MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,603
Kwa hili ninakubaliana nawe JJB, bora anyamaze yaishe. Sisi tunaotaka aseme sio kwa sababu yoyote zaidi ya kutaka kusoma umbea tu. Watanzania sote tumemsaliti Dr.Ulimboka na wanaharakati wote waliowahi kuthubutu kulenga jiwe la kwanza lakini sisi tukaficha mikono yetu.Bora akae kimya na aendelee na maisha yake kama kawaida. Amekosa support kutoka kwa wanataaluma wenzake, na yeye ataonekana ndio mbaya kwa serikali na wananchi.
Just be what you were doctor, let the dramma end by confronting the press and do like Mwakyembe. Do not waste our precious time waiting for the glorious moment to punish the devils who did the kill-attempt on you. Twataka kujua uko upande gani?
Moja ya maneno na rai aliyoitoa Dr. baada ya kudhulumiwa afya na uhuru wake yalikuwa kuwataka Madaktari wenzake (na Watanzania kwa jumla) kuwa yeye yamemfika yaliyomfika, lakini waliobaki wanendelee na mapambano; matokeo yake, Madaktari walifanya nini na Watanzania tumefanya nini?
Baada ya Mwanahalisi kulezea kile ilichokijua na kuwataja watu na ubini wao na nambari zao za simu, Watanzania tumefanya nini? Tuseme Dr. Ulimboka aje na habari zile zile za Mwanahalisi, Watanzania tutafanya nini? Kama tuwatendaji kweli na sio wambea tu, tuchukue hatua juu ya yale ambayo tayari tunayajua kabla ya kutaka mengine mapya.
Tumwache Dr. apumue na sisi tuendelee na woga na blah blah blah zetu. Uchune Dokta, uchune!