Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Kabla ya Gen John

-Aliongea Rev wa dini kutoka North. Alioongelea mambo ya kiroho na demokrasia. Alisisimua sana ukumbi kwa mpangilio wa hoja

-Kisha akaja Karim Al Jabar, naye aliongelea si kama kiongozi wa dini bali maudhui yaliyoakisi Uislam .

-Na kisha akaja Mr Khan, ambaye mtoto wake Khazir Khana aliuawa akiwa askari wa Marekani. Mzee alipeleka ujumbe wa patriotism akim challenge Trump kupitia kauli zake dhidi ya Immigrant na Uislam

Hawa wote waliwakilisha vizuri sana ujumbe wao
 
CHELSEA CLINTON

-Nipo kama Amerika, mama , Demorats and proud a daughter

Anaongelea malezi yake kwa Hillary


-
 
CLINTON

Anaongea

-Anashukuru familia kwa ushirikiano

-Anawashukuru Obama, Michelle, VP na Bernie Sanders

-Kwa wpenzi wa Sanders, ninawasikia, njia yenu ndiyo njia yetu

-Mbadiliko ya kweli kwa Amerika yanaanza na progressive

-Tupo Phil, eno ambalo taifa letu lilipozaliwa. Tunajua historia na hatari iliyokuwepo kwamba, historia isingeandikwa kama ilivyo

-Mbabu zetu walikumbatia ukweli wa kuwa, tuna nguvu kwa pamoja

-Nguvu za ajabu zinatishia kuuvuruga. Kama ilivyo kwa mababu, ni juu yetu kuamua kama tutafanya kazi pamoja ili tunnyunyuke pamoja

-Tumemsikia Trump akitaka kututenga na dunia, amechukua GOP kutoka morning hadi usiku tororo. Inatumbukiza chuki.

-Franklin alisema the only thing we have to fear is fear itself

- Tutakumbana na changamoto, hatutajenga kuta. Tuafungua njia kwa immigrant wanaochangia uchumi. Hatutapika marukufu dini, tutaungana kushinda magaidi

-Kuna vitisho vingi ndani na nje. Tuna Taifa lililochangamana, tunavijana wavumilivu, jeshi kubwa, wagunduzi, uhuru na haki
 
-Niwaambie nimetembea nchi 112 m watu wakisikia Hillary wanaiona Marekani

-Asiwaambie mtu sisi ni dhaifu na kwamba ataweza peke yake

-Amerika wanasema, 'sitaweza, bali husema tutaweza pamoja'

-US haiwezi kuwa nchi ambayo mtu mmoja ndiye mwenye nguvu

-Tazama kilichotokea Dallas, Polisi chifu aliomba jamii imsaidie, na katika siku 12 watu 500 walijiandikisha kujiunga na polisi

-Hakuna hata mmoja anayeweza kufanya peke yake, naamini nguvu ya pamoja si maneno ya historia au mbiu ya kampeni ni mwongozo wa taifa tunalotaka kujenga

-Kwa unyenyekuvu na heshima nakubali nomination ya urais wa Amerika
 
Clinton

-Zipo nyakati watu katika ukumbi ni wageni katika ukumbi,si mmoja wao
Nimekuwa first lady, seneta na secretary of state.

Kazi zangu zinaeleza nini nimefanya si nini nitakachofanya

-Niwambie, familia yangu ni ya ujenzi, babu akiwa mjenzi kwa miaka 50

-Aliamini kutoa kwa kizazi ni kuwa fursa, kama ilivyokuwa kwa baba aliyekuwa football. Baba alitoa nafasi kwa kaka, na mama alikuwa abandoned na wazazi

-Kila mtoto mwenye ulemavu ana haki ya kwenda shule

-Mliowasikia wakizungumza katika jukwaa /(anawataja) wamenitia hamasa kama nilivyo wahamisisha.

-Nitakuwa Rais wa wote

-Tumefikia tamati katika historia, kwa mara kwanza chama kikuu kimetoa mgombe mwanamke kwa nafasi ya Urais

-Tuendele ili wanawake milioni 112 wawe na fursa wanayopaswa kuwa nayo

-Tutafanyia nini watu wetu

-Sidhani Obama na Biden wanapata sifa kutokana na crisis ya uchumi
 
CLINTON

-Hiyo bado haitoshi, na tusiridhike na mafanikio hayo

-Kuna watu wanadhani hakuna heshima kwa kazi wanayofanya

-Dem hatufanya kazi ya kutosha ku empower Amerika
- Kutengeneza ajira na ujira mzuri hapa Amerika
- Naamini US inastawi middle class ikistawi

