Ndugu yangu umeongea mambo ya msingi sana ambayo baaadhi ya wanajamvi humu hawayaoni kabisa kiasi kwamba nachelea kuwaita great thinkers, kimsingi wanastahili kuitwa mashabiki.
Maisha ya watu wanaokufa kamwe hayawezi kuwa ndio gharama ya madai ya maslahi ya madaktari. Najua serikali yetu ni dhaifu na imeshidwa kuboresha maisha ya watanzania wote (si madaktari pekee) lakini mtindo walioamua kutumia madaktari ni wa kuumiza wananchi ambao wanaodai wanawatetea.
Hata Ulimboka ambaye leo petty thinkers wanamwita shujaa, baada ya kusomeshwa kwa jasho la walalahoi hakukumbuka kuwatumikia hata kidogo badala yake akaenda kwenye shughuli zenye maslahi mazuri kwake.Leo anasema anatetea wananchi, uzalendo huu kaanza lini??Huu hauwezi kuwa ushujaa, huu ni u binafsi tu.
Siungi mkono mgomo wa madaktari wala serikali ya magamba
ukiona watu wa zima na akili zao hawajitambui na wapo kipropaganda zaidi kupindisha ukweli utambue kwamba tunawakati mgumu wa kujikomboa majinga mengi ambayo yanadhani madaktari ndio walioleta hali ya kukosa x-ray katika hospitali zetu za wilaya
CT-scan katika hospitali za rufaa
na vitanda bora vya kujifungulia wazazi katika zahanati zetu ndio wanaokwamisha maendeleo ya nchi kwa vile tuu wamekalia viti vya kuzunguka maofisini
hawa akili zao zimejaa nta lakini japo kwa kuchelewa na kwa kupitia njia ngumu ya akina Ulimboka kumwaga damu bado kuna siku tutafika,Sata kaingia Zambia juzi apa jambo la kwanza anafanya sasa ni kuboresha skta ya afya
Majambazi ya CCM yakiong'olewa fedha zinazokusanywa nina uhakika zitaboresha sekta hii muhimu kwa jamii