Eddie Ganzel

Mkuu hebu cheki tena taarifa zako. Hammie Rajab amefariki lini? Huyu nadhani bado yupo ila siku hizi anashiriki zaidi kwenye utengenezaji wa filamu na sio uandishi wa Vitabu. Kama sikosei.

Hajakosea mkuu.........

Hammie Rajab amefariki wiki iliyopita tarehe 21/04/2011 katika hospitali ya Amana Ilala ambako alilazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.....Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi,Amina

Aisee! Thanks Balantanda kwa taarifa hii! Sikuwa na habari kabisa! Maambo ya kukimbilia vijijini hayo wakati wa Pasaka. Kibaya zaidi ni kwamba kabla sijaenda kijijini kama wiki 3/4 hivi zilizopita Hammie alionekana kwenye kipindi cha Bongo Movie akiongelea kuhusu sekta ya filamu nchini na kutaja wale aliodhani kuwa ni waigizaji wa kweli wa sekta hiyo.hali yake kwa kweli haikuwa njema hasa kwa mtunzi ambaye alikuwa na zaidi ya vitabu kumi sokoni vya riwaya za kusisimua akiwa pia miongozi mwa waanzilishi wa majarida dizaini ya Sani ile ya mwanzo kabisa yeye akiwa na Wisdom/Busara kwenye miaka ya 1979/80. RIP Hammie Rajab. Dah, nimeshituka mno. RIP Hammie Rajab.

Uandishi haulipi niliwahi kujidanganya after being inspired nikaandika HEKAHEKA ,kashifa .hadithi zikatoka msanii miaka ya tisini malipo yakawa kidogo na sikupata mtu wa kunisponser nikaghairi.baadae nikaona nitest novel.nikaandika HÖTSOUP in the beginning.ni cha kijasusi kinahusu gulfwarone irag .nilikua bush skupata spönser miaka hyo ya tisini na tano.
Mwisho nkaandika HOTSOUP the aftermath hicho miaka 2005 after gulfwar two nikaishia chapter six nikawa nimepata ajira nikabullshit.
Kwa hapa bongo fani hailipi labda upublish na kuuzia majuu
Uandishi siku hizi umerahisishwa kwa sababu ya mitandao. Vile vile unaweza kuchapisha vitabu vyako na kuwa e books. Kwa mfano ninanunua vitabu vingi tu Amazon na kuvisoma kupitia Kindle. Unawza kuwasiliana na Amazon na watakuambia ni vipi unaweza kuchapisha vitabu vyako. Nimeshaona vitabu kadhaa vya kiswahili huko.

sio vitabu.niliandika manuscript nikapeleka msanii magazeti zikawa zinatoka gazetini every wknd.
Ila copy zake nilihifadhi .na sio kwamba kipaji kilipotea bado nnacho sema mda wa kukaa kuandika ukichukulia hailipi mtu unaamua kuacha
Mkuu kama utajali naomba unitumie nakala za hivyo vitabu vyako kaka.

Shukran.

mkuu mimi nimevisoma mzimu wa watu wa kale na duniani kuna watu bado ni navyo nimevihifadhi...ningependa kupata hivyo vingine vya bwa msa, ni wapi vinauzwa?
Mkuu kama una mtu unamfahamu uko Mombasa au Nairobi unaweza kumuagizia.

Mimi niliwahi kuagiza baadhi ya vitabu kutoka Kenya nikaletewa.

...Mkuu, wewe ndio hasa umetaja vitabu hasa vya riwaya za kusisimua za kiafrika hasa. Vingi vilivyotajwa na wachangiaji hapa vilikuwa ni cut-paste za visa vya James Hadley Chase, Nick Carter na kadhalika. Ni riwaya ambazo zilikuwa hazina uhalisia wa maisha ya kiafrika kama zilivyo nyingi ya sinema za kitanzania za leo zinazoonyesha maisha tofauti kabisa na hali halisi!

Katika orodha uliyoandika unaweza pia kuongeza Dunia Uwanja wa Fujo, Kuli, Nyota ya Rehema, Rosa Mistika, Simu ya Kifo na kadhalika. Hizi vitabu vingi vya hadithi za kusisimua vya watunzi kama Ben Mtobwa, kajubi Mukajanga, Evis Musiba et al vilianza hasa miaka ya mwishoni ya sabini.
kabla ya hapo tulikuwa tunasoma vitabu vya riwaya vilivokwenda shule kama Mzimu wa Watu wa Kale, Roza Mistika, Simu ya Kifo, Pili Pilipili, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, Roza Mistika, Tumgidie bwe.ge na kadhalika!
Mkuu kweli wewe wa enzi zetu, hapo nimekumbuka mbali sana, yaani ukisoma hivyo vitabu, ni kama unaangalia senema (si sinema) vile.

...Mkuu, wewe ndio hasa umetaja vitabu hasa vya riwaya za kusisimua za kiafrika hasa. Vingi vilivyotajwa na wachangiaji hapa vilikuwa ni cut-paste za visa vya James Hadley Chase, Nick Carter na kadhalika. Ni riwaya ambazo zilikuwa hazina uhalisia wa maisha ya kiafrika kama zilivyo nyingi ya sinema za kitanzania za leo zinazoonyesha maisha tofauti kabisa na hali halisi!

Katika orodha uliyoandika unaweza pia kuongeza Dunia Uwanja wa Fujo, Kuli, Nyota ya Rehema, Rosa Mistika, Simu ya Kifo na kadhalika. Hizi vitabu vingi vya hadithi za kusisimua vya watunzi kama Ben Mtobwa, kajubi Mukajanga, Evis Musiba et al vilianza hasa miaka ya mwishoni ya sabini.
kabla ya hapo tulikuwa tunasoma vitabu vya riwaya vilivokwenda shule kama Mzimu wa Watu wa Kale, Roza Mistika, Simu ya Kifo, Pili Pilipili, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, Roza Mistika, Tumgidie ***** na kadhalika!

BabaDesi uko sahihi tena umenikumbusha kitabu kinaitwa kasri ya Mwinyi Fuad nafikiri kimeandikwa na Shafi Adam Shafi pia kuna kitabu kilinifurahisha sana kinaitwa ALIYEONJA PEPO kimeandikwa na Farouk Topan. Kwa sasa naona waandishi wazuri wapo lakini wanaishia kwenye magazeti ya udaku sijui inakuwaje sitasahau jinsi nilivyosisimka kwa riwaya ya MZIGO ambayo niliisoma kwenye KIU mwisho wa siku hakuna hata dalili ya kutolewa kitabu nasikitika sana!

Pia tusimsahau Hayati Said M. Bawji.....Alikuwa mtunzi mahiri sana wa riwaya huyu.......Mojawapo ya riwaya zake tamu ninayoikumbuka ni ile ya Maji Mazito(ya mzee Dickson Zakwa Mkongwe na Omari Kissila).........

Hata mdogo wake Amri Bawji naye anafanya vizuri kwenye utunzi wa riwaya

Katika orodha uliyoandika unaweza pia kuongeza Dunia Uwanja wa Fujo, Kuli, Nyota ya Rehema, Rosa Mistika, Simu ya Kifo na kadhalika. Hizi vitabu vingi vya hadithi za kusisimua vya watunzi kama Ben Mtobwa, kajubi Mukajanga, Evis Musiba et al vilianza hasa miaka ya mwishoni ya sabini.

kabla ya hapo tulikuwa tunasoma vitabu vya riwaya vilivokwenda shule kama Mzimu wa Watu wa Kale, Roza Mistika, Simu ya Kifo, Pili Pilipili, Gamba la Nyoka, Dunia Uwanja wa Fujo, Roza Mistika, Tumgidie ***** na kadhalika!

mkuu hivi vitabu kwa sasa vinaweza kuwa vinapatikana madukani???nina shida navyo sana ningependa kuwa na nakala zangu,niliwahi kuvitafuta mtaa wa samora kwenye maduka ya vitabu sikuvipata,kwa anayejua vinapopatikana naomba msaada plz...