-Tunataka kuchagua supreme justice, na kama ni muhimu tutafanya mabadiliko ya katiba

-Naamini wall street haitpora main street again

Naamini climate change ni kweli, na tunaweza kutumia renewable energy kuiweka dunia salama

-Immigration reform ni jambo jema na litaweka familia pamoja

-Kama unaamini haya, hii ni kampeni yako

-Kama unaamini ujira unatakuwa utoshe ili tulsilee kwa umasikini, tuunge mkono

-Kama unaamini kusema no to unfair trade deal tuungane

-Kama unaamini haki za wanawake na social security, tuunge mkono

-Kama unaamini mama, dada wana haki sawa ya malipo, tuunge mkono

-Haa ndiyo yatasukuma uchumi

-Tutapitisha sharia ya kazi na ajira ili kuwekeza katika 100 days
 
Clinton

-Tutafanya tuition affordable na kuokoa watoto wenye madeni ya ada

- Tutawasidia wanaotaka kufanya kazi za trade na si lazima degree peke yake

-Tutawasaidieni ku balance, family leave

-Mashirika na taasisi zitalipa shea yao ya kodi

-Wengi wanasema utafanyaje haya yote? Angalia rekodi yangu

-Chaguo letu katika uchaguzi linakuja katika usalama

-Tunahangaika na adui aliyedhamiria na lazima tuwashinde

-Watu wanaangalia kiongozi wa kuwafariji, kufanya kazi na washirika na kuweka mambo sawa hapa nyumbani

-Ninajivunia kuzuia Iran nuclear prog bila risasi.

-Ninafurahi tumeweka hali ya mazingira sawa, na sasa ni kila mmoja awajibike

- Jeshi letu ni hazina, Rais lazima aheshimu wanaojitoa mhanga

-Jiulize Trump anaweza kuwa kamanda in chifu!

-Hawezi kukabliana na changamoto za uchaguzi, fikiria akiwa white house

-Mtu unayeweza kumtibua kwa tweet, utamwamini vipi na silaha?
 
Clinton

-Kama unadhani nchi inatakiwa kuwa salama, hatuwezi kuwa na Rais aliyewekwa mfukoni na chama cha wauza silaha

-Tutafanya kazi na wamiliki wa silaha kuziweka mbali na wahalifu

-Tuongee na kusikilizana, tuvae viatu kwa vijana wanaokabiliana na ubaguzi wa kimfumo. Tuvae viatu kama Polisi asiyejua nini kitamtokea

-Tutarekebisha criminal justice system

-tutalinda haki za makundi yote

-Tutasimama dhidi ya kauli za kutugawa, mwaka jana watu walimfanyia mchezo Trump wakimwita mburudisha.

Walimwacha akitukana akina mama, mashujaa kama Mcain, walemavu n.k.
 
ct-trump-republican-convention-2016-20160718

Wakati tukisubiri tathmini murua kutoka kwa Nguruvi3, mimi nadhani Democrats wamejikita zaidi katika hizi wanazozioana kama tofauti zao kimsingi na za Republicans.
  1. Upendo dhidi ya chuki (love vs hate)
  2. Umoja dhidi ya utengano (unity vs division)
  3. Matumaini dhidi ya wasiwasi (hope vs cynicism)
Tofauti hizi zimeonekana katika kauli zao na mabango yaliyotamalaki kwenye Convention yao yakisomeka...
  1. Love trumps hate (Upendo hushinda chuki)
  2. Together we are strong (Umoja ni nguvu)
  3. America is great. (America ni taifa kubwa)
Democrats: We don't build walls around us, we build bridges to unite us.
Republicans: We are going to build a wall and Mexico will pay for it.

367E0AB300000578-3702651-image-a-29_1469163412982.jpg
Mkuu mag3 wakati tunasubiri analysis ya HC kutoka kwa nguruvi3. Hebu kwa faida ya wanajukwaa wengi tukumbushe mara ya mwisho hawa wamarekani kukipa uongozi chama tawala awamu mbili mfululizo. Hapa namaanisha kwa mfano,Democrat wamepata fursa ya kuongoza miaka yote 8 ya obama. Mara nyingi hapa wamarekani wakikipa chama uongozi wa miaka 8 mfululizo,uchaguzi unaofuata(km huu) mara nyingi huwa wanafanya mabadiliko. Nataka unikumbushe mara ya mwisho chama kupata uongozi kwa miaka 12 au 16 mfululizo ilikuwa mwaka gani!!?? Najua chama kikivurunda huwa kinaishia miaka 4 km ilivyokuwa kwa George bush senior miaka ya 90.
 
