ya kuwahudumia watoto wako.

Mtoto wa O'level hasa nyakati za likizo hashindwi kufanya kazi akapata hiyo 50,000 kwa ajili ya kujilipia ada. Ni kuendekezana tuu, tunafundisha watoto wetu uvivu, unakuta toto ipo likizo labda ni ya mwezi wa sita, kusoma halisomi, kufanya vibarua halifanyi, kazi kukaa tuu nyumbani, kuangalia muvi, kwa nini lisione maisha ni bure, kazi kukaa vijiweni, kwa nini lisijifunze uhuni, wapo watoto ninaowajua hivi leo wamefika mpaka elimu za juu na wamefanikiwa na walikuwa wanajisomesha. Na kwa waliofeli shule kwa sasa wanamaisha yao kwani tayari wanajua kufanya kazi za vibarua.

Elimu bure huzalisha kizazi cha bure bure

Mwanafunzi wa A' level hashindwi kuipata 100,000 kwa ajili ya ada yake. Akishamaliza kidato cha nne mwezi novemba, anakaa nyumbani zaidi ya mieiz sita, kama ni mtu wa kujishughulisha anakosaje hiyo 100,000? Lakini kwa vile wazazi ni wavivu si ajabu watoto wakikosa hiyo laki moja. Unajua mtu mvivu haoni kazi ya kufanya hata kama kazi zipo zimemzunguka. Wewe angalia hata wavivu wa nyumbani, unakuta limekaa tuu lakini vyombo vichafu, sebule chafu, nguo zake chafu, ukimuuliza huoni kazi sio ajabu akakuambia haoni. Ndivyo hata katika kazi za uzalishaji, wavivu husema hakuna kazi kwani hawazioni. Mvivu hupenda rahisi.

Serikali irudishe Ada, watu walipie Ada

UMUHIMU WA ADA
1. Chanzo cha mapato ndani ya serikali
2. Kuongeza thamani ya elimu katika jamii
3. Kuondoa uvivu katika jamii,watu watafanya kazi kwa ajili ya kulipa ada
4. Kuongeza Ari ya kujifunza kwa wanafunzi kwani watakuwa na uchungu wa hela zinazotolewa na wazazi wao.
5. Ada inaweza kutumika kuongeza mishahara au posho kwa walimu
6. Ada inaweza kutumika kununua na kuboresha vitendea kazi na miundo mbinu ya shule
7. Ada ni sehemu ya uzazi wa mpango, kwani watu watashindwa kuzaa watoto hovyo hovyo kwa kuogopa kushindwa kulipa ada. Jamii zinazosomesha watoto bure huzaa sana tofauti na zile jamii zinazopeleka watoto shule za kulipia ada
8. Ada huongeza thamani ya mwanafunzi kwani hasomi bure bali anachangia sehemu ya kile anachofundishwa, hivyo hupunguza unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waalimu. Uchunguzi wangu umebaini kwamba, shule zinazotoa Ada kubwa unyanyasaji huwa ni mdogo, waalimu huwaheshimu wanafunzi, tofauti na shule wanaotoa ada ndogo. Tuliosoma shule za ada ndogo kila mmoja ataungana na mimi kuwa kuna yule mwalimu aliyekuwa anatoa maneno ya shombo akitunyanyasa enzi zile twasoma.

9. Mtoto akifukuzwa Ada, husaidia kujua ukweli kuhusu maisha, na kuachana na yale mawazo kuwa akimaliza shule atajenga ghorofa.
10. Ada hujenga mtazamo wa mtoto kuwa " hakuna kitu cha bure" kila kitu lazima ulipie
11. Ada humjengea mtoto kujiamini na kumuwajibisha mwalimu ikiwa hataingia darasani. Ni kawaida kwa wanafunzi wanaolipa Ada kubwa kumuwajibisha mwalimu mzembe asiyeingia darasani. Lakini wanaosoma bure hawana uwezo huo kwani mwalimu atawajibu kwani mnalipia ninachowagea, ninyi si mnasoma bure. Kisha mwalimu atamalizia, niingie nisiingie darasani mimi mwisho wa mwezi pesa inaingia. Lakini mwalimu hawezi thubutu kuongea hilo shudu mbele ya shule zinazotoza ada kubwa, kwani kitumbua chake kitaingia mchanga.

HASARA YA ADA
1. Baadhi ya watu wavivu waliojipa jina masikini watashindwa kupeleka watoto shule na hivyo kuwakosesha watoto haki ya elimu.

Nafikiri tumeona kuwa Faida ni nyingi kuliko hasara ambayo ni moja.

Mwisho, Serikali rudisheni Ada, achaneni na mawazo ya kivivu kivivu, mambo ya bure mara nyingi ni kwa jamii zilizobobea kwenye uvivu.
Nafahamu, wapo watu watasema kuwa mbona kuna nchi zinatoa elimu bure, hakuna nchi yoyote makini inayoweza kufanya jambo la kivivu kama hilo.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mikumi, Morogoro
 
Naam Mkuu,nini maoni yako
Maoni yangu hapo kama nyongeza napendekeza uanzishwe mfuko wa elimu msingi ambao kazi yake kubwa ni kugaramia mahitaji ya shule zote za sekondari na msingi hapa pamoja na kushughulikia na maslahi ya walimu hasa upande wa posho n.k. mfuko huo uwe na bajeti yake pamoja na vyanzo vya mapato ambavyo kupata fungu kutoka serikalini,ada zitakazolipwa na wanafunzi pamoja na wadau wa maendeleo kutoka nchi za nje.
 
Maoni yangu hapo kama nyongeza napendekeza uanzishwe mfuko wa elimu msingi ambao kazi yake kubwa ni kugaramia mahitaji ya shule zote za sekondari na msingi hapa pamoja na kushughulikia na maslahi ya walimu hasa upande wa posho n.k. mfuko huo uwe na bajeti yake pamoja na vyanzo vya mapato ambavyo kupata fungu kutoka serikalini,ada zitakazolipwa na wanafunzi pamoja na wadau wa maendeleo kutoka nchi za nje.

Hakika umewaza kwa akili sana Mkuu. Hongera sana
 
Ukiwa unatoa Hoja angalia muktadha wa jamii kwa ujumla usiegamize fikra zako katika mlengo binafsi

Ni kweli kabisa, Muktadha wa jamii yetu ni jamii masikini uliochangiwa na sababu lukuki, kuu ni uvivu, ujinga, na unafiki. Kwenye uvivu ndipo sababu nyingi zipo mathalani kupenda mserereko, vya bure

Jamii lazima ibadilishwe kifikra mambo ya bure ni sehemu ya chanzo cha umasikini.
 
Elimu Bure imeathiri sehemu nyingine zikiwemo;

1. Wazazi wamekuwa wavivu kuhudhuria mikutano Shule.

2. Wazazi kukosa uchungu wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao. Sasa hivi hawatofautishi Shule ya msingi na sekondari

3.Kupunguza ziara za ukaguzi wa Shule na wakaguzi elimu.

4. Shule kuongeza madeni ya wazabuni

5. Hakuna masomo ya ziada/remedial

6.Serikali kushindwa kuajiri walimu wapya licha ya uhaba wa walimu.

7.Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kushindwa kutimiza majukumu yake na baadhi ya malipo na hivyo kutupia walimu majukumu ikwemo-
i. Kugeuza walimu maafsa TEHAMA wa kusajili wanafunzi
ii.Kugeuza walimu/kuwapa walimu kazi ya kuchapa na kuingiza data na majina ya watahini
iii. Kugeuza walimu kuwa wapiga picha tena bila malipo
iv. Kutupa jukumu la kuchapa leaving certificate kwa Shule.
 
Jamaa nimeuona wa ajabu sana kwa utopolo alioandika hapa. Wakati tunataka essence ya kodi zetu tunazolipa ionekane through social services kumbe kuna majitu yanataka tuendelee kusomewaga budget tu bungeni huku hela zikiwa hazifikishwi au zinaliwa na ma afisa elimu.

Mkuu, unajua ni watanzania wangapi wanalipa kodi hasa ile Direct Tax?
 
Kwani kipindi hizo Ada zinalipwa malalamiko haya hayakuwahi kuwepo? Too worse walimu walikuwa wanajitengenezea michango isio na ukomo mara twisheni, mara usafi, mara mtihani, mara sijui nini. Yani unalipishwa michango from January - December

Mkuu, michango sio Ada lakini
 
Back
Top Bottom