Dr. Ulimboka yupo mafichoni, kuzungumza wakati wowote!

We chama,
Hapa tunazungumzia habari ya Dr.Ulimboka na Usalama wake kwa sasa baada ya kurejea nchini toka Sauz kwenye matibabu.Sasa wewe unatuletea habari ya intelijensia ya CHADEMA, kuna uhusiano gani????Watu walio na chuki na CHADEMA ambao ni kutoka CCM utawajua kwa kauli zao. Hii inaonyesha tu kwamba wewe chama ni mtu wa chama cha magamba yaani CCM!

Nakupa pole sana mwanakwetu!

Mimi ni CCM hilo sina shaka nalo, kwani Chadema issue ya Dr. Ulimboka si imeshakuwa yao au hilo pia nalo hulijui?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mh CDM na Hii kesi wapi na wapi. Ndio kuthibitisha kuwa lina usiasa kidogo. liwalo na Liwe.
 
ulimboka.jpg
Dk. Stephen Ulimboka

KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha, jana baba mzazi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, aligeuka mbogo, baada ya kuwafukuza waandishi wa habari nyumbani kwake.
Tukio hilo, lilitokea baada ya waandishi wa habari wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kufika nyumbani kwa mzee Ulimboka, eneo la Ubungo Kibangu, mjini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuomba kuonana na Dk. Ulimboka.

Baada ya kuwasili waandishi hao, walipokelewa kwa maneno maneno, huku akiwatolea macho, jambo ambalo liliashiria wazi hayuko tayari kuzungumza nao.

Alianza kwa kusalimiana na waandishi hao, kisha akaulizwa kama Dk. Ulimboka yupo, alijibu kwa kifupi hayupo, lakini kwa maneno makali.

Mwandishi: Sahamani ningependa kujua Dk. Ulimboka yupo?

Baba: Hayupo, ametoka tangu asubuhi hapa kwa kutumia gari lake.

Mwandishi: Je, amekuaga kwamba anaelekea wapi?

Baba: Sikuagwa, nasema ondokeni jamani, siwezi kusema na sitasema chochote kuhusiana na mwanangu,” alisema mzee Ulimboka kwa mshituko na jaziba kubwa.

Lakini katika kuonekana mzee Ulimboka kujaa jazba, muda wote alipokuwa akizungumza alikuwa amezungukwa na baadhi ya ndugu, huku wengi wao wakizungumza lugha ya Kinyakyusa, ili waandishi wasielewe kinachoendelea.

Hali ya ulinzi katika eneo la mji wao, ilikuwa ya hali ya juu tofauti na siku zote.

Lakini MTANZANIA ilipata fursa ya kuzungumza na akina mama wawili waliokuwa wakitoka ndani ya nyumba ya Dk. Ulimboka, ambao bila kificho walisema wamefurahi mno kumuona mpendwa wao amerejea akiwa salama kabisa.

Pamoja na kuzungumza hivyo, akina mama hao walikataa katakata kutaja majina yao.

MTANZANIA ilipowataka wathibitishe kama Dk.Ulimboka yupo nyumbani, wakina mama hao waliruka kimanga, huku wakitoa majibu ya kujiumauma, kwamba Dk. Ulimboka ametoka tangu asubuhi.

“Hapana kijana….ila…mmmh, Dk. Ulimboka alitoka asubuhi na hatujui alipokwenda jamani….kwa muda wote ule tulikuwa tunaongea na mkewe,” alisema mmoja wao.

Baada ya muda kupita likafika gari moja lililokuwa limebeba geti kubwa lenye rangi nyekundu, lilirushwa na mafundi walianza kazi ya kuliweka katika lango kuu la kuingia wageni.

Kushushwa geti hilo, ilikuwa ishara tosha inayoonyesha kazi kubwa ya ujenzi wa uzio wa nyumba inaendelea.

Dk. Ulimboka alipelekwa nchini Afrika Kusini, Juni 30 mwaka huu, kwa ajili ya matibabu, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kutupwa katika msitu wa Pande.

Daktari huyo ambaye alikuwa akiratibu mgomo wa madaktari kwa kupitia Jumuiya ya Madaktari, Juni 27 mwaka huu aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu, akiwa katika hali mbaya.

Kutokana na tukio hilo, wanaharakati wa haki za binadamu waliituhumu Serikali kuhusika na tukio hilo, huku Serikali ikikana tuhuma hizo, na Jeshi la Polisi liliunda tume kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.
 
Liko mahakamani hivyo Ulimboka haruhusiwi kuingilia uhuru wa mahakama Hahahahaaaa...naota tu ila kwa sauti.
 
Lazima mzee wa watu awe Mbogo, uchungu wa mwana eti. Maana hawa kina Rama/Abedi/David wanaweza wakaja tena kwa njia ya waandishi wa habari. Ukishaumwa na nyoka, hata jani lazima likustue.
 
Bora Dr. Ulimboka umerudi salama ili uondoe huu mkanganyiko wa habari nyiiingiii sana!
 
Ni vema akazungumzia ushiriki wa KUBENEA na Dk. DEO katika sakata la kutekwa kwake ili kukomesha tabia ya uchochezi ambayo inaweza kuhatarisha mshikamano wa Watanzania.

Eh ! mshikamano wa kuwapiga wengine na kuwaziba midomo ? Mh ! sijaelewa.
 
Kuna uzi humu ndani unaobashiri uwezekano wa Dr. Ulimboka kuwekwa chini na kuonywa kamwe asiongee jambo lolote. Na hii kazi ilitakiwa apewe Mzee Mengi, ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye alichangia gharama za Ulimboka kwenye nje.

Hili mnalionaje wadau kwa move hii ya familia, Baba na Dr. Ulimboka mwenyewe??
 
JUMANNE, AGOSTI 14, 2012 06:07 NA EVANS MAGEGE

KATIKA hali ya kushangaza na kusikitisha, jana baba mzazi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, aligeuka mbogo, baada ya kuwafukuza waandishi wa habari nyumbani kwake.

Tukio hilo, lilitokea baada ya waandishi wa habari wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kufika nyumbani kwa mzee Ulimboka, eneo la Ubungo Kibangu, mjini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuomba kuonana na Dk. Ulimboka.

Baada ya kuwasili waandishi hao, walipokelewa kwa maneno maneno, huku akiwatolea macho, jambo ambalo liliashiria wazi hayuko tayari kuzungumza nao.

Alianza kwa kusalimiana na waandishi hao, kisha akaulizwa kama Dk. Ulimboka yupo, alijibu kwa kifupi hayupo, lakini kwa maneno makali.

Mwandishi: Sahamani ningependa kujua Dk. Ulimboka yupo?

Baba: Hayupo, ametoka tangu asubuhi hapa kwa kutumia gari lake.

Mwandishi: Je, amekuaga kwamba anaelekea wapi?

Baba: Sikuagwa, nasema ondokeni jamani, siwezi kusema na sitasema chochote kuhusiana na mwanangu," alisema mzee Ulimboka kwa mshituko na jaziba kubwa.

Lakini katika kuonekana mzee Ulimboka kujaa jazba, muda wote alipokuwa akizungumza alikuwa amezungukwa na baadhi ya ndugu, huku wengi wao wakizungumza lugha ya Kinyakyusa, ili waandishi wasielewe kinachoendelea.

Hali ya ulinzi katika eneo la mji wao, ilikuwa ya hali ya juu tofauti na siku zote.

Lakini MTANZANIA ilipata fursa ya kuzungumza na akina mama wawili waliokuwa wakitoka ndani ya nyumba ya Dk. Ulimboka, ambao bila kificho walisema wamefurahi mno kumuona mpendwa wao amerejea akiwa salama kabisa.

Pamoja na kuzungumza hivyo, akina mama hao walikataa katakata kutaja majina yao.

MTANZANIA ilipowataka wathibitishe kama Dk.Ulimboka yupo nyumbani, wakina mama hao waliruka kimanga, huku wakitoa majibu ya kujiumauma, kwamba Dk. Ulimboka ametoka tangu asubuhi.

"Hapana kijana….ila…mmmh, Dk. Ulimboka alitoka asubuhi na hatujui alipokwenda jamani….kwa muda wote ule tulikuwa tunaongea na mkewe," alisema mmoja wao.

Baada ya muda kupita likafika gari moja lililokuwa limebeba geti kubwa lenye rangi nyekundu, lilirushwa na mafundi walianza kazi ya kuliweka katika lango kuu la kuingia wageni.

Kushushwa geti hilo, ilikuwa ishara tosha inayoonyesha kazi kubwa ya ujenzi wa uzio wa nyumba inaendelea.

Dk. Ulimboka alipelekwa nchini Afrika Kusini, Juni 30 mwaka huu, kwa ajili ya matibabu, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kutupwa katika msitu wa Pande.

Daktari huyo ambaye alikuwa akiratibu mgomo wa madaktari kwa kupitia Jumuiya ya Madaktari, Juni 27 mwaka huu aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu, akiwa katika hali mbaya.

Kutokana na tukio hilo, wanaharakati wa haki za binadamu waliituhumu Serikali kuhusika na tukio hilo, huku Serikali ikikana tuhuma hizo, na Jeshi la Polisi liliunda tume kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.

Baada ya kurejea nchini akiwa mzima wa afya taarifa nyeti zinaeleza kuwa Dr.Steven Ulimboka huenda akaita waandishi maalum ktk eneo ambalo halijatajwa mkoani morogoro..Nyeti zinadai kuwa tayari ana orodha ya watu wanne anaowatuhumu..stay tune til tommorow jamaa anatavyomwaga MBOGA.
 
Sirikali iko kwenye kikaango cha moto hata kabla ya hio press conference. Mtujuze jamani
 
Season hii sijui tuipe jina gani? "TRUTH UNLEASHED" nadhani inafaa kua jina la hii season
 
Back
Top Bottom