Duru za siasa - Matukio

Ben nadhani reform ys UN haitahusu kuondoa Veto. Marekani inajua kuwa bullying ni matokeo ya kuwa na Veto na kuiondoa ni kuinyima 'Marekani haki ya kuongoza''.

Expansion ya UN security council nayo naiona ina matatizo. Tunaowategemea ni wanachama wa BRICS kama India, Brazili n.k. Mhindi hawezi kusimama na kusema this is right or this is wrong! Hapo tu tunaona tatizo.
Labda Brazili lakini nao pia wataweza kusimama katika ukweli katika masuala kama ya Israel-Palestine conflicts?

Kumbuka kuwa Brazil ndiyo nchi yenye wafuasi wa Roman Catholics kwa wingi sana duniani kama sijaskosea. Sasa inapofikia masuala ya mideast sidhani kama kutakuwa na matokeo tofauti na sasa.

EU ni wajomba wa US lakini ukweli unabaki kuwa sasa wameonyesha kuchoshwa sana na ubabe wa Israel. Mwaka jana waliazimia hata kuitenga katika biashara kwa kile Tonny anachosema kuwa wao ni kikwazo cha mazungumzo mashariki ya kati. Kilichoudhi zaidi ni pale waisrael walipotumia 'ugaidi' wa kuiba Passport za nchi za EU na Australia kufanya mauaji ya kiongozi wa Hamas kule Dubai.

Uhusiano wa EU na Israel si strong kama ulivyokuwa awali umebaki kuwa traditional tie with lose strings and holes everywehere.

Nchi za kusini zimeshindwa katika south south relation kwasababu ya uchoyo, ubinafsi na ujinga ndani yake.
Fikiria hapa nyumbani utaona tuna safari ndefu sana. Wakati EU wanaleta nguvu pamoja sisi tunabaki kudanganya kuwa ukishapata mafuta basi hutahitaji muungano tena (Zanzibar). Sasa panua wigo wa ufikiri za ZNZ uhusishe na nchi zote za Africa na south of Sahara desert utaona ni umimi tu. Tunahitaji kutawaliwa kwa miaka zaidi hadi tutakapokuwa na akili.

Kuhus Afrika kuwa na kiti UNSC hilo napinga sana. UNSC inasababu na malengo, Afrika tunatakiwa kwanza tuhakikishe usalama wa chakula, tuweze kumudu vurugu za bara letu kabla hatujaomba nafasi ya kushughulikia matatizo ya dunia.
Sasa hivi nusu ya matatizo ya duni ni Afrka.

Nimeangalia ripoti ya IMF kuhusu uchumi, inaonyesha uchumi wa china utakuwa na -0.3 growth, Europe -0.2, US .0.3 na kwingineko. Afrika inatajwa by the way tu. Sasa kwanini Afrika ipewe nguvu isiyostahili. Tunapaswa kwanza tusimamie rasilimali zetu, tuinue hali za maisha za watu wetu ndipo tufikiri kiti UNSC.
 
Mkuu Ben Saanane Nguruvi3 & Ritz hili la south south relation nakumbuka Hayati Mwl Nyerere alilipigia kelele sana nadhani kulikuwa na commision yake sijui baada ya Mwl kufariki bado ipo au nayo ilifariki ?.

Ni kweli ilikuwepo mkuu na sasa haina dira tena.

US imekuwa ikitumia nguvu zake kuyagawa mataifa yanayoendelea.

Kwa mfano kupitia containment policy wamekuwa wakiitumia India oflate kupunguza nguvu za China.Wamekuwa wakiitumia Egypt na Saudia kwa ajili ya Interest middle East

-Leo hapa SADCC haiwezi kuwa na umoja au Africa hawawezi tu kuwa na msimamo mmoja katika global stage.Utaona Malawi wanamtangaza Bashir persona grata kinyume na maimamo wa AU(Ingawa AU Chatter nayo ni ambiguous kwenye kipengele cha non interference masuala ya ndani ya member states)
-Pia kwenye WTO tulishuhudia India,China na Brazil tu zikiungana dhidi ya imperialists ambition huku mataifa kama Afrika Kusini(The weakest economy in BRICS) wakihofia kuumiza Trade relation na North.
 