Ni muda wa Rais atakayeifanya America great again kwa budget

- Ninamuona baba kama mtu anayeipenda nchi yake na aliyetayari kuifanya great again

-Nina charity inayoongozwa kwa maadili na uadilifu na siyo charity zenye 'corruptions'

-Kwa wasio na ajira, baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa veteran waliopuuzwa baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa undocumented illegal worker , baba anagombea kwa ajili yenu

-Kwa single mom na walemavu, baba anagombea kwa ajili yenu

-Nov nawaomba mpige kura kwa mgombea anayejua kwanini anagombea, ambaye si mwanasiasa na ambaye hajui gov cheque

-Mgombea asiyenunulika au kushawishika.

-Pigeni kura kwa mgombea asiyehitaji hii kazi. Najivunia Trump na mtoto wake, na najivunia kuwa sehemu ya kampeni. Baba ulitufundisha kwa mifano, ni shujaa na rafiki na Rais ajaye wa America
Hayo maneno yamenivutia sana kutoka kwa Mtoto WA Trump...
 
TATHMINI

Mkutano mkuu wa vyama RNC au DNC ina malengo yafuatayo
1.Kumthibitisha mgombea wa chama 'standard-bearer'
2. Kuunganisha wanachama baada ya maumivu na mkovu ya chaguzi za ndani
3.Kutangaza sera za chama 'platform'

Kwa pamoja RNC na DNC walikuwa na presumtive nominee 'watarajiwa'
Na wote wamethibitshwa kupitia kura za maoni na kura ndani ya Convention.

Pamoja na hati hati za kupeleka uchaguzi katika convention, wagombea wote waliepuka hilo kwa kuwa na idadi ya kutosha ya wajumbe

Swali, je iliwahi tokea wagombea kutopatikana hadi convention? Jibu, ni ndiyo

Hivi karibuni Ronald Reagan na Gerald Ford(Republican), Nixon na Rockefeller (Republican). T.Kennedy vs J.Carter(Dem) n.k.

Brokered au contested convention au open convention huacha makovu makubwa na kuondoa ili azama ya 2(kuunganisha wanachama)

2016, pamoja na kutokuwa na contested convention vyama vyote vimekabiliwa na tatizo la kuunganisha wanachama.

Republican wakimkataa Trump hadharani (Never Trump)
Democrats wakiwa na 'Sanders Supporters'

Kwa GOP licha ya never Trump viongozi waandamizi walisusia mkutano.
Haikuwepo familia ya Bush, Mitt Romney, John Mcain na key figure nyingine

Walioshiriki ima hawakuwa na ujumbe mzito kama Rubio, au walitumia fursa kubomoa (Ted Cruz) na wengine kujijenga kwa siku za usoni

Kulikosekana ile 'conservative au basi progressive conservative'

Republican hawakuwa na 'A list' tofauti na A list ya Dem iliyoita vigogo wote

Never Trump wameondoka Clev wakiwa na morali ule ule
Sanders Supporters wameondoka Philly wakiwa na morali, idadi ikipungua

Kuwepo kwa A list ya Dem, mkutano umewaunganisha kwa kiasi kikubwa
Kukosekana kwa A list kwa GOP, mkutano haukubadili hali ya mambo

Hata hivyo, hoja ya 3 hapo juu inaeleza matokeo zaidi

Tutajadili
 
Taratibu za uchaguzi wa Marekani

Mwaka 2008 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Democrat
Mwaka 2012 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Republican
Na mwaka 2016 mkutano mkuu wa kwanza ni Republican
Nguruvi3 Kwani USA ina vyama viwili tu vya siasa.. Na ndio vimesimamisha wagombea Urais.. Je mgombea binafsi anapewa nafasi gani, maana kama yupo na hapewi nafasi, je kwa Nchi yetu ambayo watu wanataka mgombea Urais.. Je itakua na tija gani
 
Tathmini

Hoja ya 3, kutangaza sera za chama

Republican: Kinachowatia hofu kuhusu Trump ni kutomwelewa kama ni conservative au progressive cons. Maisha binafasi hayaakisi, sera zake zinakinzana na zile za GOP

Republican wanamuona habebi zile sera zao.
Kutokana na mtafaruku GOP, muda wa kutengeneza plaform ya pamoja haukwepo.Kilichopo ni falsafa ya Trump

Kwavile hakukuwepo na platform, Trump anatumia hoja za Sanders kama sera
Anakwenda mbali kwa kutenga makundi katika jamii kama watu wa rangi.

Hofu ya usalama inamsaidia kujenga hoja dhidi ya wahamiaji na makundi mengine muhimu katika uchaguzi 'electoral college'

Kinachotokea Ujerumani/Ufaransa kinamdhihirisha kuwa sahihi.
Kauli mbiu yake ya law and order inasikika vema katika jamii kwa wakti huu

Sera zake za uchumi zimejikita katika business zake.
Kukiwa na idadi ya watu wasio na kazi, kauli zake zinabeba uzito

Trump hakutumia mkutano kupambanua sera zake kwa undani.

Alitumia nguvu za Republican (ulinzi na usalama) bila kuoanisha na sera za kiuchumi na za mambo ya nje.

RNC ilitumia muda mwingi katika kusafisha taswira ya mgombea
 
Democrats
Walichofanikiwa ni kumaliza mkutano kwa nguvu. Siku 2 za awali zilikuwa kusafisha taswira ya Clinton ambaye kama Trump ina matatizo

Siku ya 3 na 4 zilikuwa za nguvu. Kwanza, kuonyesha madhaifu ya Trump, kisha kushirikisha makundi ya jamii kama waathirika wa mauji, iwe akina mama, Polisi, au wanajeshi. Tatu kujenga taswira ya Utaifa 'patriotism'

Siku ya mwisho, iliwahusisha viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, wanajeshi, Polisi na Republicans kama mshauri wa Reagan na independents kama Bloomberg n.k.

Hili lilisaidia sana kutuliza hofu iliyotanda na inayotumiwa na Trump kuhusu usalama
Lilisaidia sana kuonyesha madhaifu ya Republican na Trump katika eneo lao la ulinzi

Mwisho, Hillary akaeleza msimamo wa chama 'platform' kwa undani kwasababu kazi nyingine zilishakamilika na waliotangulia

Tatizo linalowakabili ni kuwa madarakani! Wanatetea vipi haya ynatotokea?
Sanders supporters ambao haijulikani nini hasa kipo nyuma yao

Pamoja na kushirikisha sera zao , bado upo upinzani.

Tofauti na Trump anayefahamu 'mahasimu wake ndani ya chama' Hillary na kampeni hawajui nini hasa kinasukuma kundi la Sanders

Trump ana deal na known, Hillary ana deal na unknown!

Kwa ujumla, 'choreography' ya convention ya DNC ilikuwa organized kuliko RNC. Swali, ni je, wamegusa jamii kwa uhalisia kama anavyogusa Trump?

Ni haki kusema kuwa, pamoja na kususiwa na matatizo mengine, Trump amefanya convention kama 'familia' lakini amefanikiwa kwa kiasi chake

Tusemezane
 
Mkuu mag3 wakati tunasubiri analysis ya HC kutoka kwa nguruvi3. Hebu kwa faida ya wanajukwaa wengi tukumbushe mara ya mwisho hawa wamarekani kukipa uongozi chama tawala awamu mbili mfululizo. Hapa namaanisha kwa mfano,Democrat wamepata fursa ya kuongoza miaka yote 8 ya obama. Mara nyingi hapa wamarekani wakikipa chama uongozi wa miaka 8 mfululizo,uchaguzi unaofuata(km huu) mara nyingi huwa wanafanya mabadiliko. Nataka unikumbushe mara ya mwisho chama kupata uongozi kwa miaka 12 au 16 mfululizo ilikuwa mwaka gani!!?? Najua chama kikivurunda huwa kinaishia miaka 4 km ilivyokuwa kwa George bush senior miaka ya 90.
Naomba nichangie tukimsubiri mkuu Mag3 atusaidie zaidi

Rais wa mwisho wa Democrats kuwa na vipindi 5 mfululizo alikuwa Harry Truman kama kumbukumbu zangu zipo sahihi. Na hii ilikuwa 1948

Chama cha mwisho kuwa na vipindi 3 mfululizo ni Republican, baada ya Reagan na kufuatiwa na George Bush senior
 
Mr Khan

Huyu alipangwa kuongea siku ya tatu. Khan aliopoteza mwanae vitani
Aliongelea kauli za Trump kuwatenga Waislam na kumtaka asome katiba.
Ujumbe wake ulijaa hisia kali dhidi ya Trump na ubaguzi

Kwa wapenzi wa Trump, ujumbe huo hauna athari zozote
Kwa wasiomtaka Clinton ujumbe huo hauna athari zozote

Kwa independents ujumbe huo hauna athari kwasababu wanataka kushawishiwa na hoja zaidi

Kwa kundi lenye chuki na Trump, ujumbe huo umekoleza chuki

Kwa kundi lenye wasi wasi na halina uhakika, ujumbe ule uliondoa mashaka na wasi wasi waliokuwa nao dhidi ya Trump

Tusemezane
 
Back
Top Bottom