Ukweli vitabu hivi labda uvikute tu kwa bahati kwa wale wauza vitabu vikuu kuu wanaopanga bidhaa zao barabarani. Ni kama vimetoweka kabisa. mimi mwenyewe kwa mfano nimejaribu kwa muda mrefu sana bila mafanikio kupata vitabu vya Roza Mistika, Mashimo ya Mfalme Suleiman, Titi la Mkwe, Kisiwa chenye Hazina (Treasure Island) na Jamaa hodari Kisiwani (Swiss Family Robinson), Aliyepanda tufani na kadhalika. Kwa hakika, ningependa sana hawa dotcom wangu wasome 'Almasi' kama hizi...

Kuna riwaya inaitwa 'Haramu!'. mwandishi chipukizi ambaye kaandika pia vitabu kama Mganga Pazi, Kama Ningeweza Kupaa, Simba toka Serengeti. Jamaa mwandishi mzuri sana kwa kizazi cha sasa. kwa watakaobahatika kuvisoma watujuze.

Huo ni ukweli, vitabu ivi vilivutia sana. Chukulia njama, kikosi cha kisasi, hofu vy Msiba, tutarudi na roho zetu, mikononi mwa nunda vya Ben mtobwa. Kwa kweli nilikuwa nikianza kukisoma silali kabisa. enzi hizo makwetu na vibatari macho hayakuchoka kabisa.

kuhusu eddy ganzel habari za mwisho mwaka jana kulikuwa na romous kama amefariki ila sina ihakika sana.

Hivi Eddie Ganzel aliandika KITANZI ? Jamani kuna mtu anajua mtunzi wa vitabu Kosa la bwana Msa, Kisima cha giningi vitabu hivi vilikuwa vyamtumia local sleuth Bwana Msa

Hicho cha tumgidie *****, hukooooo dar is salam na pili pilipili nilivisoma primary jamani hata kitabu kimoja controversial 'dogodogo wanitesaaaa'

Faraj katalambula alitunga kitabu gani au 'simu ya kifo' kwa yeyote mwenye hazina hii adimu ya vitabu naomba sana ani PM ili nimuazime nisome vitabu hivi vya utoto wangu, vinanikumbusha mbali sana

Ukweli vitabu hivi labda uvikute tu kwa bahati kwa wale wauza vitabu vikuu kuu wanaopanga bidhaa zao barabarani. Ni kama vimetoweka kabisa. mimi mwenyewe kwa mfano nimejaribu kwa muda mrefu sana bila mafanikio kupata vitabu vya Roza Mistika, Mashimo ya Mfalme Suleiman, Titi la Mkwe, Kisiwa chenye Hazina (Treasure Island) na Jamaa hodari Kisiwani (Swiss Family Robinson), Aliyepanda tufani na kadhalika. Kwa hakika, ningependa sana hawa dotcom wangu wasome 'Almasi' kama hizi...

Kuna kitabu kimoja nadhani kiliandikwa na mtunzi wa Rosa mystika kilikuwa kinamhusu padri in the making kinaitwa'PETE' sikumalizia kukisoma and I have often wondered about it...kama hiyo ndio correct title nijuveni

Jibu lako lipo hapo kwenye nyekundu
Shigongo anaiga sana. Kwa mfano matukio mengi kwenye kitabu chake cha RAIS ANAMPENDA MKE WANGU yanafanana na matukio ya kwenye THE OTHER SIDE OF MIDNIGHT cha Sidney Sheldon...tafuta vitabu hivyo viwili uvisome kisha unambie

kuna kitabu kinaitwa "utu bora mkulima" jamani hivi mtunzi wa kitabu hicho ni nani?

Utata wa 9/12,mdunguaji,mkimbizi,bondia.Hapa namzungumzia Issa Tuwa, sijui ameishia wapi huyu jamaa.Hadithi ya kwanza hapo juu ilikua ni utunzi wa aina yake kuzungumzia viumbe waliogombana sayari ingine wakaja kutafutana hapa duniani

Similar Discussions

Back
Top Bottom