Kufuatia sakata la Israel kushambulia kiwanda cha silaha nchini Sudun. Jeshi la wanamaji la Iran lawasili Sudan.

Umeonekana msururu wa meli za jeshi la Iran umetia nanga katika bandari ya Sudan kuwasilisha kile ambacho shirika la kitaifa la habari Iran ISNA linasema ni ujumbe wa amani na usalama. Ziara hiyo katika bandari ya Sudan inajiri siku sita baada ya shambulio la angani dhidi ya kiwanda cha silaha mjini Khartoum ambalo serikali nchini humo imeilaumu Israel kulitekeleza.

Sudan imelalamikia Umoja wa Mataifa kuwa Israel ilishambulia kiwanda chake ambacho kinaaminiwa kuendeshwa na Iran. Hata hivyo Iraele haijathibitisha au kukana kama ilihusika na shambulio hilo.

Meli hizo na zingine zikiwa zimebeba helkopta za kivita, Iran inasema ziara hiyo ni ishara ya uhusiano wa kiusalama kati ya nchi hizo mbili.
 
Kufuatia sakata la Israel kushambulia kiwanda cha silaha nchini Sudun. Jeshi la wanamaji la Iran lawasili Sudan.

Umeonekana msururu wa meli za jeshi la Iran umetia nanga katika bandari ya Sudan kuwasilisha kile ambacho shirika la kitaifa la habari Iran ISNA linasema ni ujumbe wa amani na usalama. Ziara hiyo katika bandari ya Sudan inajiri siku sita baada ya shambulio la angani dhidi ya kiwanda cha silaha mjini Khartoum ambalo serikali nchini humo imeilaumu Israel kulitekeleza.

Sudan imelalamikia Umoja wa Mataifa kuwa Israel ilishambulia kiwanda chake ambacho kinaaminiwa kuendeshwa na Iran. Hata hivyo Iraele haijathibitisha au kukana kama ilihusika na shambulio hilo.

Meli hizo na zingine zikiwa zimebeba helkopta za kivita, Iran inasema ziara hiyo ni ishara ya uhusiano wa kiusalama kati ya nchi hizo mbili.

-Ofcourse hii move ya Iran ilitarajiwa.Inaitwa Convetional detterence theory

Hii ni mbinu ya kumtisha adui na kuonyesha superiority .Pia ni katika risk strategy ya kuleta balance of power na bargaining kwenye medani za kimataifa
 
UCHAGUZI MAREKANI

Zikiwa zimebaki siku 6 kabla ya kupiga kura ya mwisho kuamua rais ajaye wa Marekani, dhoruba ya Sandy nayo imetikisa miji ya New York na state za karibu kama New Jersey, Ohio n.k.
Kwa ukaribu sana huu ulikuwa mtihani mwingine kwa Obama. Kama tunavyokumbuka Katrina na George Bush basi ndicho kilichokuwa kinamkabili Obama.

Dhoruba ya Sandy ni kubwa sana katika historia ya New York. Maeneo kama Long Island yanaonekana kana kwamba yamepigwa mabomu. Nishati ya umeme imekuwa ni tatizo na hadi leo wakazi wapatao milioni 5.3 hawana Umeme.
Maji yamejaa na kuvuruga huduma za kiuchumi na zile za kijamii. Hospitali zinahamisha watu kwa kukosa umeme kwasababu hata majenereta ya dharura nayo yameonekana kushindwa kazi.
Huduma za reli na viwanja vya ndege zimesimama pia

Rais Obama amefanya ziara katika jimbo la New Jersey. Huko alipokelewa na gavana Christie wa jimbo hilo.
Gavana huyu ndiye alitoa key note speech katika mkuatano wa Republican. Christie amejitokeza hadharani na kusifu ushirikiano anaoupata kwa Obama. Katika nyakati hizi hilo nalo limezua utata kwa kuzingatia kuwa linampa Obama Plus katika usimamizi kama Rais.

Kampeni zilisimama huku Romney naye akitengeneza vichwa vya habari kwa kukusanya michango ya watu waliopatwa na maafa. Zikiwa zimebaki siku 6 wazungu wanamsemo wao unaosema 'play safe' na hicho ndicho anachokifanya Romney.
Kwamba naye alisitisha kampeni ingawa kichini chini bado alikuwa anaendelea.

Dhoruba ya Sandy inaathiri sana kampeni za Wagombea. Jimbo la New York, New Jersey na Ohio ni maeneo Obama anatarajiwa kushinda. Kwa bahati mbaya sana sehemu zizlizoathirika sana ni zile zile za wpiga kura wa Obama huku maeneo yaliyo salama yakiwa na wapiga kura wa Romney.

Hii maana yake ni nini! Kuna uwezekano mchuano ukawa mkali sana Ohio kwasababu kura za maoni zinaonyesha tofauti ndogo sana. Ohio ni Must win kwa Romney na kama atashinda hilo litamweka Obama katika wakati mgumu sana.
Katika siku 6 haitarajiwi huduma za REli, umeme na nyinginezo kurudi katika hali ya kawaida. Hivyo uwezekano wa wapiga kura wa Obama kushindwa kupiga kura ni mkubwa sana.
Kwa uchache kimbunga hiki kimeathiri sana Democrat kuliko Republican.

Kura za maoni zinatofautina na kubadilika kila mara. Zile za CNN zinaonyesha mchuano wa karibu sana ''neck to neck' na zile zilizotolewa leo na CBC/NYT/Quillack zinaonyesha advantage kwa Obama.
Hata hivyo ukweli unabaki kuwa kuna uwezekano wa mmoja kushinda viti 270 'electoral college'' na mwingine kura za watu 'popular vote'.

Tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu kinachojiri.
 
UCHAGUZI MAREKANI

Zimebaki takribani siku 3 kitendawili kitenguliwe. Uchaguzi ni mchuano mkali sana.
Leo wagombea wamejikita katika uwanja wa vita ''battle ground' kule Ohio.
Kura za maoni zinaonyesha Obama akiwa mbele kidogo sana ya mpinzani wake Mitt Romney.

Kinachofanyika ni kuwa Mitt Romney anataka kuchukua Ohio kwa kujua kuwa ina wajumbe wengi sana ili afikishe namba ya wajumbe 270. Ukweli kuwa hakuna Rais aliyetoka Republican bila kushinda Ohio una msukuma sana Romney kubaki Ohio. Wakati huo huo Obama anataka kushinda Ohio ili iwe kizingiti kwa Romney na pia kumshinikiza abaki Ohio na asiende maeneo mengine.

Kwa kuangalia ramani hakika uchaguzi ni mkali sana na pressure ipo kwa Obama. Akiwa incumbet president alitakiwa awe mbele kwa point 7 au zaidi. Lakini pia kwa kutazama hali ya uchumi Romney alitakiwa naye awe mbele kwa kiasi cha point alau 6 hadi 7.

Takwimu za ajira zinaonyesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimeongezeka mwezi huu kutoka 7.8 za mwezi september hadi 7.9. Katika takwimu hizo jambo zuri kwa Obama ni kuwa ajira zilizotengenezwa ni 185,000 kinyume na matarajio ya 125,000. Takwimu zinamsaidia Obama kwasababu kinyume chake Romney angetumia fursa hiyo kummaliza.

Jambo moja linalojitokeza ni kuwa mdahalo wa 2 na 3 umezuia kwa kiasi fulani nguvu ya Romney.
Je,umemjenga Obama? Hilo ni swali linabaki kuwa gumu.

Wanajamvi na wasomaji wa duru za siasa matukio, tunapenda kuwataarifu kuwa tutakuwa tunaleta kila kinachojiri katika muda muafaka.

Siku ya jumanne ambayo ndiyo kilele cha kampeni na upigaji kura tutaanza kuwaletea habari in ''Real time' kwamba kila linalotokea llitaripotiwa kwa muda huo huo a.k.a live.

Stay tune na fuatilia hapa Duru za siasa matukio.
 
Rais atakayekuwa kinyume na Israel hawezi kuachwa hai kama akishinda.

Times are changing pretty fast. There was a time when non WASP could not even think of running for office in US, not any more. Changes that we see in the region could change that thing entirely, it has already done that in some ways. Ukiangalia sasa inaonekana hata jews wa Marekani wamekuwa na mtizamo tofauti sana na miaka 10 au 20 iliyopita, what made Israel special to America 20 and 30 years ago, is waning so fast.

