mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,306
- 6,514
Mkuu Chakaza kwa hiyo kwa sasa tusikusikie tena unawaita viongozi wengine mafisadi kwa kuwa na wao bado hawajapelekwa mahakamani...Hata mimi naweza kukubaliana nawe bwana mcubic kuwa Lowasa sio msafi. Na kwa kweli kama mtu ni mhalifu hata kama ni mwanao hakuna haja ya kumtetea bali kuhakikisha sheria inafuatwa kumhukumu. Hata vitabu vya Mungu vinaruhusu sheria kufuata mkondo.
Tatizo linalonipa mashaka ni kuwa, huyu Lowassa huyu tunaambiwa ana madhambi mengi na mwenyewe kajitetea lakini mwisho kajitoa muhanga kabisa kuwa mwenye ushahidi apeleke mahakamani. Sasa jee tukiacha watu individual, kweli vyombo vyote vya ushtaki kama Polisi, TAKUKURU, DP, Tume ya maadili na nini sijui wote hawa wameshindwa kumpeleka mbele ya sheria? Tena mtu aliyekinyima chama tawala raha na kukikosanisha na watu wake wanaweza kumwangalia na makosa yake bila kumfanya lolote?
Jaribu tuu kuwaza kwa undani, vinginevyo mniambie kuwa makosa hayo ya Lowassa basi yakiwekwa hadharani yatasababisha watu/mtu wasioguswa/asiyeguswa akaathirika.
Leo miaka karibu 9 tunaimba Lowassa fisadi no action, mwisho itafika 30 hata hawa watoto ambao watakuwa watu wazima watatuona wanafiki kupindukia. Hakuna kesi basi ni msafi full stop