Duru za siasa - Matukio

SIASA ZA MAREKANI
Rais Obama ameapishwa kwa muhula wake wa mwisho. Obama ameapishwa mara mbili kwasababu kikatiba siku ya uapishaji wa Rais ni tarehe 20 na kwa vile ilikuwa Jumapili basi ilirudiwa tena Jumatatu.

Ni kipindi cha pili chenye changamoto nyingi ikiwemo uchumi. Kwa kuanzia tu Obama alikabiliwa na tatizo la fiscal clif ambalo limepatiwa ufumbuzi. Ufumbuzi si wa kudumu bali kuweza kuepusha kudorora kwa uchumi wa dunia kwa mara nyingine, bado linarindima ingawa si kwa kiwngo kile kilichotishia uchumi wa dunia.

Kuna tatizo la deni la taifa na kiwango chake ''debt ceiling'' hili nalo linaonekana kupewa afueni ili bajeti ya serikali iendelee n.k.

Lipo suala la uhamiaji ambalo halikuwahi kuguswa hapo awali. Kutokana na matokeo ya uchaguzi, Obama ana nafasi nzuri ya kulipatia ufumbuzi kwasababu kura za Walatino zimeiumiza sana Republican na watafanya kila wawezalo ili kuepuka hasira za Walatino waliompigia kura G.Bush kwa asilimia 44 na Mitt Romney asilimia 20

Nafasi aliyo nayo Obama ni ile hali ya kuwa hana chochote cha kupoteza tena na wakati huo huo Republican wakiwa wameshindwa jaribio la kumfanya rais wa muhula mmoja kama ilivyokuwa kwa Jimmy Carter.

Hata hivyo bado Obama hawezi kufanya lolote alitakalo kwasababu kuna uchaguzi wa senate na Congress katika ya muhula, hivyo anaweza kukabiliana na upinzani hata ndani ya chama chake.

Katika usalama wa taifa, Obama atatakiwa ahakikishe kuwa vita ya Afghan inaisha na askari wanarejea.
Baada ya kufaulu kule Iraq changamoto nyingine ya mageuzi ya mashariki ya kati ilizuka.

Mashariki ya kati Marekani ilifaulu kumuondoa Ghadafi lakini yametokea mengine kule Syria na Egypt ambako hali bado si shwari.

Mashariki ya kati imezaa tatizo lingine la Mali. Tatizo hilo halikuanzia Mali bali Ageria na sasa nchi za Magaharibi zinafanya jitihada kukabiliana na wapiganaji wa kiislam.

MZOZO WA MALI
Mali imekuwa katika ramani kwa muda mrefu kama sehemu ya kufundishia wanamgambo wa Alqaeeda na inajulikana kwa nchi za magharibi kama Alqaeeda in Magreb Region. Magreb region ni pamoja na Algeria na Morocco.

Tunakumbuka jinsi uchaguzi wa Algeria pale chama cha FIS kiliposhinda lakini ulikataliwa na mataifa ya magharibi.

FIS ni waislam wenye msimamo mkali sana na washirika wazuri sana wa Alqaeeda.
Mahusiano yao na nchi za kiarabu ni makubwa na lengo lao ni kuigeza Algeria kuwa nchi ya Kiislam.
Ingawa hilo lingeweza kutokea kwa taabu lakini kuwapa serikali ilikuwa ndio mwanzo wa kufungua kituo cha ugaidi.

Baada ya kuangushwa kwa Ghadafi silaha nyingi na baadhi ya wapiganaji wamekimbilia katika nchi kama Mali.
Mali ni nchi kubwa sana kuliko Afganistan au Pakistan.
Eneo la vita vya sasa ni kubwa kuliko Afghan kwa kusema kwa uchache tu.


Itaendelea......
 
VATICAN NA TANZANIA

Usiku wa Leo papa Ben
edict ameacha rasmi kiti cha enzi katika uongozi wa kanisa Katoliki duniani.
Kujiuzulu kwake kumezua maswali mengi kuliko majibu na hakika siri hiyo itabaki kwa Vatican na jopo la Makadinali duniani lijulikanalo kama Conclave.

Kujiuzulu kwa Papa kumetokea huko nyuma miaka zaidi ya 600 iliyopita na imekuwa kama mazoea Papa kufariki akiwa madarakani.

Papa Benedict aliyejulikana kama kadinali Ratsinger ndiye alikuwa msaadizi wakati wa siku za mwisho za uhai wa John Paul
Yeye alijulikana sana kwa misimamo kama kadinali ''No'' kwa maana ya kuwa alitaka kanisa libaki kama lilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ni kwa bahati mbaya kuwa hali ya ukatoliki duniani imepungua sana kasi yake.
Huko Ulaya ni asilimia 20 tu tena ya wazee waliowaumini wa dini za kikristo achilia mbali madhehbu.
Kinyume chake ustawi wa kanisa umekuwa Afrika, Asia na Latin America.
Hili lina maana sana kama tutakavyoliangalia mbeleni.

Inasemekana kuwa Benedict ana tatizo la moyo na amekuwa anaishi kwa kifaa maalumu katika moyo wake.
Hilo ndilo alilosema ni chanzo cha yeye kujiuzulu. Pengine uzito wa majukumu na umri wake havimruhusu kuendelea.

Bado alikuwa na nafasi ya kuendelea kuwa Pope akisaidiwa na wasaidizi wake wakuu. Hakupenda kufanya hivyo.

Kuna taarifa kuwa papa ameamua kujiuzulu ili kujenga msingi wa mapapa wajao kujiuzulu ukifika umri flani.
Pengine ni kutokana na uzito wa majukumu alioubeba wakati wa John Paul ndio maana akaona ni vema aweke msingi huo

Habari ambazo zimezagaa sana na zimekanushwa na Vatican ni kuhusu kashfa zinazolikumba kanisa kuanzia zile za ulawiti hadi za rushwa.

Kuna taarifa kuwa kashfa za ulawiti zilizofanyika wakati akiwa kadinali anazifahamu na amezifukia.
Wachunguzi wa mambo wanadai kuwa kashfa hizo zimefikia mahali ambapo papa angeweza kuitwa ili kutoa ushahidi kwa vile nyingi alizijua.

Hilo tu lingeondoa imani ya waumini wake kwasababu kama kiongozi wa kiroho hatakiwi kufanya ''justice obstructions''

Ili kuepuka dhahma hiyo ndio maana imemlazimu aachie ngazi ili kujinusuru na kulinusuru kanisa.
Zote hizo zinabaki kuwa dodoso lakini ukweli tunao ujua ni kuwa papa kajiuzulu.

Katika kumtafuta mrithi, jopo la makdinali limekutana mjini Vatican.
Jopo hilo hujulikana kama conclave ndilo litalaomchagua Pope ajaye.

Kazi ya kumtafuta mrithi hufanywa kwa siri sana hadi pale majina yatakapopelkwa mbele ya conclave.
Hili hufanywa na intelejinsia

Wapo wanaosema sasa ni wakati Papa atoke Africa kwa kuangalia ukuaji wa kanisa.
Miongoni mwao ni kadinali kutoka Nigeria mwenye heshima sana ndani ya Vatican.

Wapo wanaosema atoke Latin America na wengine kusema atoke Asia kama Philipine.
Hata hivyo kadinali kutoka Canada katika jimbo la Quebec ameonekana kuwa mbele ''front runner'' miongoni mwa wengine

Tatizo moja ni kuwa bado kuna imani kuwa Papa lazima atoke maeneo ya Ulaya.
Imani hii pia inashadidia ukweli kuwa ni ngumu sana mwafrika kukubalika kama Papa mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Huu ni ubaguzi ambao hauwezi kufichwa na unabaki kuwa ukweli.

Hivyo hadi sasa tubaki tukiamini kuwa papa ajaye huenda akatoka Canada au Philipine na pengine ulaya.
Uwezekano wa kutoka Afrika ni kama haupo japo lolote laweza kutokea.
Tusubiri conclave itasemaje.

TANZANIA
Wiki hizi mbili nchi imekumbwa na migogoro ya kidini kuanzia kule Mwanza, Geita hadi Zanzibar.
Katika matukio yote ambayo ni ya kiovu bila kujali nani yu sahihi au la, tukio lililozizima ni lile la Zanzibar.

Tukio la Mwanza na Geita ni mgogoro ambao unajulikana.
Hii haijengi uhalali bali ina unafuu kwasababu tunajua ni watu wa aina gani na kwasababu gani.

Tukio la Zanzibar ni la kutisha. Hii si mara ya kwanza au ya pili.
Matukio ya kuchoma moto kanisa, kunusurika padri kuuawa na hatimaye padri kuuawa na watu waliojificha bila kujulikana linaleta picha nzito na mbaya sana kuliko matukio mengine.

Narudia kusema uovu ni uovu lakini hata uovu una madaraja na hili la Zanzibar daraja lake ni kubwa.

Tukio hili limelenga kuleta hofu. Kwa tafsiri tukio ni la kuwatisha waumini wa kikristo kwa lugha ya kigeni ni terror. Tendo la kumtisha mtu huitwa terrorism na afanyaye hilo ni terrorist.
Kwa hiyo tukio la Zanzibar ni la kigaidi kwa vigezo vyote vya maana ya ugaidi.

Ni kwa muktadha huo tutaliangalia tukio hilo kwa ukaribu sana na maana yake kwa mustakabali wa taifa.

Itaendelea.............
 
Asante Mkuu Nguruvi3 kwa kuendeleza uzi huu...

Kujiuzulu kwa Papa ni kitu ambacho hakijazoeleka kabisa hasa ukizingatia kuwa mara ya mwisho hilo kutokea ilikuwa miaka 600 iliyopita hivyo ni kitu kigeni mno...Lakini kwa kuwa utaratibu wa kujiuzulu upo na unakubalika kwa mujibu wa kanuni za Vatican, na kwa kuwa ametoa sababu za kiafya ambazo hazipingiki kutokana na umri wake mkubwa then suala hili mwishowe litakuja kukubalika na wengi na hatimaye kuzoeleka hata kwa viongozi watakaofuatia.

Kuhusu vurugu zinazoendelea hapa nyumbani niseme tu kwamba Serikali inaposhindwa kusimama katika nafasi yake. Inaposhindwa kusimamia sheria na taratibu kwa ukamilifu na ujasiri bila kujali nani anavunja sheria na anatoka wapi na anasali wapi ndiyo inatufikisha hapa. Mungu atusaidie kwa kweli!
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu Nguruvi3 kwa kuendeleza uzi huu...

Kujiuzulu kwa Papa ni kitu ambacho hakijazoeleka kabisa hasa ukizingatia kuwa mara ya mwisho hilo kutokea ilikuwa miaka 600 iliyopita hivyo ni kitu kigeni mno...Lakini kwa kuwa utaratibu wa kujiuzulu upo na unakubalika kwa mujibu wa kanuni za Vatican, na kwa kuwa ametoa sababu za kiafya ambazo hazipingiki kutokana na umri wake mkubwa then suala hili mwishowe litakuja kukubalika na wengi na hatimaye kuzoeleka hata kwa viongozi watakaofuatia.

Kuhusu vurugu zinazoendelea hapa nyumbani niseme tu kwamba Serikali inaposhindwa kusimama katika nafasi yake. Inaposhindwa kusimamia sheria na taratibu kwa ukamilifu na ujasiri bila kujali nani anavunja sheria na anatoka wapi na anasali wapi ndiyo inatufikisha hapa. Mungu atusaidie kwa kweli!
Ni kweli kuwa hakuna papa katika kipindi cha karne 6 aliyewahi kufanya hivyo.

Hata hivyo Benedict alifanya kazi na John Paul ambaye siku za mwisho za uhai wake kanisa liliongozwa na ''inner circle'' ya Vatican akiwemo Benedict. Nadhani kwa kuona hilo yeye ameamua ku-set a platform kwa wajao ili isifike mahali Papa anakuwa hana uwezo lakini bado anaongoza kwa kutumia jina.

Kuna hili la kashfa za ngono ambalo limeitafuna sana kanisa.
Siku chache zilizopita kadinali mmoja ametuhumiwa katika kashfa kama hiyo na leo conclave ikikaa yeye hayumo.

Uzito wa madai hayo umeifanya kazi ya papa kuwa ngumu sana kwani kila mahali alipozuru ilibidi atangulize samahani kwa makosa ya watu walio chini yake tena kwa kashfa za ngono.

Dunia inabadilika sana, hili suala la yeye kuhojiwa kwa kujua uchafu na kuufunika chini ya kapeti nalo halipaswi kupewa kisogo. Kashfa nyingi zilijulikana lakini katika kulinda hadhi ya Vatican zilifichwa.

Zimeandikwa sana na jinsi mawasiliano yalivyokuwa yanafanyika na makao makuu.
Wakati huo Ratsinger alikuwa mshauri mkuu ndani ya st Peter.
Pengine hofu ya kuitwa kuhojiwa nayo yaweza kuwa ni sababu.

Swali linalosumbua akili yangu ni kuwa kwanini hawa watawa, walei, mapadri na maaskofu wanaingia katika kashfa za ulawiti na si ngono kama ya mume na mke?
Tunafahamu wao ni binadam na ni dhaifu tu kimaumbile, lakini basi ingetokea wao kuwa na mahusiano, mathalani mapadri na watawa, au viongozi na wanawawke pengine lingeleeweka japo kwa taabu.

Kiichoeleweka na hasa upande wangu ni wao kuwalawiti vijana wadogo. Kwanini kuwalawiti na si kufanya ngono na wanawake? Sijui kama nitaeleweka lakini ndivyo ninavyojiuliza.
Kwanini weakness yao iwe katika vitoto vidogo vya kiume na si watawa, wanawake, machangudoa?

Ikumbukwe kuwa sasa hivi kanisa katoliki duniani linaongozwa na college of Cardinals ambao wapo Vatican katika kikao cha Conclave kitakachomchagua papa ajaye. Hili litatokea kabla ya pasaka.


TANZANIA
Kuhusu yanayotokea hapa nyumbani, nakubaliana nawe kuwa serikali imechangia sana katika kuzorota kwa hali.
Haiwezekani mtu auze DVD za kuhamasisha mauaji aachwe tu aendelee kusambaza sumu hiyo.

Tumeona kule Zanzibar Watu wakichomwa moto na vibanda vyao kwa kisingizio cha muungano.
Hiki tulionya kuwa ni kisingizio tu kwani wakati wanafanya hivyo lengo lilikuwa Mtanganyika kwa jina na mkristo kwa lengo.Wote waliofanya ujinga ule waliachiwa huru.

Likaja la kunusurika Padri kuuawa, hadi leo hakuna aliyefikishwa mbele ya sheria bali ni zuga za uchunguzi.
Limefika la Padre kuuawa sasa.

Nasema huu ni ugaidi kwasababu lengo ni kuwatisha waumini wa dini nyingine au kuweka shinikizo ili serikali ikubaliane na madai ya kuwaachia huru masheikh walioko magereza.

Serikali ingefuatilia kwa umakini tahadhari za watu na makundi mbAli mbali tusingefika hapa tulipo.

Kuna msomaji wa safu hii kaniuliza kuna tofauti gani ya yale ya Mwanza, Geita na Zanzibar? Kama ni ugaidi kwanini isiwe kote iwe Zanzibar.

Jibu langu ni kuwa wote ni uovu tu lakini uovu unatofautiana.
Kule Mwanza na Geita kunajulikana ni suala la kuchinja nyama. Kwamba tatizo linafahamika na limekuzwa kijinga na watu wasio na uelewa au pengine tu kwa kuchochewa.Pande zote zimekosa busara na kupelekea yaliyotokea.

Zanzibar ni Ugaidi kwa sababu tafsiri ya ugaiDi ni tisho (terror) na tendo ni kutishia (terrorism) na afanyaye ni gaidi(terrorist). Gaidi siku zote hujificha na hata sababu zake huzificha. Anachotaka ni kufikia lengo lake la kutishia.

Zanzibar wanaua ili kuwatisha Watanganyika na hasa Wakristo ima kuhama Zanzibar au kuacha kazi zao.
Kwa uelewa mdogo hili ni jambo la hatari sana kwa mustakabali wa Zanzibar.

Sifa ya Zanzibar mbali na nyingine nzuri nyingi ni kuwa Kiota cha kuzalishia watu wenye misimamo mikali kisiasa.
Sifa hii imeondoa sifa ya Zanzibar kuwa sehemu ya ustaraabu wa kale katika pwani ya Afrika mashariki.

Hivi sasa Zan inaangaliwa kwa jicho kali na mataifa mengine hasa ya maghAribi.
Mataifa hayo yangependa kuona Zanzibar inadhibitiwa ili isije ikawa Somalia au Mali nyingine.
Kwa haya yanayotokea ndio kwanza yanashadidia hoja ya mataifa haya.

Kuna mambo mengi yatatokea. Kwanza ni kuzuia sekta ya utalii kukua kwa kuonya watalii kutozuru Zanz.
Uchumi wa Zanz unatEgemea sana utalii. Hapo kutakuwa na hali ngumu sana na huenda wawekezaji wakakimbia kama si kuishi kwa machale.

Pili, Tanzania itashinikizwa kuhakikisha kuwa muungano hauvunjiki ili kuweza kudhibiti Zanzibar kwa ukaribu.
Wakati mchakato wA katiba ukiendelea tuataona nguvu ya kuzuia hilo ikijitokeza.
Kwa kuanzia tu vitambulisho vya taifa la Tanzania vimetolewa. Hii maana yake ni kuwa iwe iwavyo muungano utakuwepo

Miongoni mwa waliochukua ni Maalim Seif. Hii ilifanywa makusudi ili kuonyesha kuwa hata Seif anaunga mkono muungano.
Maana yake ni nini? Ni kuwa zile ndoto za Zanzibar huru haZitatimia kwasababu uwepo mkataba au serikali 3 , 4 au 5 bado kuna mambo ambayo Zanz itabaki katika udhibiti.

Hii haitokani na Tanganyika bali shinikizo la mataifa makubwa kuhakikisha kuwa kisiwa hiki kinapewa ukaribu katika uangalizi.

Lingine linaloweza kutokea ni kuwaunga mkono wajitenge kabisa katika mambo yao.
Mataifa ya magharibi yatafanya hivyo ili kuweza kutoa msaada na huenda kuifanya Zanzibar ijione kuwa bora zaidi kuliko ndani ya muungao.

Hata hivyo misaada hiyo itakuwa na masharti na si aghalabu tutasikia Zan huru ikishinikizwa kukubali matakwa kama kuheshimu haki za binadamu katika imani na pengine kukubali mambo kama ya ndoa za jinsia moja, ushoga n.k.

Yote hayo yatafanywa ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zina uakribu sana na Zanz ili kujua na kudhibiti hali itakayojitokeza.
Hivyo mauaji ya kigaidi kama yanayoendelea hayaisaidii Zanz hata kidogo.
Yanazidi kuiweka katika ramani ya dunia kwa alama mbaya sana.

Twende mbele na nyuma lakini lawama zinabaki kwa serikali. Serikali zilizopita ziliweza kudhibiti hali kabla ya uharibifu,
Kutoa uhuru wa kuabudu bila bughudha, kuweka mipaka ya dini na siasa na hata kuwashughulikia wakorofi mapema.

Udhaifu wa kiongozi wa serikali ya leo ndio umetufikisha hapa. Hata baada ya maonyo ya kila aina serikali hiyo haikuchukua hatua na sasa inapigana kujenga ukuta na si kuziba ufa.

Hili liwe fundisho kwa Watanzania, wakikaa na kujua kuwa kiongozi wa nchi si mcheza mpira au mpiga zumari.
Ni mtu muhimu sana katika mustakabali wa taifa na upatikanaji wake ni lazima uzingatie, uwezo, uadilifu na maono ya kiongozi na siyo ucheshi,tabasamu au undumila kuwili.

Tusemezane
 
Niwatake radhi kwanza. kwasbabu za kifundi duru za siasa hazikuweza kubandika matukio kama ilivyokawaida.

Tutaendelea kuangalia

Kifo cha Hugo
Uchaguzi wa pope Jumanne na yale yaliyo nyuma ya pazia
Uchaguzi na matokeo yake Kenya
Kuumizwa kwa mwanahabari Kibanda.

Tuta upload mambo yakiwa tayari.
 
COMMANDANTE HUGO CHAVEZ
Rais Hugo Chavez amefariki dunia na mazishi yake ya kitaifa yalifanyika Ijumaa.
Hugo amekuwa mgonjwa matibabuni nchi Cuba kwa muda mrefu.

Chavez alikuwa anaugua Cancer na katika hatua za mwisho za maisha yake ilionekana ni vema arejee nyumbani kukutana na kifo chake katika nchi aliyoipenda na kuingoza kwa miaka 14.

Kuingia kwa Hugo madarakani kuliambatana na misuko suko hata hivyo baada ya kuingia amekuwa anachaguliwa katika chaguzi tatu. Hugo anakumbukwa kama kingozi aliyejua njaa ni kitu gani na umasikini ni nini.
Venezuela ni nchi yenye mafuta hivyo kukodolewa macho sana na mataifa makubwa.

Kiwango cha mafuta ya Venezuela kinatosha kuathiri soko la dunia kwa namna flani.
Ikizingatiwa kuwa yupo America kusini hilo tu lilimfanya aonekane ''toto tukutu''.
Hugo aliamua kufuata siasa za kisoshalisti na role model wake alikuwa Fidel Castro.

Ikumbukwe kuwa wakati Castro akiwa mgonjwa sana ni Hugo ndiye aliyekwenda kumjulia hali.
Ni urafiki huo pia ulizaa maadui wengi kwa kutambua kuwa siasa za CUBA bado zina wafuasi katika Latin America.

Hugo ndiye kiongozi aliyeongelea kwa undani na uchungu kuhusu makazi duni ''slam'' na umasikini wa watu wake.
Aliamua kutumia pato la taifa katika kuendeleza makazi duni, kutoa elimu kwa kila mmoja na kuwawezesha wanachi wake kupata huduma za afya kwa kila mtu katika mazingira mazuri zaidi.

Imemchukua miaka 14 kupunguza tatizo la umasikini kwa kiwango cha asilimia 50.
Kama kuna jambo analokumbukwa nalo hili ni moja wapo.

Hata hivyo pamoja na yote Hugo alitengeneza maadui wengi na mkubwa akiwa mmarekani.
Ni kwa muktadha huo Hugo alijikuta akipata marafiki kama akina Putin na Ahmadinajeda kwasababu ya misimamo yake mikali dhidi ya ubeberu na ukoloni mambo leo.

