Dr. Ulimboka azimwa

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,060
309
DHAMIRA ya Mwenyekiti wa Jumuiya yaMadaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka yakutaka kuwafichua polisi na watu wengine wanaodaiwa kuhusika katika tukio la kumteka, kumpiga, kumtesa na kumtupa katika Msitu wa Mabwepande, imezimwa na vigogo waserikali, Tanzania DaimaJumatano limebaini.

Uchunguzi ambao gazeti hili limekuwa likiufanya tangu Dk. Ulimboka awasili nchini, umebaini kuwa kinara huyo wa mgomo wa madaktari uliotikisa nchini, amekuwa na vikao na vigogo wa idara za ulinzi na usalama na kumshawishi awe mtulivu katika kipindi hiki ambapo serikali inafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumteka nyara.

Watu wa karibu na daktari huyo, walilieleza gazeti hili kuwa, katika kipindi kifupi amekutana na vigogo kadhaa wa serikali wakimtaka asiseme chochote kwa hofu ykuvuruga uchunguzi. Wakati vigogo wa serikali wakifanikiwa kumzima Dk. Ulimboka, upande wa pili wa wanaharakati, ndugu na madaktari wenzake, wamekuwa wakimbana kumtaka awe jasiri kueleza umma ukweli, na hata kuwataja kwa majina waliohusika kumteka.

Hata hivyo, Joshua Mulundi aliyetajwa kuwa raia wa Kenya amefikishwa mahakama akituhumiwa kuhusika na tukio hilo. Habari kutoka ndani ya uongozi wa Chama cha Madaktari (MAT), zilidai kuwa, hali ya ushawishi kutoka kwa vigogo wa serikali na mbinyo anaoupata kutoka kwame wanaharakati na madaktari wenzake, umemweka njia panda Dk. Ulimboka kiasi cha kushindwa kuamua kama atoke hadharani kueleza ukweli au atulie ili kulinda maisha yake.

Mara baada ya kurejea nchini akiwa na afya njema, Dk. Ulimboka amekuwa akikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari, kwamba anajiandaa kueleza ukweli wa tukio nzima na hata kuwataja waliohusika na unyama aliofanyiwa.

"Kwa jinsi hali ilivyo, Dk. Ulimboka atabaki na siri moyoni maana amekutana na watu wazito, wamezungumza nae na kumshawishi anyamaze, ndiyo maana hadi sasa hayuko tayari kuueleza umma kile alichopania kusema.

Lakini pia wanaharakati na hata wanasiasa kila siku wanajaribu kumshawishi atoke hadharani kusema ukweli kabla tukio hilo halijaanza kusahaulika masikioni mwa watu," alisema daktari mmoja ambaye ni mtu wa karibu na Dk. Ulimboka. Katika kuthibitisha kwamba Dk. Ulimboka hayuko tayari kusema chochote, juzi gazeti hili lilikutana nae katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo ambapo alisema kuwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa, anamwachia Mungu.

Dk. Ulimboka ambaye aliongozana na familia yake kanisani hapo kwa nia ya kutoa sadaka na kumshukuru Mungu, alipobanwa hakuwa tayari kusema chochote zaidi ya kusema muda ukifika ataweka ukweli hadharani na kukanusha tuhuma za kunyamazishwa na vigogo.

Duru za kiintelijensia zililieleza gazeti hili kuwa, katika hali ya kawaida Dk. Ulimboka hawezi kusema chochote kama ilivyotokea kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe aliporejea kutoka kwenye matibabu.

Dk. Mwakyembe ambaye aliugua ugonjwa ambao hata mwenyewe aliamini ulitokana na sumu, uliosababisha aoze kucha, kutoka unga mwilini na miguu kupasuka, alipata kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba atakuja kueleza ukweli jinsi alivyopewa sumu iliyomsababishia ugonjwa huo.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe tangu aliporejea hadi kuteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi, hajawahi kueleza chochote kama alivyoahidi na kumweka mahali pabaya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta ambaye ndiye aliyeshikia bango kwamba Dk. Mwakyembe alipewa sumu.

Dk. Ulimboka ambaye alipelekwa Afrika Kusini akiwa hawezi kutembea wala kula mwenyewe baada ya Juni 27 mwaka huu kutekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, amekuwa akiwakwepa wanahabari na anaishi kwa kujificha. Kiongozi huyo wa madaktari amerejea nchini huku serikali na madaktari wakiwa hawajafikia mwafaka kuhusu madai yao.

Madai ya madaktari hao ni hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.

Safari ya Dk. Ulimboka kwenda kwenye matibabu nchini Afrika Kusini ilitawaliwa na usiri mkubwa alipoondoka nchini Juni 31 mwaka huu, akisindikizwa na Dk. Pascal Lugajo, kaka yake, Dk. Hobakile Ulimboka na mke wake, Dk. Judith Mzovela. Kutekwa Dk. Ulimboka alitekwa na kufanyiwa vitendo vya ukatili wakati akiratibu mgomo wa madaktari uliokuwa ukiendelea na aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu akiwa katika hali mbaya.

Kutokana na tukio hilo, wanaharakati wa haki za binadamu waliituhumu serikali kuhusika na tukio hilo, huku yenyewe ikikana na kuliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka waliohusika.

Wakati Dk. Ulimboka alipokuwa akiendelea na matibabu Afrika Kusini, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali haihusiki na kilichomtokea daktari huyo kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu katika majadiliano baina ya serikali na madaktari. Rais Kikwete alisema hayo katika hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

"Dk. Ulimboka alikuwa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.

Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na serikali," alisema Rais Kikwete.

Alisema alichofanyiwa Dk. Ulimboka kimemsikitisha na kumhuzunisha kwa kuwa ni kitendo cha kinyama na kinyume kabisa na mila na desturi za Tanzania.

Kauli ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa madaktari inafanana na ile iliyokuwa imetolewa awali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema wanatambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka kuhusu kilichomtokea Dk. Ulimboka, lakini ameshangazwa na hisia hizo akisema haoni sababu ya serikali kufanya hivyo.

Source: Tanzania Daima
 
teh teh teh..imekaa vibaya, hii bado haijatulia! Sijui ule wimbo aliuimba nani. In short, kutulia ni muhimu sana maana papara na haraka haraka bila kuwa na matayarisho ya kueleweka unaweza kukosea step.
 
Tumeshasema habari za Dr. Ulimboka zimetuchosha hapa JF pelekeni Issa Michuzi Blog hizo habari
 
This is very clear! Huu mgomo ni wa madaktari wote,mshikamano wao wote ndio muhimu.sometimes namuelewa Ulimboka,hakuna jemedari anaweza kusimama imara bila uhakika wa jeshi analoliongoza.

Ulimboka kupigwa tu Madaktari wakasambaratika hadi leo alafu wanataka yeye alianzishe tena!

nafikiri mwenendo wa madaktari umemkatisha tamaa Ulimboka na alitarajia wenzake wangekomaa zaidi baada ya kuumizwa vibaya lakini ikawa kinyume! kumbe hata kama wangemuua kabisa mgomo ungeisha hivi hivi kiuoga!

naelewa nafasi ya Dr Ulimboka!
 
tatizo upande moja kuna icc, na upande wa pili kuna Dr ulimboka , sasa mtu ukiambiwa uchague upande wa kufuata ni wa Dr Uli
 
Godwinnko
Ilishasemwa humu JF kuwa Ulimboka ni mtaalamu na siyo mwanasiasa, hawezi kupelekwa pelekwa na wanasiasa na wanaharkati kwa maslahi yao binafsi. Haya sasa mmeanza kuja na "azimwa" Chanzo chenyewe cha taarifa Tdaima, ndo wale wle Kubenea type. Mwacheni Dr. wa watu apumzike ili aiendeleze taaluma yake, kama waliokuwa wakimtumia hawajaridhikana wabuni mbinu nyingine ya kujipatia umaarufu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Odb
Tumeshasema habari za Dr. Ulimboka zimetuchosha hapa JF pelekeni Issa Michuzi Blog hizo habari

Dr Ulimboka mshukuru Mungu kwakuwa bado unao uhai. Achana na yaliyopita a.ka potezea na fungua ukurasa mpya. Familia yako bado inakuhitaji sana.
 
This is very clear! Huu mgomo ni wa madaktari wote,mshikamano wao wote ndio muhimu.sometimes namuelewa Ulimboka,hakuna jemedari anaweza kusimama imara bila uhakika wa jeshi analoliongoza.

Ulimboka kupigwa tu Madaktari wakasambaratika hadi leo alafu wanataka yeye alianzishe tena!

nafikiri mwenendo wa madaktari umemkatisha tamaa Ulimboka na alitarajia wenzake wangekomaa zaidi baada ya kuumizwa vibaya lakini ikawa kinyume! kumbe hata kama wangemuua kabisa mgomo ungeisha hivi hivi kiuoga!

naelewa nafasi ya Dr Ulimboka!

Yule ni binadamu, anaweza kutafakari na kuchukua uamuzi sahihi, issue hapa siyo madaktari kumsaliti, kishaona suala lake linatumiwa kisiasa wakati yeye ni mtaalamu. Namuunga mkono Ulimboka kwa uamuzi huo. Awaachie akina Kubenea ndo size ya majungu.
 
Ulimboka, ni dhambi kubwa kuudanganya uma wa watu wote waliolia kwaajiri yako na kukuona kama mpigania haki,then leo unanunuliwa.fanya maamuzi mazuri la sivyo hautokaa kwa amani rohono mwako.hata mungu hapendi.
Shauri yako.
 
Dr family. kaka daktari, mke daktari na yeye mwenyewe ni daktari. kama rate ni watu 555 kwa daktari, maana yake ni kwamba watu 1665 watakosa tiba. Ulimbokas please msigome tena mtatuua.
 
Waliopitia madhila kama haya ya Dr Ulimboka ni nadra kusimama hadharani wakayasema yote. Niliwahi kumsikia mtu mmoja tu aliyetoka hadharani akayazungumza haya. Ni Ngugi wa Thiong'o kule Kenya. Hapa kwetu ni wengi waliwahi kuteswa hivi. Baadhi bado wako hai lakini hawatakaa waseme hadharani.
 
Bora akae kimya na aendelee na maisha yake kama kawaida. Amekosa support kutoka kwa wanataaluma wenzake, na yeye ataonekana ndio mbaya kwa serikali na wananchi.
Just be what you were doctor, let the dramma end by confronting the press and do like Mwakyembe. Do not waste our precious time waiting for the glorious moment to punish the devils who did the kill-attempt on you. Twataka kujua uko upande gani?
 
mwacheni ulimboka apiganie uzima wake,acheni siasa katika maisha ya watu,acheni kumtumia ulimboka kisiasa
 
mwacheni ulimboka apiganie uzima wake,acheni siasa katika maisha ya watu,acheni kumtumia ulimboka kisiasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom