Eddie Ganzel

Yap nami namkumbuka sana huyu mwandishi pamoja na akina Sam Kitogo, S.M.Bawji, faraj Katalambula, Agolo Andulu. kwani na hammie rajab yu wapi?
Baadhi ya vitabu nilivyosoma vya waandishi hawa ni hivi
>Roho mkononi
>Awe hai au amekufa namtaka
>Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi
>Njama, Kikomo, Kikosi cha kisasi & kufa na kupona
>Simu ya Kifo
>Joto la fedha

ha ha ha ilikuwa raha kwakweli wakati ule.

paullih uko juu sana vitabu vya agoro anduru vilikuwa balaa, hammie rajab na huyu kajubi d mukajanga na yeye alikuwa balaa mwisho kuna mtu anaitwa Emmanuel Makaidi alikuwa na kitabu chake kinaitwa baada ya kisa mkasa yaaani ukikisoma unaweza patwa na hasira ya ajabu jinsi jamaa alvyokuwa akifikia kufanikiwa tu mkasa unatokea dah umenikumbusha mbaliiii mnoooo
 
Yap nami namkumbuka sana huyu mwandishi pamoja na akina Sam Kitogo, S.M.Bawji, faraj Katalambula, Agolo Andulu. kwani na hammie rajab yu wapi?
Baadhi ya vitabu nilivyosoma vya waandishi hawa ni hivi
>Roho mkononi
>Awe hai au amekufa namtaka
>Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi
>Njama, Kikomo, Kikosi cha kisasi & kufa na kupona
>Simu ya Kifo
>Joto la fedha

ha ha ha ilikuwa raha kwakweli wakati ule.

Paullih umenikumbusha mbali sana, maana nakumbuka kuvisoma hivyo vitabu vyote ulivyotaja hapo wakati huo nilikuwa shule ya msingi,,, mdingi (marehemu) alikuwa polisi hivyo vitabu vya kipelelezi vilikuwa rundo ndani ya nyumba,
Nasikitika tu kuwa waandishi wa Riwaya za sasa hawana mvuto kama wale wa zamani sijui ni kwa nini au taaluma ndo imekufa?
 
Da,mmenikumbusha mambo ya ,kamlete akibisha mlipue,kabwe makanika,sifi mala mbili,usiku wa balaa,buriani .nilikua silali aisee
 
Ni kweli Eddie Ganzel Hatunaye tena namsikitikia sana yule jamaa kwani kuna mtu kutoka Ulaya alikuja kumuona yeye tu, alipoonyeshwa hakuamini jamaa alikuwa kachoka ile mbaya tena chapombe, alifikiri waandishi wa Tanzania ni kama wale wa ulaya. Maslahi madogo ndio maana inakuwa vigumu kupata watunzi wazuri wa riwaya, pia Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu siku hizi ukiona mtu anasoma ujue anajiandaa kwa mtihani. Lakini hakuna mwandishi mfano wa Husein Tuwa wengine huwa nawasoma kiu lakini hawachelewi kupotea nafikiri tatizo ni maslahi mfano nilisoma riwaya inaitwa MZIGO sijui yule mwandishi kapotelea wapi!
 
DAAH UMENIKUMBUSHA MBALI SANA HICHO KITABU SASA KIPINDI NIPO DARASA LA NNE NIKAKIPATA KITABU CHAKE KINAITWA "BURIANI" YAANI IKIFIKA USIKU NIKIKUMBUKA STORY NAANZA KUTETEMEKA NAOGOPA NITAOTA USINGIZINI DAAH MUNGU AWABARIKI WATUNZI HAWA ENZI ZILE HAMNA TV WALA VIDEO,,STAREHE NI RADIO NA RIWAYA ZA HADITHI NA GJARIDA LA SANI LA KILA MWEZI MARA MOJA
QUOTE=Masatu;306205]Umenikumbusha mbali nakumbuka kusoma kitabu kimoja cha Eddie Gazel Jogoo la shamba that was masterpiece![/QUOTE]
 
Kuna mtunzi anaitwa anaitwa Hussein Tuwa.........Jamaa ni mzuri sana kwenye utunzi,anatunga Riwaya/Vitabu vitamu sana...