Lakini pia Hugo alipata marafiki kama akina Morales na Rais wa Argentina achilia mbali nchi nyingi za Latin America.
Yeye alikuwa kiungo muhimu sana katika nchi hizi. Alizisadia hasa kwa mafuta kwa kutoa bei za kudumu ''constsnt price'' hata pale soko la dunia lilipo yumba. Lakini pia alitoa unafuu wa kupipa na hata kubadilishana bidhaa ilimradi kila mmoja awe mshindi ''win win situation''

Pamoja na utundu wake Hugo alikuwa karibu sana na wananchi wake na hivyo haikuwa rahisi kwa njama za mataifa makubwa kumuathiri ingawa njama za mapinduzi zimekuwepo.

Katika kumpiga vita, Hugo amekuwa na maadui hasa kwa kutumia propaganda za vyombo vya habari.
Yeye akiwa kama mwanadamu na Rais alikuwa na mapungufu yake.
Hata hivyo mapungufu yake yalikuzwa zaidi ya mema mengi aliyofanya.

Ni rahisi kusikia raia wa nchi nyingine wakimtuhumu hata bila sababu za msingi.
Na raia hao wameshindwa kuona kile nchi za magharibi isichokisema kama kuinua hali za maisha ya watu wake, kujenga misingi imara ya uchumi na kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumia kwa wananchi.

Kwa kuangalia hatua alizopiga commandante Chavez ni zaidi ya miaka 30 tangu tumejitawala na awamu tatu za uongozi kwa pamoja. Hugo ameweza kushinda kile kitendawili cha wananchi kunafaika na rasilimali zao.
Leo bado wananchi kama wa Mtwara, Mwanza na kwingineko hawajui rasilimali zinazowazunguka zinawasaidiaje.

Hugo alivuka vikwazo vya rushwa kubwa za kuuza nchi kama tunavyoshuhudia hapa kwetu.
Hakuweza kumaliza rushwa na hakika hakuna awezaye lakini yeye alikuwa na utashi wa kisiasa wa kuwatumikia watu wake.

Ni kutokana na utashi na dhamira yake, maelfu kwa malaki ya wana wa Venezuela walifurika mjini Carcas katika kumuaga hata kulazimu serikali kuongeza siku 7 zaidi za kuaga mwili wake.

Wengi wa waliojitokeza ni wale waliokuwa wamekata tamaa na masiha ya dunia hii lakini kupitia Championante Hugo waengi wameuona mwanga japo kwa mbali.

Huyu ni kiongozi aliyeacha legacy ya kukumbukwa kwa maiaka mingi ijayo.
Hugo ni ushahidi kuwa uongozi ni kujituma, kudhamiria na maono na kwamba marafiki si muhimu kuliko wale wanaoshinda kwa njaa na kulala katika slams.

Leo dunia inaomboleza kifo cha kamanda Hugo.

R.I.P el commandante championante Hugo Chav.

Tusemezne.
 
UCHAGUZI VATICAN

Uchaguzi wa papa au pope unatarajiwa kuanza leo.
Uchaguzi huo unafuatia kujiuzulu kwa papa Benedect kutokana na hali ya kiafya.
Mengi yamezungumzwa kuhusiana na hatua yake kama tulivyowahi kueleza huko nyuma.

Makadinali 116 wapo mjini Vaticana kwa kile kinachoitwa Conclave,yaani mkutano wa kumpata baba mtakatifu kwa imani za Wakatoliki.

Waumini wa kikatoliki wamekuwa wanapungua sana Ulaya hata kulazimu baadhi ya makanisa kufungwa.
Wengi waendao makanisani ni wazee waliostaafu. Imefika mahali katika nchi ya Ufaransa mapadri na viongozi wengine wamechukuliwa kutoka nchi za kiafrika kama Cameroun (francophone) ili kwenda kuendeleza makanisa na kuwasaidia watu kiimani katika kuendesha ibada zao.

Huko Marekani hali pia si shwari, lakini tofauti na Ulaya, wananchi wengi wa Marekani wanakatishwa tamaa na kashfa nzito za ulawiti zinazowakumba viongozi wa kanisa kama zile zilizotokea ambako zilimlazimu Papa Benedict aombe radhi kwa niaba ya kanisa.

Sehemu zilizobaki na nguvu kubwa ya ukatoliki ni America kusini, visiwa vya Carrebian, Afrika na mashariki ya mbali kama Ufilipino n.k.

Inasemwa kuwa idadi ya wakatoliki wa china ni kubwa kuliko ile ya Ulaya.
Hili ni changamoto kubwa kwa papa ajaye katika uchaguzi wa leo.

Habari za ndani zinasema kuwa kumekuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya conclave.
Waitaliano wanegependa papa atoke maeneo ya Karibu ili kulinda hadhi na utamaduni uliodumu miaka dahari.
Wamarekani wanasema sasa ni wakati Papa atoke Marekani ili kuifungua dunia kutoka katika mazoea.

Katiaka uchaguzi unaoanza leo kuna uwezekano Papa akatoka nchini Canada.
Inasemekana hili linaweza kutokea ili kuondoa mvutano unaojitokeza.

Ingawa kuna chapuo la kadinali mmoja wa Afrika lakini haionekani kuwa mataifa mengine yatakubaliana na kuwa na Papa mweusi. Hili halisemwi lakini ndivyo vyombo vingi vinavyolitazama.
Ni ngumu kwa hakika kusema nani ni mtarajiwa kwasababu utaratibu wa uchaguzi unajulikana kwa makadinali wa Conclave tu.

Kitu kinachozungumzwa katika vyombo vya habari ni ile taarifa iliyotolewa na Vatican kuwa hakuna ruhusa kwa mtu ku-twit au kutumia vyombo vya habari vya kijamii kumtangaza Pope hadi pale atakapotangazwa rasmi.

Kinachoshangaza ni kuwa ndani ya Conclave kuna makadinali 116 ni vipi basi hawa watumishi wenye daraja na hadhi hiyo wasiaminiwe hadi kuwekewa mizengwe kiasia hicho?

Utaratibu ni kuwa,ndani ya Conclave atachaguliwa Papa. Kuna kitanuru juu ya jumba ambacho kitatoa moshi.
Moshi ukitoka kama si mweupe basi duru la uchaguzi linaendelea hadi utakapotoka moshi mweupe.

Ni hadi hapo ndipo watatoka viongozi na kumtangaza Pope kwa mara ya kwanza makadinali wakiwa bado wapo ndani.
Ni utaratibu wa mazoea na kwa mara ya kwanza picha ndani ya conclave zilipigwa wakati wa uchaguzi wa Benedict.
Hili lilionekana kama modernization kwasababu haikuwahi kutokea huko nyuma.

Kitendawili cha nani ataongoza watu wapatao milioni 800 kitatengeuliwa kama si leo ni kesho lakini kwa uhakika misa ya jumapili St Pter Vatican itaendeshwa na Papa mpya. Ni nani huyo? Tusubiri

Tusemezane.
 
Roman catholic ina experience growth in africa,south america and parts of asia,that's where the future lies in terms of wingi wa waumini kwani katika nchi za magharibi hakuna meaningful growth ya waumini tena,so logic ingekuwa kuchagua pope kutokea latin america at least.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
UCHAGUZI WA VATICAN NA TUKIO LA KUUMIZWA A.KIBANDA

Kitendawili kimetanguliwa na kama tulivyowahi kusema kulikuwa na mvutano mkubwa sana kuhusu nafasi hiyo kwenda nje ya Ulaya au kubaki ulaya. Ilikuwa ni wazi kuwa nguvu ya Catholics ulaya imepungua sana.

Hata hivyo tujikumbushe huyu Pope ni nani.
Huyu ni kadinali wa jimbo la Buenos Aris-Argentina. Wazazi wake ni wahamiaji kutoka Italy miaka mingi.
Yeye anaongea lugha za Kitaliano, kilatino na Kiingereza.

Kwahiyo ana asili ya Italia na hiyo inaweza kumpa karata ya ushindi dhidi ya wapinzani wake wa karibu akiwemo kutoka jimbo la Quebec- Canada.

Mshangao kidogo ni kuona dunia ilikuwa tayari kuona papa mweusi kwani duru za habari zimekuwa zikimtaja sana Kadinali mmoja kutoka Afrika magharibi anayeonekana ni kichwa ndani ya Vatican.

Papa Francis alikuwa wa pili wakati wa kinyang'anyiro cha kumchagua Benedict aliyejiuzulu.
Haionekani kama umri utampa nafasi zaidi ya kutumikia watu wake kwani katika 78 uwezo wa kuhimili mikiki ya utawala wa watu wapatao bilioni 1 ni suala linalohitaji nguvu. Je atafuata nyayo za Benedict hilo linabaki kuwa swali

Papa Francis ni mtaalam wa kemia, Saikolojia na literature. Maisha yake yalikuwa ya kawaida sana kwa jinsi anavyojulikana.

Ingawa anaonekana kuwa na msimamo wa kihafidhina, kuna nyakati amenukuliwa akisema matumizi ya kondom ni muhimu hasa katika kuzuia maambukizo. Hili limewatia kiwewe wahafidhina wa kweli kwa kudhani mbele ya safari yanaweza kutokea mabadiliko yasiyotarajiwa.

Kazi kubwa anayokabiliana nayo ni kurudisha heshima kutokana na kashfa zinazolikumba kanisa kila uchao.
Kazi nyingine ni kurudisha imani kwa wafuasi wa kanisa Ulaya na kulijenga upya bila kuathiri nguvu ya kanisa ilipo ambayo ipo Latin America na Afrika.

Pamoja na ukweli kuwa historia imebadilika kwa kuwa na papa kutoka nje ya uerope lakini ukweli kuwa ana asili ya Europe na hasa Italia haupaswi kufumbiwa macho. Kwamba ndani ya Vatican bado kuna uhafidhina hata kama si wa dhahiri.


KUUMIZWA KIBANDA
Katika tukio jingine mwandishi wa habari A.Kibanda alishambuliwa na watu wasiojulikana na kuumizwa vibaya.
Kibanda yupo Afrika kusini kwa matibabu na hali yake inasemwa kuimarika licha ya kupoteza viungo vya mwili wake.

Tukio hili si la kwanza, ni mtitiriko wa matukio yanayoonyesha uwepo wa ombwe kubwa la ulinzi na usalama wa wananchi hasa wale wanaojulikana kwa kazi zao.

Ni tukio linalotisha kwasababu limefanywa katika mtindo ule ule uliotumika kumuumiza Dr Ulimboka.

Kwa hali ilivyo ni matukio yanayoonekana kuwa yameandaliwa na kuratibiwa kwa utaalam na wala si matukio ya uhalifu mwingine unaojulikana.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida makamu wa rais alimtembelea mwandishi huyu akiwa hospitali ya Muhimbili.
Kwanini viongozi wa serikali wamepata ''knee jerk reaction'' hilo ni swali la kujiuliza sana.

Tunakumbuka mwandishi Saed Kubenea alivyovamiwa na kuumizwa kwa tindikali.
Hadi leo hakuna anayetajwa kuhusika au kufikishwa katika vyombo husika.

Hata pale kubenea alipotaka kutaja sababu za shambulizi lake, jitihada zilifanyika kukamata watu ambao imebainika wala hawakuhusika.

Katika tukio lililomhusu Dr Ulimboka, nalo pia limebaki kitendawili huku raia asiyeonyeshwa kutoka Kenya akihusishwa na tukio hilo. Hata pale wahusika wengine walipotaja majina muhimu ya kufanyiwa kazi kama alivyofanya mchangaji Kwajima,na mhusika Dr Ulimboka hatua hazijachulkuliwa dhidi ya watuhumiwa au kukanushwa na Polisi

Tukio lililofuata lilikuwa la kuuwawa kwa Mwangosi. Hili lilileta utata hadi waziri wa mambo ya ndani akipinga na IGP hadharani. Haraka ikaundwa tume kuchunguza, tume iliyokuja na matokeo ya kuchekesha, kukejeliwa na kudharauliwa.

Ghafla akakamatwa askari aliyefyatua risasi na kufikishwa mahakamani hata kama ni wazi kuwa walikuwepo zaidi ya sita katika shambulizi lile.

Katika tukio la wiki hii kuna mwanasiasa amehusishwa na kuhojiwa na Polisi.

Pamoja na kutoa nafasi kwa uchunguzi lazima tukiri kuwa jeshi letu la polisi lina tatizo.
Tatizo ni kubwa kiasi cha kuonekana kutokuwa na professional ''utaalama'' au kufuata maadili ya kazi ''professional ethics'' au kuwa na mkakati wa kuzuia matukio haya ya kimkakati yanayoonekana kuwa fashion katika nchi inayojifaragua kuwa ya amani na utulivu.

Kwakweli kuna kila sababu serikali kualika wataalamu wa nje kwasababu hawa wa kwetu kiwango chao ni cha hatari sana.

Kwanini tunasema kuna tatizo Polisi?

Inaendelea.....
 
Inaendelea...kutoka post 150.

Tuna tatizo katika jeshi kwasababu hicho ndicho chombo kinachosimamia usalama wa raia na mali zao bila kujali itaikadi za aina yoyoye. Jeshi halitakiwi lifungamane na siasa, dini au chochote kiwacho.

Katika nchi za wenzetu Polisi ni chombo huru na kinaweza kufanya uchunguzi kwa raia yoyote na kwa wakati wowote.
Kwa bahati mbaya sana na ya kusikitisha jeshi la Polisi limekosa utaalam, watalaam na kutumikakisiasa zaidi.

Tutoe mifano kadha wa kadha kudhihirisha kile tunachokisema.

1.(a) Jeshi letu halina wataalam: Kwamba kumetokea ajali na mchunguzi ni Polisi asiyejua sheria za barabarani, hawezi kutofautisha kati ya tyre na regetor. Huyu ndiye tunategemea atupe uchunguzi wa kitaalamu!!

(b)Jeshi halina wataalam wa uchunguzi (Forensic).
Matokeo yake ni kufanya uchunguzi kwa hisia na kuacha vithibitisho ambavyo vingeweza kuwa ushahidi wa kutosha.
Hivi uchunguzi wa kifo unafanyikaje bila kukusanya vithibitisho kama alama za mwili (DNA) za mavasi n.k.?

(c)Jeshi halina wataalam wa Teknohama:
Kwamba uhalifu sasa hivi unatumia teknoloji, je kuna wataalam wangapi wa vyombo vya elektoniki kama computer katika jeshi letu na je wana vifaa na wanatumika kama ipasavyo?

(d) Jeshi la Polisi haliwatumii wataalam kama wa sheria katika kazi zake.
Limewekeza katika nguvu na silaha zaidi ya matumizi ya akili, weledi na ufahamu.
Matokeo ya haya ni jeshi kushindwa kufanya maamuzi muhimu na kwa wakati kwasababu halizingatii sheria.

Hii ni sehemu ndogo sana ya mapungufu ya jeshi letu kiutaalamu na wataalam.
Orodha ni ndefu na hviyo kulifanya jeshi lionekane kama mkusanyiko wa watu wenye unifomu na si wataalam

KISIASA:
Jeshi limekuwa mstari wa mbele kupambana na wanasiasa hasa wasio wa chama tawala.
Matokeo ya haya ni kuwa na viwango tofauti katika kusimamia sheria zinazotoa haki kwa raia.

Ni kwasababu ya mapungufu makubwa ndani ya jeshi mambo yafuatyo yamekuwa yakijitokeza

(a) Polisi wameshindwa kufanya uchunguzi wa uhalifu.Kwa vile hawana utaalamu wa kutosha mara nyingi taarifa zao zimekuwa zikichanganya kama habari ya Marehemu Mwangosi ilivyolichanganya jeshi.

Msemaji wa Polisi anakuja na taarifa inayokinzana na mkuu wa jeshi, kamanda wa mkoa au kanda n.k.

Kwa mapungufu hayo jeshi linajikuata likitegemea
(i) kuundwa kwa tume ambazo kisheria hazina nguvu za kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria.
Wakati tume zinaundwa jeshi linakuwa limemaliza kazi kama kwamba taarifa ya tume ndiyo taarifa ya kitaalamu ya jeshi.

(ii) Watuhumiwa wamekuwa wanafikishwa mahakamani na kushinda kesi kwasababu tu jeshi si makini na wengi wao ni mbuzi wa kafara zinazohusiana na mambo ya kisiasa

(b) Jeshi kutumia mbinu za zimamoto kutafuta suluhisho la kisiasa na si la tatizo la uhalifu

(i)kukamata watuhumiwa ili kesi iende mahakamani na isizungumwe tena.
Hili limetokea kama tulivyoona hapo awali kwa matukio yaliyowahusu Ulimboka, Kubenea, Mwangosi na hata hili la sasa.

Katika watu wote waliokamatwa hakuna aliyehukumiwa kwasababu moja tu kuwa hakukuwa na ushahidi kwa vile watuhumiwa ni wa kusingiziwa.

(iii)kutumia habari za magazetini na mitandanoni kukamata watu bila tafakuri, ushahidi au kielelezo.

Leo kuna mwanasiasa kakamatwa kisa ni video ya mtandaoni.
Inawezekana tukio hilo ni la kweli au la!

Jeshi lilitakiwa kwanza lijiridhishe kuwa teknoloji iliyotumika ni ya kweli na kwamba hakuna uchakachuaji kwa vitu kama picha za teknolojia na sauti.

Halafu walipaswa wamfuatilie mtuhumiwa na kama wanaridhika na ushahidi uliopo ndipo wamkamate.
Hili lingesaidia mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria na muda stahiki.

Inashangaza mtu anakamtwa na kukaa mahabusu kwa siku tano bila kutokea mbele ya mahakama.
Jambo hili ni ukiukwaji mkubwa wa haki za raia unaotokana na kukosa maadili ya kazi na wataalam husika ndani ya jeshi.

Pamoja na hayo, tutajiuliza hivi ni kwanini jeshi la Polisi lichague matukio mengine yakiwa hayana ushahidi na kuyafanyia kazi kwa nguvu huku ikipuuza habari nyingine muhimu sana zinazolihusu taifa?

Mathalan,
(i) spika wa bunge wakati huo mh Samwel Sita aliwahi kusema na kuomba ulinzi kwa habari za ajali ya kupangwa iliyokuwa imtokee. Jeshi halikuwahi kufanya uchunguzi na suala hilo limekufa daima dawamu.

(ii) Dr W.Salaa alishawahi kusema amewekewa vinasa sauti chumbani na ameripoti tukio hilo.
Hadi leo hakuna chochote kilichofanyika

(iii) Kesi ya kubenea ndio imekwisha jeshi likiwa halina habari nani walihusika na kwanini.

(iv) Kibanda na Bashe walitoa taarifa tena hadi kwa waziri wa mambo ya ndani kuhusu usalama wao. Jeshi halikuchukua hatua hadi leo tunaona lifanyia kazi habari za you tube kwa nguvu ya ajabu

(v)Wizi unaosemwa kila siku katika mashirika na hata ndani ya serikali, jeshi limekaa kando likisubiri taarifa za tume.

(vi) Uhasama wa wafanyibiashara maarufu umewekwa kapuni kwasababu tu jeshi halijui wala haliwezi kushughulikia high profile kesi kama hizo.

Orodha inaendelea. Sasa kwa mwendo huo ambao wananchi wanaita sinema za Kova nani ataamini tena jeshi la Polisi hata kama kweli kuna tukio lenye ushahidi?

(v)Kesi ya Ulimboka imebaki kupigwa dana dana. Sasa kama Polisi walikuwa hawajakamilisha uchunguzi, ni kwanini walimkamata raia wa Kenya? Tunafahamu kuwa raia yule alikamatwa kama kweli yupo kwa kisingizio cha kuzuia vyombo vya habari na vya jamii visiandike au kulizungumzia.

Hali ndiyo hiyo kwa Kubenea, Ulimboka na wengine wengi tu.
Kazi ya jeshi si kukakamta tu na kupeleka mahusbusu raia. Kwa nchi za wenzetu uzembe na ujuha wa jeshi letu, serikali ingeshafilisika. Kumkamata mtu lazima kuwepo na ushahidi wa kutosha na wa kuridhisha kuwa uhalifu umefanyika.
Siyo suala la kuvaa unifomu, kubeba kitambulisho na kwenda kusweka watu mahabusu.

Huu ni utendaji kazi za zama za ujima na katika dunia ya leo hauna nafasi achilia mbali kuwa ni dhalili.

Kwa vile hakuna imani tena na jeshi sasa ni wazi tunaishi kwa sheria za mwituni ''rule of the jungle'' kwamba mwenye ubavu atapata na asiye atabaki kuwa kitoweo cha wenzake.

Hiki ndicho kinapelekea hili jeshi kuonekana kama mkusanyiko wa watu na wala si watu wenye taaluma.
Hakuna njia ya kurudisha imani katika jeshi la Polisi isipokuwa kulivunja na kulisuka upya.

Jeshi lisukwe upya kwasababu ndani ya jeshi lenyewe, rushwa, siasa na uzembe vimekuwa sehemu ya utendaji kazi wake. Kama Polisi 100 wanaajiriwa kwa rushwa sijui nani aliyebaki kukamata rushwa.

Kwanini suala la Kibanda lina utata sana? itaendelea.....
 
KWANINI SUALA LA KIBANDA LINA UTATA

...Inaendelea
Utata wa suala hili ni jinsi lilivyotokea na kupokelewa.
Hakika kwa mwenye utu hili ni tukio lililokusudiwa kutoa roho ya Mwanadamu na sote twapaswa kuwa na uchungu wa kibinadamu.

Bila kujali mitafaruku na maadui wanaomzunguka Kibanda hakuna namna yoyote tukio hili linaweza kupewa uhalali hata kwa bahati mbaya.

Ni haki na matakwa ya kila raia wa nchi kuona wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

Tukio hili linaonekana kupoteza mkondo wake na kuchukuliwa kisiasa zaidi ya kibinadamu.
Jeshi la Polisi nalo halionekani kukaa mbali na mayowe ya wanasiasa na kujikuta likiingia kichwa kichwa katika mtafaruku.

Jeshi limemkamata kiongozi wa chama cha CDM ndg Lwakatare kufuatia video iliyowekwa katika mtandao wa you tube.
Kabla ya hapo kiongozi wa CCM ndg Nchemba alikaririwa akisema anao mkanda unaoonyesha mipango ya uhalifu.

Polisi hawakuanza na yule mwenye mkanda hadi pale walipopata video ya you tube.
Hatuwezi kusema tukio lilikuwepo au la, tunachosema hapa ni kuwa watu muhimu hawakufuatiliwa kutoa ushuhuda hadi ilipoonekana jina la kiongozi wa CDM.

Katika mazingira ya utaalam, jeshi lilipaswa kwanza kukusanya ushahidi na kuufanyia kazi kabla ya kukurupuka kukamata mtu. Pengine jeshi lilifanya hayo kwa maagizo ya wanasiasa na hilo tu linatosha kusema ile maana ya professional imeshapotea.

Ningefarijika kama jeshi kwanza lingeendesha uchunguzi kwa kumhusisha Kibanda.
Tukio hili laweza kuwa la kisiasa au la kijamii na hivyo Kibanda ni mtu muhimu sana katika kusaidia uchunguzi.

Kilichofanywa na jeshi ni kutaka kujenga dhana kuwa ile video ni mali ya CDM na kwamba mipango ile ni ya chama.
Kuna uwezekano ikawa ya CDM, au ya Lwakatare mwenyewe bila kuhusisha CDM au kutokuwa na uhusiano wowote na CDM kabisa.

Ikumbukwe kuwa Kibanda alihama kutoka katika chombo kimoja cha habari kinachomilikiwa na kiongozi wa CDM.
Chombo hicho si mali ya CDM kama inavyoaminishwa.

Huenda kukawa kuna mzozo kati ya waajiri na wafanyakazi wa pande zote mbili na hilo linabaki kuwa suala la uchunguzi. Kuna tetesi kuwa kuhamia chombo anachokifanyia kazi kumeleta sintofaham miongoni mwa wafanyakazi.

Kuna habari kuwa kutokana na umahiri wa Kibanda kujenga hoja, inawezekana kukawa na wanasiasa mahasimu ambao wangependa kupata coverage au kutotupiwa madongo hasa wakati huu wa mbio za uchaguzi kuelekea 2015.

Ninachokusudia kukisema ni kuwa kuna utata wa mambo mengi yaliyoingiliana ambao jeshi la Polisi linahitaji busara kubwa vinginevyo litazidi kujivunjia hadhi na heshima kidogo iliyobaki.

Tunakumbuka jinsi suala la Ulimboka lilivyoivua nguo serikali na jeshi.
Leo kuna msemo maarufu mitaani wa sinema ya kova. Hili si jambo la kufurahisha hata kidogo.
Kwamba jeshi linaonekana kuwa mtambo wa kuchonga na kutunga uongo badala ya kuwa sehemu ya kusimamia ukweli.

Hata kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya kile jeshi linachokusudia kwa manufaa ya wanasiasa hasa wa chama tawala, itakuwa ni jambo gumu sana umma kukubaliana na uchunguzi huo.
Kwanza, harakati za kufuatilia jambo hili zina kasi ya ajabu sana hadi kuacha sehemu muhimu sana za uchunguzi.

Pili, kuna maswali ambayo jeshi la Polisi halina majibu hadi sasa.
Hadi hapo majibu yatakapopatikana kila kifanywacho na jeshi letu ni ze comedy kwa uelewa wa raia wengi waliopoteza imani na matumaini na jeshi hili.

Watu wanajiuliza, ikiwa Dr Mwakyembe aliwahi kufikisha ushahidi wa maandishi katika mpangilio wa muda ''real time'' na kuwataja wahusika na majukumu yao katika njama za kumuua kule Morogoro na hadi leo hakuna kilichofanyika, ni kwa vipi mtu aamini mkanda wa you tube?

Lakini hili haliishi kwa jeshi la Polisi, kuna usalama wa taifa nao.
Inapofikia mahali wahalifu wametengeneza mtandao wa kufanya ukatili na hakuna anayeweza kutengua kitendawili hicho basi lipo tatizo kubwa la usalama wa nchi.

Na wala haishii hapo, nchi inapoonekana kuwa na tatizo la kiusalama, mwenye jukumu hilo ni kiongozi wa nchi kwani yeye ndiye anayeteua wasidizi wake katika maeneo hayo muhimu bila kuhusisha chombo chochote.
Kwa mintaarafu hiyo wazungu wanasema ''the buck stops with him/her'' na hapa ni Rais wa JMT.

Tatizo linaloonekana haraka haraka ni kuwa kiongozi wa nchi ameshindwa nguvu na kundi la wahalifu kiasi kwamba yeye na kundi lake la usalama wa taifa linalohusisha viongozi wa sehemu nyeti hawaelewi nini kinatokea au kwanini na kutokea wapi. Hapa ndipo tatizo linapokuwa kubwa zaidi.

Lakini pia inawezekana wanajua nini kinaendelea na hivyo hawawezi kuchukua hatua kwa mtu au kikundi chochote kile kwavile watu hao watakuwa wamefanyia kazi maagizo waliyopewa.

Hapa tulipofika ni mahali pa kutisha na pana hitaji akili na fikra zetu sote.
Sijui nani ni salama miongoni mwetu

Tusemezane.
 
Tatizo letu Wanaafrika wa Tanzania, tumeruhusu tamaduni BATILI kwetu, zinazosababisha hata vyombo vya dola kutumika na wanasiasa au makundi ya watu fulani hata mtu mmoja mmoja kulinda maslahi yao, na si ya UMMA. Hili ni JANGA.
Leo vyama vya siasa vina nguvu juu ya vyombo vyetu vya dola kuliko UMMA. Je, havijatumika bado kulinda political interest zao hata kuua watu? Watu wanahonga kupata kazi usalama wa taifa, undugu unawapa kazi usalama wa taifa, urafiki, kujuana, ngono, chuki, umakundi, n.k. Ndio maana leo mtu haoni tabu kujinasibu kuwa watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake. Ni kinajengeka hapa? Je, watumishi hao hawakupaswa kuwa watiifu kwa umma tu kupitia serikali yao halali? Labda imetokana na serikali kusaliti raia wake kutoona haja tena ya kuripoti kwa WASALITI NA WANAFIKI! Au ndio hao waliopachikwa kwa vigezo batili, hivyo ni rahisi kurubunika na kuihasi serikali yao. Au kila kundi lilitumia mwanya huo kupandikiza watu wake. Lakini, yote hayo kwetu hayaondoi ukweli kuwa, vyombo vya dola vinapofanya kazi kwa MAHABA ya kikundi fulani cha watu nje ya serikali, basi raia wa kawaida ndio wanaoumia. Ndicho kilichowakuta kina Mwangosi, Kibanda, n.k. Ushahidi wa kuhusika kwa watumishi wa vyombo vya dola u wazi. Swali; Kwa vile makundi ya kisiasa yamegawana milki ya watumishi wetu wa vyombo vya dola, je wahusika hao katika matukio ripotiwa ni watiifu kwa kundi gani? Je, ni la watawala(CCM) au wapinzani(CDM)? Je, ni la Lowasa, Sitta au Membe? Je, ni la Zitto, Slaa, Mbowe au Masalia? Wapumbavu wanachezea uhai wetu kwa maslahi yao binafsi. WANAFIKI! Damu yetu i tayari kumwagika, lakini si kwa maslahi ya wapumbavu wachache...ILA UMMA wa mwanaafrika wa Tanzania. Walivyo wanafiki, ni hao hao waliogawanyika hivyo, ndio waliopewa dhama na kupeleleza matukio yao wenyewe. Kila mtu atamlinda yule anayemtii. Yatapita-Yatafunikwa. Nasi kila siku tutakuwa midoli ya wao kuwa wanajifundishia shabaha ya vitu vyenye ncha kali. Keshokutwa watatushindisha juani na nyimbo za ukombozi, maisha bora, nasi tutaimba na madonda yetu mabichi ya akina Mwangosi, jioni tutarudi kwenye viota vyetu, wenyewe wakijivinjari kwenye kumbi za starehe, building the Nation in different ways, NEVER HAPPEN.
UKOMBOZI NI HESABU. MAISHA BORA NI HESABU. MAENDELEO NI HESABU. Hata tafsiri ya maendeleo, hujui unanakirishwa tenzi za Maendeleo. Mwishoni unaambiwa msongamano wa magari ni ishara ya maendeleo. Na TUJILAUMU WENYEWE.
Chakusitisha, HATUONESHI KAMA TUNA HAJA YA KUONDOKANA NA HAYA. Inauma sana!
Mungu wetu anaita sasa. AMKA MWANA wa AFRIKA. ITIKA SASA.
 
Tatizo letu Wanaafrika wa Tanzania, tumeruhusu tamaduni BATILI kwetu, zinazosababisha hata vyombo vya dola kutumika na wanasiasa au makundi ya watu fulani hata mtu mmoja mmoja kulinda maslahi yao, na si ya UMMA. Hili ni JANGA.
Leo vyama vya siasa vina nguvu juu ya vyombo vyetu vya dola kuliko UMMA. Je, havijatumika bado kulinda political interest zao hata kuua watu? Watu wanahonga kupata kazi usalama wa taifa, undugu unawapa kazi usalama wa taifa, urafiki, kujuana, ngono, chuki, umakundi, n.k. Ndio maana leo mtu haoni tabu kujinasibu kuwa watumishi wa vyombo vya dola wanaripoti kwake. Ni kinajengeka hapa? Je, watumishi hao hawakupaswa kuwa watiifu kwa umma tu kupitia serikali yao halali? Labda imetokana na serikali kusaliti raia wake kutoona haja tena ya kuripoti kwa WASALITI NA WANAFIKI! Au ndio hao waliopachikwa kwa vigezo batili, hivyo ni rahisi kurubunika na kuihasi serikali yao. Au kila kundi lilitumia mwanya huo kupandikiza watu wake. Lakini, yote hayo kwetu hayaondoi ukweli kuwa, vyombo vya dola vinapofanya kazi kwa MAHABA ya kikundi fulani cha watu nje ya serikali, basi raia wa kawaida ndio wanaoumia. Ndicho kilichowakuta kina Mwangosi, Kibanda, n.k. Ushahidi wa kuhusika kwa watumishi wa vyombo vya dola u wazi. Swali; Kwa vile makundi ya kisiasa yamegawana milki ya watumishi wetu wa vyombo vya dola, je wahusika hao katika matukio ripotiwa ni watiifu kwa kundi gani? Je, ni la watawala(CCM) au wapinzani(CDM)? Je, ni la Lowasa, Sitta au Membe? Je, ni la Zitto, Slaa, Mbowe au Masalia? Wapumbavu wanachezea uhai wetu kwa maslahi yao binafsi. WANAFIKI! Damu yetu i tayari kumwagika, lakini si kwa maslahi ya wapumbavu wachache...ILA UMMA wa mwanaafrika wa Tanzania. Walivyo wanafiki, ni hao hao waliogawanyika hivyo, ndio waliopewa dhama na kupeleleza matukio yao wenyewe. Kila mtu atamlinda yule anayemtii. Yatapita-Yatafunikwa. Nasi kila siku tutakuwa midoli ya wao kuwa wanajifundishia shabaha ya vitu vyenye ncha kali. Keshokutwa watatushindisha juani na nyimbo za ukombozi, maisha bora, nasi tutaimba na madonda yetu mabichi ya akina Mwangosi, jioni tutarudi kwenye viota vyetu, wenyewe wakijivinjari kwenye kumbi za starehe, building the Nation in different ways, NEVER HAPPEN.
UKOMBOZI NI HESABU. MAISHA BORA NI HESABU. MAENDELEO NI HESABU. Hata tafsiri ya maendeleo, hujui unanakirishwa tenzi za Maendeleo. Mwishoni unaambiwa msongamano wa magari ni ishara ya maendeleo. Na TUJILAUMU WENYEWE.
Chakusitisha, HATUONESHI KAMA TUNA HAJA YA KUONDOKANA NA HAYA. Inauma sana!
Mungu wetu anaita sasa. AMKA MWANA wa AFRIKA. ITIKA SASA.
Jinga la falsafa, hakika kuna kitu umekigusa muhimu sana. Ni kweli kuwa vyombo vya usalama vimeacha jukumu lao la awali na kuwa watumishi wa wanasiasa.

Hili halina ubishi kwasababu ukiangalia mambo na matukio haionyeshi kama kuna usalama wa taifa kwa maana ile iliyokuwepo au iliyokusudiwa.

Haiwezekani mauaji yanatokea na mambo yanaonekana kuwa 'tambarare'' kama wasemavyo.
Kuna kashfa ya jeshi la polisi kupokea watu 300 kujiunga na mafunzo CCP Moshi.
Watu hao walipokelewa kwa hadhi zote kama Polisi wanafunzi na hakuna aliyejua nini kimetokea.

Kwamba rushwa imeendeshwa huko mikoani kwenye mafisa usalama na RPC bila kujulikana.
Ndani ya jeshi hakuna aliyejua nani anaratibu shughuli.

Ndani ya chuo cha kijeshi CCP moshi hakuna aliyeshughulisha akili kufahamu endapo walioripoti tena kwa kuletwa na mabasi walikuwa wanafunzi halali na kwamba usalama wa chuo ulikuwa madhubuti.

Kwa utaratibu huo tutegemee kupata askari mwenye uwezo na weledi achilia mbali mapenzi ya kazi yake kweli!
Kwamba, askari ametokana na mfumo wa rushwa halafu yeye aje asimamie vita dhidi ya rushwa.

Lakini usalama wa taifa walitakiwa wahoji kwa undani nini kimetokea hadi ilipofikia na wahusika walitakiwa wachukuliwe hatua za kijeshi kwa kuhatarisha usalama wa jeshi ab initio.Hakuna! na imebaki utaratibu ule ule wa ''huo ni upepo utapita''.

Zama hizo kupata kazi usalama wa taifa ilikuwa suala nyeti na watu hawakujua nani yupo wapi na anafanya mafunzo gani.
Nina kumbu kumbu ya jamaa yetu aiyewahi kukimbia na kujificha kama mwaka mmoja. Sababu kubwa ilikuwa kufuatwa na watu wa usalama akajiunge nao. Kitu kilichomshangaza ni kuwa jamaa walikuja wakiwa na full data zake bila kuacha kitu.
Jamaa akala kona kujificha akijua ni zaidi ya kazi!

Nadhani wale mliokuwa katika majeshi miaka hiyo (JKT) ikiwa kweli JKT, kulikuwa na watu wanapita kutafuta vijana wa kujiunga na usalama wa taifa. Nakumbuka kuwa hawa jamaa walikuwa na data na ni wazi walifanya home work zao kwanza.

Sijui nini kimebadilika siku hizi kazi hiyo imekuwa lulu kwamba hupati mpati krosi.
Ok! lakini basi kuna vetting ya watu?Kutokana na mwingiliano wa mataifa ipo siku mtu wa nchi jirani atakabidhiwa taarifa za serikali ya Tanzania tukiamini huyo ni Mtanzania.

Haiwezekani kukawa na mauji na mateso kirahisi rahisi na taifa halijui nani anafanya uharamia huu.
Tumeweka orodha ndefu ya matukio mengine yakiwa na taarifa zenye majina na watu, hakuna anayeshtuka wala kufanyia follow up!

Sidhani kama kuna njia nyepesi ya matukio haya kutohusishwa na serikali hata kama haiuhusiki.
Kuhusishwa kunatokana na ukweli kuwa hata panapotolewa taarifa, kuna njama za makusudi za kufunika taarifa hizo.

Hussen Bashe na mwenzake Kibanda walifuatiliwa na Polisi na walitoa taarifa Polisi na kwa waziri wa mmbo ya ndani.
Si waziri mwenye dhamana, mkuu wa jeshi la Polisi, mkuu wa usalama au yoyote mwenye dhamana aliyechukua hatua uchunguzi.

Leo kuna kuhaha kwa Polisi kutafuta ushahidi wa video, kwenda kupekua ofisi za CDM n.k.
Hatujui uhakiki wa video ya you tube, lakini swali kubwa ni kuwa kwanini Polisi hawakuhaha kutafuta waliokuwa wanamfuatilia Kibanda na Bashe kwanza?

Kinachofanywa hapa ni political score point, kwamba wanahusisha CDM na uhalifu.
Kitu ambacho jeshi pengine na usalama wa taifa hawakifahamu ni kuwa the more they politicize the issue ndivyo wanajichangaya.

Kwanza wawalisiliane nakupata maelezo ya Kibanda halafu wafanye scientific investigation.
Pili, maswali yafutayo yanawasubiri wakati wakiendelea na harakati za kisiasa.

1. Dr Mwkayembe alitoa taarifa na kutaja watu na magari yaliyohusika katika ajali iliyokuwa imepangwa.
Je, jeshi limefuatilia na kupata majibu gani katika kesi hii isiyohitaji ramli isipokuwa Mwakyembe mwenye ushahidi wake unaojitosheleza?

2. Sitta akiwa Spika alinusurika ajali ya kupangwa kama alivyo dai. Je, jeshi lilifanya uchunguzi na kubaini nani au chama gani kimehusika?

3. Kubenea alimwagiwa tindikali, jeshi limefanya uchunguzi na kubaini ni nani au chama gani?

4. Dr Slaa aliwahi kudai kuwekewa vinasa sauti na watu wa serikali. Je, jeshi limewahi kufanya uchunguzi na kupata matokeo gani?

Suala la Kibanda kama yalivyo mengine yanahitaji majibu thabiti kama serikali inataka kunawa mikono.
Vinginevyo jitihada za kulifanya hili jambo kuwa la kisiasa linazidi kuimarisha zile tuhuma zinazoiandama serikali.

Tutaona na kusikia mengi kwasababu kuna wakati uongo ukikithiri basi ukweli hujitokeza wala hautafutwi.
Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu amekanusha habari za Ikulu kuhusika!!

kinachomtoa kuja kutoa taarifa ni yale mawasiliano ya ndugu Michuzi yaliyonaswa.Tunaambiwa Michuzi alikuwa anawasiliana na wenzake wa Ikulu!!!

Kama ilivyo video ya you tube nadhani Michuzi naye angekuwa sehemu muhimu sana ya uchunguzi huu.
 
Mkuu Nguruvi3, thanks for all this, please keep up the good job. Kwenye hili la Rwakatare, angalau Chadema wameanza kuifanyia kazi ile hoja yako ya damage control kwa kuibuka promptly on time, yaani they did "the right thing!", japo sina uhakika if "they did it right!".

La Kibanda, ile movement toka kwa Mbowe kwenda kwa King Maker, imeogopesha sana ila sio Chadema, bali CCM!, tukubali tukatae, RA ni master planner, hivyo kuna watu wali foresee kuundwa kwa timu ya mtandao mpya, kama ule wa Salva na Muhingo. Muoga numberi moja ni yule aliyetangaza hadharani maadui 11 wakiwemo waandishi wawili!. Hata baada ya kuitoa ele ile, polisi haikufuatilia!, whay if kwenye hao waandishi wawili, Kibanda yumo?. Ila pia kitendo cha Kibanda kwenda huko its like defection!. Kama ni kweli ile video ilikuwa ni ya kumshughulikia mwandishi wa Mwananchi kwa ajili tuu ni best wa ZZK, then why not wasimshughulikie defector?!. Ile Ulimboka style ni kupoteza tuu maboya kwa kufanya "look alike ili watu wadhanie ni watu wale wale wa Ulimboka!.

Tusubiri kesho tusikie nini kitakachoendelea.

Pasco.
 
Mkuu Nguruvi3, thanks for all this, please keep up the good job. Kwenye hili la Rwakatare, angalau Chadema wameanza kuifanyia kazi ile hoja yako ya damage control kwa kuibuka promptly on time, yaani they did "the right thing!", japo sina uhakika if "they did it right!".

La Kibanda, ile movement toka kwa Mbowe kwenda kwa King Maker, imeogopesha sana ila sio Chadema, bali CCM!, tukubali tukatae, RA ni master planner, hivyo kuna watu wali foresee kuundwa kwa timu ya mtandao mpya, kama ule wa Salva na Muhingo. Muoga numberi moja ni yule aliyetangaza hadharani maadui 11 wakiwemo waandishi wawili!. Hata baada ya kuitoa ele ile, polisi haikufuatilia!, whay if kwenye hao waandishi wawili, Kibanda yumo?. Ila pia kitendo cha Kibanda kwenda huko its like defection!. Kama ni kweli ile video ilikuwa ni ya kumshughulikia mwandishi wa Mwananchi kwa ajili tuu ni best wa ZZK, then why not wasimshughulikie defector?!. Ile Ulimboka style ni kupoteza tuu maboya kwa kufanya "look alike ili watu wadhanie ni watu wale wale wa Ulimboka!.

Tusubiri kesho tusikie nini kitakachoendelea.

Pasco.
Mkuu Pasco, nadhani umekuja mahali tunapofikiria wengi kuwa lipo tatizo.
Utakumbuka kuwa Mwanahalisi ndilo gazeti lililotoa mwanga sana kuhusu Richmond likiweka cheque number, zilipotoka na zilipoingilia. Kwa ufupi ndilo gazeti lililozama na EL na washirika wake. Kilichompata Kubenea tunakikumbuka.

Kubenea alikaaa India bila jeshi la Polisi kusema lolote. Siku mbili kabla hajarudi alisema atakaporudi atakutana na waandishi kuwaelezea nini kilitokea. Kilichofuata ni vibaka wawili kukamatwa na kufikikishwa mahakamani.
Hapo tukafungwa midomo kwasababu suala hilo lipo mhakaamani.

Kinachotokea kwa Lwakatare nadhani ni mbinu zile zile za kutaka umma unyamaze.
Kwa taratibu ni kuwa mtuhumiwa akikamatwa anatakiwa ndani ya muda fulani afike mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka. Lwakatare amekamatwa siku za kazi na hadi leo hajafikishwa mahakamani.

Kitakachotokea ni kufikishwa mahakamani halafu tutaambiwa uchunguzi haujakamilika.
Hii ni style ya stone age katika mambo ya ulinzi na uchunguzi.
Katika nchi za wenzetu Lwakatare hadi sasa alipaswa apewe compensation.
Katika nchi yetu sheria zipo lakini kwabahati mbaya tumeridhika kuwa ndivyo ilivyo.

Unapomkamata mtu tayari kuna ushahidi wa kutosha, iweje akamatwe tu kwasbabu ya video ya you tube?
Inawezekana ni kweli lakini tukubali kuwa utaratibu unaotumika ni ule wa ushabiki na wala si utaalamu.

Ni ushabiki kwasababu video ngapi ikiwemo ya Ilunga zimekaa mitandaoni bila Polisi kuwa na habari za kuwakamata wahusika?
Na kwa kutambua kuwa Lwakatare ni mtu maarufu Polisi walishindwaje kumfuatilia taratibu hadi wakawa na ushahidi wa kutosha! Nasema ushahidi wa kutosha kwasababu kesho utasikia uchunguzi haujakamilika. Third world!

Kuhusu king make na planner, ndiyo maana nimesema Polisi wamekurupuka.
Hili suala ni very complicated.
Wanapotaka kuihusisha CDM nadhani tutaishia katika filamu nyingine ya kova.

Ndani ya CCM kuna mtifuano na kujipanga kwa hali ya juu.
Kuna makundi hasimu makubwa mawili. Kundi la king maker, former speaker na lile la Foreign affairs.
Kwa kuelewa umuhimu wa vyombo vya habari kuna uwezekano hili likawa ni ''family feud''.
Au pia inawezekana kukawa na competition ya waajiri kwa lengo la 2015.

Mtu anayeweza kutoa hints na thorough analysis ni Kibanda.
Yeye ni victim na anaweza kuwa na watu anaowafahamu katika sakata zima.
Kwanini Polisi hawafanyi uchunguzi kwake wanakimbilia video kama ndio kitu muhimu sana!

Ni kosa lile lile la kumkamata Mkenya halafu Ulimboka anakuja na jina halisi. Polisi wanabaki kuhaha bila kujua nini wafanye.
Tutaendelea kuwa na jeshi la ujima namna hii hadi lini? Karne ya 21 bado tunatumia mbinu za enzi za mawe!!

Hivi Kibanda na akina Bashe waliotoa taarifa za kufuatiliwa na Polisi wakija na ushahidi mwingine tofauti na video, serikali itabaki na nini?

Kwamba hata video ikiwa authenticated, Lwakatare atashitakiwa kwa uchochezi na kama ni hivyo na kwa mujibu wa nyuzi yako ya jana haionekani kama tunasheria za electronics, serikali itatuambia nini kuhusu Kibanda.

Hadi hapo kitendawili cha Kibanda kitakuwa hakijatenguliwa na serikali itakuwa imebeba dhamana yote bila chembe ya wasi wasi.

Polisi walitakiwa wafahamu kuwa suala la Kibanda ni very sensitive and complicated kutokana na historia ya matukio yaliyotangulia. Linahitaji political and social factors ziangaliwe kwanza kabla ya kulihusisha na CDM au mtu mwingine.

Taifa lipo katika hatari kubwa sana inapofikia mahali vyombo vya usalama vinakuwa sehemu ya waamuzi na washabiki.

Tumefikaje hapa, hilo ndilo swali la leo.
 
Mkuu Pasco, nadhani umekuja mahali tunapofikiria wengi kuwa lipo tatizo.
Utakumbuka kuwa Mwanahalisi ndilo gazeti lililotoa mwanga sana kuhusu Richmond likiweka cheque number, zilipotoka na zilipoingilia. Kwa ufupi ndilo gazeti lililozama na EL na washirika wake. Kilichompata Kubenea tunakikumbuka.

Kubenea alikaaa India bila jeshi la Polisi kusema lolote. Siku mbili kabla hajarudi alisema atakaporudi atakutana na waandishi kuwaelezea nini kilitokea. Kilichofuata ni vibaka wawili kukamatwa na kufikikishwa mahakamani.
Hapo tukafungwa midomo kwasababu suala hilo lipo mhakaamani.

Kinachotokea kwa Lwakatare nadhani ni mbinu zile zile za kutaka umma unyamaze.
Kwa taratibu ni kuwa mtuhumiwa akikamatwa anatakiwa ndani ya muda fulani afike mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka. Lwakatare amekamatwa siku za kazi na hadi leo hajafikishwa mahakamani.

Kitakachotokea ni kufikishwa mahakamani halafu tutaambiwa uchunguzi haujakamilika.
Hii ni style ya stone age katika mambo ya ulinzi na uchunguzi.
Katika nchi za wenzetu Lwakatare hadi sasa alipaswa apewe compensation.
Katika nchi yetu sheria zipo lakini kwabahati mbaya tumeridhika kuwa ndivyo ilivyo.

Unapomkamata mtu tayari kuna ushahidi wa kutosha, iweje akamatwe tu kwasbabu ya video ya you tube?
Inawezekana ni kweli lakini tukubali kuwa utaratibu unaotumika ni ule wa ushabiki na wala si utaalamu.

Ni ushabiki kwasababu video ngapi ikiwemo ya Ilunga zimekaa mitandaoni bila Polisi kuwa na habari za kuwakamata wahusika?
Na kwa kutambua kuwa Lwakatare ni mtu maarufu Polisi walishindwaje kumfuatilia taratibu hadi wakawa na ushahidi wa kutosha! Nasema ushahidi wa kutosha kwasababu kesho utasikia uchunguzi haujakamilika. Third world!

Kuhusu king make na planner, ndiyo maana nimesema Polisi wamekurupuka.
Hili suala ni very complicated.
Wanapotaka kuihusisha CDM nadhani tutaishia katika filamu nyingine ya kova.

Ndani ya CCM kuna mtifuano na kujipanga kwa hali ya juu.
Kuna makundi hasimu makubwa mawili. Kundi la king maker, former speaker na lile la Foreign affairs.
Kwa kuelewa umuhimu wa vyombo vya habari kuna uwezekano hili likawa ni ''family feud''.
Au pia inawezekana kukawa na competition ya waajiri kwa lengo la 2015.

Mtu anayeweza kutoa hints na thorough analysis ni Kibanda.
Yeye ni victim na anaweza kuwa na watu anaowafahamu katika sakata zima.
Kwanini Polisi hawafanyi uchunguzi kwake wanakimbilia video kama ndio kitu muhimu sana!

Ni kosa lile lile la kumkamata Mkenya halafu Ulimboka anakuja na jina halisi. Polisi wanabaki kuhaha bila kujua nini wafanye.
Tutaendelea kuwa na jeshi la ujima namna hii hadi lini? Karne ya 21 bado tunatumia mbinu za enzi za mawe!!

Hivi Kibanda na akina Bashe waliotoa taarifa za kufuatiliwa na Polisi wakija na ushahidi mwingine tofauti na video, serikali itabaki na nini?

Kwamba hata video ikiwa authenticated, Lwakatare atashitakiwa kwa uchochezi na kama ni hivyo na kwa mujibu wa nyuzi yako ya jana haionekani kama tunasheria za electronics, serikali itatuambia nini kuhusu Kibanda.

Hadi hapo kitendawili cha Kibanda kitakuwa hakijatenguliwa na serikali itakuwa imebeba dhamana yote bila chembe ya wasi wasi.

Polisi walitakiwa wafahamu kuwa suala la Kibanda ni very sensitive and complicated kutokana na historia ya matukio yaliyotangulia. Linahitaji political and social factors ziangaliwe kwanza kabla ya kulihusisha na CDM au mtu mwingine.

Taifa lipo katika hatari kubwa sana inapofikia mahali vyombo vya usalama vinakuwa sehemu ya waamuzi na washabiki.

Tumefikaje hapa, hilo ndilo swali la leo.
Mkuu Nguruvi3, kiukweli polisi wetu wameshindwa kazi siku nyingi. Baada ya tukio la Kibanda, nilipandisha uzi jinsi TISS walivyoshindwa kazi, modes waliufukia mahali uzi ule. Niliuliza kama mtu anaibuka hadharani na kudai anayo video ya jinai, alifanywa nini?. Membe kaibuka na list ya maadui 11 na kuwapa ole wao asioteshwe!, amnefanywa nini, au angalau juhudi gani zimefanyika kuwabaini hao maadui 11 ni kina nani?!.

Wenzetu wangepata mkanda kama huo, wangeuhesabu its just a tip, wangempa ulinzi mtuhumiwa na track wanaomfuatilia wakishapata uhakika ndipo wanafanya arrest with evidence, ile ile siku ya arrest, wanakuja na search warrant na mtandao mzima unakuwa arrested at the same time!.

Wenzetu South Africa, wame extend jurisdiction time, mtu anakamatwa jioni, anafikishwa kwa hakimu usiku hadi saa mbili usiku ili kusomewa shitaka ndipo anatupwa mahabusu!.

Kiukweli tunafanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu kwa ignorance na watu kutojua haki zao. Polisi walipomuua Imran Kombe, familia ililipwa kifuta machozi cha Shilingi milioni 300,000. Hili liliwezekana kwa sababu familia ilikuwa na uwezo wa kuweka wakili. Daudi Mwangosi ameuwawa mikononi mwa polisi, baada ya criminal case, sidhani kama family hata wanajua remedy ya civil case ili familia ifidiwe!.

Nchi yetu tunafuata mfumo wa comon law wa Uingereza, mtuhumiwa anakuwa "asummed not guilt until proven beyond reasonable doubt before the court of law of competent jurisdiction!" hivyo hawaruhusu kupiga picha ndani ya vyumba vya mahakama wala kuingiza video kamera, huko ni kuwahukumu kabla!. Tunashuhudia wapigapicha wakiruhusiwa kupiga picha mahakamani!, na polisi wetu mpaka wanawa parade watuhumiwa mbele ya waandishi wa habari!.

Haki zipo, zimeandikwa na zimeainishwa, ila haziletwi kwenye kisahani cha chai, zinatakiwa kupiganiwa!.
Japo tuna wanaharakati wengi tuu wa haki za binaadamu, wengi ni wanaharakati msimu, jambo likitokea wanapiga sana kelele, likitulia limekwisha!. Mimi mpaka leo na kesho, nikimkumbuka tuu Mwagosi, ile picha yake ya mwisho, inanijia na kuifikiria familia yake!.

Kitu kimoja kizuri, mimi ni muumini wa "law of the karma" kila jema utendalo au ovu utendalo, malipo ni hapa hapa duniani!. Watalipa very dearly, na waliodhulumiwa, watafidiwa!.

Pasco.




Pasco.
 
Swali la Leo: TUMEFIKAJE HAPA?
Mkuu wangu Nguruvi3. Je, ni kweli hatufahamu tumefikaje hapa? Je, kweli huu si wakati wa kujiuliza Tunatokaje hapa badala ya Tumefikaje hapa? Tangu yatokee haya, ni miaka mingapi bado tunaulizana TUMEFIKAJE HAPA? Majibu yalishatoka zamani, TUPO TULIPO BAADA YA KUJIKATAA WENYEWE, KUUA MAADILI NA MIIKO YETU NA KUGEUKIA TAMADUNI KINZANI KWA NYAKATI NA MAZINGIRA YETU. Mara ngapi watu wamelilia kurejesha miiko na maadili yetu? Je, si kuwadhihaki kuuliza tena, Tumefikaje hapa!? Je, kuna yeyote aliyepinga ukweli huo? Kwa hoja zipi? Na lini tulikubaliana nae? SHAME ON OUR SOULS-Yangu na Yako. MIIKO YETU IMESHAKUFA, thamani yetu haipimwi tena kwa UTU WETU bali KITU CHETU, kipi kigeni kukishangaa leo na KITU CHAKO NDIO THAMANI YAKO?
Labda nitasema hili leo kwako Mkuu wangu Nguruvi3 na kwa wanajamvi wengine.."HUU SI WAKATI WA KUKAA NA KUSUBIRI FULANI ATAFANYA NINI KUTUTETEA. The Whole Land is Corrupted. Kama sisi tuonayo haya, tunahisi kuna watu maalamu wa kuhangaikia hayo, TUNAJIDANGANYA. No One to Trust"
Si wakati wa kungoja au kumwambia fulani afanye hivi kutuokoa, ni wakati wa kufanya wenyewe.
Swali la leo, Tunaanzaje? Si wapi tena, maana ilishasemwa-turudishe/tuwe na maadili na miiko yetu kulingana na mazingira na nyakati zetu! Sasa TUNAIRUDISHAJE? Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU katika hilo, tuzame katika tafakari kuu, tuumize vichwa kutegua na kutega HESABU, TUTAFIKA TU, AMINI HILO. Tusidunishe nafasi zetu tulizonazo leo, TUZITUMIE-TUNAWEZA! Ubunifu haujawahi kufika mwisho!
Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa.
a4afrika.
 
Mkuu Pasco hapo#150
Umeongea mengi na hili la wananchi kunyimwa haki ni tatizo kubwa sana Tanzania.
Sheria zipo kwamba huwezi kukamatwa bila kuelezwa kwanini unakamatwa na wala huwezi kuwekwa ndani bila kufunguliwa mashataka kwa muda kadhaa.

Katika nchi za wenzetu Jumamosi na Jumapili watu wanasomewa mashtaka.
Sisi Polisi anaamua tu kusweka mtu ijumaa ili ateseke hadi Jumatatu halafu anamwambia ondoka, kimbia tumekusamehe na mtu huyo anajiona ana bahati.

Watu wanauawa hakuna fidia. Hatudhani kama kuna fidia ya maisha ya mwanadamu lakini kupitia madai serikali ingekuwa macho na askari wake kufanya fyongo halikadhalika kusaidia familia zilizoathirika. Leo Mwalimu na Mwangosi wameacha familia zao, hatujui walikuwa bread winners kwa kiwango gani katika ujumla extended family za kiafrika.

Kuna mtu amefungwa kwa makosa Marekani. Amekaa jela miaka 25 na kuachiwa baada ya ushahidi kuonyesha hakuhusika, alilpwa fidia ya maisha aliyopeteza akiwa gerazani unconditional.

Kauwawa mwalim kwa kutovaa helmet, basi imeishia hapo!!
Watu wanapanda mabasi yanapata ajali hawafahamu kuwa mabasi yana bima.
Watu wanapata ajali za miguu hata za magari hakuna anayejua kuwa bima wanawajibu wa kulipa.

Na kweli haki zipo zimeandikwa na hatuwezi kuzipata katika kisahani (silver plate) hili nakubaliana nawe Pasco 100%
Ni hapa pia ndipo naungana na Jingalafalsafa kusema kuwa hili si jambo la kusubiri tufanyiwe, ni jambo la sisi kufanya.

Labda nitoe mfano, wanapokaa Dodoma wanasema hospitali ya Muhimbili ni ya taifa.
Wakipatwa na maradhi wanakimbilia Ujerumani, South Africa, Uingereza na India.
Hawawendi huko kwa makosa au ufisadi , wanakwenda kwasababu sheria walizoziandika wao zinawaruhusu.

Kupata matibabu ni haki yetu,sheria zimeandikwa na hao hao. Tunachoshindwa kufanya sisi wananchi ni kutumia sheria zinazotuhusu kupata matibabu bora hapa nchini.

Tulipaswa tusimame kwanza na kuwauliza kwanini wao waende nje na si Muhimbili. Wakituambia ni ukosefu wa MRI tuwabane wanunue ili atakaye kwenda nje aende kwa pesa yake. Leo mgonjwa wa Malaria natibiwa South Africa!

Kwa bahati mbaya na kwa wao kutumia uzezeta wetu, siku hizi hatuangalii tatizo tunaanza upuuzi wa kuangalia huyu ni dini gani. Wao wakipelekana nje ya nchi utawaona hima hima wakikimbia huku na huko kukodi ndege bila kuulizana wewe ni wa wapi na imani gani. Sisi tumezama katika ujinga wa kuangalia majina!

Hebu angalia sinema wanayoicheza sasa hivi kwa kujua sisi ni mazuzu. Siku moja iliyopita nimeandika kuwa wanachokifanya ni ukosefu wa utaalam na kitawatokea pabaya.
Wamekurupuka kumkamata Lwakatare leo inasemekana si kuhusu Kibanda ni mwandishi wa Mwananchi.

Kinachofanyika hapa ni kututoa katika mada (divert attention) ili waweze kupumua wakati wanapanga sinema nyingine.
Harakati zote za kumkamata Lwakatare hazikuwa na maana bali kutughilibu. Kwanini Lwakatare?

Jibu ni rahisi walitaka kulihusisha tukio la Kibanda na CDM ili kupata mtaji wa kisiasa na kujiosha mbele ya uso wa dunia kuwa vurugu zinatoka nje ya serikali na chama tawala.

Salva Rweyemam amekaririwa akisema mawasiliano ya Michuzi yalikuwa baina ya wafanyakazi wa Ikulu.
Hakukanusha kuwa yaliyomo ni uongo.

Serikali imebanwa na inatafuta namna ya kujikwamua. Njia nyepesi ni kutafuta ''prominent figure'' kama Lwakatare ili macho ya watu yaondoke kwa Kibanda.

Hivyo ndivyo walivyofanikiwa kwasababu hatuongelei Kibanda tena tunaongelea video ya you tube ambayo haimhusu Kibanda. Wanajua jinsi ya kuchekecha nasi tumeamua kuwa pumba, ni wepesi na tunaruka popote penye chujio.

Hatujapata majibu ya jaribio la kuuawa kwa Sitta kwa kutumia ajali
Hatuna majibu ya jaribio la Mwakyembe kutengenezewa ajali
Hatuna majibu ya Kubenea kujeruhiwa na kunusurika
Hatuna majibu ya Mwangosi wala Uliomboka
Orodha ni ndefu, niseme tu hatutakuwa na majibu ya Kibanda.

Labda tukubushane kuhusu nini wenzetu wanachosimamia.
Kule India wananchi walisimama kidete hadi wabakaji wa mwanamke mmoja walipotiwa mbaroni
Kule Marekani wananchi walisimama kuhusu mauaji ya Tevor Davis hadi Zimmerman kufikishwa mbele ya sheria
Kule Uingereza nchi nzima ilisimama kumtete ''Yaya'' aliyehukumiwa kifungo cha maisha kule Marekani hadi akaachiwa

Hizi ni nchi kubwa zenye mamilioni ya watu. Marekani ikiwa na milioni 300 na India Milioni 900.
Inapofikia haki ya mtu mmoja watu wanasimama pamoja kwa kusema sisi ndio nchi na ninyi viongozi ni waajiriwa wetu.

Sisi tumebaki kusema 'ah hiyo ni kazi ya mungu, mungu anajua tumwachie yeye, watalipwa na mola n.k.''
Hata kama vitabu na dini zinazosukuma watu waseme hivyo zinahimiza kutenda na kutendewa haki bado tumeinamisha vichwa chini. Wanatuburuza wanavyotaka na wala hatuonekani kushtuka.

Tusubiri, kesho vibaka watakamatwa manzese na kuambiwa ndio walihusika na tukio la Kibanda.
Hiyo ndiyo njia yao ya kufunga watu midomo. Baada ya hapo tunakaa kimya tukisubiri nani anafuata!
 
BOSCO NTAGANDA AJISALIMISHA

Mmoja wa makamanda waliounda kundi la M23 amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda akitaka apelekwe mahakama ya kimataifa the Hugue kukabliana na tuhuma za mauaji, ubakaji n.k. alizotuhumiwa nazo mwaka 2006.

Ntaganda alikuwa sehemu ya jeshi la Kongo lililoungana katika mkataba wa Kampala na baadaye kujiengua na kujiunga na kundi la M23.

Katika siku za karibuni jumuiya ya kimataifa imeilaumu Rwanda kama sehemu inayochochea maasi kule DRC.
Rais Kagame amepinga hayo akisema ipo siku ukweli utajulikana na kwamba Rwanda haihusiki.

Katika siku za karibuni nchi za SADCC zimeunda jeshi la kwenda kuweka hali ya mambo sawa.
Katika safu ya duru matukio tulishawahi kueleza kwa kina kwanini kuna uwezekano mkubwa wa majeshi ya SADCC kufanya vema kuliko yale ya Umoja wa mataifa.

Ikumbukwe kuwa jeshi la SADCC lina idhini ya umoja wa mataifa likiwa na kipengele cha Neutral force.
Tulisema kuwa nchi kama Tanzania inafahamu vema miundo mbinu ya DRC kwasababu ilishiriki katika kuunda jeshi la DRC.(Rejelea habari za nyuma)

Tukasema kuwa SADCC ina msaada wa kijeshi kutoka nchi za magharibi na teknolojia itakayotumika huenda waasi wa DRC akina Makenga na Ntaganda wasiweze kuihimili.

Katika wiki mbili zilziopita M23 imegawanyika na kwa bahati mbaya makamanda wawili maarufu wa Ntaganda walikamatwa.

Hakuna ubishi kuwa Ntaganda alikuwa na nguvu kutokana na msaada wa Rwanda.
Inasemekana alikuwa anapokea maagizo kutoka kwa waziri wa Ulinzi wa Rwanda.
Hata makamanda wake wawili wamekamatwa na serikali ya Kagame.

Ntaganda amesafiri kutoka DRC hadi Kigali tena kwenye ubalozi wa Marekani na kujisalimisha.
Hili lisingewezekana bila msaada wa serikali ya Rwanda. Mtu wa kwanza kutoa habari hizi ni waziri wa serikali ya Kagame.

Ni jambo la kushtusha kuona mtu aliyepigana miaka 20 anajitoa mwenyewe kwenda kupata hukumu.
Maswali ni mengi kwanini amefikia hatua hiyo?

Zipo nadharia nyingi sana ambazo hazina uhakika wala ithbati lakini ni muhimu tukaziangalia kwa uchache wa kuanzia.

1. Kuvurugika kwa M23 ni matokeo ya tishio la SADCC na kwamba tayari kundi limeanza kusalatiana na hivyo Ntaganda anafahamu kuwa zake zimefika na ni bora the Hague kuliko Segerea au Lukaranga

2. Kukakamtwa kwa makamanda wake kumevunja nguvu yake na hivyo kujiona hana lake tena.

3. Kipigo kilichotokana na uhasimu wa makundi alichokipata kinamweka katika hali ya kutokuwa na ulinzi na amani tena

4. Rwanda imeona ni heri imtose pengine katika kujinasua na dhahama inayotokana na kemeo la wakubwa wa magharibi

5. Ntaganda ameona hana jingine na hana lake hivyo atafute sehemu ya kujibanza huko ulaya na akina Taylor

Nadhari ni nyingi sana na hakika itachukua muda kujua kwa dhati kwanini amechukua hatua hizo.

Duru matukio itaendelea kufuatilia na kuwahabarisha.
 
Back
Top Bottom