Lowassa awaachia watu hatia moyoni, Watubu wapi?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411

LOWASA: Mfupi wa Maisha na Mrefu wa Historia.

Edward Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgawo wa umeme wala usanii wetu wa Kibongo. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito, kuna makundi makuu matatu.
- Wanaolia sana
-Wanaofurahia sana
-Wasiojua kama walie au wafurahie.

Yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui kundi langu lakini niseme manne ninayomkumbukia Edward Lowasa:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini kwa njia ya Edward Lowasa, alisababisha mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:
- Spika Samwel Sitta
-Wabunge mitume
-Edward Lowasa akiwa Waziri Mkuu.
Bunge lile halitasahaulika kwa wema na ubaya wake.

2. Alikuwa mtetezi asiyekuwa na mtetezi.
- Alikitetea chama chake, nacho kikamtelekeza.
-Alimtetea Rais wake bila kujali kama anatetewa ama la!
-Aliitetea nchi (maji, umeme na elimu) lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda na kuwatetea Wamasai. Watesi wake wakamchonganisha nao. Wakahoji umasai wake na U-Laigwanani wake. Upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za kiitikadi. Akiwa hai hadi kifoni - Edward ni Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia na kummaliza, alibaki na Regina. Viongozi tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa madaraka, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone tutakavyoliziba hilo pengo hata kabla ya mazishi!

UBINADAMU WA LOWASA

a. Aliwaamini watu kuliko alivyoaminiwa.

b. Alikataa kuamini au kuutukuza umaskini. Kwa njia hii akatengeneza giza la kutuhumiwa na watesi wake.

c. Aliamini kwa dhati kuwa unaweza kuwa tajiri na mzalendo kuliko dhana ya kuwa umaskini ndio uzalendo.

d. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Ameondoka akiwa mshindi wa vyote viwili. Anatukuzwa na waliombeza.

Nilibahatika kuwa karibu naye. Niliona furaha yake na machozi yake. Ameishi miaka ya kibiblia (70). Historia yake ni ndefu kuliko miaka hii. Nenda Edward.

Alipofanya vibaya, tumwachie yeye na muumba wake.

Alipofanya vizuri, ni juu yetu na muumba wetu.

Pole Mama Regina, Watoto na wajukuu
 
Siku Chadema wakijitambua ni pale wakijatambua
Badilisheni uongozi wa juu. Kuna watu wanatumia watu kujijenga wao na familia zao…
Kila mtu atatoa hesabu yake kwa muumba
Hizi sifa za huyu mwendazake hii nchi ilipakwa makaa ya moto
Hatujitambui
Tumesahau Richmond na mengineyo…
 
Back
Top Bottom