Binafsi nimebahatika kusoma Riwaya zake kama Mdunguaji,Mtuhumiwa,Mkimbizi,Mfadhili, Bondia na Utata wa 9/12.......Jamaa anatisha hasa

Hussein Tuwa, Ahsante sana kwa kunikumbusha huyo mtu. Pia nimebahatika kusoma hizo Riwaya zake zote, Bondia sikuimalizia aisee... ila aliishia kutoa kitabu cha "MKIMBIZI" tu hivyo vingine nilisoma kwenye gazeti tu. Sijui kuna tatizo gani na kijana Tuwa sijui kapotelea wapi, nilijaribu sana kumtafuta, akafunguaga na website........... ila dooo sijui vipi kijana, alisema anandaa MTUHUMIWA.
Mageziti ya MIA kipindi kile yalikuwa na riwaya nzuri sana, kuna riwaya nilisoma kidogo inaitwa "hazina iliyofichika" sijiu aliandika nani ila ni mtu ambaye nilimkubali.
Pia kuna mtu anaitwa Ephraim Kezirahabi (kama sijakosea) ameandika, Gamba la Nyoka, Nagona, Dunia Uwanja wa fujo (kwa ninavyovifahamu).
 
Hussein Tuwa kwa sasa ni Mwajiriwa katika ofisi fulani ya Ubalozi sidhani kama anaweza kuwa na muda wa kuendelea na utunzi.
 
Kuna hivi vitabu nilivipenda sana, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, mtunzi alikuwa Muhammed Said Abdulla a.k.a Bwana Msa

Vitabu vingine ni Asali Chungu, Dunia Mti Mkavu, Utengano, Kiza katika Nuru, Tata za Asumini, Babu Alipofufuka mtunzi alikuwa Said Ahmed Mohamed

Wapo wachache waliobakia kama huyu Farouk M. Topan mtunzi wa kitabu cha Mfalme Juha, vile vile Mzee wetu Adam Shafi Adam bado pia yupo hai.
 
Uandishi haulipi niliwahi kujidanganya after being inspired nikaandika HEKAHEKA ,kashifa .hadithi zikatoka msanii miaka ya tisini malipo yakawa kidogo na sikupata mtu wa kunisponser nikaghairi.baadae nikaona nitest novel.nikaandika HÖTSOUP in the beginning.ni cha kijasusi kinahusu gulfwarone irag .nilikua bush skupata spönser miaka hyo ya tisini na tano.
Mwisho nkaandika HOTSOUP the aftermath hicho miaka 2005 after gulfwar two nikaishia chapter six nikawa nimepata ajira nikabullshit.
Kwa hapa bongo fani hailipi labda upublish na kuuzia majuu
 
Basi mkuu, hivyo vitabu vyako Heka heka na hicho cha Kashfa, watafute wataalam wakutengenezee script, ili utoe movies basi, au wewe unaonaje?
 
Basi mkuu, hivyo vitabu vyako Heka heka na hicho cha Kashfa, watafute wataalam wakutengenezee script, ili utoe movies basi, au wewe unaonaje?

wazo zuri ntalifanyia kazi mkuu sema nko remote area and a little bit busy kiasi siwezi kusafiri kwa sasa
 
Poa mkuu, mambo mazuri hayataki haraka.

Sasa hivyo vitabu vyako bado vinapatika?

sio vitabu.niliandika manuscript nikapeleka msanii magazeti zikawa zinatoka gazetini every wknd.
Ila copy zake nilihifadhi .na sio kwamba kipaji kilipotea bado nnacho sema mda wa kukaa kuandika ukichukulia hailipi mtu unaamua kuacha
 
Hapo zamani nilikuwa nasoma katika magazeti hadithi za kusisimua za Eddie Ganel. Pia ameandika kitabu, Ndoto Ya Mwendawazimu. Kuna mtu ambaye ana habari za huyu mwandishi?

Eddie Ganzel alikwishafariki. Kwenye dibaji ya riwaya yake ya 'Msako wa Hayawani' iliyochapwa mwaka 2006, Mchapaji Sabbi L. Masanja (mmiliki wa jarida la Bongo) alizungumzia hilo. Hakusema tarehe halisi ya kifo chake, hivyo yawezekana ni kabla ya mwaka huo ama mwanzoni mwa mwaka huo.
 
Kuna hivi vitabu nilivipenda sana, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, mtunzi alikuwa Muhammed Said Abdulla a.k.a Bwana Msa
mkuu mimi nimevisoma mzimu wa watu wa kale na duniani kuna watu bado ni navyo nimevihifadhi...ningependa kupata hivyo vingine vya bwa msa, ni wapi vinauzwa?
 
Kuna hivi vitabu nilivipenda sana, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, mtunzi alikuwa Muhammed Said Abdulla a.k.a Bwana Msa

Vitabu vingine ni Asali Chungu, Dunia Mti Mkavu, Utengano, Kiza katika Nuru, Tata za Asumini, Babu Alipofufuka mtunzi alikuwa Said Ahmed Mohamed

Wapo wachache waliobakia kama huyu Farouk M. Topan mtunzi wa kitabu cha Mfalme Juha, vile vile Mzee wetu Adam Shafi Adam bado pia yupo hai.

...Mkuu, wewe ndio hasa umetaja vitabu hasa vya riwaya za kusisimua za kiafrika hasa. Vingi vilivyotajwa na wachangiaji hapa vilikuwa ni cut-paste za visa vya James Hadley Chase, Nick Carter na kadhalika. Ni riwaya ambazo zilikuwa hazina uhalisia wa maisha ya kiafrika kama zilivyo nyingi ya sinema za kitanzania za leo zinazoonyesha maisha tofauti kabisa na hali halisi!

Katika orodha uliyoandika unaweza pia kuongeza Dunia Uwanja wa Fujo, Kuli, Nyota ya Rehema, Rosa Mistika, Simu ya Kifo na kadhalika. Hizi vitabu vingi vya hadithi za kusisimua vya watunzi kama Ben Mtobwa, kajubi Mukajanga, Evis Musiba et al vilianza hasa miaka ya mwishoni ya sabini.
kabla ya hapo tulikuwa tunasoma vitabu vya riwaya vilivokwenda shule kama Mzimu wa Watu wa Kale, Roza Mistika, Simu ya Kifo, Pili Pilipili, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, Roza Mistika, Tumgidie ***** na kadhalika!
 
Vipi kuhusu Eric James Shigongo? Mbona anaandika sana hadithi, je yeye siyo gwiji kuzidi akina Hammie Rajab, Ben Mtobwa na Eddie Ganzel? Kuna watu wanadai kuwa anatafsiri riwaya za watu wengine je ni riwaya zipi?

Jibu lako lipo hapo kwenye nyekundu
 
Eddie Ganzel, A. E. Musiba, Ben Mtobwa na Hammie Rajabu wameshatutoka. Je baada yao ni mtanzania gani aliyeweza tena kuandika vitabu vinavyovutia kusoma kiasi cha kumfanya msomaji kusisimka, au tuseme fani ya uaadishi wa tamithilia ndio umekiwsha kabisa. Niliwahi kuosoma tamithilia moja iliyoandikwa na Eric SHigongo nikapata kichefuchefu kabisa.

Mkuu hebu cheki tena taarifa zako. Hammie Rajab amefariki lini? Huyu nadhani bado yupo ila siku hizi anashiriki zaidi kwenye utengenezaji wa filamu na sio uandishi wa Vitabu. Kama sikosei.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom