Edward Lowassa kutua kwa kishindo Dodoma leo, bunge lahaha

Hata mimi naweza kukubaliana nawe bwana mcubic kuwa Lowasa sio msafi. Na kwa kweli kama mtu ni mhalifu hata kama ni mwanao hakuna haja ya kumtetea bali kuhakikisha sheria inafuatwa kumhukumu. Hata vitabu vya Mungu vinaruhusu sheria kufuata mkondo.
Tatizo linalonipa mashaka ni kuwa, huyu Lowassa huyu tunaambiwa ana madhambi mengi na mwenyewe kajitetea lakini mwisho kajitoa muhanga kabisa kuwa mwenye ushahidi apeleke mahakamani. Sasa jee tukiacha watu individual, kweli vyombo vyote vya ushtaki kama Polisi, TAKUKURU, DP, Tume ya maadili na nini sijui wote hawa wameshindwa kumpeleka mbele ya sheria? Tena mtu aliyekinyima chama tawala raha na kukikosanisha na watu wake wanaweza kumwangalia na makosa yake bila kumfanya lolote?
Jaribu tuu kuwaza kwa undani, vinginevyo mniambie kuwa makosa hayo ya Lowassa basi yakiwekwa hadharani yatasababisha watu/mtu wasioguswa/asiyeguswa akaathirika.
Leo miaka karibu 9 tunaimba Lowassa fisadi no action, mwisho itafika 30 hata hawa watoto ambao watakuwa watu wazima watatuona wanafiki kupindukia. Hakuna kesi basi ni msafi full stop
Mkuu Chakaza kwa hiyo kwa sasa tusikusikie tena unawaita viongozi wengine mafisadi kwa kuwa na wao bado hawajapelekwa mahakamani...
 
Pole sana muulizeni kikwete mbona humpeleki lowasa mahakani? Au ni kweli wewe ndio ulibariki hayo mbona hamthubutu? Acheni kukariri vihoja badala ya hoja.
hata mimi nitakwambia mfuate mnyika akupe ushahidi aliosema anao juu ya lowassa.......usijifanye unaegemea upande mmoja wakati hao viongozi wao ndio walikuwa wapiga matarumbeta wakubwa juu ya hili swala,na ndio ishu iliyowapatia umaarufu........
 
Lowassa is finished!

Kwa sasa yupo kwenye mapito ya kisiasa ambayo ameyapitia Augustino Mrema.

Mwezi uliopita Jijini Mwanza wakati wa Mkutano wa hadhara wa kumtambulisha Katibu Mkuu, Dk. Mashinji , aliwashangaza wananchi alipoanza kuwauliza kama wamemsahau. Alitegemea tena vijana watadeki barabara anayopita.

Kuna uwezekano hata udiwani utakuwa ni vigumu kuupata!
lowassa ni shujaa alipo tupo.
 
Uzuri wa sisi watanzania ni wagumu kuelewa alafu wepesi wa kusahau,jamani naomba niweke records very clear,wakati wa mrema hatukuwa na uelewa wa kisiasa kama sasa,wakati wa mrema baba wa taifa alikuwepo na alikuwa akisikilizwa sana na watanzania,kipindi hiki watanzania wanauelewa wa kupiliza,kipindi hiki CCM wote wamekuwa wezi,kipindi hiki sasa tuna social media na watu wanapata habari bila shida hata kama bunge halioneshwi live,so ni ujunga na upumbavu kumfananisha lowasa na mrema,lakini cha mwisho kwa kuwasaidia lowasa is far by far ahead of mrema kwa maswala ya kisiasa na experience kwa hiyo mfano huu hauendani kabisa,na kingine lowasa ana hela hayuko kama mchovu mrema ambaye anakuwa omba omba ili apate chochote kitu
 
Bado hajatua tu huyo fisadi Lowasa? Angalieni asije kuchafua hali ya hewa hapo Dodoma
Hata akitua hana uzito wa kutoa kishindo tena kwani uzito wake ni sawa gunia la pamba, mwenye kishindo sasa hivi ni Magufuli tu.
 
Mbona km unapanic hv! Acha kuropoka

Edo ni waziri mkuu aliyejiudhuru hana jipya na bado ataongea kwa dak 3. Sumaye naye ni waziri mkuu mstaafu Hana Jipya na hatumkumbuki kwa lolote, wote wanaweweseka tu!! Lakini wanatakiwa kukaa kimya maana JPM anatekeleza ilani yao kwahiyo hata kuondoa Bunge Live ni Uchadema pia.
 
hata mimi nitakwambia mfuate mnyika akupe ushahidi aliosema anao juu ya lowassa.......usijifanye unaegemea upande mmoja wakati hao viongozi wao ndio walikuwa wapiga matarumbeta wakubwa juu ya hili swala,na ndio ishu iliyowapatia umaarufu........
Ushahidi aliokuwa nao mnyika na viongozi wote wa chadema LOWASA alioneshwa na kusema ni wa UONGO na kama serikali ina uhakika ni kweli APELEKWE MAHAKANI NA HUO USHAHIDI, kwa kuwa serikali imeshindwa kupeleka huko amabako ndiko haki hupatikanan sasa nani muongo jibu ni aliekimbia haki.
 
Hata akitua hana uzito wa kutoa kishindo tena kwani uzito wake ni sawa gunia la pamba, mwenye kishindo sasa hivi ni Magufuli tu.
Kweli kabisa Mkuu. Amebaki na kishindo kikuu kimoja tu. Cha kuchafua hali ya hewa kama alivyofanya kule Chato
 
Ni kiongozi wa mapunguani ndio anaweza kusema Rich mond ni ya Lowasa, hivi una miaka mingapi? ulijua kuhusu rich mond haikuwa UMILIKI bali mMAKUBALIANO/ MKATABA uliohusu rich mond? Eti ya Lowasa? Kamuulize mwakyembe what was the reason mmiliki au makubaliano ya serikali yaliyohusu rich mond.
Kwa nini Lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu?

Hivi Mwakyembe ana nguvu gani hadi yeye pekee asababishe Lowassa aache uwaziri mkuu?

Ni kwa nini tuongozwe na mtu mwenye kashfa/ tuhuma zisoisha za mafisadi?

Wakati wa BMK Lowassa na ccm wenzie walikuwa wanakejeli maoni ya wananchi, na alikuwa anadharau umoja wa wapinzani.....na alishiriki katika kupiga kura katiba mbovu inayopendekezwa. Leo hii ametoka anaanza kusema katiba mbovu, still nyie ambaye mmemuacha afikirie kwa niaba yenu mnamtetea.

Yumkini mkiitwa nyumbu kwa misimamo hafifu iso na afya.

Lowassa yupo kimaslahi zaidi na si kwa ajili ya watanzania. Kumbuka kabla ya uchaguzi kutwa kuandaa harambee makanisani na misikitini......uchaguzi umeisha, mungu pia hayupo.
 
Pole sana muulizeni kikwete mbona humpeleki lowasa mahakani? Au ni kweli wewe ndio ulibariki hayo mbona hamthubutu? Acheni kukariri vihoja badala ya hoja.
Jk alishasema Richmond ni ya Lowasa. Alifanya mambo kinyume na maagizo ya baraza la mawaziri.....Lowasa anahusika na ufisadi wa Richmond
 
Ushahidi aliokuwa nao mnyika na viongozi wote wa chadema LOWASA alioneshwa na kusema ni wa UONGO na kama serikali ina uhakika ni kweli APELEKWE MAHAKANI NA HUO USHAHIDI, kwa kuwa serikali imeshindwa kupeleka huko amabako ndiko haki hupatikanan sasa nani muongo jibu ni aliekimbia haki.
miaka yote walikuwa wapi,kuprove wrong ushahidi waliokuwa wanajidai wanao??
sitakaa ni shabikie uongo na unafiki kama huu,cha msingi baki na imani yako na matumaini yako kwa huyo unayemwamini na mimi nibaki na ninachokiamini,kwa kuwa hatuwezi kuwa sawa kimawazo na kimtazamo...
 
ni wazo zuri kwani wamekuwa kimya sana lazima atoe matamko mbali mbali ili usisahaulike na wale wapiga kura wake takribani milioni 7.
 
miaka yote walikuwa wapi,kuprove wrong ushahidi waliokuwa wanajidai wanao??
sitakaa ni shabikie uongo na unafiki kama huu,cha msingi baki na imani yako na matumaini yako kwa huyo unayemwamini na mimi nibaki na ninachokiamini,kwa kuwa hatuwezi kuwa sawa kimawazo na kimtazamo...
Lazima wangeamini kwa kuwa yale majungu yalipikwa na mawaziri na lowasa akiwa waziri wakati chadema hawaingii kwenye baraza la mawaziri, lakini baada ya kuambiwa na mtuhumiwa kuwa hawa jamaa kule ndani walinisingizia ndio na wa nje amepata ukweli maana mtuhumiwa kajisafisha anasubiri walio mchafua wampe adhabu hawathubutu.
 
Jk alishasema Richmond ni ya Lowasa. Alifanya mambo kinyume na maagizo ya baraza la mawaziri.....Lowasa anahusika na ufisadi wa Richmond
Ndani ya bunge wakati LOWASA ameyasema hayo JK alikaa kimya, JK amekuja kuyasema hayo kwenye kampeni ili kuwaaminisha watu kuwa LOWASA ni mchafu, mbona hakukana pale bungeni ambako serikali nzima ilikuwepo? JK ni mnafiki hajathubutu kuongea rich mond LOWASA akiwa ccm, amekuja kujisafisha baada ya LOWASA kutoka, any way twendeni mahakmani basi.! Tumechoshwa na tuhuma tuhuma tunatka hatia iwepo ili tujue tumeamini sicho.
 
Ushahidi aliokuwa nao mnyika na viongozi wote wa chadema LOWASA alioneshwa na kusema ni wa UONGO na kama serikali ina uhakika ni kweli APELEKWE MAHAKANI NA HUO USHAHIDI, kwa kuwa serikali imeshindwa kupeleka huko amabako ndiko haki hupatikanan sasa nani muongo jibu ni aliekimbia haki.
Mkuu mwasu unaweza kutuonesha au kutuelezea huo ushahidi wa uongo aliokuwa nao Mnyika ama Mbowe?
 
Lazima wangeamini kwa kuwa yale majungu yalipikwa na mawaziri na lowasa akiwa waziri wakati chadema hawaingii kwenye baraza la mawaziri, lakini baada ya kuambiwa na mtuhumiwa kuwa hawa jamaa kule ndani walinisingizia ndio na wa nje amepata ukweli maana mtuhumiwa kajisafisha anasubiri walio mchafua wampe adhabu hawathubutu.
kwahiyo unaprove kuwa viongozi wachadema huwa wanaongeaga kufurahisha jamii na hawanaga ushahidi wa ukweli kuthibitisha hayo wanayoyasema......asante unanipa sababu nyingine ya kutokuwa na imani na chama chako
 
Tumia akili kwa kusoma na kuelewa maana ya habari, mzazi wako akikutuhumu kuwa mwizi ndani ya nyumba jirani atakataa bila wewe kuthibitisha asemacho mzazi wako sio kweli? Umetoka nje na kumwambia mzazi wako aseme kwa uma ulicho iba na yeye akashindwa na kujifungia ndani, jirani atakae endelea kumuamini mzazi wako lazima zitakuwa hazimtoshi.
 
Lazima wangeamini kwa kuwa yale majungu yalipikwa na mawaziri na lowasa akiwa waziri wakati chadema hawaingii kwenye baraza la mawaziri, lakini baada ya kuambiwa na mtuhumiwa kuwa hawa jamaa kule ndani walinisingizia ndio na wa nje amepata ukweli maana mtuhumiwa kajisafisha anasubiri walio mchafua wampe adhabu hawathubutu.
Mkuu mwasu kwa hiyo Lowassa kasema kwa mdomo kuwa amesingiziwa, na wewe unaamini daah......mahaba haya
 
Back
Top Bottom