Zamani Israel ilikuwa inadetermine sera za Marekani mashariki ya kati, lakini sasa economic interests ndio zina determine, sasa hivi nchi za kiarabu karibu zote zinasambaratika hakutakuwa na serious threat kutoka kwa state actor. Ndio maana unaona Netanyahu na kelele zake za umessiah amepuuzwa karibu na kila mtu (ispokuwa Romney) na ameambiwa kuwa akijaribu kuishambulia Iran cha moto atakiona, mwenyewe amefyata.
 
Times are changing pretty fast. There was a time when non WASP could not even think of running for office in US, not any more. Changes that we see in the region could change that thing entirely, it has already done that in some ways. Ukiangalia sasa inaonekana hata jews wa Marekani wamekuwa na mtizamo tofauti sana na miaka 10 au 20 iliyopita, what made Israel special to America 20 and 30 years ago, is waning so fast.

Zamani Israel ilikuwa inadetermine sera za Marekani mashariki ya kati, lakini sasa economic interests ndio zina determine, sasa hivi nchi za kiarabu karibu zote zinasambaratika hakutakuwa na serious threat kutoka kwa state actor. Ndio maana unaona Netanyahu na kelele zake za umessiah amepuuzwa karibu na kila mtu (ispokuwa Romney) na ameambiwa kuwa akijaribu kuishambulia Iran cha moto atakiona, mwenyewe amefyata.
Obama anachofanya ni more of a politcal strategy.Kwa maana kwamba anataka kujiweka kwenye position ambayo anaweza kuzileta pande zote mbili mezani pale inapokuja kwenye mgogoro wa Palestine and Israel.Kwasababu kiukweli,marekani chini ya Obama, wanawasaidia Israel kijeshi kuliko wakati mwingine wowote ule.Lakini asichotaka Obama ni bullying ya Netanyahu ambaye anataka akikohoa basi Obama aitikie kama ilivyokuwa kwa marais waliopita ambao waliongoza pia kwa kutegemea nguvu na kura za evangilicals.Sasa hivi votting blocks zimebadilika sana,kuna kizazi kipya ambacho Obama alikitegemea sana kwenye uchaguzi uliopita.Ndiyo maana hakujali hata kwenye ku repeal "don't ask don't tell",jambo ambalo lisingewezekana kufanywa na rais yoyote aliyepita wa marekani.
 
Obama anachofanya ni more of a politcal strategy.Kwa maana kwamba anataka kujiweka kwenye position ambayo anaweza kuzileta pande zote mbili mezani pale inapokuja kwenye mgogoro wa Palestine and Israel.Kwasababu kiukweli,marekani chini ya Obama, wanawasaidia Israel kijeshi kuliko wakati mwingine wowote ule.Lakini asichotaka Obama ni bullying ya Netanyahu ambaye anataka akikohoa basi Obama aitikie kama ilivyokuwa kwa marais waliopita ambao waliongoza pia kwa kutegemea nguvu na kura za evangilicals.Sasa hivi votting blocks zimebadilika sana,kuna kizazi kipya ambacho Obama alikitegemea sana kwenye uchaguzi uliopita.Ndiyo maana hakujali hata kwenye ku repeal "don't ask don't tell",jambo ambalo lisingewezekana kufanywa na rais yoyote aliyepita wa marekani.
Absolutely! Pia nakubaliana na Bongolander kuwa siasa za dunia zimebadilika sana. Siyo Marekani tu hata EU wanaiangalia Israel kwa jicho tofauti sana.
Mshindi wa uchaguzi atatokana na matakwa ya wengi.
 
MTAOKEO YA UCHAGUZI

Kituo cha kwanza kitafungwa baada ya dakika 40 kuanzia sasa na matokeo yataanza kuletwa.

Tutaendelea kuwahabarisha
 
UCHAGUZI

Matokeo hadi sasa yanaonyesha Obama ameshinda kwa kupata viti 290.
Bado matokeo ya Virginia, Ohio na Florida.
Idadi ya viti inayohitajika ni 270, kwahiyo Obama yupo mbele kwa zaidi ya viti 20.

Romney amekataa kutoa pongezi kwa Obama na kuzuia shughuli nzima ya kutoa hotuba kwa Obama.
Romney anadhani kuwa kwa ukaribu wa matokeo ya sehemu zilizobaki huenda ana nafasi.

Ukweli wa mambo ni kuwa hata kama atashinda Florida, Ohio na Virginia bado hataweza kufikia 270.

Kwahiyo shamra shamra za ushindi wa Obama zimezuiliwa na Romney hadi sasa.

Tutawajuza
 
Hatimaye Romney amekubali yamekwisha salama. Kwa viti 303 hakuna namna ya yeye kuweza kuwa mshindi hata kwa kuiba.
Obama keshaongea.

Sasa tutaangalia mwelekeo wa uchaguzi kwa undani, plus na minus.
 
Ubashiri wa watu wengi ulikuwa Obama angeshinda lakini kwa viti 272. Inavyoonekana ni Landlslide victory.
Kuna mambo mengi ya kujifunza kutokana na mkakati wa uchaguzi huu.
Romney ni kama alipigwa na butwaa maana matumaini yake yote yaliyeyeku katika muda mfupi sana kuliko ilivyotarajiwa.
 
Mkuu Nguruvi3 vyombo vingi vya habari tayari vimeshamtangaza Obama kashinda.
Kuna wakati alikuwa amesita kukubali matokeo na hivyo Obama ingebidi asubiri lakini baadaye aliona hakukuwa na jinsi akampigia simu Obama mambo yakaisha.
 
TATHMINI YA UCHAGUZI WA MAREKANI NA SOMO KWA TANZANIA

Ile taharuki kuwa kungekuwa na mvutano mkubwa katika uchaguzi sasa imefikia mwisho. Ingawa kuna majimbo ambayo hayajaleta matokeo ya mwisho ni dhahiri Rais Obama atakuwa amevuka 303 au kufikia 330 kama FL itakwenda kwake kama ilivyo kwa muda huu.

Republican wamepigwa na butwaa hasa kwa kuzingatia umaarufu wa ghafla alioupata mgombea wao Mitt Romney.
Kitu kimoja kilichojitokeza ni kuwa unapoyavunja vunja matokeo na kuangalia vigezo kama uchumi, sera, mguso wa jamii n.k. Obama anamzidi Romney. Hii ni tofauti na kura za maoni zilivyowahi kusema kabla ya uchaguzi.
Yaani exit poll zinatoa picha tofauti na Opinion Polls.

Hata hivyo kura za maoni zimebaki kuwa na ukweli hasa zilipoonyesha kuwa Obama alikuwa anaongoza katika swing state nyingi na ukweli wa matokeo ndio huo.

Obama amekuwa rais wa Marekani aliyerudi kipindi cha pili akiwa na kiwango cha ukosefu wa ajira(unemployment zaidi ya 7.1).

Baada ya matokeo haya mabaya Republican wameanza kukamatana uchawi.
Kutakuwa na safu za tathmini katika wiki nzima tukiangalia uchaguzi huu na kuoanisha na hali ya mambo nchini Tanzania.
Tutayaangalia mambo yafutayo:
1. Uandikishaji wa wapiga kura
2. Idadi ya wapiga kura na mgawanyo wa kura
3. Wagombea uchaguzi (candidates)
4. Kunadi sera zao
5. Uhamasishaji wa wapiga kura

Idadi ya waliopiga kura mwaka huu imepungua ukilinganisha na mwaka 2008. kumekuwa na ongezeko la baadhi ya maeneo. Walatino ambao sasa ni karibia asilimia 30 ya Marekani wameonekana kuongezeka katika baadhi ya majimbo.
Kulitaka kutokea kitu kinachoitwa voters suppression yaani mbinu za kuwazuia watu wa kundi fulani wasipige kura.

Republican waliwatisha Walatino kuwa kujiandikisha kupiga kura kuatatumika katika kuwatafuta watakapohitajika kurejeshwa makwao. Mbinu hizo ziligundulika na Obama camp na kuzuia mapema kabla ya uharibifu zaidi.

Obama camp nao wakatumia mbinu ya kuhamasisha watu wasijiondikisha kama republican au Democrat waende kupiga kura katika vituo vya dharura. Ghafla idadi kubwa ya walatino ikajitokeza na hiyo kuwa dalili mbaya kwa Romney.

Hapa nitatoa mfano wa voters suppression inavyotumika. Mara zote kumekua na uandikishaji katika chaguzi za madiwani au wabunge. Voters turn out inakuwa ni ndogo sana. Watu hujiuliza nini kimetokea?
Majibu yake ni : Ununuzi wa shahada za kupiga kura na Pili udanganyifu. Huko vijijini huambiwa siku ya kwanza a uchaguzi ni CCM na ya pili ni wapinzani.

Lakini pia CCM imetumia mbinu kama za kutumia polisi na vitisho achilia mbali kuwanunua wagombea.
Tunakumbuka sakata la Mgombea Ubunge wa Chadema aliyeshindwa kurudisha form kwa wakati muafaka.

Kwa wenzetu wa Marekani, vyama huandaa wagombea wao kwa kuangalia kukubalika kwao na jitihada zao binafsi.
Wanajua nani ni Democrat au Republican, anaishi wapi na je amejiandikisha.
Siku za uchaguzi timu hupita kuhakikisha kuwa waliojiandikisha wamepiga kura.

Tunafahamu kuwa sisi bado ni wachanga lakini hiyo haituzuii kufanya yaliyopo katika uwezo. Wapinzani wanatakiwa wawe na data za nani anaishi wapi , amejiandikisha au la na anatarajiwa kupiga kura wapi.
Lakini wasiishie hapo tu ni lazima watoe elimu ya urai kuhusu upigaji kura ili kuepeuka ghiliba za kisiasa.

Vyama vya upinzani Tanzania lazima viwe na vetting system ya kujua nani mwenye uchungu na chama hivyo kuepuka ghiliba za viongozi kununuliwa au kufanya kampeni katika mazingira ya kununuliwa.
Hatari kubwa zaidi ni pale chama kama CDM kinaposubiri makapi kutoka CCM.

Katika kipindi hiki chama kinapojitanua kuna kila sababu ya kuwa na idara ya uchunguzi na usalama ili kubaini watu wenye itikadi na wanaokipigania chama siyo kutafuta idadi ya watu maarufu.
Chama kinapokuwa na mgombea anayeelewa eneo lake mambo kama voters suppression ni nadra kutokea kwasababu tayari atakuwa na info za kile kinachoendelea katika eneo lake.

Tutaendelea na mgawanyo wa wapiga kura na kwanini wagombea walilenga maeneo fulani ya kijamii.

Itaendelea
 
Mkuu Nguruvi3,
Tumeona kwenye huyo uchaguzi wa Marekani timu ya kampeni ya Obama ilikuwa inasomba wapiga kura na mabasi na kuwarudisha makwao baada ya kupiga kura. Huo utaratibu kwetu unafaa kutumika?
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea..

Idadi ya wapiga kura mwaka huu imepungua kulinganisha na 2008. Kura walizopata wagombea (popular vote) zinakaribiana sana ukilinganisha na uchaguzi uliopita. Hii maana yake ni kuwa pamoja na Obama kushinda lakini kura zilizomchagua zimepungua.Kwa taratibu za uchaguzi marekani wingi wa kura si hoja, hoja ni idadi ya wajumbe wanaohitajika kumchagua rais abao Obama amepta zaidi ya 300, wajumbe 30 zaidi ya kiwango kinachohitajika(270)

Obama aliungwa mkono na wanawake, vijana kati ya 20-29, wapenzi wa jinsia zinazofafana, weusi na Walatino.
Ukiangalia mgawanyo idadi ya wanaume waliompigia kura hasa weupe imepungua kwa kiasi sana.
Romney aliungwa mkono na weupe wengi, evangelics, wazee na wahafidhina.

Katika makundi yaliyomuunga mkono, Obama alipata uungwaji mkono mzuri sana ukilinganisha na mpizani wake.
Siri kubwa ya mafanikio ya Obama ni kuzingatia mchanganyiko(diversity), kusimamia anachokiamini bila kutetereka hata kama anajua kitamgharimu kwa upande mwingine.

Obama ameunga mkono mashoga hadharani ingawa alijua kuwa kufanya hivyo atakosa kura za evangelics na hata watu wa dini zingine kama waislam. katika uchaguzi uliokaribiana sana kila kura ni muhimu na alilifahamu hilo.
Kitu kimoja ni kuwa hajawahi kubadili msimamo kwasababu alijua kuna kura nyingine.

Obama alisimama kidete kuhusu mikopo ya wananfunzi na umuhimu wa elimu, kwahilo tu akavuna vijana wengi.
Amepitisha sheria inayohusu masilahi ya akina mama, jambo lililomuongezea uungwaji mkono na wanawake.

Kwa upande wa Walatino, Obama amekuwa mstari wa mbele kutaka watoto waliozaliwa USA na wazazi waliohamia kwa njia za haramu wapewe uraia.

Tofauti na Obama, Romney alikuwa katika nafasi isiyoeleweka. Uumini wake wa kanisa la Mormon ulihusishwa na kanisa la kishetani na wengi hawakuwa confortable hasa wale evangelics. Romney ametumia muda mwingi sana kuisafisha imani yake na si kueleza sera zake. Tumeona katika mkutano mkuu wa Republican ambapo Romney alitumia muda mwingi sana kuliongelea.

Mitt hakuwa na sera zozote zinazohusu vijana au wakina mama. Tena kwa akina mama Republican walitoa kauli zilizo wafanya Democrat washupalie ajenda ya akina mama. Kauli za kejeli na dharau.
Na ndivyo ilivyokuwa kwa mambo mengine.

Kwa upande wa Romney kampei yake ilikumbwa na mambo mengi. Kwanza walianza kumshaulia Obama kwa kejeli na matusi. Walizusha uongo na kugeuza hata hadithi. Walifikia mahali pa kusema mdororo wa uchumi ni matokeo ya sera za Obama wala si Bush. Baada ya kutumia miezi takribani 7 bila mafanikio ndipo walipogeukia agenda ya uchumi na hapo uhai ukawa umerudi. Hilo ni kosa la kwanza la Romney ambalo tutaliangalia katika mizani ya siasa zetu baadaye.

Mitt alibanwa sana na Obama camp kwasababu yakubadili sera. Wakati akiwa Gavana wa Massachussets Mitt alianzisha mpango unaofanana na Obama care, in fact wataalamu wake ndio Obama aliwatumia.
Alipoanza kampeni akawa kati na kati na mwisho wa kampeni akageuka na kusema ata repeal Obama care.

Mitt Romney alikuwa na mzigo wa kauli zake kuhusu auto bail aliyeosema haina maana na makampuni ya magari yaachwe yafisilisike tu. Viwanda vingi vipo Michigan na Ohio. Kwahiyo Ohio aliyo ihitaji sana ilikuwa kikwazo kwake.Akatumia muda mwingi sana Ohio bila kujua kuwa Colarado ilikuwa inamponyoka.

Romney amenukuliwa akisema 47 asilimia wanaishi kwa foodstamp na hao watampigia Obama. Kauli ilimmaliza kisiasa.
Wakati anasema anajua jinsi ya kutengeneza ajira, kumbu kumbu zinaonyesha aliua kampuni ya BAIN na watu kupoteza ajira, Hadi hapo wapiga kura wakalazmika kuiangalia historia yake kwa ukaribu jambo lililomletea matatizo

Ingawa mdahalo wa kwanza Romney alionekana kuibuka kidedea, inajulikana sasa kuwa uungwaji mkono mkubwa ulitokana na hamasa ya Republican waliokuwa wamekata tamaa na wala siyo sera. Katika mdahalo huo Mitt alionekana kuvuruga historia ya serikali ya Obama kwa makusudi na upotoshaji huku akiwa hana majibu ya sera zake.

Midahalo miwiwli iliyofuata Obama akatumia Chicago style na kumvuruga sana Mitt. Mdahalo wa mwisho ndio ulivuta kasi ya Romney nyuma. Baada ya hapo Romney akawa hana hoja kwasababu hoja za uongo zote zilitenguliwa.

TUANGALIE FUNDISHO.
Hapa tunajifunza kuwa ni lazima wagombea na vyama vyao visimame kidete katika misimamo inayohusu masuala ya kitaifa hata kama hayapendezi kundi lolote. Obama ndivyo alivyofanya kama nilivyowahi eleza.

Utashangaa chama cha upinzani kama cha Chadema hatujui msimamo wake halisi kuhusu baadhi ya masuala ya kitaifa. Mfano ni suala la katiba mpya na muungano. Hadi leo hakuna ajuaye CDM inasimamia wapi, kwa misingi ipi na kwanini.
Ni vema misimamo ikawekwa wazi ili kujua nani anasimamia wapi na wala siyo kuwa ''opportunist''

Pili, kuna funzo kuwa kumwangusha adui yako kisiasa si kumshambulia.
Hivyo ndivyo inavyotokea kwa upinzani kuweka hoja za ubadhirifu kama sera za chama.
Ni haki na vema kufanya hivyo, lakini basi tuambiwe mbadala.
Wananchi wanataka kusikia mbadala na si 'mabomu' ya wala rushwa tu.

Hapa pia nina mfano wa CDM. Chama hicho kina sera ya majimbo, labda atoke mmoja miongoni mwetu aeleze kwanini majimbo, yana manufaa gani ukilinganisha na muundo ulioopo. Huwezi kulisikia hili hata siku moja.
Wananchi wanataka kusikia kilimo, elimu na afya vitashughulikiwaje tofauti na ilivyo sasa.

Tatu, tunajifunza kuwa kampeni si mikutano ni mikakati. Hivi leo kuna sehemu wapinzani wameaacha kabisa kuingia na hakuna sababu za misingi pengine ni woga tu au kutokujua. Kwanini Iringa iwe ngome kubwa ya wapinzani na si Morogoro!

Kwa msingi huo wapinzani wanacheza karata ya Romney ya kuwatenga wapiga kura. CCM inalifhamu hilo ndio maana mara zote imejipanga katika maeneo dhaifu ya Upinzani. Haieleweki kwanini wapinzani waache jimbo kama la Korogwe kwa mtu asiye na elimu kabisa.

Lakini pia wapinzani waangalie sana makundi kama ya akina mama. Inasikitisha kuona kuwa chama cha upinzani kama CDM hakuna sauti ya akina mama. BAWACHA imebaki kuwa sehemu ya viti maalumu badala ya kiunganisho cha akina mama wa Tanzania. Kwa msingi huo watu wanaifahamu UWT zaidi kuliko chama kingine kwasababu tu ya udhaifu.
Kundi hili limemuumiza sana Romney na huenda dhambi hiyo ikatafuna wapinzani Tanzania.

Naomba ieleweke kuwa mijadala yetu haichukui sura za kisiasa. Ninaposhindwa kuongelea CCM ni pale ukweli unapojidhihiri kuwa huwezi kumfunza mbwa mzee mbinu mpya!

Tutaendelea....
 
Mkuu Nguruvi3 umegusia hoja muhimu sana hasa chama kikuu cha upinzani kutokutoa sera na misimamo yake kueleweka wazi kwa wapiga kura wa kawaida.

Mpaka leo CDM haielezei vizuri na kwa uwazi juu ya sera yake ya majimbo jinsi itakavyomnufaisha mwananchi wa kawaida mijini na vijijini.Kuacha kutoa ufafanuzi mzuri juu ya sera yako kunatoa nafasi nzuri sana kwa CCM kuikosoa na kueleza ubaya wake kwa kutoa mifano jinsi ilivyoshindwa kufanyakazi katika nchi nyingi za kiafrika Nigeria ikiwemo.

Msimamo wa CUF kuhusu muungano unajulikana wazi lakini msimamo wa CDM haujulikani,tunachokifahamu ni misimamo ya baadhi ya viongozi wake kama Tindu Lissu.Mikutano mingi ya M4C imejaa ubabaishaji wa hali ya juu kiasi wananchi wengi badala ya kuchota elimu ya uraia wamekuwa wakikumbana na vijembe na mipasho usiowasaidia na hili limeshaanza kuzoeleka.
 
Last edited by a moderator:
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom