Edward Lowassa: Usahaulifu na hadithi za kusadikika

NI kweli, Lowassa ni mtu wa vitendo. Uamuzi wake wa kuipa kazi Richmond, ndiyo huu unaotugharimu leo. Hakuna umeme. Tanesco baada ya kutumia fedha inayopata kuwekeza, inajikuta inaishia kulipa makampuni ya umeme wa dharula.

Baada ya kutumia fedha kubresha maisha ya wafanyakazi wake, inatumia fedha inayopata kulipa mawakili wa kuendesha kesi kupambana na makampuni ya kitapeli ya Lowassa na swahiba wake Rostam Aziz.

Baadala ya kutumia fedha kuboresha miundo mbinu ya umeme, Tanesco inalazimika kuingia kwenye mikataba mingine ya kinyonyaji kwa kuwa Lowassa na wenzake wameshindwa kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la umeme nchini.

Mungu atuepushe na Lowassa kurudi tena madarakani.
 
Waingereza husema "give a dog bad name to kill it". Ndicho wewe ulichokifanya hapa kuhusu Hon. Lowassa. Ukweli utabaki pale pale kuwa alipokuwa PM alisimamia kwa ustadi mkubwa ujenzi wa shule mpya [ kata?] pia akiwa na master plan ya nini kifanyike ili elimu bora itolewe kwa wanafunzi. Unfortunately, baada ya yeye kujiuzulu viongozi waliobaki pamoja na Pinda wakaitelekeza mipango ya kuhakikisha elimu bora inatolewa. Kumbuka Lowassa alikuwa na mkono wa chuma ktk kusimamia utekelezaji wa mipango ya serikali something which Pinda and JK lack it.
Naona kama umejitoa akili namna flani hivi.
 
Ondoa matapishi yako hapa. Hon. Lowassa ni mchapa kazi asiyechoka. Ni rais wa JMT 2015.

Pangua hoja kwa hoja. Usigeuke Lusinde au Nchemba.

Samahani sana, nimepitiwa kidogo. Kumbe sera zenu ccm siku hizi zimeongezwa nguvu, baada ya uongo mmeongeza matusi kwa Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.
 
EL nimtu ambaye hafai kuwa KIONGOZI WA TAIFA kitugani kinamfanya atamani uraisi?. Mtu ambaye anajulikana hata kwa watoto wadogo kuwa ni fundi wa kugawa rushwa, jke,akipata nchi si hata kutembea itabidi tutoe rushwa?
 
Ondoa matapishi yako hapa. Hon. Lowassa ni mchapa kazi asiyechoka. Ni rais wa JMT 2015.

Acha uvivu wa kufikiri kati yako na mleta thread nani ametapika?alicho eleza ni ukweli usiopingika najua ukweli unauma....chungu lakini dawa
 
Huyu bwana EL naroho gani maana hana hata soni. Yote yaliyosemwa bado ana ujasiri wa kusimama na kumnadi mtu kupewa nafasi!! Ama kweli TZ ni jalala, kila uchafu unanafasi ya kutupwa humu. Mola hamsha hisia na uzalendo kwa watz wa kweli ili nchi ikombolewe na CDM hapo ARUMERU na 2015 iwe kama ulivyonena...
 
Back
Top Bottom