Edward Lowassa hafai kuwa Rais na ni balaa kwa Taifa

Rev. Mtikila

R I P
Dec 1, 2008
3
34
Wana Jamii Nawaletea ujumbe ambao jana niliwapatia waandishi. Siasa ya kweli ipo DP peke yake ndani ya nchi ya Tanganyika. Machafu yote ya CCM yataanikwa hapa na wanasiasa bandia waliopo UKAWA nao nitayaanika hapa wiki ijayo.
Rev Mtikila.
KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU
TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA
Edward Lowasa ni balaa kwa Taifa!

Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine, kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.

1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowasa na wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!

2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake,katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowasa amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.

3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi,kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini,upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani,kumehusika ''Money laundering' au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa.


Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa Sheria

4 Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa yammwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi nzima makundi ya ng'ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi!

Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya "Kilimo kwanza" kuwa porojo tu ya kisanii!

5 Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.

6 Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere anayeenziwa na CCM lama "Baba" yao, alipotaka kugombea urais, kwasababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa "kununua mvua Thailand" na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi. Ni mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa,anayeweza kumruhusu fisadi Edweard Lowasa agombee urais.

Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama "Baba" yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!

Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward.

Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.

Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi
kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!

7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais!

Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila
mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:

a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.

b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji wa akili zake.

c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa,hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote.

d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!

e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k.

Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya afya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa dhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya anagombea asichokiweza kabisa.

Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli tunalithamini na kuliheshimu Taifa.

Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA. Ni dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency'.

8 Edward Lowasa ni msaliti wa Nchi yetu, kwa kulazimisha kwa ufisadi akisaidiwa na mwuaji mkuu dikteta Paul Kagame kuutwaa Urais wa Nchi yetu, ili tuwe koloni la Hima (Tutsi) empire. Ni taraja la dikteta Kagame kuwa wakimpa urais mtu wao Edward Lowasa, eti Bandari ya Dar es Salaam itakuwa yake, kwa ajili ya kusafirishia utajiri wa koloni lake la Congo (DRC), hila chafu ambayo Rais Kikwete aliipinga vikali kwa uzalendo wake, ikawa sababu mojawapo ya kuchukiwa na beberu huyo.

Mwuaji Kagame ni jemadari wa Watusi wenye ile imani chafu sana,kwamba mungu wao aliumba Wabantu kwa ajili ya utumwa kwa Watusi,ila Watusi eti aliwaumba kuwa watawala wao! Imani hii ndiyo chimbuko la mkakati wa Watusi wa kuliteka eneo lote la Maziwa Makuu chini ya Hima au Tutsi empire, ambayo mkono wake umo katika Uchaguzi huu na mtu wao ni Edward Lowasa!.

Lowasa anapigiwa debe kwa nguvu zote katika vijiwe vya Watusi nchini Rwanda, Burundi, Uganda na hapa nchini. Kagame anamiliki binafsi zaidi ya dola za Marekani Bilioni 2 anazolipora koloni lake la Congo, ndiyo sababu kampeni nzito ya urais wa Lowasa inayo mapesa ya kutisha! Miezi mitano iliyopita walimwagwa wanawake mia tatu Kigoma na Kagera, na wengi zaidi jijini Dar es Salaam, na kusambaa mikoani, wakimhubiri Lowasa kwamba ndiye anayefaa (kwa Watusi) kuwa Rais.

Kampeni ya urais wa Lowasa inaendeshwa kila mahali na maajenti wa Hima empire waliopenyezwa au kununuliwa katika kila taasisi, vijiweni,makanisani na misikitini ambako Lowasa anamwaga rushwa ya kufuru,kutoka katika bahari yake ya pesa chafu.

Ni Bi Janet mkewe Kagame aliyeleta mapesa mengi Kigoma akafikia Coast View Hotel, yaliyotumika kumpokonya Ubunge mzawa Dr. Walid Kaburu na kumpa raia wa Rwanda aitwaye Peter Serukamba mwenye ukoo na Kagame, ambaye safari hii amepangiwa na Kagame Ubunge wa Kigoma Kaskazini, kwa ajili ya udhibiti wa maeneo ya Manyovu na Kagunga, lango lake la utajiri wa Congo kuja Bandari ya Dar es Salaam, ambayo anatarajia kuitia mkononi kwa Urais wa mtu wao Edward Lowasa. Hii ni moja ya sababu za Kagame za kuweka rais wake yeye Burundi hata kwa mabavu. Saa ya ukombozi mni sasa!

Wakati jasusi wa Kagame Peter Serukamba anapiga kampeni ya nguvu sana ya Edward Lowasa, hatuushangai pia kumwona Ana Tibaijuka aliyepoteza Uwaziri wa Ardhi kwa kashfa ya Escrow Account, akipigania bila aibu urais wa chaguo la Watusi, Edward Lowasa! Kwani mwanamke huyu alitangulia kupewa na Museveni takrima ya ng'ombe 100 akawaruhusu Kagame na Museveni kuingiza malaki ya ng'ombe zao katika Hifadhi za Taifa letu Mkoani Kagera, pamoja na wanajeshi wao ambao walidhani ingekuwa rahisi kuliteka hilo eneo letu!

Pamoja na mapesa ya Kagame, bahari ya mapesa ya urais wa Lowasa ni pamoja na mabilioni yanayotuhumiwa kutokana na ufisadi wa mamia ya mamilioni ya dola za Marekani yaliyoinyima Serikali yetu pamoja na Kampuni ya Vodacom mapato ya kutisha. Tunavitaka vyombo vyote vinavyohusika vichunguze taarifa hizi kwa msaada wa taasisi za nje kama FBI na Scotland Yard, ili ukora ukithibitika wafikishwe mbele ya Sheria mafisadi hawa wote!

Fisadi Edward Lowasa, anasaidiwa na Mwajemi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rostam Aziz, ambaye ameikomba nchi yetu Dola za Marekani zaidi ya 550 milioni, zikiwa ni pamoja na mauzo ya hisa zake Vodacom,mapesa ya Taifa letu aliyojipatia kwa kutumia kampuni tata ya Dowans,na mapesa ya Taifa ya EPA aliyolitapeli Taifa kwa ukora wa kitumia kampuni hewa ya Kagoda Agriculture Ltd.

--------- Rostam Aziz alihusika hata katika kuua Shirika letu la Reli,na ndiye anayetuhumiwa kuleta vichwa 54 vya treni, kisha akavivushia Kenya, ili ikitimia ndoto ya urais wa Lowasa avirudishe, na waweze hata kujimilikisha Shirika lote la Reli.

KAGAME NA HIMA EMPIRE NYUMA YA LOWASA

Nchi yetu iliyokamiwa na Watusi wenye ile imani chafu sana, kwamba mungu wao aliumba Wabantu kwa ajili ya utumwa kwa Watusi, ila Watusi eti aliwaumba kuwa watawala wao! Imani hii ndiyo chimbuko la mkakati wa Watusi wa kuliteka eneo lote la Maziwa Makuu chini ya Hima au Tutsi empire, ambayo mkono wake umo katika Uchaguzi huu, watu wao wakiongozwa na Edward Lowasa!

Mkakati wa Hima empire ulianza tangu tulipopata Uhuru. Mimi kwa kuwa niliujua undani wake Mungu aliniongoza kuupiga vita tangu ulipokuwa unqjengwa misingi imara ubeberu huu. Sote tunajua jinsi huko Burundi na Rwanda Wahutu ambao ni asilimia 85% walivyokuwa watumwa wa Watusi ambao ni asilimia 14% tu, kwa zaidi ya miaka 400, hadi mapinduzi ya ukombozi wa Wahutu yaliyoongozwa na Gregory Kayibanda nchini Rwanda mwaka 1959.

Watusi hawakuikimbia nchi yao ya Rwanda kwa ajili ya mateso, bali waliikimbia laana (abomination) ya kuwa sawa na Wahutu, na zaidi kuwa chini ya uongozi wa Wahutu wanaoamini kuwa ni watumwa wao! Ni kwa imani hii potofu kwamba genocide katika Maziwa Makuu ilianzia Burundi, baada ya mapinduzi ya Rwanda, mpaka Umoja wa Mataifa ukakiri kwamba maangamizi ya Wahutu yaliyokuwa yanafanywa na Watusi nchini Burundi ilikuwa genocide. Kwani Wahutu wanaume, wanawake na watoto wasio na silaha walikuwa wanaangamizwa kinyama na Watusi kwa malaki na maelfu! Kosa pekee la Wahutu lilikuwa ‘uasi' wa kudai usawa na Watusi! Hata uvamizi wa RPF nchini Rwanda tangu mwaka 1990 uliitwa "ukombozi" yaani kurejesha haki ya Watusi ya kuwatawala watumwa wao.

Kutokana na kutumiwa vibaya sana na Bill Clinton alipokuwa Rais wa Marekani na Tony Blair alipokuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Umoja wa Mataifa umefedheheka sana kwa kunyamazia genocide ya Burundi kwavile ni Wahutu waliokuwa wanaangamizwa na Watusi! Lakini Rwanda ambako Watusi nao waliuawa, ingawa RPF (Watusi) waliua Wahutu mara nne zaidi, liliitwa janga la dunia, na ukweli ukabadilishwa usomeke kwamba Wahutu au Interahamwe eti ndio wameangamiza Watusi 1.2 milioni!!

Mungu ashukuriwe kwamba sasa Jumuiya ya Kimataifa inageukia ukweli, kwamba hiyo genocide ya Rwanda wauaji wa mamilioni ya watu ni RPF ikiongozwa na dikteta Paul Kagame, aliyeanza kwa kuwaua Marais wawili Wahutu, Habyarimana wa Rwanda na Cyprien Ntaryamira wa Burundi.

Ulimwengu sasa unafunguka akili, kwamba kwavile ilipoanzishwa hiyo genocide nchini Rwanda na Kagame Aprili 1, 1994 idadi ya Watusi haikufika hata 400,000, hivyo kwamba katika hao 1,200,000 waliouawa ni dhahiri kwamba zaidi ya laki tisa walikuwa Wahutu, kwani hata Watusi si wote waliouawa, wengi wao walibaki hai baada ya genocide, ambayo hata wale Wahutu takriban 2,000,000 walioukimbizia uhai wao Congo, Kagame na RPF waliwafuata kule na kuwaangamiza wote!

HIMA EMPIRE INAIVA

Utawala wa Watutsi walioukusudia ukamate eneo lote la Maziwa Makuu na hata Kusini mwa Afrika kama mizimu na mikakati yao itafanikisha, umeshika kasi kubwa sasa, baada ya kumaliza kuiteka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambako Kagame alifanikiwa kumwua Rais Laurent Kabila na kumkabidhi nchi kijana wake Mnyarwanda aitwaye Hypolite Adrien Kanambe, aliyembandika jina bandia"Joseph Kabila", na kumpa makamanda karibu wote wa juu wa Jeshi na watawala wote muhimu wa koloni lake hilo kutoka Rwanda. Ni Rwanda inayoitawala Congo!

Baada ya kuikamata Congo na utajiri wake wote, Watusi sasa wana nguvu za kutisha za kiuchumi kwa kuipora nchi ya watu, na Kagame anao uwezo mkubwa sana wa kununua watu, kugharamia propaganda za kuudanganya ulimwengu, na hasa kuhusu damu ya mamilioni ya watu anayoimwaga usiku na mchana, na kuendesha mauaji ya wapinzani wake duniani kote, pamoja na Watutsi wenzake wote wanaopinga itikadi yake ya Tutsi Supremacy, wanaotetea usawa wa binadamu wote na undugu wa kifamilia wa raia wote wa nchi yao,ambao kwa Kagame ni wasaliti na wahaini!

Kagame amekuwa anaendesha mauaji ya kinyama katika nchi mbali mbali, kama vile Nchi Za Magharibi, Kenya alikowaua Sendashonga,Lizinde na wengine, Africa Kusini alikomwua hivi karibuni ndugu Kalegeya, na ambako amejaribu mara kadhaa kumwua Jenerali Kayumba Nyamwasa.

Unyama wa Kagame uliliumiza sana Taifa letu, alipomwua mtaalamu wetu wa Sheria Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kuutumia ubalozi wake. Ni Kagame aliyetishia hata kummaliza Rais wetu Jakaya Kikwete, alipotoa ushauri makini wa kidiplomasia AU, kwamba tatizo lake yeye Kagame la uhasama wa kiuaji na FDLR alimalize kwa amani kidiplomasia, kwa kukaa nao wayazungumze yaishe. Kagame akaropoka, "I will hit him at the right time!" (Nitampiga kwa wakati unaofaa) Katika kuimarisha ubeberu wake, Kagame alifanya uswahiba mkubwa sana na Rais Nkurunzinza wa Burundi, kwa lengo la kumfanya awe kibaraka wa kitumiwa ndani ya Tutsi empire yao. Lakini alipomtaka amtumie kummaliza Rais Kikwete akamkatalia, Kagame aliropoka kumng'oa Nkurunzinza madarakani, kwa ndoto ya kuikabidhi Burundi kwa Watusi wa itikadi kali tena, waliomwua kinyama hata marehemu Rais Melchior Ndadaye!

Machafuko yote yanayoendelea Burundi yanatengenezwa Kigali na Paul Kagame. Hata maandamano ya Bujumbura yalijikita katika sehemu nne tu zenye Watusi wengi. Walalahoi wengi walishawishiwa kuandamana kwa motisha ya franca mpaka 50,000. Na wengi waliokubali ukimbizi walihubiriwa na ‘manabii' kutoka Kigali kwamba unakuja mmwagiko wa damu ambao haujawahi kutokea Burundi. Wengine wakadanganywa kuwa wakiwa ukimbizini watapelekwa uhamishoni Marekani na Canada.

Lengo la maandamano na kuzalisha wakimbizi lilikuwa kuimarisha uzushi wa Kagame wa genocide, ili apate baraka za Jumuiya ya Kimataifa aendeshe maangamizi ya Wahutu Burundi, kwa kisingizio cha kukomesha hiyo genocide, kama alivyoteketeza mamilioni ya Wahutu wa Rwanda na Wakongo akalindwa na Bill Clinton na Tony Blair. Lakini safari hii Kagame ameshindwa kuipindua Burundi na kupachika mtawala wake yeye Pierre Buyoya, au Alexis Sinduhije, au Hussein Rajab aliyetuma makomando wake wakamtorosha kutoka gerezani Burundi na kumkimbizia Kigali, ili kuiweka Burundi katika Hima Empire.

Kagame ameshindwa kumng'oa Nkurunzinza, kwa sababu Warundi wanamkubali. Amewapa Wahutu karibu asilimia kubwa ya nafasi za elimu ya juu, amewapiga jeki kiuchumi, amewaingiza kwa wingi majeshini, ametoa kipaumbele kwa elimu na maendeleo ya watoto na wanawake, elimu ya bure Shule za msingi, huduma za bure za afya ya watoto chini ya miaka 5 na akina mama wazazi. Amewainua Wahutu kiuchumi mpaka soko lao Bujumbura likawa la kimataifa, kabla ya kuunguzwa na Watusi.

Watu wote wa eneo la Maziwa Makuu wanaoijua hatari ya hawa Watutsi wa itikadi kali ya Tutsi supremacy na mkakati wao wa Hima empire wa kuifanya nchi yetu iwe koloni lao kama DRC, wanasimama pamoja na ndugu zao wa Burundi. Tunaieleza hatari ya Kagame ili aepukwe Edward Lowasa, anayemdhamini aje atumiwe kuitawala nchi yetu kama anavyomtumia Hypolite Adrien Kanambe (Joseph Kabila) Congo!

UBEBERU WA KAGAME DHIDI YA NCHI YETU

Hatari waliyoishinda Warundi inaikabili Nchi yetu! Kwani kama tulivyotangulia kusema, kutekwa Nchi yetu ili iwe koloni la Watusi kulianza tulipokuwa tunapata Uhuru wetu! Watusi walianza kupenyezwa kila sehemu nyeti ya utawala wa nchi yetu, hatimaye wakaweza kuikamata Nchi yetu na kututawala bila sisi kujijua, nchi yetu ikatumika kuwatawalisha Watusi Burundi, Uganda na Rwanda.

Leo Taifa letu liko uchi kabisa mbele ya Watusi hasa wa Rwanda na Uganda. Ndiyo maana Kagame anadiriki kutudharau kama mataahira,kiasi cha kumtambia Rais wetu kwamba ‘I will hit him at the right time', na kuwaimbisha wacheza ngoma wake kwamba ‘Mwanaume ni Kagame, Kikwete ni nini?' Akajigamba kwamba eti hatuwezi kushindana naye, kwa sababu eti anazo karata nyingi za kutumaliza ndani ya nchi yetu akitaka! Ndiyo, ana majasusi wake kila mahali, na viongozi wetu wengi amefanikiwa kuwapachika wanawake zake, yaani ni victims of sexual espionage!

Kwa mfano, Seth Kamanzi tuliyemsomesha sana kuliko raia wetu,akawa mhadhiri Chuo cha Fedha IFM, akajipenyeza mpaka akawa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alipomaliza kazi aliyotumwa alitorokea kwao Rwanda na siri zetu zote, ambako sasa ni Seneta!

Taifa letu likawasomesha Profesa Silas Lwakabamba akawa Dean wa Kitivo cha Uhandisi, na Dr. Albert Butare. Hawa wakawa wakuu wa miradi ya UNDP Arusha, lakini yalipopatikana mapesa mengi ya miradi mikubwa, wakafanya kila mbinu chafu na kuyakimbizia kwao Rwanda, ambako yalitumika kuanzisha Institute of Science and Technology!

Leo Prof. Silas Lwakabamba ni Waziri wa Elimu kwao Rwanda, mwenye majukumu ya siri pia ya kushughulikia vibaraka wa Kagame katika nchi yetu, kama Edward Lowasa, kwa ajili ya Hima Empire, ambaye Watusi wanajivunia sana kama vile tayari ni Rais wa koloni lao!

Mfano mchungu zaidi ni Lt. Colonel Celestine Seromba, aliyekuwa katika sehemu nyeti sana kwa usalama wa Taifa letu, kama Mkuu wa kitengo cha IT cha Jeshi la Ulinzxi wa Nchi yetu, chenye siri zote za Jeshi letu pamoja na data zote za silaha zetu, mafunzo yetu na mikakati yote ya Ulinzi wetu tuliyo nayo, yaani nguvu zetu zote kama Taifa! Alipomaliza kazi aliyotumwa na mwuaji Paul Kagame alitoroka na siri hizo zote, na kupokelewa kwao Rwanda na dikteta Kagame kama shujaa, na kupandishwa cheo mara moja kuwa Colonel!

Lakini majasusi zaidi ya elfu kama huyu wamepenyezwa katika idara ya Usalama wa Taifa, Jeshini, Polisi, Uhamiaji, Vyuoni, katika Wizara zote nyeti za Serikali yetu, katika mashirika nyeti ya umma, katika makampuni mbali mbali, katika taasisi za kimataifa, makanisani na hata misikitini, achilia mbali majasusi wanawake wanaojifanya makahaba! Ndiyo maana Kagame ana jeuri chafu ya kumdharau Rais wetu, na hata kumpangia kummaliza eti wakati atakaoona yeye unafaa, kama vile Rais wetu anaishi kwa hisani ya mwuaji Paul Kagame! Saa ya ukombozi ni sasa!

Ndiyo maana Kagame ameropoka kwa dharau sana juu ya mapungufu ya Jeshi letu, na kulikuza sana la kwake yeye kwa ajili ya ubeberu, na kujilimbikizia silaha mpaka puani, zikiwemo rada na makombora ya kisasa ya Scud yanayoweza kupiga Dar es Salaam moja kwa moja! Ingawa nduli Idd Amin alitudharau kuliko Kagame lakini tukampiga, na ingawa karata za Kagame zimeshindwa Burundi, tayari Watutsi kule Rwanda, Burundi na Uganda wana hakika ya kuitawala Nchi yetu kama vile Congo, kwa kutubandika Rais wao Edward Lowasa!

Inafahamika juu ya wadhamini wa Lowasa wa Kigali, Kampala na Bujumbura, kwamba kwa ajili ya huyu mtu wao wamemwaga mapesa mengi, ya kuhakikisha kwamba wanamkabidhi nchi yetu atawale kwa ajili ya maslahi yao, yaani Hima empire.

Watutsi kama Meja Jenerali Anatoly Kamazima aliyepenyezwa katika Jershi letu, kisha akapewa Taasisi nyeti ya TAKUKURU, komando wa Kagame Derick Kataraiha ambaye ni mpwae Prof Lwakabamba,ambaye ni afisa mikopo wa Benki yetu ya NMB, ni baadhi tu ya Wanyarwanda waliokuwa katika kampeni nzito ya urais wa Lowasa tangu mwaka 2011, mtandao huo wa Lowasa ukiwa na nguvu kubwa mno kifedha, kwani Kagame anaipora Congo kishenzi kwa malengo haya.

Katika kufanikisha ndoto yao ya Hima empire, Watusi wameikamata Jumuiya ya Afrika Mashariki (E.A.C), viongozi wengi wakiwa majasusi wa Jeshi la Kagame, kama Katibu Mkuu Dr. Richard Sezibera ambaye ametumika kujaza askari wengi wa Kagame kama maafisa waandamizi,ambao ni mbali ya Martin Ngoga aliyeongoza genocide ya Kagame ya kuwamaliza Wahutu wa tabaka la juu kwa kutumia ICTR, ambaye sasa yumo katika Bunge la Afrika Mashariki.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imenyolewa na Watusi wa Hima Empire, Burundi inapambana isinyolewe, na sisi lazima tushikamane kama familia moja ya wahanga wa Nchi yetu katika mipaka ya ardhi yetu, na kupinga kwa sauti moja kwamba fisadi Edward Lowasa ni marufuku kugombea Urais wa Nchi yetu, kwa sababu mahali anapostahili ni JELA na kupata ukarabati wa afya yake..

Saa ya ukombozi ni sasa!

Mchungaji C. Mtikila
MWENYEKITI-TAIFA - DP
 

Attachments

  • Edward Lowasa ni balaa kwa Taifa.pdf
    101.5 KB · Views: 587
Unapoanika mabaya ya wanasiasa wenzio hebu yaanike yaliyo mema ndani ya DP ili iwe rahisi kupima kati ya mchele na ipi pumba.Karibu kwa ufafanuzi mchungaji...
 
Karibu Mchungaji wewe ni moja ya wanasiasa imara kabisa misimamo yako daima huwa haiyumbi
 
Mkuu Lowassa na UKAWA wamekufanya nini mbona unatoka unawasakama sana?
 
Wana Jamii Nawaletea ujumbe ambao jana niliwapatia waandishi. Siasa ya kweli ipo DP peke yake ndani ya nchi ya Tanganyika. Machafu yote ya CCM yataanikwa hapa na wanasiasa bandia waliopo UKAWA nao nitayaanika hapa wiki ijayo.
Rev Mtikila

Wewe Jamaa nimekupuuza sana na kukudhihaki kabisa kutokana na kutokuwa na hata uelewa wa unachikiandika sasa unataka kusema ya kwamba raisi Kagame siyo Mbantu? Eti unaandika ,,Watusi wanawanyanyasa Wabantu", ni nani amekwambia ya kwamba hao unaowaita Watusi SIYO Wabantu?

Unaijua Lugha anayoongea Raisi Kagame wewe? Inaitwaje? Unajua ya kwamba hakuna kitu kama Lugha ya Kitusi wala Kihutu nchini Rwanda? Sasa hilo la kusema Raisi Kagame siyo Mbantu umelitioa wapi?

Hapo pekee yake kumenifanya nione yote uliyoyaandika ni ya Uongo na uzushi na hauna unalolijua!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
alafu kuna mambo mengi ya taifa wewe unatuletea ya kagame ya nini?
 
Haya mkuu tumekusika, sasa tangaza chama chako kwa bidii upate wabunge wa kutosha na hatimaye upate hela za kugawa kama Lowassa
 
Mchungaji ungebakia kwenye hoja ya msingi kama inavyosomeka kwenye aya ya kwanza pengine ungeeleweka kwa wanajamii-lakini taarifa yako imejaa madudu mengine yasiyoya lazima kwa wakati kama huu- na kama hii taarifa yote ni sehemu ya madai yako yatakayofika mahakamani endelea kumchafu Lowasa kwa faida ya Maadui zake lakini si kwa masilahi ya Watanzania.

Pili vipi ile Kesi yako ya Mgombea Binafsi-lini hukumu ya Mahakama ya Afrika itatekelezwa na Serikali.

Nadhani badala ya kuhangaika na Lowassa nakushauri urudi kwenye njia kuu. Nenda mahakamani Mapema Mgombea Binafsi Uchaguzi huu iwe haki ya msingi na kipaumbele maana wengine vyama vyetu vikitupiga chini tupate pakukimbilia.


CC Rev.Mtikila

Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine,kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.
 
Tumesema hapa kuwa Lowasa hafai, nawe Mtikila wala hujachelewa, likemee hilo na yeyote atakaesema hilo na aliseme. Ni kweli Lowasa hafai na ni janga kwa taifa

Endeleza mapambano Mtikila. Hatuna sababu ya kujidhalau na kuruhusu dunia itudhalau kwa kuruhusu fisadi atuongoze
 
Eti kikwete kalitaja tu bungeni analishukuru kinafiki mibunge bila aibu inashangilia
 
I think something is wron somewhere........sijaona hoja nzuri na zenye mashiko kutoka kwa mchungaji huyu.
 
Moja ya campaign ya wazi alioifanya Lowassa ni alipokuwa Morogoro kwa kutoa ahadi ya kutatua migogoro wa wakulima na wafugaji kwa kuwaahidi kuwa akiwa raisi ataunda Tume kushugulikia migogoro hiyo.

Pili,aliahidi kuwa akifanikiwa kuwa raisi jambo la kwanza ni kufufua viwanda vya mkoa wa Morogoro.

Mtu unatafuta wadhamini ahadi hizi zinaingiaje?

Ukija kwa Membe,Mwigulu na wengineo mambo ni yale yale isipokuwa watia nia wachache.

Nasikitika hata Prof. Lipumba nae alitoa ahadi kabla ya wakati siku ile anatangaza nia na siku hiyo hiyo nakumbuka nili-post uzi hapa JF kumtahadharisha na kumuomba Dr.Slaa awe makini kama nae ataamua kutangaza nia.

Nilitoa copy kwa Tumaini Makene

Nilifanya hivyo kwa nia njema kabisa nikiamini kauli mbiu isemayo, "mabadiliko yanaanza na wewe" na si vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
Mtikila ndiyo wakati huu. Piga pesa Baba, na Lowassa akijichanganya naye unamla kichwa pia.
 
Angalau Rev. is shading light on wapi hizo pesa za Lowassa za kampeni zinatoka (i.e., kwa Rostam, Rwanda/Kagame & Uganda, n.k.). Inabidi sasa Lowassa aje na rebuttal .. atutajie marafiki wake ni akina nani ..?
 
CCM ovyo, UKAWA ovyo, CHADEMA ovyo , Mengi Ovyo; nani mwenye afadhali au DP ? hapa ndipo ninapotofautiana na wewe kama Mtikila. Hata sisi tuna nywele/akili za kutafakari na kuchambua hivyo hatuwezi kumeza kila unachosema. Sometime you're wrong some time you're right . Kumpinga Lowassa nakuunga mkono lakini hoja za kumpinga bado ongeza zege
 
Wewe Jamaa nimekupuuza sana na kukudhihaki kabisa kutokana na kutokuwa na hata uelewa wa unachikiandika sasa unataka kusema ya kwamba raisi Kagame siyo Mbantu? Eti unaandika ,,Watusi wanawanyanyasa Wabantu", ni nani amekwambia ya kwamba hao unaowaita Watusi SIYO Wabantu?

Unaijua Lugha anayoongea Raisi Kagame wewe? Inaitwaje? Unajua ya kwamba hakuna kitu kama Lugha ya Kitusi wala Kihutu nchini Rwanda? Sasa hilo la kusema Raisi Kagame siyo Mbantu umelitioa wapi?

Hapo pekee yake kumenifanya nione yote uliyoyaandika ni ya Uongo na uzushi na hauna unalolijua!

Wahutu na watusi siyo wabantu. Rejea historia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom