Duru za siasa - Matukio

Mkuu Nguruvi3 umegusia hoja muhimu sana hasa chama kikuu cha upinzani kutokutoa sera na misimamo yake kueleweka wazi kwa wapiga kura wa kawaida.

Mpaka leo CDM haielezei vizuri na kwa uwazi juu ya sera yake ya majimbo jinsi itakavyomnufaisha mwananchi wa kawaida mijini na vijijini.Kuacha kutoa ufafanuzi mzuri juu ya sera yako kunatoa nafasi nzuri sana kwa CCM kuikosoa na kueleza ubaya wake kwa kutoa mifano jinsi ilivyoshindwa kufanyakazi katika nchi nyingi za kiafrika Nigeria ikiwemo.

Msimamo wa CUF kuhusu muungano unajulikana wazi lakini msimamo wa CDM haujulikani,tunachokifahamu ni misimamo ya baadhi ya viongozi wake kama Tindu Lissu.Mikutano mingi ya M4C imejaa ubabaishaji wa hali ya juu kiasi wananchi wengi badala ya kuchota elimu ya uraia wamekuwa wakikumbana na vijembe na mipasho usiowasaidia na hili limeshaanza kuzoeleka.

Well said Mkuu wangu:
Kuna vitu huwa napenda vitenganishwe katika Harakati za Ukombozi za vyama vyetu nchini! Navyo ni Political Movements na Welfare Movements!
*Political Movement, hujikita zaidi kukisimika chama kwenye HISIA za watu(ni propaganda), focus huwa "UMAARUFU" masikioni na midomoni mwa watu, mikutanoni na kona zote mitaani! Na humo ndimo vyama vyetu vyote vilimojikita, mfano mdogo tu "omba uwe maarufu kidogo tu, then tangaza nia ya kugombea ubunge kupitia chama chochote kile, utapewa support kubwa na uongozi wa juu kabisa! Tunawaona kina Komba, Rwakatale, Sugu, sasa Afande Sele, n.k. Hizo ni Political movements, na ni JANGA la taifa! Huku kauli "mkitupa ridhaa...tupeni ridhaa muone...tupeni kipindi kingine...."n.k hutawala majukwaa. Ni Upumbavu!
*Welfare Movements, hizi huhangaikia AKILI za watu na si HISIA zao, vigezo na hoja hutangulizwa kwanza katika kila jambo! Harakati hizi huwa haziyumbishwi na chochote ila Ustawi wa Raia tu/Maslahi ya Umma. Hapo ndipo akili zinapokubaliana na chama fulani kwa kuendesha harakati hizo, hata kama Hisia zitapinga, lakini Akili ikikubali Inatosha!
Huku tatizo hubainishwa, humeng'enywa, na kufanyiwa maamuzi sahihi na hatua mahususi! Lengo ni kujenga imani kwa watu juu ya chama kupitia AKILI ZAO NA SI HISIA ZAO! Wanachama na mashabiki wapo, hakuna mtaji bora wa kutekeleza hayo kama hiyo!
CDM kama chama kikuu cha Upinzani, kikiundwa na wasomi, kilitakiwa kione tayari fursa nyingi za kuisimika imani kwa watu kupitia akili zao juu ya chama chao! Mfano, ingekuwaje kama Chdm kupitia Bavicha ikaunganisha vijana kwa kila tawi na kubuni miradi na kuifanya kama timu, kesho wameacha wizi mtaani, wazee wao wangeizungumziaje chadema?
Kuna wanasheria wengi Cdm, ingekuwaje kama wangefungua vituo vya msaada wa kisheria kila tarafa hata kwa kusema viwe vinahudumiwa na matawi ya chama, kupitia miradi yao iliyobuniwa! Chama kama Taasisi iliyoamua kujitoa muhanga, kuna atakayedai mshahara mkubwa huko vituoni, kama yupo hafai. Kila mtu ale kiapo cha kukitumikia chama katika mazngra yoyote.
Hiyo ni mifano midogo tu ya Welfare Movements za CHAMA MAKINI.
Ni kujidanganya kwamba akili za watz zitajenga imani kwa Cdm, kwa kuwataja wala rushwa hazarani, kukandia ccm hazarani, n.k atakayejenga imani zake kwasababu ya hayo leo, kesho ataiondoa na kuipeleka ccm tena kwani wamemwambia cdm ni wadini au wakanda! HISIA HAZINAGA MSIMAMO!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea...

Tukiangalia sehemu ya 3,4 na 5 tunaona kuwa wagombea walikuwa na sifa tofauti kabisa. Obama anasifa ya kupendwa' charisma' tu pengine ni kutokana na anavyoweza kujenga hoja. Tatizo lake kubwa ni kutaka kujenga hoja kwa mithili ya ufundishaji 'professerial''. Kuna wakati ni jamabo jema, inakuwa tatizo pale anapotakiwa aeleze jambo kwa muda mfupi.

Hilo lilikuwa kikwazo katika mdahalo wa kwanza kwasababu alitaka aeleweke zaidi pengine kutokana na wasi wasi juu ya maswali hasa ya uchumi. Ukiangalia mjadala wa pili na wa tatu Obama alifanya vizuri sana kwa kujibu hoja na kupata nafasi ya kumcharura mwenzake.

Obama ni Orator mzuri sana mwenye hoja za ushashi. Ni kutokana na hoja zake mdahalo wa pili na wa tatu aliweza kumkabili Romney vizuri sana na kwa mantiki huku akiwa amevaa sura yenye mamlaka 'authority'.
Inasemekana kuwa washauri wake walimpoteza katika mdahalo wa kwanza pale walipomshawishi ajibu hoja kama rais ''presidential'' aepuke kumzogoa Romney. Hili lilimfanya apwaye sana kwani alijivika wajihi wa kufundishwa na si wake wa asili.

Kwa upande wa Romney, kwanza hapendwi na jamaa zake wa Republican. Romney ana kiburi cha fedha na hujibu majibu ya hovyo yenye kejeli, dharau na majigambo. Hili lilifanya mgombea mwenzake katika hatua za chama Gingrich kuweka kinyingo japo walionekana kuwa wamoja baada ya uteuzi.

Kauli za Romney ni za mkato na hazionyeshi kuwa na connection na umma. Tunakumbuka kauli kuhusu viwanda vya magari viachwe vife huku akijua kuwa kuna mamilioni wanaovitumia. Kauli ya 47% foodstump watampigia kura Obama na kauli aliyoitoa Uingereza kuhusu utayari wa Olimpic.

Lakini pia Romney alionekana kutokuwa na msimamo kuhusu asemayo. Alijenga hoja dhaifu ambazo zilikutana na media scrutiny na hivyo ku-expose arrogance yake. Mathalan, kumshutumu Obama kama chanzo cha kuvurugika uchumi hakukumjenga bali kumbomoa. Kila mtu anajua Obama alirithi tatizo lisilo pimika kutoka kwa Bush wa Republican.
Kauli za Romney kuhusu Iran na Israel zimekuwa za kugeuka geuka ''flip flop'' na kuacha maswali mengi juu ya utayari wake katika utawala.

Kampeni zao nazo zilitofautina sana. Romney alikuwa na matajiri waliomchangia kiasi kikubwa sana cha pesa na kumzidi Obama. Wakati anatumia pesa hizo kwa matangazo ya TV, Obama alikuwa anakusanya pesa kidogo kidogo kutoka kwa watu wa kawaida na kuzitumia katika 'grass root level'' kama kutengeneza ofisi za muda za kupiga simu ''call centre'', kuwawezesha watu walioko vitongojini kufanya kampeni na kuandaa jeshi la kujitolea ''volunteers'.

Kampeni ya Obama ilikuwa Micro politics wakati ya Romney ilikuwa Advertisement.
Obama aliumia watu wake wa kawaida kufanya kampeni kama akina Alexrold, D.Plaueff n.k. Kitendo cha kumuondoa Roma Mannuel kutoka Ikulu na kuwa Meya wa Chicago kililenga kumpa Roma nafasi ya kampeni na si utawala.

Romney alimtumia Karl Rove, yule bingwa aliyemwingiza na kumrudisha Bush Madarakani mara mbili.
Karl anatumia falsafa ya pesa zaidi wakati akina Alexrold wanatumia micro politics.
Matokeo yake ni Romney aliyekuwa ameandaa kila kitu kama rais wa 45 wa Marekani kupigwa na bumbuwazi pale lilipoibuka jeshi la Obama la kujitolea kwa kukusanya watu na kuwapeleka katika vituo vya kura.

MAFUNZO YATOKANAYO:
Kwanza, vyama vya upinzani lazima vielewe kuwa kampeni ni sayansi ya hali ya juu na si wingi wa pesa au wapiga debe.
Ni wajibu wa vyama kama Chadema kuhakikisha kuwa kampeni inaandaliwa na watu wenye weledi, wanaofahamu siasa, wataalamu wa vitu kama demography, wataalamu wa sayansi ya siasa, wachumi, wanasheria na Wataalam wa Logistics.

Vyama pia vinawajibu wa kuwa na watu wanaojua kujenga au kubomoa hoja kwa hoja (Pundits) mfano wa akina Paul Bagala. Alex Castiano, Donal Brazil n.k Hii itasaidia sana kuepeuka tatizo la kila mtu kusimama na kutoa hoja.

Funzo muhimu sana ni kuhusu wagombea. Ili chama kiweze kuwa na mgombea anayekubalika, mgombea huyo lazima akidhi baadhi ya vigezo na wala si umaarufu atu. Hili linatakiwa kuanzia ngazi zote ili kuepeuka tatizo lililompata Romney la kuonekana mtu asiyeijua jamii, tajiri mwenye kiburi na kejeli.

Inaendelea....
 
inaendelea....
MAFUNZO YATOKANAYO:

Funzo lingine la kuzingatiwa ni kuhusu mikutano. Hadi ilipofika Jumanne mchana Mitt Romney alijihakikishia kuwa ni rais wa 45 wa Marekani. Ilipofika mchana hali ilianza kubadilika kwani wapiga kura wasiojulikana walijaa katika vituo.
Hawa walikuwa wafuasi wa Obama kutoka grass root level. Wakati Romney akiwa ameandaa fataki za sherehe na hotuba ya ushindi, alipigwa na mshangao mkubwa sana kuona Obama amefikisha viti 270 katika nusu saa na kuchaguliwa tena.

Ndivyo inavyoonekana kwa vyama vyetu kama CDM. Mikutano ni muhimu sana lakini lazima mikutano hiyo iache alama chanya na si mikusanyiko tu. Huko katika grass root ndiko walipo wapiga kura na hivyo CDM wahakikishe kuwa kuna jitihada za makusudi za kuwawezesha wapiganaji katika ngazi ya chini.

Hili litawezekana pale rasilimali zitakapoelekezwa sehemu husika na kwa watu sahihi. Kazi ya kutambua watu sahihi ni ya kitengo cha utafiti na usalama ili kukwepa mamluki au wachumia tumbo.
Rasimali za chama kubaki katika ngazi ya kitaifa ili kuwawezesha viongozi kutembelea maeneo kwa muda tu hakutoshi kujenga chama katika grass root level.

Ritz ameuliza swali la muhimu sana endapo ni vema vyama kubeba wananchi kwenda katika vituo vya upigaji kura. Kisheria sioni mahali panapokinzana, kwa bahati mbaya katika mazingira ya siasa changa za nchi yetu, tume ya uchaguzi, Polisi na watawala hawawezi kuliachia hilo litokee kirahisi.
Endapo wataliachia basi wao watatumia rasilimali za taifa kufanya hivyo. hapo pia ni pagumu.

Pamoja na hayo, vyama vya upinzani vinaweza kuwa na madaftari ya kuwatambua wanachama wao na kuhakikisha kuwa wanapiga kura siku ya uchaguzi. Hivyo ndivyo Obama alifanya tena kwa kutumia teknolojia ya sasa, kwamba waliweza ku-google, twit na kutumia hata face book kujua nyumba gani ina Democrat au Independet voter na kwamba huyo awaye anapiga kura.

Na funzo la mwisho ni kuhusu pesa. Katika dunia ya leo pesa ni msaada na wala si msingi.
Kinyume chake Romney angekuwa Rais leo hii. Kukubalika kwa mgombea ni jambo muhimu sana.
Inavyoonekana Romney alisusiwa na wenzake licha ya kukumbatiwa na matajairi.
Mgawanyiko huo ulilileta sintofahamu ambazo leo tunaanza kuzisikia kidogo kidogo.

Kwanza, Republican wanasema Romney alifanya kampeni kwa pesa na Obama alifanya kwa mico politics. Hilo ni tatizo.
Pili, Washiriki wenzake kama akina Gingrich, Santorum na Ron Paul wamemsusia licha ya kuwa waliongea katika mkutano mkuu kumuunga mkono isipokuwa Paul ambaye hakuwepo kabisa.

Mtoa hotuba wa mkutano mkuu ''key note speech' Gavana wa New Jersey bwana Christie, yeye alitumia nafasi hiyo kujifagilia na si kutoa sera za chama au kumnadi mgombea. Siku tatu kabla ya uchaguzi, kimbunga Sandy kikatua jimboni mwake na yeye akasimama na kumu-endorse Obama. Hili lina maana nyingi sana na tutazijadili inatosha kusema tu kuwa tamaa ya ugombea inaweza kuwa tatizo kubwa ndani ya chama.Christie anaanglia 2016 kwa ukaribu sana

Gavana wa Ohio,yeye alisimama na kumsifia Obama kwa kudhamini viwanda vya magari.
Alisema dhahiri kuwa uchumi wa Ohio unakua vema. Huu nao ulikuwa mwiba mkubwa kwa Romney.

Matatizo hayo tunayo pia. Sasa hivi vyama vya upinzani badala ya kutafuta mbinu za ushindi watu wanakimbilia kupanga mabaraza ya mawaziri. Hata bila kujua mvurugano utakaofuata au kuvunjika moyo kwa watu wa grass root wagombea hao wamedhamiria kukidhi matakwa yao na wala si chama.

Kuna uwezekano wakafanikiwa lakini historia na maonyo yanayotolewa yapaswa kuwa mwalimu mzuri.
Tuna tatizo la tume ya uchaguzi, Polisi na hata sheria za uchaguzi.
Kwa bahati mbaya hayo hayaonekani kwasababu watu wanalenga 2015 na si kuimarisha vyama vyao.
Kwa mwendo huo grass root movement itapatikanje?

HITIMISHO
Siasa ni sehemu ya taaluma zinazohitaji weledi wa hali ya juu. Ni lazima zifanywe kisayansi na kwa kutumia teknolojia.
Wagombea wapatikane kwa sifa zao na wanavyosimamia sera za vyama na wala siyo umaarufu.
Mchakato wa kupata wagombea 'vetting' lazima uzingatie mahitaji ya nyakati na chama.
Vyama vijenge na kuandaa wagombea wao kuanzia grass root level na si skusubiri makapi ya wachumia tumbo

Rasilimali za vyama zitumike kuendeleza vyama na siyo makao makuu ya vyama Dar es Salaam.
Kampeni ziongozwe kutoka katika grass root na viongozi wawe wasaidizi.Kampeni zisimaiwe na weledi wa siasa za ndani na nje ya nchi

Vyama vinadi sera zao na kuonyesha mbadala ili kuwepo na tofauti. Mashambulizi dhidi ya chama tawala ni kupoteza muda kwasababu mwisho wa yote wananchi watajiuliza, endapo Ndimu ni chungu, Nanasi lipowapi?

Vyama vipiganie uwepo wa tume huru ya uchaguzi isiyowajibika kwa Rais, Muundo wa uteuzi wa viongozi wa jeshi la Polisi, Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi inayompa nafasi mgombea kuwa rais hata kama ameshinda kwa kura moja.

Vyama vya upinzani viongoze harakati za mabadiliko ya kweli ya katiba na viache kuripoti Ikulu kile wanachokitaka bali kile kilicho sahihi kwa taifa.

Vyama vya upinzani visimame kidete kunadi sera zao na kutoa misimamo kwa mambo ya kitaifa ili ijulikane vinasimamia wapi, kwanini na kwa faida ya nani.

Vyama vya upinzani vijiulize, kwanini kuna uandikishaji mkubwa wawapiga kura na kwanini waliojiandikisha hawapigi kura.
Na mwisho, vyama viwe na oganaizesheni na kujiendesha kama taasisi na si makundi ya watu maarufu.

Bila kuyaangalia hayo kwa jicho mujarabu, basi ''mbwa mzee mwenye mbinu za zamani' ataendelea kulinda boma.

Tusemezane
 
GEN PATREUS AJIUZULU, MKUTANO MKUU WA CCM

Marekani:
Gen Patreus ambaye ni mkuu wa kitengo cha ujasusi cha CIA amejiuzulu siku 2 baada ya ushindi wa Rais Obama.
Kujiuzulu kunatokana na kashfa ya ngono akihusishwa na mahusiano na ''biographer'' wake Ms Broadwell.
Yeye mwenyewe amekiri kufanya hivyo.

Jambo hili limezua taharuki kubwa. Kwanza ni kujiuzulu baada ya Rais Obama kutangazwa mshindi wa Urais.
Wachunguzi wa mambo wanasema white house ilikuwa na taarifa hata kabla lakini ilibidi wasubiri uchaguzi umalizike.

Taharuki ya pili ni kuhusu mtu muhimu sana katika safu ya ulinzi wa taifa kuhusishwa na kashfa kama hiyo.
Hivi tunapoandika wachunguzi wa FBI wamekusanya vitu mbali mbali kutoka nyumbani kwa kimada Broadwell ili kubaini kama kulikuwa na habari nyeti.

Uchunguzi huu ambao ungeihusu CIA sasa unaishirikisha FBI na hapo kuzua maswali mengi kutokana na utendaji wa vyombo hivyo na mgawanyo wa kazi.

Gen Patrus amepatikana na ushahidi wa emails kwenda kwa bi Broadwell.
Hili nalo linaleta mhemko kwasababu email ingekuwa kitu cha mwisho kutumiwa kwa mawasiliano nyeti tena na mkuu wa ujasusi na kuacha maswali kuhusu weledi wake kama si maswali ya kisaokolojia.

Zipo habari za kufikirika kuwa Gen amejiuzulu ili kuokoa mashambulizi dhidi ya serikali ya Obama kuhusiana na shambulio la Benghaz. Inasemekana Gen Patreus alikuwa atokee mbele ya kamati ya bunge ya ulinzi kueleza nini kilichojiri wiki ijayo. Pamoja na kujiuzulu bado kamati ina nguvu za kumwita na kumhoji jambo linaloondoa shaka kuwa kulikuwa na mkakati wa kisiasa kuzima tukio la Benghaz

Ms Broadwell alikuwa mwandishi wa kumbu kumbu ''Biographer''.
Kinachoshangaza ni kuwa kwanini Patreus aandike historia yake akiwa bado katika utumishi.
Kwanini asisubiri hadi atakapostaafu kama ilivyo kawaida.

Sifa kuu ya Patreus ni kuwa Jenerali aliyeongoza vema hali ya mambo kule Iraq na Afghanistan baada ya Gen J.Abizaidi kuonekana kushindwa kimkakati. Patreus ni 4 star Gen na anaheshima kubwa sana Marekani.

Mtafaruku umepamba moto na sasa unahusisha Gen mwingine ambaye pia ana mahusiano ya ngono na kimada.
Tutaliangalia kwa undani kadri siku zinavyosonga mbele.

MKUTANO MKUU CCM
Mkutano umemalizika na katika tukio kubwa ni lile la kumrudisha Mangula kama makamu mwenyekiti bara.
Ukiutazama mkutano ,kwa ujumla ulijaa mizengwe na kutegeana sana.
Manazi wa kambi za Lowasa na Membe walionekana kuonyeshana ubabe bila kificho.

KUbadilika kwa taratibu za uchaguzi katika dakika ya mwisho kulionekana wazi kabisa kama mkakati wa kukabiliana na kundi lililokuwa linadai Kikwete apunzishwe katika nafasi na ichukuliwe na mtu mwingine.
Hapa ni wazi kuwa kundi la Lowasa lilikuwa linataka kufanya jaribio kama lile lililomuonodoa Thabo Mbeki.

Ndipo ukawekwa utaratibu wa kura kwa maeneo ili ijulikane 'wakorofi' wanatoka eneo gani.
Matokeo ya jambo hilo ni kuwa kura za Mwenyekiti, makamu zilikuwa ni asilimia 100.
Maana yake ni kuwa hakuna aliyetaka kuchukua risk kwani viongozi wa makundi wanajulikana, kilichokuwa kinatafutwa ni nani 'specific''

Kwa upande wa kura za NEC, hakuna chochote kipya zaidi ya kura za itifaki.
Fikiria mtu kama Jackson Msome ambaye ni mkuu wa Wilaya kwa sasa amewabwaga vigogo waliokuwa wanatumia 'chenji'!!!!

Msome amewahi kufanya kazi na Mangula ambaye sasa ni makamu mwenyekiti.
Uchaguzi wa Mangula ni kutaka kurudisha chama katika mstari.
Huku ni kuhangaika tu kwasababu msingi wa 'nyumba' ni mbovu sana sijui Mangula atafanya nini.

Jambo la kufikiria ni kuwa Mangula na JK hawaivi tangu wakati wa uchaguzi wa 2005.
Hata pale JK aliposhinda na kuwa Rais, Mangula alikuwa na ofisi Lumumba na JK akiwa na yake Upanga.
JK alihakikisha kuwa Mangula harudi kundini ndiyo maana alitumia mbinu hadi Mangula kushindwa na mtu asiyetarajiwa katika ngazi ya mkoa

Kwa mantiki hiyo mahusiano yatakuwa na mashaka na kinyongo.
Mangula anachukua umakamu akiwa na changamoto kuu mbili.

Kwanza kusafisha chama ambacho tayari kinamilikiwa na makundi hasa lile la mtandao.
Sijui atawezaje kuchukua hatua dhidi ya wana mtandao ambao JK bado ana deni lao.
Hicho ndicho kilichomshinda Msekwa, Mukama na Nape Nnauye.
Kwamba maamuzi magumu dhidi ya wahuni hayataafikiwa na JK.
Hapo Mangula amekatwa mkono mmoja tayari

Mkono wa Pili ni ule utakaohusu mambo mazito ambayo yanayowahusu washirika wake.
Tuhuma zote dhidi ya mkapa, Sumaye na wenzao hazitaweza kupata msukumo mbele ya Mangula.
Lazima atalazimika kuwalinda.

Kwamakundi yaliyopo sasa hivi, Mangula hataweza kuchukua hatua dhidi ya kundi moja akawa salama na kundi jingine.
Atakapochukua hatua dhidi ya EL, basi atalazimishwa achukue hatua dhidi ya BWM na Sumaye.
Mkono wa pili wa Mangula ''umekatwa''

Mngula itabidi afanye kazi na katibu mkuu atakayeteuliwa.
Kwa hali yoyote, JK hupenda kuwapendeza washirika wake.

Ni lazima katika safu ya uongozi kama katibu mkuu, na msaidizi bara mmoja atoke kundi la mtandao.
La sivyo basi katibu mwenezi anaweza kuwa miongoni mwao. Mangula atakuwa amepigwa brake!

Kikwazo cha mwisho ni kuwa, wajumbe wa NEC wapo pia wana mtandao.
Hawa watakuwa mwiba mkali katika maamuzi ndani ya vikao hasa vinavyohusu maamuzi magumu.
Mangula atakuwa na nguvu kidogo sana.

Kw aujumla, kurudi kwa Mangula hakutazuia anguko, kutaweza kupunguza kasi ya anguko, hatima ya yote ni anguko tu.
Sijui ni kwanini Mangula amejitoa mhanga kukarabati paa la nyumba inayoanguka akijua wazi tatizo si paa tatizo ni msingi.

Duru matukio itaendelea kuangaza nini kimejiri Dodoma na watu watarajie nini

Tusemezane
 
HALI TETE MASHARIKI YA KATI.

Israel imefanya mashambulizi maeneo ya Gaza siku ya jumatano na kumuua kiongozi mmoja wa kijeshi wa Hamas, Ahmed Jabar, pamoja na watu wengine 10.

Baada ya tukio ilo serikali ya Misri imemtimua balozi wa Israel nchini Misri na kumuita nyumbani balozi wake aliyeko nchini Israel.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekutana jana mjini New York kujadili suala hilo.
 
ISRAEL YAENDELEZA MASHAMBULIZI UKANDA WA GAZA.

Milipuko imeendelea usiku kucha katika eneo la Gaza, huku Israel ikiimarisha mashambulio yake dhidi ya kundi la wanamgambo wa Palestina, Hamas.
Wakaazi wa mjini wa Gaza, wanaripoti kusikia milipuko mikubwa leo alfajiri.

Mkaazi mmoja mjini Gaza ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Raji Sourani, anasema umekuwa usiku mgumu mno kwa raia wengi kutokana na mashambulio hayo.
Israel inasema imelenga zaidi ya shabaha mia tatu thelathini usiku wa kuamkia leo.
Pia imesema wanamgambo hao wa Palestina wamefyatua zaidi ya makombora kumi nchini Israel.
Serikali ya Israeli imetoa idhini kwa jeshi nchini humo kuwaita wanajeshi elfu thelathini wa ziada, huku kukiwepo uvumi kuwa huenda shambulio la ardhini dhidi ya Gaza linapangwa.
israel-gaza-conflict-bombing-ap_606.jpg


gaza-attacks-ap-670.jpg


nov-15-2012-israel-gaza-under-attack-pillar-cloud-view_1352977547.jpg


gaza-attack.jpg


20121111152620252128_8.jpg


Gaza-1-articleLarge.jpg
 
HALI YA WASI WASI MASHARIKI YA KATI

Siku chache zilizopita Israel ilimuua kamanda wa kikosi cha Kundi la HAMAS.
Kwa kipindi cha miezi kadhaa hali ilitulia na shambulio hilo limezua taharuki katika siasa za ulimwengu.

HAMAS wanajibu mpigo kwa kutumia maroketi yao ya Alqasam na Katushi. Makombora hayo hayana shabaha na huangukia popote ili mradi iwe ndani ya Israel. Jambo hilo linailazimu Israel iwaite askari wa akiba kwa shambulio la ardhini.

Kwa hali yoyote kutakuwa na maafa makubwa sana kwa Wapalestina waishio Gaza ambao ni takribani milioni 2 katika eneo dogo sana wakiwa wamezungukwa na Israel kila upande.

Licha ya kuwa walidhoofishwa sana kwa kufungiwa bila kuwasiliana na upande mwingine wa Palestina au dunia, HAMAS hawana silaha za kisasa kama zile za Israel, kwa hiyo twaweza kusema ni kushambuliwa na wala si mapigano.

Israel kama kawaida yake inasema ina haki ya kujilinda. Kisichojulikana ni kuwa haki ya kujilinda ni pamoja na mauaji yasiyo ya lazima au ni kujilinda inaposhambuliwa.

Kauli hii imekuwa inatumika sana na Israel ili kuhalalisha ''unyama'' dhidi ya binadamu wengine.
Kwamba mtoto wa gaza ana tofuati na wa Tel Aviv katika haki za kibinadamu.

Shauri limefikishwa baraza la usalama la umoja wa mataifa. Kama inavyotarajiwa Marekani itasimama na Israel hata katika uovu. Hakuna matarajio kuwa kuna lolote la maana kutoka UNSC(United Nation security council)

Ni kutokana na hayo Iran yenye mgogoro wa silaha za Nyuklia na inayotishia uhai wa Israel inaingia kasi katika mzozo. Huku upande wa Pili, Muslim Brotherhood wanaoongoza Egypt wakiwa tayari wameshasema kuwa watasimama na Wapalestina.

EU inaonekana kukaa kimya ingawa kuna habari za wao kuchoshwa na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israel kwa mgongo wa kujilinda.

Bei za mafuta zimeanza kupanda kufuatia hali tete. Hili litaongeza machungu katika uchumi wa dunia ambao upo katika hati hati ya kurudi katika mdororo. Nchi za Ulaya GDP inaonekana kurudi nyuma kama ilivyo kwa Japan na Asia yote.

Marekani kuna mzozo wa kiuchumi 'fiscal cliff'' unaotishia kuirudisha nchi katika mdororo wa uchumi kama hakutakuwa na jibu ifikapo January 2013. Majadiliano ya Democrat na Republican yanaonekana kuwa magumu kwa pande zote.
Inapotokea hali kama ilivyo mashariki ya kati basi si usalama tu hata hali ya uchumi wa dunia inayumba sana.

Tukiangalia hali ya usalama wa taifa la Israel, ni wazi kuwa Arab spring imebadilisha ramani nzima kwa Hasi na Chanya.
Kwa upande hasi (positive), Syria ipo kwaika mgogoro wa ndani wa kumuondoa Hasad na mapigano ni makubwa.
Ikumbukwe kuwa Israel inakalia milima ya Golan ambayo ni sehemu ya Syria.

Israel inaiogopa Syria pengine kuliko taifa lingine linalokaribiana nao. Woga si kutokana na silaha bali umahiri wa Wasyria katika vita(worriers). Uwepo wa mgogoro ndani ya Syria unapunguza tension kwa upande wa Israel.

Upande hasi (Negative) ni uwepo wa serikali ya kati na kati (moderate) Islamic government kule Tunisia ambako Israel ina mpaka upande wa kusini. Haieleweki hawa moderate wataendelea kuwa moderate au hali inaweza kuwasukuma na kuwa extremist kama walivyo Brotherhood ingawa inaonekana wamevaa joho la moderate Islamic group.

Brotherhood wa Egypt wamekuwa wakiona huruma na ni washirika wazuri wa HAMAS sasa wanataka kitu kifanyike(something must be done).
Tatizo si la mpaka na Egypt kwasasababu makubaliano ya Camp David yatabaki kuheshimiwa.

Mchango mkubwa sana wa Brotherhood ni kuwa chimbuko la fikra katika mashiriki ya kati na haitachukua muda suala hili litachukua sura tofauti kabisa kuhusisha nchi za jirani kama Saudia na Jordan.

Jordan ipo katika kipindi cha mageuzi huku watu wengine wakitaka Mfalme Abdullah aondoke kama Mubarak.
Jordan ni kipenzi cha Magharibi na kuondoka kwa Abdullah kunaweza kuwaweka wenye msimamo tofauti na sasa.
Hapa napo Israel ina changamoto nyingine.

Na jirani kabisa kusini mwa Lebanon kuna Hizbullah chini ya Sheikh Hassan Nasrallah.
Huyu ni wa madhehu ya Shia yanayoungwa mkono sana na Iran. Ingawa anaweza asiingie katika mzozo moja kwa moja, uwezekano wa yeye kutumiwa na Iran ni mkubwa sana. Tunakumbuka jinsi Hizboullah walivyosimama kidete na Israel.

Ingawa Israel chini ya B.Netanyahu wanataka kufanya mambo kadri wajuavyo na pengine kutokubaliana na Obama, ni lazima waiangalie jiografia, mwenendo wa kisiasa na kiuchumi wa dunia hasa mashariki ya kati.

Mara zote Obama amekuwa akiwaonya kuwa dunia inabadilika na muda wa kutumia makombora kama sehemu ya ulinzi unafikia tamati. Amewaonya kuhusu mabadiliko yanayoendelea kutokea mashariki ya kati na kwamba inaweza kufika mahali kusiwe na njia nyingine ya kuwahami.

Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanonya kuwa kitendo cha Iran kulishupalia jambo hili haraka kina maana zaidi ya inavyofikiriwa. Inaweza kuwa ni mkakati wa kuwavuta Waisrael kuingia katika vita nao katika wakati huu ambapo jiografia ya mashariki ya kati haitoi nafasi kama ile ya 1967 au 1973.

Duru matukio itaendelea kufuatilia hali ilivyo kadri twendavyo mbele.
 
-Mashambulizi ya Israel yanatoa mwanya kwa Muslim Brotherhood kuhalalisha 'Extremism' sasa.In fact mashambulizi haya yatakua mna madhara zaidi kwa utawala wa Benjamin Netanyahu na pia relation ya Israel na Egypt most probably it will suffer a setback.

-Naona hapa Iran itatumia Mwanya huo kuikomoa Israel kwa kusambaza silaha nzito hasa Tanks za kurusha Makombora ya masafa mafupi na Marefu.

-On the other hand Bashar Al Asad wa syria atapata Mwanya wa kufanya severe casuality kwa waasi na Attention itakua mgogoro wa Israel na Palestine in the coming days kama mambo hayatatutliwa mapema

-Naona huko baadae Egyptians wanaweza kurudi Tahrir Square kushinikiza Serikali yao kuchukua msimamo ambao pengine akina Morsi wasingependa mapema kiasi hiki juu ya kuchukua hatua dhidi ya maslahi ya Israel kinyume hata na mkataba wa Camp David
 
-Mashambulizi ya Israel yanatoa mwanya kwa Muslim Brotherhood kuhalalisha 'Extremism' sasa.In fact mashambulizi haya yatakua mna madhara zaidi kwa utawala wa Benjamin Netanyahu na pia relation ya Israel na Egypt most probably it will suffer a setback.

-Naona hapa Iran itatumia Mwanya huo kuikomoa Israel kwa kusambaza silaha nzito hasa Tanks za kurusha Makombora ya masafa mafupi na Marefu.

-On the other hand Bashar Al Asad wa syria atapata Mwanya wa kufanya severe casuality kwa waasi na Attention itakua mgogoro wa Israel na Palestine in the coming days kama mambo hayatatutliwa mapema

-Naona huko baadae Egyptians wanaweza kurudi Tahrir Square kushinikiza Serikali yao kuchukua msimamo ambao pengine akina Morsi wasingependa mapema kiasi hiki juu ya kuchukua hatua dhidi ya maslahi ya Israel kinyume hata na mkataba wa Camp David
Shukran Ben, siyo tu kuwa mzozo utaondoa attention Syria bali pia Iran ambako mgogoro wa Nuke bado ni mbichi na unafukuta.

Inaelezwa na wachambuzi wa mambo ya kisiasa kuwa shambulio hilililiandaliwa na Israel ili kumjenga Netanyahu kisiasa.
Mwezi January wana uchaguzi na hivyo anakabiliwa na upinzani kutoka kwa waziri wake wa mambo ya nje.
Njia hii ni kutaka kumpiku kwa kuonyesha ubabe dhidi ya Gaza.

Jambo moja ambalo watu wengi sana wanalisahau ni kuwa mzozo huu wa siku tano sasa haukuanzishwa na HAMAS.
Umeanzishwa na Israel kwa kumuua kamanda wa kikosi cha anga cha HAMAS.
Sidhani kuwa kuna kikundi kingevumilia hali hiyo tena mauaji yalikuwa ''collective punishment' kwa yoyote aliyekuwa ndani ya jengo hilo.

Vyombo vya habari vimeshupalia kuwa HAMAS inamwaga maroketi na Israel ina haki ya kujilinda.
Huo si ukweli ni propaganda za Israel ambayo kwa namna fulani imepewa haki dhidi ya wanadamu wengine.

Kauli ya Rais Obama kuwa Israel ina haki ya kujilinda kutokana na mashambulio ni ''standard statement' ambayo inatumika iwe ndani ya senate, Congress au kwingineko. Hapo ndipo nguvu ya Waisrael katika Marekani inaonekana.

Ukweli ni kuwa Israel haina uwezo kiasi kinachodhaniwa bila mgongo wa Marekani.
Kinachotokea ni kuwa Waisrael wamejipenyeza sana katika vyombo muhimu kule Marekani na ndio wanaotoa kauli.

Kwakuwa ndio wanamiliki media, ukisikiliza CNN au Channel yoyote utasikia kuhusu maroketi ya HAMAS. Hutasikia nini kilianza hadi maroketi yakaanza kurushwa. Nani alianza uchokozi.

Tatizo linakuja pale Israel itakapovutika na kuingia katika mzozo na Iran. Kwasasa Iran inaonekana kuwa super power katika mashariki ya kati licha ya kudhoofika sana kiuchumi. Wao wana kundi la SHIA ambalo ni sehemu kubwa tu ya mideast.

Huko nyuma kulikuwa na tension kati ya Turkey na Israel hasa baada ya Flotila kushambuliwa.
Ukiiangalia jiografia kwa umakini Israel ipo katika mazingira yanayohitaji amani zaidi ya vita.
Ule ubabe wa piga piga utawaletea matatizo makubwa. Kizazi kilichopo ni tofauti na kile cha akina Gamal Abdul Nasar n.k.

Kibaya zaidi ni kuwa Brotherhood wenye ushawishi wa hali ya juu katika siasa za mashariki ya kati ndio wanaongoza Egypt yenye ushawishi mkubwa kama nchi. Hapo Camp David accord ipo lakini njia panda.

Jambo lingine ambalo watu pia hulisahau ni kuwa Gaza ni refugee camp. Hakuna kiingiacho Gaza bila kupitia Israel.
Inashangaza hata hizo Qasam na katushi wanapata wapi malighafi maana wamezungukwa kila kona.

Si sahihi kusema mapigano kati ya Israel na Palestine, ni mapigo ya Israel kwa Palestine kwasababu huwezi ukawa na laiser giuded missile kukabiliana na mtu mwenye jiwe!

Katika zaidi ya miaka 4 wakazi wa gaza wamelazimika kupunguza hata milo kwasababu ya ukosefu wa chakula na madawa kwa wagonjwa. Israel inazuia kila aina ya msaada.
In other words haya ni mauji ya kimya kimya!(cold masacre) na dunia haionekani kushtuka.

Dunia ina double standard kubwa sana. Israel imekaidi maazimio ya UN mengi tu na hakuna kinachotokea.
Hayo yakitokea akina Taylor na wenzake wapo the Hague.Hii si halalishi uhuni wa mauaji yoyote, ninachotaka kuonyesha hapa ni kuwa kuna stanadard za dunia kulingana na matakwa ya wakubwa na si makubaliano au taratibu

Nakumbuka enzi hizo ungewasikia akina Jose Broz Tito, Olf Palme, Indira Gandhi, Nyerere kwa uchache japo wakipaza sauti na kusema hivi si sahihi.
Leo nani aseme, kila mtu anataka kwenda shopping washington!
 
Ben Saanane, Nguruvi3, Ngongo,
Mpaka sasa hivi Wapelestina 94 wameishauawawa kwenye mashambulizi hayo ya siku sita. Kuna wasiwasi hivi sasa Hamas imepata kuungwa mkono na mataifa ya kiarabu tofauti na hapo mwanzo.

Mataifa ya kiarabu yameisemea wazi Israel wameitaka kusitisha mashambulizi. Na kuondolewa kwa vizuizi viliyowekwa na Israel mwaka 2006.

Waziri Mkuu wa Uturuki Racep Tayyip, ameitaja Israel kuwa taifa la ugaidi kutokana na mashambulizi hayo matamshi hayo yameashiria uhasama wa wazi kwa mshirika huyo wa zamani wa Uturuki.

Waziri wa mambo ya kigeni William Hague, ameionya Israel watakosa uungwaji mkono na Uingereza kwenyewe kutokana ukandamizaji wanaowafanyia Palestina.
 
HALI YA MAMBO MASHARIKI YA KATI

Tumeshuhudia kurudi tena kwa wananchi wa Egypt pale Tahariri square.
Hali imefuatia tamko la Rais Morsi kuhusu kuchukua madaraka makubwa ya nchi ya Misri.

Ieleweke kuwa tangu enzi za Mubarak, Misri imekuwa ina vyombo vikuu vitatu vya maamuzi ambavyo ni Executive branch(utawala), Mahakama(Judicial system) na tawi la jeshi (Miltary wing).
Kuanzia zama za hizo matawi haya yamekuwa na nguvu na msuguano usiokwisha.

Hosni Mubarak alifanikiwa kuyatawala matawi haya kwa kuweka watu wake na ilionekana kana kwamba kila maamuzi yalikuwa ya pamoja. Kwa msingi huo tukawaona akina Jenerali Tantawi wakiwa na madaraka makubwa tu licha ya kuwa ni wanajeshi. Hata katika kipindi cha mageuzi jeshi lilikuwa na nguvu sana.

Tukumbuke pia ya kuwa Misri nayo ipo katika mchakato wa kuunda katiba mpya ya kudumu, mambo yaliyomwondoa Madarakani Mubarak kwasababu alitawala kiimla(Authoritarian)

Morsi aliposhika madaraka jambo la kwanza lilikuwa kuwapunzisha kazi akina Tantawi na mabaki mengine ya Mubarak. Mabaki hayo pia yapo katika mfumo wa sheria na kwingine.
Kwa ujumla wale wafuasi wa Mubarak bado walikuwa wanashikilia vitengo muhimu na hawaridhishwi na mabadiliko yaliyotokea.

Kuna habari kuwa wafuasi wa mubarak walitaka kuzuia mchakato wa katiba.
Hii maana yake ni wao kuendelea na maisha waliyozoea kuanzia enzi za Mubarak.
Ujio wa katiba mpya ungehatarisha sana masilahi yao. Kwahiyo walitaka ku-frustrate the whole process of reform.
Hiki ndicho kilipelekea Morsi kuchukua madaraka yote pengine aweze kusimamia vema mageuzi bila kuwa na kizuizi.

Kwa hakika hicho ndicho Muslim brotherhood wanachokitaka.
Lakini pia nyuma ya pazia kuna mambo mengine yanatia wasi wasi.
Zipo habari kuwa Brotherhood wanataka kutekeleza ajenda yao ya kuibadilisha Misri na kuwa taifa la kiislam kwa kupitia mabadiliko ya katiba.

Wasi wasi wa mambo hayo mawili ndio unaifanya nchi igawanyike, wengine wakihofia Morsi kujichukulia madaraka yasiyohojiwa na chombo chochote cha sheria na wengine wakihofia nchi kuingia katika Islamization.
Hicho ndicho kiini cha mzozo uliopo kwa sasa, yaani kutoaminiana.

Kwa upande mwingine Morsi amejizolea sifa ya kuwa moderator wa usuluhishi kati ya HAMAS na Israel.
Nchi za magharibi zilianza kuwa na imani kuwa usalama wa mashariki ya kati utaleta tumaini jema.
Kwamba ,Morsi kuendeleza kazi ya Misri kama mpatanishi hasa kwa mzozo wa Palestina na Israel ilikuwa ni muhimu sana.

Waziri Hillary Clinton alimsifia kwa jitihada zake zilizopelekea kupatikana kwa suluhu ya mzozo.
Kwa upande mwingine usuluhishi wa Morsi umepokewa kwa mashaka sana na nchi kama Israel.
Kwa mara ya kwanza makombora ya HAMAS yalifanikiwa kufika katika miji ya Tel Aviv na Jurasalem

Hii maana yake ni kuwa HAMAS wamepata sophiscated technology kutoka Iran kwa kupitia mpaka wa Israel na Misri.
Inaonekana kuwa HAMAS ambao ni washiriki wazuri wa Brotherhood sasa wamefanikiwa kupata 'uchochoro' wa silaha.
Hali hii inaitia Israel wasi wasi wa hali ya juu kwani idadi ya wapinzani inazidi kuongezeka na pengine hata Camp David accord ipo mashakani.

Kuchafuka kwa hali ya kisiasa mashariki ya kati hasa Misri kunatishia sana amani ya eneo hilo.
Kama tulivyoeleza huko nyuma kuhusu umuhimu wa Misri mashariki ya kati, bado hoja zinabaki zile zile kuwa ujio wa Muslim Brotherhood ni wa kitaalam na kiufundi sana.

Brotherhood hawana hamaki na ni wastahamilivu sana. Imewachukua miongo kadhaa ya kujijenga kabla ya kutwaa dola.
Ni kundi la wasomi wanaoilewa dunia vema tena wasomi waliobobea katika fani zote za elimu ya dunia hii.

Endapo Morsi anataka kuleta mabadiliko hasa ya kisiasa kwa kujitwalia madaraka ili kuwapiku wapinzani wake au anataka kufanya hivyo ili kuingiza agenda ya Brotherhood, that remain to be seen.

Tusemezane
 
HALI BADO NI TETE MASHARIKI YA KATI

Baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na HAMAS, hali imegeuka kuwa tete kwa msuluhushi Misri chini ya Rais Morsi wa chama cha Brotherhood.
Kabla hatujajadili ya Misri kuna tukio lingine kubwa limeihusisha Israel na Palestina.

Kwa takribani miongo kadhaa Palestina imekuwa mwanachama wa UN kwa hadhi ya non-member observer yaani mshiriki asiye mwanachama. Wiki hii baraza la umoja wa mataifa limepiga kura kuhusu kupewa uanachama kamili.
Kura hizo zimetoa matokeo ambayo Rais Obama aliwahi kuwaonya Waisrael.

Obama aliwahi kusema, jitihada za Palestina katika kutafuta uanachama zinaungwa mkono na kundi nyuma yake na hivyo Israel itambue kuwa muda wa military supremacy unakwisha na Diplomacy lazima iwe complimented na military power.

Hakika wanachama 138 walipigia kura wakitaka Palestina iwe mwanachama, nchi 41 zikiwa hazikupiga kura na nchi chache sana zikiongozwa na Marekanni na Canada zikipinga.

Ingawamatokeo haya huenda yasibadilishe mambo sana, lakini kuna ujumbe muhimu sana umepelekwa kwa Israel.

1. Nchi kama Italia na Ufaransa zimepiga kura kwa upande wa Palestina. Hawa ni washirika wa Israel wa muda mrefu sana. Nchi zilizokataa kupiga kura bado zinapeleka ujumbe ule ule kuwa hazipendezwi na hali ilivyo mashariki ya kati na zimejiondoa katika utetezi kwa Israel bila kuwaudhi.

2. Palestina sasa watatambulika kama taifa kwa kuzingatia mipaka ya West Bank, Gaza strip na East Jerusalem.
Hili nalo lina ujumbe kuwa Israel lazima ikubali kuwa Jerusalem ni sehemu ya Wapalestina japo upande wa Mashariki.

3. Palestina sasa wana haki ya kujiunga na taasisi za UN kama International court n.k.

4. Na Palestina watakuwa na uhuru wa kumiliki majeshi kama taifa jingine.

Ingawa Israel ime react kwa kupanua ujenzi wa nyumba kule Jerusalam Mashariki na kuzui kodi ya Palestina, hatua hiyo inazidi kuwafanya waonekane wana kiburi na dheeru.

Imekuwa hivyo miongo kadhaa na kuendelea kufanya hivyo ni kuendelea kujitenga na dunia hii.
Kwa maneno mengine upinzani dhidi ya Israel unazidi kuongezeka.

Hatutarajii mabadiliko ya haraka kutokana na tukio hilo, inatosha tu kusema kuwa hali ya mashariki ya kati inachukua sura mpya kila uchao. Sura mpya si kwa Israel na Palestina tu, hata Misri ambako hamkani si shwari kabisa.

Huko Misri, baada ya rais Morsi kujitwalia madaraka hasa ya rais kutohojiwa na chombo chochote cha sheria, maandamano yameanza tena. Safari hii ni kati ya wapinga mabadiliko na wanaounga mkono mabadiliko.

Wanachama wa Bortherhood wamezuia majaji wa mahakamu kuu kutoingia ofisini kwa madai kuwa wengi wao ni mabaki ya Mubarak na watapinga mabadiliko kwa njia za sheria.
Hayo yakitokea mahakama kuu imeahirisha kusikiliza masuala yote kama sehemu ya mgomo kutokana na hali iliyopo.

Muslim Brotherhood nao wameendelea na kuandika rasimu ya katiba mpya kwa misingi ya sheria.
Katika bandiko lililopita tulisema kuwa mzozo huu ni kati ya Brothehood na wale wanaoona nchi inaingia katika sharia.
Haionekani kama rais Morsi atarudi nyuma katika maamuzi yake.

Challenge kubwa aliyo nayo Morsi ni kuwa uwepo wake madarakani ni kwa msaada wa Brotherhood.
Kama tulivyowahi kusema huko nyuma hili ni kundi la watu waliobobea sana katika elimu zote za dunia na akhera.
Ni kundi lenye ushawishi na hufanya mambo kwa mipango sana.
Ni ngumu sana kwa Morsi kukabiliana au kupingana na hoja zao.

Kwa nchi kama Misri yenye wasomi wengi jambo kama hilo analotaka kulifanya Morsi huenda likamletea matatizo.
Kwanza ana uhasimu na mabaki ya Mubarak ambayo hakuweza kuyaondoa yote

Pili, anakabiliana na kundi la wasomi kama wanasheria na wananchi wengine wasiopendelea Misri iingie katika sharia za dini. Makundi haya yana nguvu sana na mengine yanasaidiwa na nchi za nje.

Nchi za magharibi hazingependa kuona taifa lenye ushawishi mkubwa wa siasa za mashariki ya kati likigeuka kuwa la sharia za kiislam.

Hilo litakuwa ni kosa kwa upande wa nchi hizo kwa kutambua kuwa Misri ni mama wa dunia kama anavyojulikana mashariki ya kati ''umul dunia'' kwahiyo yaweza kuambukiza mataifa mengine ya kiarabu.

Lakini muhimu ni kuwa usalama wa Israel utakuwa mashakani sana kwani makundi yote yeynye itikadi kali yataweza kuazima kitabu kutoka Misri na huenda mashariki ya kati ikabadilika kabisa kwa muda mfupi na usiotarajiwa.
Kuna makundi kama Hakhan, Izboullah, Hamas na mengine yasiyo na majina yanayosubiri tu '' kipenga kilie''

Kwa muktadha huo survival ya Morsi itakuwa na wakati mgumu sana na kuifanya mashariki ya kati kuwa tete kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita. Mzozo wa Misri bado ni mbichi sana kujua hatima yake kwa sasa.

Tutaendelea kufuatilia na kuwajulisha kinachojiri.

Tusemezane
 
DURU MCHANGANYIKO (MAREKANI, EGYPT NA TANZANIA)

Wiki hii aliyetarajiwa kumrithi Hillary Clinton kama secretary of state bi Susan Rice ameondoa jina lake katika kufikiriwa kwa nafasi hiyo. Bi Rice alikumbuna na kikwazo cha Republican ambao walimkomalia kutokana na tatizo la Benghazi ambapo bi Rice alisema halikuwa la kigaidi na lilisababishwa na filamu ndani ya U-tube na kisha kubadili kauli tena

Bi Rice ambaye ni balozi wa Marekani UN amekubali yaishe pengine kumwezesha Rais Obama kuteua mtu mwingine.
Habari zilizopo ni kuwa John Kerry aliyekuwa mgombea na G.Bush mwaka 2004 na ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje ndiye atakayerithi mikoba ya Hillary Clinton.

Bi Clinton anaachia ngazi kama sehemu ya maandalizi ya 2016. Kujiuzulu nafasi hiyo kutamwezesha kujikita katika ujenzi wa timu ya ushindi na wakati huo huo kumwepusha na matatizo yanayoweza kujitokeza katika kipindi cha sasa hadi 2016.

Endapo John Kerry atapata nafasi hiyo ambayo hakuna shaka atathibitishwa bila kikwazo na seneti, kutakuwa na uteuzi wa senata kutoka Massachussets kabla ya uchaguzi. Nafasi hiyo ya useneta ni muhimu sana kwa Democrat ndani ya seneti. Zipo fufunu kuwa Obama itabidi alibadili baraza lake la mawaziri na pengine kumshirikisha seneta mmoja wa Republican katika nafasi kama alivyowahi kufanya kwa Robert G.

EGYPT
Hali bado ni ya mashaka hata pale Rais Morsi alipoondoa kauli zake zilziozua mtafaruku. Wakati hayo yakiendelea rasimu ya katiba mpya ambayo imeandikwa kwa matakwa ya Brotherood imepigiwa kura ya awali. Inaonekana kuwa kura za maoni zimekubaliana na rasimu hiyo kwa ushindi wa asilimia 56. Duru la pili litafanyika baada ya wiki moja.

Kama tulivyowahi kuwachambua hawa Brotherhood sasa wameanza kutoa makucha yao rasmi. Kikwazo wanachokumbana nacho ni jinsi wa Egypt ambao wengi wanapenda modern life wasivyoafikiana nao. Lakini pia Brotherhood wanasahau kuwa katika nchi ya Misri wapo watu wa imani zingine na kuifanya kama taifa la kiislam ni kukaribisha matatizo zaidi.

Utete wa hali ya mambo nchini Misri unakwenda mbali zaidi na kuathiri mataifa ya kiarabu. Misiri ni kiungo muhimu sana katika amani ya mashariki ya kati, hivyo kuchukua sura ya udini ni hofu kwa mataifa jirani,magharibi na Israel kwa ujumla.

Kitu cha kushangaza ni kuona madhehebu ya Salhafi yameunga mkono Brtherhood.
Tofauti ya makundi haya mawili ni kuwa brotherhood ni wasomi na wanafanya mambo yao kisomi sana hata kama mtu hakubaliani nao.

Salhafi ni wahafidhina wanaotaka kuishi maisha ya karne kama 10 zilizopita.
Salhafi hawana uvumilivu na ni wazi kuwa mbele ya safari hawaweza kuafikiana na Brotherhood, tatizo hilo ni kiporo !!

TANZANIA
Habari kubwa ni ile ya wanachama wa CHADEMA baadhi yao kumtaka Dr Slaa ajiuzulu kufuatia tuhuma kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa. Hoja hiyo ilitumbukizwa katika mitandao na Nape Nnauye na imeonekana kuleta madhara kisiasa.

Tuhuma za Nape ukiziangalia kwa namna yoyote hazina mantiki. Ukizingalia kwa kutumia sheria ya msajili wa vyama, katiba ya CCM na akili za kwaida za kibinadamu.
Hata hivyo kwa kutumia udhaifu uliojijenga kwa muda sasa hali inaonekana kuwa na madhara kisiasa.

Ukweli unabaki kuwa pamoja na tuhuma hizo za kubumba, haikutarajiwa wana CDM hasa vijana kubabika hadi kufikia kumtaka katibu mkuu wa chama ajiuzulu.
Nyuma ya kundi la vijana hao kuna nguvu kubwa sana kisiasa inayotokana na mnyukano wa kugombea madaraka.

Kila mara linapotekea jambo BAVICHA imekuwa katikati ya tatizo. Safari hii makamu mwenyekiti akihusishwa rasmi achilia mbali wajumbe wengine waliojitokeza hadharani.

Kuna habari kuwa kundi linalojinasibu kuwa la vijana likisimamiwa na kiongozi mshauri wa chama na mwezake mwanadamizi wamekuwa msaada mkubwa kwa kundi hili la ''waasi''

Waasi hao wanasaidiwa sana na mtu ndani ya CDM anayejulikana kwa jina la Tuntemekee. Kwa uchache naweza kusema kuna viongozi wakuu 4 wanaotumika ndani ya CDM. Wote hao wamekuwa na mkakati wa kupiga pande mbili kwa mwenyekiti na katibu mkuu na kati yao makamu mwenyekiti BAVICHA anatumika sana.

Tatizo la CDM ni kuwa wazito sana katika kuzuia madhara hadi pale yatakapoleta madhara. Tumeliona Arusha, Mwanza, BAVICHA na katika uongozi wa taifa.

Hili suala la kadi Dr Slaa ambaye ni mtuhumiwa hakupaswa kuliongelea bali kulitolea ufafanunuzi.
Yupo Mwenyekiti, makamu mwenyekiti, naibu katibu mkuu, mwenyekiti BAVICHA n.k ambao walipaswa kusimama na kulielezea vema.

Wote hao wamekaa kimya kana kwamba kila mmoja anasema halimhusu. Sasa team work na collective responsibility ipo wapi? Kwanini chama kiwe Slaa kila mahali?Mbona suala lenyewe ni jepesi sana na linaweza kujibiwa kirahisi tu.
Ni jepesi kwa wenye kufikiri, sijui kama huko vijiweni ni rahisi pia.

Sasa hivi tunasikia kila mkoa ukitoa kauli kuhusiana na mzozo. Nadhani badala ya umoja wa vijana wa kila mkoa kuto kauli, ingetolewa na mwenyekiti wa BAVICHA na kuungwa mkono na wengine na si kufanya kazi kama separate units.

Jambo linalotia hofu mustakabali wa CDM ni kuona ule utamaduni wa kuogopana uliopo ndani ya CCM sasa umehamia huko. Kumbu kumbu zinaonyesha kuwa CDM ilipata umaarufu baada ya kuchukua hatua kali hata kama kufanya hivyo kulionekana kudhoofisha chama.

Kundi la Kafulila lilitimuliwa na bado CDM ipo na nguvu tena mara kumi zaidi.
Hakuna aliyedhani kuwa Kafulila alikuwa na nguvu zaidi kuliko chama. Madiwani walitimuliwa na hata wenyeviti wa mitaa.
Inashindikanaje kuwaondoa waasi na vigogo wao ili waende mahali wanako dhani chama ni mtu na si watu?

CDM haiweze kukabiliana na chama tawala katika udhaifu ulioonekana. Sasa hivi kampeni zote za kuimarisha chama zimebaki solo huku tukisikia Sangara, M4C na sasa Join the chain. Ukiona makundi namna hiyo ujue lipo tatizo.

CDM lazima waangalie kuna nini ndani ya BAVICHA na wataendelea kuwalea wahalifu hadi lini?
Ni kwanini kuna watu wanaogopwa ndani ya CDM kuliko chama chenyewe?

Hoja iliyopo si Nape Nnauye ni udhaifu unaotumiwa na Nape kama ule uliotaka kutumiwa na Kafulila kuhusu ukabila.
Bila chadema kusimama na kuchukua hatua kali za kusafisha nyumba yake, mipango yote na mikakati inaweza kuishia katika makabrasha nakurudi kule kwa TLP, NCC,CUF n.k.

katika duru matukio, wiki hii tutazijadili kauli za viongozi wa CDM kama kiashirio cha mzozo mkali ndani ya chama.
Tutaangalia udhaifu wa kila kiongozi bila kumuonea au kumpendeza.
Tutaangalia kiini na chanzo cha tatizo la BAVICHA

Tutaendelea.
 
MGOGORO WA CHADEMA

Wanajamvi na washiriki wa duru za siasa (1,2). Kutokana na mtifuano unaoendelea ndani ya Chadema, kesho tutawaletea nyuzi zote za nyuma zilizo onya kuhusu mtafaruku ndani ya CDM na ushauri wa kipi kifanyike halafu uchambuzi wa kina juu ya gogoro hili zito.

Tutabandika zote hapa Duru za siasa na kuzifanyia tathmini kikamilifu.
 
Nguruvi3, Ritz, Jasusi, Ben Saanane,

..hii ni thread endelevu.

..lakini hebu tupia jicho eneo la maziwa makuu hapa Afrika na mgogoro wa Congo.

..nimesikia mcheza sinema Ben Afleck ameanza kuuvalia njuga huu mgogoro na amekwenda kwenye US congress ku-testify.

..kuna uwezekano wa-Marekani wakachanga karata zao upya na kuja na msimamo tofauti na waliokuwa nao huko zamani.

..jumuiya ya SADC nao wako mbioni kupeleka majeshi ya kulinda amani mashariki ya Congo. tanzania ndiyo itakuwa nchi kiongozi wa majeshi hayo.

..jeshi hilo linakwenda kufanya nini ikiwa tayari kuna majeshi ya UN?? je, vikosi vya SADC vitakuwa na "utaratibu tofauti" na vikosi vya UN katika suala zima la kulinda amani??

..CNN wameripoti kwamba wananchi wa Congo takriban milioni 5 wamepoteza maisha tangu mgogoro huo uanze.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

..habari moto-moto ni kwamba Raisi Obama "amemshauri" Raisi Kagame aache kutoa msaada wa aina yoyote ile kwa waasi wa M23.

.."ushauri" huo ulitolewa ktk mazungumzo ya simu baina ya viongozi hao wawili.

..vilevile US Treasury Dept imewa-blacklist viongozi wawili wa kikundi cha waasi wa M23.

..things r changing so fast and not in favor of Kagame and the rebel group M23.

NB:

..kitendo cha Tanzania kuongoza kikosi cha SADC cha kulinda amani Congo kitapokelewa namna na Rwanda na Uganda, na zaidi ndani ya EAC??
 
Last edited by a moderator:
MZOZO WA CONGO NA M23

Mkuu Joka kuu,
naona ume ni pre-empty maana nilikuwa naliangalia kwa ukaribu sana suala la DRC.
Suala hili lipo complicated na ni ngumu sana kusema kwa uhakika M23, Kagame na Museveni wanataka nini.

Niseme kuwa M23 inatokana na March 23 tarehe ya kuanzishwa kwa kundi hilo kama sehemu ya makubaliano ya kukamatwa kwa Laurent Nkunda aliyekuwa anasumbua kama wao.

M23 inaundwa na wanajeshi tena wa ngazi za juu sana. Mathalani kamanda Gen Sultan Makenga alikuwa katika mapinduzi ya Habyrimana na Mobutu.Sehemu kubwa ya M23 inaundwa na Watusi wa Rwanda.

Kwasasa kundi hilo linamiliki sehemu kubwa ya Congo mashariki inayopakana na nchi nyingi jirani na hivyo kudhibiti sehemu kubwa sana ya biashara kupitia mipaka.

Kwa ufupi kundi lililokuwa la Laurent Nkunda ndilo limejiegua na kuwa M23.
Uasi wao kwasasa una madai kuwa serikali ya Congo haikuwapatia wafuasi wao vyeo katika jeshi au kisiasa.

Kundi hili linaungwa mkono na Kagame kwa kila kitu kuanzia silaha, matibabu na logistic zote.
Ni heri basi Museveni amekiri kuwa kundi hilo lina makao Kampala kuliko Kagame anayedhani kuwa dunia inaweza kupumbazika kwa ulaghai wake.

Lengo la Kagame halijulikani kama ni Usalama, Uchumi au kijamii na kitamaduni katik kuuunga mkono M23.
Nikumbushe kuwa Kagame alilazimishwa kumkamata Nkunda na viongozi akina Obasanjo, Mkapa na Kofi Anan kule Nairobi.
Kagame alipewa ultimatum na hapo hakukuwa na ujanja tena.

Ilikuwa ni jambo gumu kutumia EAC kwasababu washiriki wa mzozo ndio hao hao wanachama.
Na hali ilivyo sasa hivi ndivyo ilivyokuwa kabla ya kukamatwa kwa Nkunda.

M23 ni Nkunda B na wanaoshiriki ni Kagame na Museveni. Museveni anashiriki kwasababu za kiuchumi.
Kagame siyo usalama kwasababu asilimia kubwa ni Watusi kwahiyo hakuwa na sababu ya kuwaogopa.

Kinachotokea ni kuwa Rwanda ina eneo dogo na kama ilivyokuwa kabla ya mauji, wao walikuwa na agenda ya Bahima Empire. Wanataka kuchukua Congo Mashariki ili kupunguza congestion kwa nchi yao.

Rwanda yenye population ya watu milioni 9 ni ndogo sana kuliko Tanzania yenye watu milioni 40 na eneo kubwa sana. Population density ya Rwanda ni zaidi ya kiwango cha kawaida cha kimataifa (people/sq km).

Na katika kuthibitisha hilo, wiki hii waasi wamekuja na madai ya kutaka kuigawa Congo ili kule wanakotawala iwe nchi inayojitegemea. Hapo watakuwa wametoa unafuu kwa Rwanda katika mambo kama ardhi na uchumi tukizingatia utajiri uliopo eneo hilo.

Ni kwa msingi huo suluhu haiwezi kupatikana Kagame akiwemo ndani ya EAC.
Congo imeamua kutumia SADC kama msuluhishi.

Pamoja na ukweli kuwa UN wana majeshi, bado blue Helmet za UN ni kwa kulinda amani na si combat operation na hivyo wana limitation katika kukabiliana na waasi ambao si waasi bali wavamizi wa kinyarwanda.

Tanzania inajikuta katika mzozo huo kwasababu kuu zifuatazo.
1. Congo stable ni muhimu sana kwa Tanzania historia isije kujirudia kubeba wakimbizi mamilioni kama ilivyokuwa wakati wa machafuko Rwanda na Burundi.

2. Kuruhu Wanyarwanda kujitwalia ardhi ni dalili za hatari sana kwa Tanzania inayopakana na Rwanda.
Pindi Congo mashariki itakapoangukia kwa watu hao mpaka wa Tanzania na Rwanda utakuwa eneo lote la ziwa ikiwa ni pamoja na eneo la mpaka wa sasa.
Hili litafanya usalama wa kuwa mgumu kwasababu hakuna ajuaye baada ya Congo nini kinafuata

3. Tanzania kwa sasa ni mwenyekiti wa usalama wa nchi za SADC. Hata kama Tanzania itakuwa katika EAC bado haiwezi kukwepa jukumu la SADC linalokwenda kwa mzunguko. Hivyo si sahihi kusema Tanzania imewasaliti washiriki wa EAC ingawa pia inapenda kuwa nje katika suala hili kwa vile haiwezi kujadiliana amani na yule asiyetaka amani kama Kagame

3. Tanzania inahitajika sana na SADC kwasababu ya jeshi. Hapa haina maana jeshi ni kubwa au lenye vifaa, ni kwasababu JWTZ wana uzoefu katika nchi za kigeni kama walivyowahi kufanya Mauritius, Comoro na pia katika kulinda amani kupitia UN kule Darfu, Liberia na Lebanon.

Muhimu zaidi ni kuwa JWTZ ndilo lililoisaidia Congo baada ya Mobutu kuondolewa. Nakumbuka mmoja wa washauri wa kijeshi alikuwa ni Brig Gen Ambrose Bayeke ambaye aliwahi kuwa kamanda wangu katika nyakati fulani za maisha wakati huo akiwa Brigedia chini ya Major Gen Maneno.

Kwa maana hiyo, jeshi la Tanzania linafahamu vema mazingira na hata infrastructure muhimu katika medani ya vita kule Congo.Pamoja na kuwepo kwa jeshi la UN, hili la SADC linaonekana kwenda katika combat mission na siyo kulinda amani.

Kagame amelifahamu hilo na sasa waasi wanapanga kuwa na mazungumzo na serikali wakipima upepo na hali halisi.
Wakati hayo yakiendelea, ndani ya bunge la Marekani kumepelekwa taarifa rasmi kuhusiana na mgogoro huo na ushiriki wa Kagame katika mzozo.

Hilo nalo linamweka Kagame katika wakati mgumu sana kwasababu CIA watakapoingia basi kibao kinaweza kugeuka.

Hizi nchi za magharibi zinaangalia masilahi zaidi kuliko urafiki au utu kama tunavyodhani.
Congo ni nchi kubwa sana Afrika na instability yake ni tishio kwa nchi za magharibi hasa wakati huu Mchina akiwa amejichimbia Zambia na Congo akichukua kila anachokutana nacho.

Tunaposema tishio hatuna maana kwa silaha,tunamaanisha tishio la usalama kiuchumi.
Kwa wenzetu usalama siyo silaha bali njia zote za uchumi, siasa na hata utamaduni.
Hivyo Congo ni muhimu sana na mzozo wake hautaachwa ufikie pale Rwanda ilipofikia

Mzozo huo ni mbichi kabisa na duru za siasa zitaufuatilia kwa karibu sana na kujulisha nini kinajiri.

Tusemezane
 
From our file- chadema


nguruvi3;4391174]mkuu jmushi1, zitto ni polarizing figure. Bila kujali ametendewa au amatenda dhambi ninasema kwa uhakika he is a polarizing figure.

Kama unafuatilia habari zake tangu 2010 amekuwa mtu wa utata sana hasa pale chama kinapoonekana kuimarika.
Sina maana anakihujumu, lakini utakumbuka operesheni sangara ilipopamba moto ni yeye aliyesababisha ikafifia.

Sasa suala la uenyekiti wa kamati ya bunge na urais vinatoka wapi?
Suala la wabunge wenzake kumpiga vita linatoka wapi?
Huko kwenye kamati nadiriki kusema hakuwa makini.
Haiwezekani awe mwenyekiti siku zote halafu baada ya kuvunjwa ndipo atoke na kusema kuna madudu.

Zitto bado anaamini kuwa kafulila alionewa na wala hajakanusha kauli za udini au ukabila kwasababu kafulila aliyetoa maneno machafu na mazito bado ni mshiriki mkubwa wa zzk, yeye alijotoa mhanga kwa aijili ya zzk.
Tamasha la kigoma ni mwendelezo wa falsafa ya ujana hata kama kufanya hivyo kutaleta madhara ndani ya chama

mh zzk anaamini kuwa yeye peke ni chadema na hivyo hahitaji timu ya chama.
Ukifuatailia utaona jinsi gani mwezi huu alivyoua m4c kwa hoja na mambo yanayoonyesha political immaturity nzuri tu.

jambo lolote linaloweza kuleta mtafaruku ndani ya chadema basi ni mtaji kwa ccm.
hakuna ubaya kwa zitto kutanganza nia, lakini alizingatia nyakati na busara za kufanya hivyo?

Hoja yangu ni kuwa hadi utakapopatikana ushahidi wa kutosha, cdm hawana haki ya kumchukulia hatua.
Zitto naye asifikirie political career kama solo candidate, lazima afanye kazi na wenzake na ajue ni maarufu kwasababu ni sehemu ya chama maarufu. zzk anatakiwa awe kiungo cha cdm na si kigawe au kigawo.

I stand to be corrected, historia inaonyesha zzk ni muumini wa siasa za ujana,anadhani ni beacon cdm, mara nyingi amekuwa anakigawa chama, ana misimamo yenye utata sana hata yale yenye masilahi ya taifa.

Chadema nao wanapaswa kubeba lawama, tumewatahadharisha mara nyingi sana juu ya mfumo wao wa kufichana na kuficha matatizo. Haya tunayoyaona ni mwendelezo wa akina juliana shonzo, kafulila,tuntemeke n.k.
cdm wamechukua mfumo wa kufuga watu na si taasisi kama lilivyo ccm.

kwa mahali ilipo cdm wanatakiwa wawe na uangalifu sana, ni make au break.
wakiongozwa na kanuni, sheria na taratibu watavuka mawaimbi haya, wakifuata upepo na emotional decision they're done! Very fine and thin line to walk on
 
MGOGORO WA CHADEMA

ZITTO NA JULIANA WANAPASWA KUJIUZULU KWANZA

Yaliyotokea wiki hii nyote mnayajua. Yaliyosemwa huko nyuma pia mwa yafahamu.
Mzozo wa CDM ni jambo lilokuwa wazi takribani miaka miwili au mitatu iliyopita.
Kilichochagiza mzozo huo ni uchaguzi wa baraza la vijana la Chadema ndipo wasioamini wakaanza kujua lipo jambo.

Ikumbukwe si mara moja au mbili kumekuwa na mtafaruku mkali hadi kupelekea uchaguzi wa BAVICHA kuahairishwa.
Fukuto lilianza kujitokeza pale akina Kafulila walipotaka kugeuza Chadema kuwa uwanja wa mapambano ya kuchafuana na si mapambano ya kifikra.

Kuondoka kwa Kafulila na wenzake kulionekana kama ni kudhoofisha CDM.
Kafulila alichukizwa na kitendo cha kunyang'anya baadhi ya nyadhifa zake.
Alijitoa na kutoa maneno yanayohusu Ukigoma na ukabila.
Maneno ya Kafulila yalihusishwa sana na Zitto ambaye hakuwahi kuyakanusha.

Zitto anajulikana kuendeleza siasa kwa misingi ya kuonewa iwe kikabila au kidini.
Haijawahi kutokea Zitto kukanusha tuhuma hizo na kila mara amekuwa anazunguka mbuyu.
Mahojiano yake hapa JF mwezi uliopita yalidhihirisha kuwa lipo jambo asilokubalina nalo si kisera za chama bali kimazingira.

Mabandiko kutoka ndani ya kambi ya PM7 yanamtaja Zitto kila upande, uwe wa mashitaka au washitakiwa.
Kibaya zaidi ametajwa kwa heshima kubwa na kundi linaloongozwa na Juliana Shanzo bila kutarajia.

Akiwa naibu katibu mkuu, Zitto hakupaswa kuchukua upande na alipaswa kukinusuru chama.
Tofauti na matarajio hayo Zitto ameongoza vikundi kwenda kwa masangoma kama alivyotoa ushahidi wa maneno yake.

Huko nyuma Zitto aliwahi kuitwa katika vikao na kusitishwa katika nafasi yake ya unaibu katibu mkuu.
Zitto pia aliwahi kutoa tuhuma kali kuhusiana na uongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
Safari hii pamoja na usangoma mheshimiwa ana madai ya kuwekewa sumu.

Safu hii isingependa kuchukua upande wowote kuhusiana na sakata hilo.
Inatosha kusema kuwa tuhuma za Zitto kuongoza vijana kuleta uasi ndani ya chama ni nzito na zinahitaji hatua za dharura.

Tuliwahi kuonya kuhusu nguvu kubwa aliyokuwa nayo Juliana Shanzo kama makamu BAVICHA.
Ingawa haonekani katika siasa za majukwaa au vingienvyo,jina lake limekuwa kubwa sana katikati ya mitafaruku.
Ni kuanzia kwa sakata la Shibuda na sasa ushiriki katika kundi la usangamo kama mkakati wa kisiasa

Suala hili limeleta mtafaruku baada ya Nape wa CCM kuingiza sumu ya madai dhidi ya Dr Slaa wa CDM.
Madai ya Nape ni hafifu na yasiyo na mantiki ukilinganisha hoja zake, umri wake na nyadhifa zake.

Madai kuwa Dr Slaa bado analipia kadi ya CCM yanaonyesha jinsi asivyokijua chama, asivyojua katiba ya chama au taratibu za serikali yake kuhusu uanachama na vyama vya siasa.

Hata hivyo kauli yake si ya kubezwa kwani ndio chimbuko la matatizo haya ndani ya CDM.
Katika tuhuma zinazotolewa wametajwa akina Hussein Bashe ambaye ni kiongozi wa kundi la Lowassa na Nape wa CCM.
Maneno ya Nape ndiyo yaliyowaibua vijana wa kundi la usangoma na kuanza kuwashambulia viongozi wa CDM.

Kauli za kashfa zinafuatia kauli za kiongozi mzito ndani ya CDM aliyesema ni uzuzu kushangilia ujenzi wa bara bara akimlenga mwenyekiti wa CDM kwa maneno aliyoyatoa kule Hai.

Bila kujali mantiki ya maneno ya Mbowe, kauli ya kiongozi huyo iliashiria kujenga mazingira ya kumwezesha Zitto katika harakati zake.Kiongozi huyo pia ni mahiri katika kujenga hoja magazetini. Hoja nyingi kati ya hizo zinashabihiana sana na timbwili la kurushiana madongo linaloendelea

Kilichotokea ndani ya CDM ni piga kulia na kushoto, kwa mwenyekiti na katibu ili anguko lao lifuatiwe na ustawi wa kundi la sangoma kushika madaraka.Tulionya kuwa umafia si njia nzuri ya kupambanisha fikra, fikra zinapambana kwa hoja na mantiki.

Ni kwa mtazamo huo na mlolongo wa matukio lukuki kama yale ya Zitto kususa shughuli mbali mbali za chama ikiwa ni pamoja na misimamo kama ya bungeni, safu hii inaona kuwa ni wakati sasa Zitto achukue hatua za kukinusuru chama.

Hatua hizo ni yeye kuonyesha uwajibikaji kwa kuachia nafasi za uongozi ndani ya chama ili abaki kama mwanachama.
Hili linatoa nafasi kwa uchunguzi huru kwa kuwaweka washiriki wote katika mizani iliyo sawa kama watuhumiwa.
Haki ikitendeka ukweli na uongo utajitenga.

Kwa wale washiriki wengine wa Usangoma unaolenga kuangamiza CDM, wao nao wabaki kama wanachama na kama yupo mwenye nyadhifa kama Juliana basi naye atoe nafasi ili natural justice ifanye kazi yake.

Kwa upande wa Chadema hii ni nafasi adhimu sana ya kuudhihirishia umma kuwa CDM ni chama tofauti na kile walichozoea, kwamba ni watu na si mtu na hakuna mwenye haki miliki ya chama awe mwanzilishi au mfuasi, kiongozi au mwongozwa.

Ni nafasi ya kuonyesha kuwa CDM ipo serious katika kushughulikia nidhamu ndani ya chama na nchi kwa ujumla na ya kwamba miaka 50 ya kubabaishana, kufichiana siri na kuiba sasa inafikia tamati kwa vile kuna mbadala.

Kinyume chake hili ndilo litakuwa anguko la CDM kwasababu wananchi watahitimisha kwa uelewa kuwa ni mvinyo ule ule ndani ya chupa mpya.

Siku zote wananchi wamechoshwa na siasa za kinafiki, udanganyifu, ulaghai n.k.
Kwahiyo huu ni mtihani muhimu sana kwa CDM kudhihirisha kuwa wao si kama wengine na wanamwelekeo tofauti.

Kwa vile haionekani kuwa Zitto au Juliana wamejifunza kutokana na makosa ya nyuma yaliyodhihirika na kusameheka, viongozi hawa wamepoteza imani, uadilifu na sifa za kiuongozi. Wamekosa political will ya kuwaunganisha wanachama, wamevunja trust kwa kushiriki siasa za umafia na usangoma na hawana mamlaka ya kiroho tena mbele ya jamii.
Ni Muafaka wapewe nafasi ya kujiuzulu.

Ni kwa hali hiyo CDM inapaswa kuitisha kikao cha dharura kutekeleza yafuatayo
1. Kwamba, Zitto na Juliana wanaachia ngazi ili kutoka nafasi ya uchunguzi huru
2. Kwamba, iundwe tume huru ili kubaini chanzo cha mgogoro na washiriki wake pande zinazohasimiana
3. Kusimamisha uanachama wale wote watakaobainika kuwa na hatia
4. Kuivunja BAVICHA na kuiunda upya kukiwa na hali ya utulivu itakayotokana na namba 3 hapo juu

CDM inapaswa kuongozwa kama taasisi kwa misingi ya sheria haki na usawa na kwamba CDM ni watu na si mtu mmoja mmoja. CDM lazima ielewe kuwa ufanisi wa chama hautegemei personality bali mambo mengine kama committment, dedication, trust, moral etc

Kuendelea kuwaacha wahalifu kwa lengo la kuyamaliza katika vikao ni kulea ujinga na donda ndugu sawa na lile linalowaumiza CCM. Muhimu zaidi tutauliza nini tofauti ya CDM na CCM?

Ninaposema uhalifu sina maana ya kutoa hukumu bali uhalifu ambao umedhihirika wa kushiriki siasa za usangoma na kuuana ambazo hazijakanushwa na wahusika wa sakat hili.
Hayo mengine yabaki kuwa tuhuma hadi yatakapothibitika vinginevyo.

Ndani ya wiki moja Zitto na Juliana wanapaswa kujiuzulu na kama hawatafanya hivyo basi chama kishike hatamu ya kuwawajibisha bila woga au hofu. Hili lisipotokea political base ya CDM itapigwa na butwaa, kutakuwa na uundwaji wa makundi zaidi, kutoaminiana katika vikao na mikakati.

Mgogoro wa NCCR ya Mrema na akina Lamwai ulipuliziwa ubani kwa maneno matamu, ni wamoja hatuna ugomvi n.k.
Mgogoro wa TLP nao ulifunikwa kwa kitambaa cheupe chenye maandishi sisi ni wamoja na wabaya wetu ni CCM.
Mgogoro wa CUF ulipuliziwa utuli kwa maneno yenye ladha, hamu na yanayoleta bashasha kuyasikia.
Vyama vyote hivyo vimetoka wodini na vingine kubaki katika historia.

Huko ndiko CDM inaelekea kama haitachukua hatua za haraka, makusudi na ngumu.

Tusemezane
 
Heri ya mwaka mpya wana duru za siasa.
In pipeline;
-Siasa za Marekani(Obama na kipindi cha pili)
-Mzozo wa Mali (Ushiriki wa mataifa ya magharibi na kwanini Ufaransa)
-Mzozo wa mali (Nini wasi wasi wa mataiaf ya magharibi kuhusu katiba mpya na Zanzibar ''huru'')
-Mtazamo kuhusu maoni ya katiba mpya kwa ujumla.

Itaanza kuwajia kuanzia kesho.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom